Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote

Wednesday, September 30, 2009

Mwanaume mmoja afunga ndoa na wanawake 4 kwa wakati mmoja

Mwanamme mmoja huko Afrika ya kusini kafunga ndoa na wanawake 4 kwa wakati mmoja . Mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Milton Mbhele mwenye umri wa miaka 44 aliingia kwa mbwembwe sehemu ya sherehe hizo huku akitumia usafiri wa gari ya kifahari aina ya limousine na kuwavisha pete na kuwabusu wake zake wote kwa zamu. Bwana harusi alisema harusi hii ya mara moja imemsaidia sana kubana matumizi kuliko angefunga harusi 4 tofauti. Serikali ya Afrika ya Kusini inatambua harusi za namna hii na imekuwa jambo la kawaida kwa watu wa jamii ya Wazulu alikotokea Raisi wa nchi hiyo Jacob Zuma ambaye nae ana wake 3.
Hii ni picha inayomuonyesha Milton akiwa na wake zake wote aliowaona kwa wakati mmoja

Mambo usiyoyajua Kuhusu Jose Chameleon

Jina halisi : Joseph Mayanja
Kazi : Mwanamuziki
Mke : Danniella Atim

Chameleon ni mmoja wa wanamuziki maarufu na waliotokea kutamba na kupendwa katika ulimwengu wa Muziki kwenye nchi za Afrika mashariki, pia ameonyesha kipaji cha kuimba nyimbo kwa kutumia lugha za nchi mbalimbali ikiwemo nje ya Afrika Mashariki na hii imeonekana pale alipotoa singo yake ya Maokao & Maoko aliyoiimba ya lugha ya kizimbabwe. Binafsi anazungumza kuwa muziki ni vile wewe unavyoupenda na kuukubali haijalishi hata kama huelewi maana halisi ya nyimbo ( nafikiri anamaanisha midundo)
Chameleon akiwa na Asali wa Moyo wake Danniella Atim siku ya harusi yao.Inasemekana siku ya Harusi Chameleon aliwasili kanisani akitumia usafiri wa ndege ndogo huku bibi harusi Danniella akiwa na msafara wa magari 7 aina ya Benz. Harusi yao ilifanyika Kampala Serena Hotel na inakadiriwa kuwa moja ya harusi maarufu zilizowahi kufanyika nchini Uganda. Nyepesi nyepesi zetu zimetujulisha kuwa watu walikunywa, walikula na kusaza na inakadiriwa kulikuwa na Krate za bia zaidi ya 500 bila kuhesabu vinywaji laini, mivinyo na pombe kali.Baadhi ya picha zinachomuonyesha Chameleoan akiwa Kitandani baada ya kupata ajali mbaya ya gari 2008.Dawa ya Mning'inio( Hangover ) hii hapa


Kama utaamka na uchovu au uumwaji wa kichwa uliosababishwa na unywaji wa pombe fanya mambo yafuatayo:-

1. Kunywa maji mengi mara tu unapoamka

2. Kama utaumwa na kichwa ni vizuri kutumia dawa yenye Asprini

3. Unashauriwa kuoga maji ya uvuguvugu kwani yanasaidia kupunguza toxini mwilini

4. Unashauriwa kula ndizi mbivu 2 hadi 3 kabla ya kupata kifungua kinywa

5. Kunywa mchanganyiko wa juice ya limao au ndimu na kikombe 1 cha kahawa nyeusi

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote