Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote

Friday, October 30, 2009

Kesi ya EPA yaahirishwa hadi Mwakani

UGONJWA wa mshtakiwa Farijara Hussein umekwamisha kuendelea kusikilizwa kwa kesi ya wizi wa Sh 3.8 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) inayomkabili yeye pamoja na wenzake watano na sasa kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mwakani ili kutoa nafasi ya mtuhumiwa huyo kupata matibabu. Kesi hiyo ilishindwa kuendelea kusikilizwa jana mbele ya jopo la mahakimu watatu lililokuwa likiongozwa na Hakimu Samuel Kalua mara baada ya Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya kudai kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuendelea kuisikiliza na kwamba wana mashahidi wawili. Baada ya maelezo hayo, Wakili Majura Magafu anayemtetea mshtakiwa Farijara, aliiomba mahakama iahirishe kesi hiyo kwa sababu mteja wake huyo anaumwa na amepewa muda wa mampuziko wa siku tatu (ED) kuanzia juzi, jana na leo. Magafu aliendelea kudai mbali na mapumziko hayo pia alitakiwa aonane na mtaalamu wa hospitali ya Burhan, Profesa Aboud. Kufuatia hoja hiyo hakimu Kalua alikubaliana na maombi hayo na kuiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na si kuendelea kusikilizwa ambapo alisema kuwa Desemba 21, mwaka huu kesi hiyo itatajwa tena na kuongeza kuwa kuanzia Februari Mosi hadi 5, 2010 kesi hiyo ndio itaendelea kusikilizwa mfululizo. Awali Oktoba 27 mwaka huu, mahakama ililazimika kusimama kusikiliza ushahidi katika kesi hiyo baada ya mshtakiwa huyo kuomba kwenda haja ndogo mara kwa mara kutokana na kusumbuliwa na tatizo la figo. Mshtakiwa huyo aliomba kwenda haja ndogo mara kwa mara na kusababisha hakimu kuamua kumruhusu aondoke. Akitoa ushahidi wake Msajili Msaidizi kutoka ofisi ya Msajili wa Majina ya Biashara na Kampuni (Brela), Rehema Kitambi alidai kuwa mshtakiwa Farijara na mtu mwingine aliyemtaja kwa jina la Kiza Selemani walighushi jina la biashara la Mibale Farm lililotumika kuchota fedha hizo za EPA. Alidai kuwa hati zenye jina la Mibale Farm hazitambui kwasababu hazijatolewa na Brela na hata saini inayoonekana katika baadhi ya hati hizo imeghushiwa na kufanana na ya kwake. Shahidi huyo alidai kuwa Septemba 2 mwaka 2005 Farijara na Kiza waliomba kusajili jina la biashara la Nibale Farm na kwamba Septemba 5 mwaka 2005 walipeleka maombi mengine ya kubadili jina hilo ili liwe Mibale Farm. Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Rajabu Maranda, Ajay Somani, Imani Mwaposya, Ester Komu na Sophia Kalika. Washtakiwa hao wanadaiwa kuiibia BoT Sh 3.8 bilioni baada ya kudanganya kuwa kampuni ya Mibale Farm imepewa deni na kampuni ya Lakshmi Textile Mills ya nchini India.

FIFA & TFF kuzindua Program ya kuimarisha SOKA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na lile la kimataifa, Fifa wamezindua programu maalum ya soka ya watoto kati ya miaka 6-12 ambayo itaanza hivi karibuni nchini kote. Lengo la kuanzisha programu hiyo nchini ni kutaka soka la watoto liweze kukua na kufika mbali pamoja na kupata wachezaji bora ambao wataiowakilisha nchi baadae katika mashindano mbalimbali. Rais wa TFF, Leordegar Tenga alisema jana kuwa waliomba mradi huo toka Fifa na wamekubali kwa kufuata kanuni zake hivyo kuwataka watoto wengi wajitokeze. Alisema walikutana na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Mkurugenzi wa Fifa kwa nchi za Afrika, Ashford Mamelodi na kukubaliana jinsi ya kuendesha programu hiyo nchi nzima pamoja na kupata wadhamini. "Tayari tumekutana na wahusika mara baada ya kupata kibali kutoka Fifa na wamekubalina hivyo kwa sasa wako katika mchakato wa kupata wadhamini watakaowasaidia kuendesha mradi huo,"alisema Tenga. Mkurugenzi wa Fifa, Ashford Mamelodi alisema wamezindua programu hiyo nchini kote ambayo itashirikisha jinsia zote na wamefurahishwa na serikali kwa kuonyesha moyo wa kuwasaidia. Alisema Fifa watasaidia katika mashindano mbalimbali watakayoandaa pamoja na kufundisha walimu vifaa mbalimbali ambavyo vitahitajika na kuwataka TFF kuwa makini katika kuendeleza hilo. "Lazima tuanzie ngazi za chini tukitaka kufika mbali kisoka kwani hakuna njia mbadala ya kufika mafanikio makubwa bila njia hizo",alisema Mamelodi.

MAGUFULI kugawa samaki Bure

Serikali imeamua kugawa bure samaki waliokamatwa kutokana na wavuvi haramu wa kimataifa kupatikana wakivua kwenye eneo la bahari ndefu kinyume cha sheria. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, alisema jana kuwa samaki hao watatolewa bila malipo kwa vyuo, shule za sekondari za bweni na hospitali. Kwa mujibu wa Magufuli, taasisi nyingine zitakazonufaika kwa mgawo wa samaki hao ni vyuo vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Wananchi (JWTZ), vyuo vya uganga, taasisi za kidini zinazotoa huduma za kijamii kama vile kuwalea na kuwatunza watoto yatima na wazee. Alisema taasisi itakayohitaji samaki hao italazimika kutuma maombi kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo ama kwa Mkurugenzi wa Uvuvi. Magufuli alisema hatua ya kuwatoa samaki hao imefikiwa baada ya kupata amri ya mahakama, iliyoamuru kwamba serikali inaweza kuwauza ama kuwagawa bila malipo samaki hao. Hata hivyo, Magufuli alisema kipaumbele cha ugawaji wa samaki hao kitaelekezwa kwa taasisi zilizopo jijini Dar es Salaam, kwa kuwa wanufaika watalazimika kujigharamia gharama za usafirishaji. Magufuli alisema kwa kuwa samaki hao hawatauzwa, serikali imeweka utaratibu utakaowezesha watu watakaokiuka maelekezo hayo na kuwauza tofauti na malengo, watachukuliwa hatua za kisheria.

Wachezaji SIMBA waahidiwa Milioni 30/=

Wakati kesho watani wa jadi nchini Simba na Yanga zikiingia uwanjani kupambana katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara, uongozi wa timu ya Simba umewaahidi wachezaji kuwapa Sh. Milioni 30 kama watashinda mchezo huo. Hatua hiyo ni kujibu mapigo kwa Yanga, ambapo gazeti moja la kila wiki lilidai kuwa wachezaji wa timu hiyo wameahidiwa kiasi cha sh. milioni moja kwa kila bao litakalofungwa dhidi ya Simba. Habari za ndani kutoka katika kambi ya timu hiyo iliyopo Zanzibar, wachezaji hao wameahidiwa fedha hizo na kundi la wanachama wa klabu maarufu kama Friends of Simba endapo watashinda mchezo huo. Ni kweli tumeambiwa kuna milioni 30 ambazo tutapewa kama tutafanikiwa kuwafunga Yanga katika mchezo wetu wa Jumamosi, alisema mmoja wa wachezaji waliopo kwenye kambi ya timu hiyo ambaye akupenda jina lake litajwe gazetini. Alisema tangu kuanza kwa kambi ya timu hiyo mjini Zanzibar wiki iliyopita wachezaji wamekuwa katika mazoezi makali kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo.
Aidha, alisema wachezaji wenzake wapo kwenye morali kubwa na wanaamini wataibuka na pointi tatu katika mchezo huo wa ligi kuu Tanzania bara. Alipoulizwa msemaji wa timu hiyo, Cliford Ndimbo juu ya ahadi hiyo alisema hana uhakika na suala hilo kwa kuwa hajapewa taarifa rasmi na uongozi wa juu wa klabu hiyo.

Babu wa Miaka 112 aoa Binti wa Miaka 17

Babu mwenye umri wa miaka 112 wa nchini Somalia ambaye ana jumla ya watoto 18 amefunga ndoa na binti mwenye umri wa miaka 17 katika sherehe kubwa iliyohudhuriwa na mamia ya watu nchini Somalia. Mamia ya watu walifurika kwenye harusi ya babu mwenye umri wa miaka 112 wakati alipokuwa akifunga ndoa na mwanamke ambaye amemzidi jumla ya miaka 95.Ahmed Muhamed Dore ambaye tayari ana watoto 18 kutokana na wake zake watano alisema kuwa anahitaji watoto zaidi kutoka kwa mkewe mpya Safia Abdulleh, ambaye ana umri wa miaka 17."Leo Mwenyezi Mungu amenitimizia ndoto yangu", alisema Ahmed baada ya harusi iliyohudhuriwa na mamia ya watu kwenye mji wa Galguduud.Familia ya bi harusi ilisema kwamba binti yao ana furaha sana kuolewa na Ahmed.Ahmed alisema kuwa mke wake ambaye kwa umri wake ni sawa na umri wa kitukuu chake wa kike, wanatoka kijiji kimoja.Ahmed alidai kwamba alimsubiria kwa miaka mingi sana Safia afikie umri wa kuolewa ili atimize ndoto yake ya kumuoa."Sikumlazimisha aolewe na mimi, nilitumia ujuzi na uzoefu wangu wa kuwavutia wanawake ili anikubali nimuoe na hatimaye alikubali nimuoe", alijisifia Ahmed.Ndoa hiyo imeelezewa na wanahistoria wa Somalia kuwa haijawahi kutokea nchini humo watu wakafunga ndoa wakiwa na tofauti ya umri miaka 95, miaka mitano tu pungufu ya karne moja.

Kenya kufanya sensa ya mashoga

Serikali ya Kenya iko mbioni kufanya sensa ya kuwahesabu mashoga waliopo nchini humo katika jitihada zake za kuwaelimisha watu juu ya ugonjwa wa ukimwi.
Serikali ya Kenya inajiandaa kuwahesabu mashoga waliopo nchini humo ingawa kwa sheria za Kenya mashoga huadhibiwa kwenda jela miaka 14 wanapokamatwa.Nicholas Muraguri, mkuu wa taasisi ya kuzuia kuenea kwa ukimwi ya Nascop, akiongea na shirika la habari la BBC alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa serikali ya Kenya kufanya takwimu ya mashoga nchini humo.Alisema kuwa mashoga wengi hawana elimu kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi.Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanahofia kuwa mashoga wengi watahofia kujitokeza kuhesabiwa kwa kuhofia kukamatwa na kutupwa jela.Muraguri alisema kwamba takwimu hiyo itahusisha pia mashoga kutajana wenyewe kwa wenyewe huku maafisa wengine wakiwapima kama wameambukizwa virusi vya ukimwi pamoja na kuwafundisha njia salama za mapenzi."Wakenya hawawezi kusema kuwa mashoga ni jamii iliyotengwa, ni miongoni mwa jamii zetu", alisema Muraguri."Kundi hili inabidi lifikiwe na lipewe mafunzo ya jinsi ya kujilinda wasiambukizwe", alisema.Sensa hiyo ya mashoga imewagawanya Wakenya wengi huku baadhi yao wakisema hawaamini kama itasaidia chochote katika kuzuia kuenea kwa ukimwi.Baadhi ya mashoga waliohojiwa na BBC walitanabaisha kuwa wako tayari kuhesabiwa iwapo sensa hiyo itafanyika kwa siri.

Habari Njema Kwa Matasa

Wapenzi ambao hawana uwezo wa kupata mtoto kutokana na mmoja wao kuwa tasa, watapata nafasi ya kuwa na watoto kufuatia ugunduzi mpya wa wanasayansi ambapo mtoto atatengenezwa kwenye maabara kutokana na mbegu za kiume na mayai ya uzazi ya mwanamke vyote vya kutengeneza kwenye maabara. Wanasayansi nchini Marekani wako njiani kutengeneza watoto kwenye maabara baada ya kufanikiwa kutengeneza mayai ya uzazi ya mwanamke na mbegu za kiume kwenye maabara kwa kutumia mchanganyiko wa vitamini kwenye damu na kemikali mbalimbali.Mbegu za kiume na mayai ya uzazi ya mwanamke yatatengenezwa kwenye maabara bila kuhitajika kuwepo kwa mwanamke wala mwanaume.Ugunduzi huu umeshangiliwa sehemu nyingi duniani wakati ambao wanasayansi wako kwenye hatua za mwisho za kujaribu kutengeneza mtoto mwenye afya njema kutokana na mbegu za kiume na mayai ya kike vyote vya kutengeneza kwenye maabara.Ugunduzi huu utawapa nafasi watu ambao ni tasa na hawawezi kupata watoto au wale waliopoteza uwezo wa kupata mtoto kutokana na matibabu ya kansa, waweze kupata watoto kutokana na damu zao.Serikali ya Marekani ndiyo iliyodhamini utafiti huo uliofanyika kwenye chuo kikuu cha Stanford University ambapo wanasayansi walitumia mchanganyiko wa kemikali na vitamini kuweza kutengeneza seli ambazo baadae zitatumika kutengeneza mayai ya kike na mbegu za kiume.Wanasayansi hao walisema kuwa lengo kubwa lililopo hivi sasa ni kujaribu kujaribu kupata mtoto mwenye afya njema kwenye maabara.

Thursday, October 29, 2009

Awekwa chini ya Ulinzi kwa kuongopa kaibiwa mtoto

MWANAMKE anayejulikana kwa jina la Maua Ally (29) amejikuta anashikiliwa na polisi baada ya kupiga mayowe ya uongo akilalamika kuwa mtoto wake aliyemzaa katika Hospitali ya Temeke ameibwa na watu wasiofahamika. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Temeke, Liberatus Sabasi amesema, Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Nusura Simba (49), kuwa kuna mwanamke analalamika kuwa ameibiwa mtoto wake.Kamanda alisema kuwa kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo alidai kuwa, alifika katika hospitali hiyo akiwa anaumwa uchungu wa kujifungua na alipofika hapo alipokelewa na daktari kisha kupelekwa chumba cha kuzalisha [labour wodi], ambapo alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume.Mwanamke huyo alidai kuwa cha kushangaza baada ya kutoka chumba hicho hakumuona mtoto wake na ndipo alipoamua kutoa taarifa kwa uongozi wa hospitali hiyo.Baada ya jeshi la polisi kupokea taarifa hizo kutoka kwa uongozi wa hospitali hiyo, walifika hospitalini hapo na kumhoji mwanamke huyo chini ya ulinzi wa polisi na katika kumuoji kwa kutumia mbinu za kipolisi mwanamke huyo alikiri hakujifungua wala hakuwahi kuwa mjamzito na alifika hospitalini hapo kwa kuwa alikuwa na shida ya mtoto.Alidai kuwa aliamua kufanya hivyo na kutoa taarifa za uongo kwa sababu mume wake amekuwa akimshinikiza kubeba mamba na kutaka mtoto kwa muda mrefu na alimuongopea mume wake huyo alikuwa mjamzito.Ndipo alipoamua kufanya mbinu hiyo ili mume wake huyo ajue ni kweli alijifungua na mtoto wake aliibiwa na manesi na kuomba samahani kwa mapolisi hao na kwa uongozi wa hospitali hiyo kwa kitendo alichokifanya cha kudanganya.Kamanda Sabasi amesema kutokana na taarifa hizo, uchunguzi wa kitaalamu ulifanyika dhidi ya mwanamke huyo na walibaini kuwa mwanamke huyo hakujifungua na hakuwa na dalili hata ya kuwa na mimba. Kamanda Sabasi amesema kuwa, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika kujibu shtaka hilo kwa kuuongopea umma.

Mechi ya Simba na Yanga Viingilio hivi hapa

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambapo kiingilio cha chini kitakuwa shilingi 5000 na kile cha juu kikiwa shilingi 60,000.
Mchezo huo unaosubiriwa na mashabiki wengi unatarajia kufanyika Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mwamuzi wa pambano hilo atakuwa Oden Mbaga.Katibu mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kuondoa msongamano siku ya pambano hilo na kusema siku hiyo tiketi hazitauzwa.Kuhus mpangilio wa viti, Mwakalebela alisema viti vya kijani mzunguko, kiingilio kitakuwa 5,000,viti vya kijani mzunguko 7,000, orange 10,000, orange VIP 20,000, VIP C, 30,000, VIP B 50,000 na VIP A 60,000.Mbali na viingilio hivyo, Mwakalebela aliwataka mashabiki wa timu hizo kuwa watulivu wakati wa mchezo huo na kuondoa dhana potofu ya ushirikina pamoja na kuwataka kuwa makini kila wanaponunua tiketi ili kukwepa udanganyifu na tiketi feki.Nao makatibu wa klabu hizo, Mwina Kaduguda wa Simba na Lawrence Mwalusako wameeleza wao hawana la kusema kuhusiana na matokeo ya mchezo huo, hivyo kuwaachia makocha wao pamoja na manahodha wa timu hizo kwani wao ndio wanao uwezo wa kuelezea jinsi walivyojipanga.Alisema ili kuondoa msongamano siku ya pambano tiketi hazitauzwa, hivyo kuwataka mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kununua tiketi hizo mapema ili kuondoa vurugu."Tunawashauri mashabiki wanunue tiketi zao mapema kwani siku ya mchezo hatutaruhusu tiketi kuuzwa kwani chanzo cha vurugu ni ucheleweshaji wa tiketi na hivyo ili kukwepa matatizo kama hayo, leo tutaanza kuuza tiketi mpaka Ijumaa jioni ,"alisema Mwakalebela.

Odhiambo na Maftah ruska kuivaa Simba

MWENYEKITI wa kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kamishna wa Polisi Mstaafu, Alfred Tibaigana amewatoa kifungoni wachezaji Amir Maftah na Moses Odhiambo wa Yanga, na kutangaza kuwa wako huru kuichezea timu yao dhidi ya Simba.
Tibaigana alisema wachezaji hao wamefutiwa kifungo cha kukosa mechi tatu na faini ya shilingi 500,000 baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ya TFF kuketi Jumatatu ya wiki hii.Kushindwa kuwasilishwa kwa aina ya matusi waliyotukanwa na wachezaji hao ni moja ya sababu za kuachiwa huru na kufutiwa faini ambayo ilitakiwa kulipwa na wachezaji hao.Mwenyekiti wa kamati hiyo Kamishna wa Polisi Mstaafu, Alfred Tibaigana alisema kamati yake imeshindwa kugundua kosa na kutoa maamuzi ya kuwapa uhuru wachezaji hao kwa kushindwa kugundua sababu halisi ya makosa waliyoshitakiwa.''Hukumu inaonyesha kuwa wachezaji hao walimtukana msaidizi wa mwamuzi wa kwanza mara baada ya mpira kumalizika na taarifa hizo zikaandikwa kwa taarifa ya kamisaa,''alisema Tibaigana.''Hukumu ambayo bado haina uhakika kwa kuwa walishindwa kuandika aina ya matusi ambayo yalitukanwa na wachezaji hao, na sisi kama kamati hukumu za namna hiyo huwa tunazihukumu kwa kumpa haki mshatakiwa kwa kuwa zinakuwa za shaka kwa kutokamilika.''Itakuwa bora yanapotokea matatizo kama hayo , basi waamuzi wanapoandika ripoti zao wanatakiwa kuandika aina ya matusi ambayo wanatukanwa kwa kuwa wao ni binadamu na tukio kama hilo halikuwa na ushahidi,'' alisema Tibaigana.Alisema wao kama kamati ya mashindano wamewaachia huru wachezaji hao tangu kufanyika kwa kikao hicho kilipokutana na kubaini kushindwa kwa waamuzi na kamisaa kuweka bayana matusi kutambua makosa kazi ambayo wamewaachia TFF kama itakatwa rufaa nyingine.Kutokana na uamuzi huo, Maftah na Odhiambo waliotiwa hatiani na kupewa adhabu na faini hiyo wakidaiwa kumtukana mwamuzi siku ya mchezo baina ya Yanga na Azam FC mchezo uliomaliza kwa suluhu ya bao 1-1, wameondolewa kifungoni.Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo kutolewa msemaji wa Yanga, Louis Sendeu alisema, ''Kwa sasa tunasubiri siku tu kwani kikosi kazi kimekamilika kuona tunashinda mchezo huo.''

Wednesday, October 28, 2009

Mwakyembe agoma kuhojiwa na Takukuru

Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amegoma kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa (Takukuru) kwa madai kuwa, hatua hiyo ina lengo la kuwatisha na kuwafumba midomo wabunge. Pia, Dk Mwakyembe amesema Takukuru haikupaswa kuwahoji wabunge katika kipindi hiki ambacho Bunge linasubiri taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio 23 ya Richmond, likiwemo kumchukulia Mkurugenzi Mkuu wake, Dk. Edward Hoseah, ambaye anadaiwa kuisafisha kampuni hiyo ya kitapeli. Dk. Mwakyembe alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana kuhusu taarifa zilizochapishwa na gazeti moja la kila siku (si Nipashe), likielezea kuhusu kuhojiwa kwake na Takukuru. “Takukuru walinipigia simu niende kuhojiwa nikakataa kwa sababu mazingira yaliyopo yanaonyesha wanataka kuwanyamazisha wabunge, hiyo ni kinyume cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge,” alisema Dk. Mwakyembe, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Teule ya Bunge kuchunguza mchakato wa utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura wa megawati 100 kwa kampuni ya Richmond. Dk. Mwakyembe ambaye pia ni mwanasheria aliyebobea, alisema kitendo cha kukataa kuhojiwa na Takukuru hakipaswi kutafsiriwa kwamba ni kuhamaki kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo, bali ni ujasiri unakidhi matakwa ya kisheria, kanuni na taratibu.
“Bunge linapokuwa kwenye mchakato wa kutaka Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru achukuliwe hatua, kisha taasisi hiyo ikaanza kuwahoji wabunge wanaosubiri utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa, ni kinyume cha utawala wa sheria,” alisema. Kwa mujibu wa Mwakyembe, watendaji wa Takukuru walianza kuwahoji wabunge mbalimbali katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja, wakitaka taarifa kuhusu madai ya wabunge kupewa posho wanapotembelea taasisi za umma, licha ya kulipwa stahiki zao na ofisi ya Bunge. Dk. Mwakyembe alisema hatua iliyochukuliwa na Takukuru kuwahoji wabunge, inatia mashaka hasa kwa vile taasisi hiyo imewahi kuwalipa posho wabunge mara kadhaa. Kwa upande mwingine, Dk. Mwakyembe alisema watuhumiwa wa ufisadi wanatumia baadhi ya vyombo vya habari (akivitaja jina) kuwachafulia majina wananchi wanaotetea maslahi mapana ya umma. “Si jambo la ajabu nilivyoandikwa na gazeti la (analitaja jina), hili linamilikiwa na mafisadi, linatetea maslahi ya mafisadi kiasi cha kupoteza mvuto wake kwa wasomaji,” alisema mbunge huyo machachari.
Suala la kuhojiwa kwa wabunge kuhusiana na posho wanazodaiwa kuchua mara mbili, kwenye Bunge na kwa taasisi wanakofanya kazi, linaelezwa kuwa ni juhudi za kutaka kupunguza makali ya wabunge. Jana baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao, walisema wanaona mbinu hizi kama mapambano ya kitaasisi. Takukuru mwishoni mwa wiki walitoa taarifa kwa vyombo vya habari wakisema wabunge kama walivyo wananchi wengine wanawajibika kuitikia mwito wao wa kuhojiwa katika masuala mbalimbali yanaohusiana na rushwa.

Waaga Dunia wakijaribu kumuokoa mwenzao


WATU wawili: Pili Daud (29) na Amina Masud (44) wakazi wa Kawe Ukwamani, jijini Dar es Salaam, wamefariki dunia wakati wa harakati za kumuokoa Mariam Mwinyimvua (65) aliyekuwa amenaswa na umeme. Mariamu bado ni majeruhi huku wale waliotaka kumuokoa wakiwa wameaga dunia! Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya asubuhi, katika eneo hilo wakati Mariam Mwinyimvua (65) alipokuwa akitaka kuanika nguo katika kamba. Kwa mujibu wa Kamanda Kalunguyeye, kifo cha watu hao kilitokea baada ya Mariam Mwinyimvua kufua nguo zake na kuzianika kwenye waya wa umeme na kusababisha kunaswa ghafla. Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya Mariam kunaswa ndipo Pili Daud alitokea kwa lengo la kumuokoa katika ajali hiyo na kwamba wakati akiwa kwenye harakati hizo naye alinaswa na umeme na kufariki papo hapo. Alisema baadaye alitokea Amina Masoud kwa lengo la kutoa msaada kwa wote wawili naye alinaswa pia na kufa papo hapo! “Walikufa wote wawili wakiwa katika harakati za kumuokoa ndugu yao aliyenaswa wakati akianika nguo,” alisema Kalunguyeye. Baada ya kutokea hali hiyo, Jeshi la Polisi, kwa kusaidiana na majirani, lilifanikiwa kumpa huduma ya kwanza Mwinyimvua na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Mwananyamala. Halikadhalika maiti za Pili na Amina zilipelekwa hospitalini hapo. Tanzania Daima Jumatano, ilipowasiliana na Kamanda Kalunguyeye baadaye kwa njia ya simu, alisema kuwa hali ya majeruhi huyo ni mbaya na wamemhamishia katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Wazungu wezi kutoka ATM machine wapigwa kalenda

NEDKO Stanchen (34) na mkewe Stella Nedelcheva (28) raia wa nchini Bulgaria walioiba fedha zaidi ya shilingi Mil 70 kutoka kwenye mashine ya ATM ya Benki ya Baclays kesi yao imepigwa kalenda na kuahirishwa kwakuwa upelelezi wa shauri hilo kudaiwa kuw
Watuhumiwa hao walifikishwa leo mbele ya Hakimu Mkazi, Bingi Mashabara ambaye ameahirisha kesi hiyo kwa sababu hiyo na kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza shauri hilo. Kesi hiyo ilikuja mahakamani hapo leo kwa ajili ya kutajwa.Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai mwaka huu waliiba katika mashine za kutolea fedha za ATM sh.milioni 14.5 mali ya Baclays.Kesi hiyo itakuja tena mahakamani hapo, Novemba 2, mwaka huu.

Tuesday, October 27, 2009

Historia kuibeba simba Jumamosi

SIMBA inayojiandaa kuikabili Yanga mwisho wa wiki katika mchezo mgumu wa Ligi Kuu ya Vodacom imeweka rekodi ya kushinda mechi tisa kati ya tisa katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku, Ikilinganishwa na watani zao, Yanga, wao bado hali si nzuri tofauti na misimu miwili iliyopita ambayo walitwaa ubingwa wakiwa chini ya mtaalam Dusan Kondic aliyeondoka.Timu hizo zinakutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba inashikilia usukani wa ligi kwa pointi 27 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 18 sawa na Mtibwa Sugar , lakini zikiwa na tofauti ya mabao na Azam ya nne.Vijana hao wa Mzambia Patrick Phiri watajitangazia ubingwa wao wa majira ya joto na kujiweka kwenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu kama watapata ushindi kwenye mechi mbili za mwisho dhidi ya wapinzani wake kwenye kinyang'anyiro cha taji hilo, Yanga na Mtibwa Sugar.Mabingwa watetezi, Yanga pamoja na ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Moro United mwishoni mwa wiki bado wanajua kuwa wanahitaji ushindi kwenye mechi yake ijayo ili kurudisha matumaini yake kwa kufikisha pointi 24 wakati Simba wao watamaliza ligi hiyo kwa kushinda mechi zao mbili zilizosalia watakuwa na pointi 33.Endapo wataishinda Yanga na baadaye Mtibwa, Wekundu wa Msimbazi watakuwa wamezidi kuwawashia indiketa wapinzani hao ambao itabidi wafanye kazi ya ziada kuwashusha kileleni kwenye mzunguko wa pili wa ligi utakaoanza Januari mwakani.Kwa upande wao, Yanga ambayo walianza kwa kusuasua, tayari imecheza mechi tisa imeshinda tano, imetoka sare tatu na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Majimaji ya Songea bado wanacho kibarua kigumu cha kubaki nafasi ya pili kutokana na upinzani mkali kutoka kwa Azam na Mtibwa Sugar.Azam inayofundishwa na Mbrazili Amourin Itamaar wameonekana kuwa na kasi kubwa ya kuwania nafasi mbili za juu huku mshambuliaji wao, John Boko , maarufu Adebayor akishikilia rekodi ya kufunga mabao manane katika mechi tisa za msimu huu.Vijana wa Manungu, Mtibwa Sugar pamoja na kuwapoteza nyota wake kadhaa msimu huu, Salum Sued, Uhuru Seleman, Zahoro Pazi, waliohamia klabu nyingine bado wameendelea kuonyesha kiwango cha juu na sasa wanashikilia nafasi ya tatu sambasamba na Yanga wakitofautiana kwa mabao ya kushinda.Wakati mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo unaeleka mwishoni Novemba 11, vita nyingine ipo kwa timu za mkiani zinazosaka kujinasua, ambazo ni Prisons ya Mbeya, African Lyon na Toto Africa ya Mwanza na JKT Ruvu (Pwani), zote zipo kwenye hati hati ya kushuka daraja iwapo hazitabadilika mwenendo wao kwenye mzunguko wa pili wa ligi hiyo, kati ya hizo zitajikuta ligi daraja la kwanza.Prisons ambayo ni ya 10 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi nane tayari imecheza michezo tisa, ikifuatiwa na Lyon yenye pointi saba huku Toto inashika mkia kwa pointi nne, kabla ya mechi ya jana.

Mshtakiwa wa Kesi ya EPA hoi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilishindwa kusikiliza kesi ya wizi wa Sh 3.8 bilioni inayomkabili Farijala Hussein na wenzake baada ya mshtakiwa huyo kushindwa kusimama kizimbani kutokana na kusumbuliwa na tatizo la figo. Kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikilizwa mfululizo jana kwa mashahidi wa upande wa mashtaka, lakini Farijala ambaye alikuwepo mahakamani hapo alionekana amevimba uso na tumbo na hivyo kushindwa kusimama kizimbani. Wakili anayemtetea mshtakiwa huyo, Majura Magafu aliomba mahakama iahirishe kesi hiyo baada ya kudai kuwa mteja wake hataweza kukaa kizimbani kusikiliza kesi kutokana na kuumwa. Hata hivyo, wakili wa serikali, Frederick Manyanda alipinga hoja hizo na kudai kuwa si za msingi kwani upande wa utetezi ulipaswa kuithibitishia mahakama kwa kuonyesha vyeti.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, kiongozi wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo, Samuel Karua aliahirisha kesi hiyo hadi leo ili kuangalia hali ya mshtakiwa huyo. Katika hatua nyingine, mshtakiwa wa pili, Rajabu Maranda jana aliwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka aruhusiwe kusafiri nje ya Dar es Salaam ili aende kwenye shughuli za kisiasa. Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Ajay Somani, Imani Mwakosya, Esther Komu na Sophia Kalika. Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa waliiba zaidi ya Sh3 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu (BoT) baada ya kudanganya kuwa kampuni ya Mibare Farm imepewa deni na kampuni ya Textile Mills Ltd ya nchini India. Wakati huohuo, mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jana iliridhia maombi ya mfanyabiashara Jayant Kumar, maarufu kama Jeetu Patel, anayekabiliwa na kesi ya wizi wa Sh3.3 bilioni ya kutaka kesi hiyo isitishwe mahakamani hapo ili jalada liende Mahakama Kuu kwenye kesi aliyoifungua ya kikatiba. Akitoa uamuzi huo huku akinukuu kesi mbalimbali na vifungu vingine vya sheria, Hakimu Mkuu Mkazi Richard Kabate alisema upande wa mashtaka umeshindwa kutoa tafsiri sahihi kuhusu mwenendo wa kesi. Awali upande wa mashtaka ulipinga jalada hilo kupelekwa Mahakama Kuu baada ya kudai kwamba hoja za upande wa utetezi hazina msingi wowote kwani maneno yanayolalamikiwa ni ya mitaani na wala hayajaathiri mwenendo wa kesi hiyo.
Hakimu Kabate alisema kwa mujibu wa sheria Mahakama ya Kisutu haina uwezo wa kuyatolea maamuzi malalamiko yaliyotolewa na Jeetu. Katika malalamiko yake Jeetu anadai kuwa mwenendo wa kesi yao umeingiliwa kutokana na matamshi aliyoyatoa mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reginald Mengi kwamba wao ni mafisadi papa. Alidai kuwa katika matamshi hayo ambayo yalitolewa kupitia kipindi maalumu kilichorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, Mengi aliingilia uhuru wa mahakama kwa kuwahukumu wakati kesi yao bado inaendelea mahakamani.
Alidai kuwa kutokana na matamshi hayo jamii iliwaona wao wana hatia dhidi ya tuhuma zinazowakabili. Tayari mahakama ya Kisutu imeridhia kusitishwa kwa kesi nyingine mbili zinazomkabili Jeetu na wenzake ili majalada ya kesi hizo yapelekwe Mahakama Kuu kwenye kesi ya kikatiba aliyoifungua. Kesi hiyo itatajwa Novemba 6 mwaka huu. Jeetu, Devendra Patel na Amit Nandy wanadaiwa kuiibia BoT Sh 3.3 bilioni baada ya kudanganya kuwa kampuni yao ya Navy Cut Tobacco (T) Ltd imepewa deni hilo na kampuni ya Matsishuta ya nchini Japan.

ADHT karibuni nyumbani karibuni Tanzania

Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe ulio mithili ya mnyororo kuzindua rasmi kongamano la tano la Watu Wenye Asili ya Afrika Ulimwenguni (African Diaspora Heritage Trail(ADHT), jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni waziri wa Maliasili na Utalii Shamsa Mwangunga, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dk Gaynelle Henderson, Mkurugenzi wa mikutano na ushirikiano wa tasisisi hiyo. Jacob Henderson.

Baunsa mdogo kuliko wote duniani huyu hapa

Pamoja na kuwa na umri wa miaka mitano, mtoto Giuliano Stroe ndiye mtoto mwenye nguvu kuliko watoto wote duniani na kutokana na mazoezi makali anayofanya tumbo lake limekatika miraba sita. Mtoto Giuliano Stroe alianza kubeba vyuma, kupiga pushapu na kufanya mazoezi makali tangia alipokuwa na umri wa miaka miwili.Giuliano anaishi na wazazi wake ambao wote ni raia wa Romania katika mji mmoja nchini Italia.Giuliano aliingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia mwaka huu baada ya kufanya shoo ya maguvu yake iliyowaacha watu wengi midomo wazi.Shoo hiyo ilirushwa Live na televisheni za nchini Italia.Baba yake Giuliano, Iulian Stroe, 33, alisema kwamba alianza kwenda naye gym tangia alipokuwa mdogo sana. Giuliano alianza kubeba vyuma vya uzito mdogo wakati huo.

Monday, October 26, 2009

Kitu gani chamrudisha IRENE UWOYA ?

Hatimaye Mrembo huyu inasemakana yupo jijini ikiwa ni miezi mitatu tu tangu alipofunga ndoa na mcheza soka wa kimataifa wa Rwanda anayejulikana kwa jina la Kataut , anayeishi ndani ya jiji la Nicosia, Cyprus ambako anacheza soka la kulipwa kwenye Klabu ya AEL Limassol., inasemekana Kataut alisaini mkataba wa miaka mitatu na Limassol Julai 18, mwaka huu, hata hivyo kutokana na mkataba huo inaonyesha ana muda mrefu wa kuishi katika kisiwa hicho cha Cyprus ambacho ni cha tatu kwa ukubwa kwenye Bahari ya Mediterranean.

Wanaume wawili wa kikenya waoana huko LondonHarusi iliyofungwa hivi karibuni jijini London, Uingereza, kati ya wanaume wawili, raia wa Kenya, Daniel Chege Gichia (mwenye umri wa miaka 39) na Charles Ngengi (40), kama wanavyoonekana pichani imezua gumzo kubwa miongoni mwa wananchi nchini Kenya

Mgombea wa CCM afariki dunia akisubiri kutangazwa mshindi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo, kimepata pigo baada ya mwanachama wake aliyepita bila kupingwa katika nafasi ya Mwenyekiti, Ashery Kigava wa Kitongoji cha Amani katika Kijiji cha Lukani, kufariki dunia wakati akisubiri kutangazwa kuwa mshindi.
Akitoa taarifa ya kifo hicho, mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Profesa Peter Msolla wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lukani, Diwani wa Kata ya Ukumbi, Chesco Ngimba alisema kifo cha mwenyekiti huyo mteule kilitokea juzi. Kwa upande wake, Profesa Msolla mbali ya kutoa rambirambi kwa wafiwa, alisema CCM imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha kiongozi huyo mratajiwa na kuongeza kuwa, ni pingo ndani ya chama na kitongoji hicho.

Wanachama wa DECI Arusha wafungua kesi ya Madai

WANACHAMA 300 wa Kampuni ya Development Entrepreneurship Community Initiative (DECI) mkoani Arusha, wamefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kudai fidia ya sh bilioni 2. Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kutajwa rasmi leo mahakamani hapo kwa mahakama kupanga rasmi tarehe ya kuanza kusikilizwa. Wanachama hao wanaowakilisha wenzao 4,700 katika kesi hiyo, wanataka viongozi wakuu wa kampuni hiyo kuwalipa fedha zao walizopanda na riba baada ya kuvunja mkataba baina yao. Akizungumza kwa niaba ya wananchama wenzake, msemaji wa wana DECI hao, Leonard Kilasi, alisema wameamua kufungua kesi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa viongozi wa kampuni hiyo hawana mpango wa kurejesha fedha zao. “Mpaka sasa hatufahamu hatma ya fedha zetu, hivyo tumeamua kufungua kesi ili mahakama iweze kutenda haki na sisi tupate fedha zetu tulizopanda kabla ya kampuni hiyo kufutwa,” alisema Kilasi. Aidha, Kilasi alisema wadaiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni wakurugenzi wa DECI makao makuu, na mwakilishi wao mkoani hapa, Salome Ilungu. Hata hivyo, wakati wana DECI hao wakikusudia kufungua kesi, tayari wakurugenzi wa taasisi hiyo inayojishughulisha na kazi ya kupanda na kuvuna pesa, wameshafunguliwa kesi na serikali wakidaiwa kuendesha mchezo huo wa upatu kinyume cha sheria.

Mapacha walioungana wakataa kutenganishwa

Mapacha wa nchini India walioungana kuanzia kiunoni wenye miguu mitatu ambao wamejipatia umaarufu duniani kwa kucheza sarakasi kiasi cha kufananishwa na Buibui wamekataa ushauri wa daktari wa Marekani anayetaka kuwatenganisha ili kila mmoja ajitegemee.
Mapacha wa nchini India, Ganga na Jamuna Mondal wenye umri wa miaka 39 maarufu duniani kama "Spider Sisters" wameungana katika namna ambayo ni nadra sana kutokea duniani kwani wameungana kuanzia kiunoni lakini kila mmoja ana mguu wake mmoja huku miguu yao ya pili imeungana pamoja na kufanya mguu mmoja wa tatu wenye vidole tisa.Awali madaktari walionya kuwa kujaribu kuwatenganisha kutahatarisha maisha yao lakini daktari mtaalamu wa mapacha walioungana wa nchini Marekani, Dr James Stein aliwafanyia uchunguzi mapacha hao na amedai kuwa mapacha hao wanaweza kutenganishwa bila kuhatarisha maisha yao.Lakini mapacha hao wamekataa kutenganishwa na kusema "Tutaishi kama jinsi ambavyo Mungu ametuumba".Kila pacha mmoja ana kichwa chake na mikono yake miwili.

Je tutafika? Malawi Yajiandaa Kuhalalisha Uhakaba

Serikali ya Malawi inajiandaa kupitisha sheria itakayohalalisha biashara ya ukahaba nchini humo kwa kuwaruhusu makahaba wafanye ukahaba kwenye majumba yao badala ya kusimama barabarani. hatua hiyo ya serikali ya Malawi inakusudia kuwalinda wanawake wanaojiuza barabarani kutokana na manyanyaso wanayopata kutoka kwa wateja wao.Waziri wa masuala ya jamii na maendeleo wa Malawi, bi Patricia Kaliati akiongea na shirika la habari la Reuters alisema kwamba muswada wa kuruhusu biashara ya ukahaba majumbani nchini humo uko kwenye hatua za mwisho kupelekwa bungeni ili upitishwe uwe sheria."Tunataka watoke mitaani wakafurahie tendo la ngono kwenye majumba yao na hivyo kuepukana na kunyanyaswa kijinsia au kubakwa na wateja wao na hivyo kuwalinda na gonjwa la ukimwi", alisema Kaliati.Ugonjwa wa ukimwi nchini Malawi yenye idadi ya watu milioni 13 umeishaua zaidi ya watu laki nane tangia ulipoingia nchini humo mwaka 1985.Jitihada za kuwaelimisha watu kujikinga na ugonjwa huo zimesaidia kupunguza idadi ya waathirika toka asilimia 14 hadi 13. Madawa mengi yanayotolewa bure kwa waathirika yamesaidia kupunguza idadi ya vifo vya waathirika kwa asilimia 70.Hata hivyo muswada huo wa kuhalalisha ukahaba tayari umeishakumbwa na upinzani toka taasisi mbali mbali.

Hatimaye Mtoto amzaa mtoto mwenzie

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 wa nchini Bulgaria ambaye jina lake liliwekwa kapuni amepata mtoto mwenzie baada ya kujifungua salama mtoto wa kike usiku wa siku ya alhamisi kwenye hospitali moja iliyopo kwenye mji wa kusini mashariki mwa Bulgaria wa Sliven.Taarifa za kujifungua kwa mtoto huyo zimethibitishwa na mganga mkuu wa wadi ya wazazi katika hospitali ya Sliven Hospital, Dr. Sonya Mihaylova, ambaye alisema awali katika hospitali hiyo hiyo mtoto mwingine mwenye umri wa miaka 12 aliwahi kujifungua mtoto.Mama huyo mtoto mwenye umri wa miaka 11 alijifungua mtoto mwenye afya njema mwenye uzito wa kilo 2.5.Alijifungua mtoto huyo baada ya kupewa mimba na kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake nalo halikutajwa.Wazazi wa binti huyo wako wanaishi nchini Hispania na binti huyo alikuwa akilelewa na mama wa kijana aliyempa ujauzito huo.Binti huyo aliingia leba saa tatu na nusu usiku na alijifungua ndani ya lisaa lisaa limoja na hapo hapo alitaka kuondoka kurudi nyumbani kwake kwakuwa harusi yake na baba wa mtoto wake ilikuwa ikifanyika usiku huo huo."Baada ya kujifungua tu alitaka kuondoka kwakuwa harusi yake ilikuwa usiku huo huo", alisema Dr. Mihaylova.“Kulikuwa hakuna ndugu yoyote toka familia yake na hakuna mtu yoyote ambaye tungeweza kumshauri chochote, wazazi wake wako Hispania na hakuna mtu anayeweza kumualia jambo zaidi ya kujiamulia mwenyewe anavyotaka", alisema Dr. Mihaylova.Dr. Mihaylova alikataa kumruhusu binti huyo aondoke mpaka atakapohakikisha binti huyo na mtoto wake wote wapo kwenye afya njema.Taarifa zaidi zilisema kwamba hospitali hiyo imetoa taarifa ya tukio hilo kwa taasisi ya kutetea haki za watoto.Waendesha mashtaka walisema wanalifanyia uchunguzi suala hilo kabla ya kutoa uamuzi kwani kufanya mapenzi na watoto wenye umri mdogo ni kosa la jinai nchini humo.

Mtoto Shiloh Pepin maarufu kama 'Nguva Mtoto' Afariki Dunia

Mtoto Shiloh Pepin ambaye alikuwa maarufu duniani akijulikana kama NGUVA MTOTO baada ya kuzaliwa miguu yake ikiwa imeungana pamoja kama nguva huku akiwa hana sehemu za siri amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 10.
Alipozaliwa katika hali hiyo madaktari walidai atafariki ndani ya siku chache lakini ameweza kuishi miaka 10 duniani.Shiloh Pepin maarufu kama "Nguva Mtoto" alizaliwa miguu yake ikiwa imeunganika na kukusanyika sehemu moja kuanzia kiunoni mpaka chini kama nguva alivyo.Madaktari hawakuweza kuitenganisha miguu yake kutokana na kwamba ilikuwa imekusanyika pamoja na kuzungukwa na mishipa mikubwa ya damu hivyo kujaribu kuitenganisha miguu hiyo kungehatarisha maisha yake.Shiloh alizaliwa akiwa na ugonjwa unaoitwa "mermaid syndrome" ambao pia unajulikana kama "sirenomelia" na kutokana na maelezo ya madaktari hakuna aliyetegemea angeishi miaka 10.Shiloh Pepin "Nguva Mtoto" alizaliwa katika mji wa Kennebunkport, Maine nchini Marekani mwezi wa nane mwaka 1999.Alizaliwa akiwa hana utumbo mdogo, tumbo la uzazi wala uke na alikuwa na figo moja tu na ovari moja tu. Miguu yake iliungana pamoja kuanzia kiunoni mpaka chini.Shiloh alikuwa maarufu duniani kupitia televisheni mbali mbali duniani zilizofanya mahojiano naye, video zake nyingi zipo kwenye mitandao duniani.Shiloh alitokea kupendwa na watu wengi sana na aliwapa changamoto watu wengi kwa kuendelea na maisha yake kwa furaha kama walivyo watoto wengine ingawa alikuwa hawezi hakutembea akitembea kwa kujiburuza chini.Shiloh aliwahishwa hospitali mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kusumbuliwa na mafua na baadae kugundulika ana pneumonia.Shiloh alilazwa hospitali kuanzia oktoba 10 mwaka huu akipewa dripu za antibiotics na akipumua kwa kutumia mashine.

Wachapwa Bakora Kwa Kuangalia Video za Ngono Kwenye Simu

Wanaume wawili wa nchini Somalia wamecharazwa bakora 25 mbele ya kadamnasi ya watu na kisha kutupwa jela siku 15 baada ya kukamatwa wakiangalia video za ngono kwa kutumia simu zao za mkononi.Maafisa wa ulinzi wa kundi la Al shabab waliwafumania vijana hao wakiangalia video za ngono kwa kutumia simu zao siku ya ijumaa na walicharazwa bakora hizo siku ya jumamosi katika mji wa kusini mwa Somalia wa Kismayo unaotawaliwa na Al shabab."Vijana hawa wawili walikamatwa wakiangalia video za ngono kwa kutumia simu zao na baada ya kukiri makosa yao wameadhibiwa kwa mujibu wa haria za kiislamu", alisema Sheikh Omar Mohamed, afisa wa mambo ya dini wa Al shabab alipokuwa akiongea na shirika la habari la AFP."Kila mmoja wao alichapwa bakora 25 na atatumikia siku 15 jela kwa vitendo vyao viovu walivyovifanya", aliongeza Sheikh ohamed.Wakazi wa eneo hilo walithibitisha kucharazwa bakora kwa vijana hao.Kundi la Al shabab linatumia sharia za kiislamu katika maeneo wanayoyatawala. Wezi hukatwa mikono au miguu kulingana na kosa lenyewe na wazinzi hucharazwa bakora.

Je haki imetendeka? Ahukumiwa kifungo cha miezi 8 kwa kosa la Mauaji na kuachiwa huku baada ya kutumikia miezi 3

Mlowezi wa kizungu aliyemuua kwa kumpiga risasi raia wa Kenya aliyeingia kwenye shamba lake na baadae kutupwa jela miezi minane ameachiliwa huru kabla ya kumaliza kifungo chake baada ya kuonyesha tabia nzuri.
Mlowezi Tom Cholmondeley alihukumiwa kwenda jela miezi minane baada ya kesi yake ya mauaji kubadilishwa kuwa kesi ya kuua bila kukusudia.Mlowezi huyo tajiri alimuua kwa kumpiga risasi raia wa Kenya, Robert Njoya aliyeingia kwenye shamba lake lililopo kwenye mkoa wa Rift Valley ili kuwinda wanyama pori.Mlowezi huyo aliachiwa huru ijumaa kabla ya hata ya miezi minane aliyohukumiwa kuisha kwa kile kilichoelezwa kuwa alionyesha tabia nzuri.Wakati alipokuhumiwa kutumikia kifungo cha miezi minane jela mwezi wa tano mwaka huu, mlowezi huyo alikuwa ameishakaa jela miaka mitatu akisubiria hukumu yake.Jaji wa mahakama kuu ya Kenya, Muga Apondi ndiye aliyetoa hukumu hiyo ya miezi minane jela na kusababisha hasira za wananchi mbali mbali wa Kenya waliokuwa wakilalamika kuwa sheria imepindishwa ili kuwabeba matajiri.Jaji Apondi akiielezea hukumu aliyoitoa alisema kuwa mlowezi huyo hakuua kwa kukusudia kwani baada ya kumpiga risasi Robert Njoya, alijaribu kutoa huduma ya kwanza na alimpeleka hospitali.Mwaka mmoja kabla ya kumuua Robert Njoya mlowezi huyo huyo alimuua raia mwingine wa Kenya lakini kesi yake ilifutwa katika hali ya utatanishi.

Ashikiliwa kwa kumlawiti binti yake

MWANAUME mmoja aitwae Daniel Makundi (40) anashikiliwa na Polisi mkoani Tanga kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Simon Sirro, alisema tukio hilo lilitokea juzi, majira ya 7 za usiku katika Kata ya Nguvumali mkoani humo.Kamanda huyo alisema kuwa mtoto huyo alipohojiwa na jeshi hilo alieleza kuwa ni mara kwa mara mzazi wake huyo alikuwa anamfanyia kitendo hicho.Na kusema hiyo ni mara yake ya sita kufanyiwa kitendo hicho na ndipo ilipogundulika.Kamanda huyo amesema kuwa katika uchunguzi uliofanyika na madaktari ilibainiuka kuwa mtoto huyo alishawahi kufanyiwa kitendo hicho kabla ya hapo.Hivyo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mwanzoni mwa wiki ijayo ili kujibu shtaka linalomkabili.

Thursday, October 22, 2009

Mbwa huyu amponza Boss wake

Mwanamke mmoja mkware wa nchini Italia amefumaniwa akila uroda na mmiliki wa baa baada ya mumewe kumuona mbwa wake akiwa amefungwa nje ya eneo la tukio. Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake mwenye umri wa miaka 35 alimuaga mumewe kuwa anaenda nje kumtembeza mbwa wake na atakutana na rafiki zake kwenye kibanda cha kahawa na atarudi nyumbani baada ya masaa machache.Mumewe mwenye umri wa miaka 40 na yeye pia aliamua kuwatembeza nje watoto wao wawili wadogo na ndipo aliposhangaa kumuona mbwa wa mkewe akiwa amefungwa kwenye nguzo ya taa ya barabarani pembeni ya baa moja katika mji wao.Mbwa huyo kwa furaha alibweka na kuruka ruka alipomuona mume wa mwanamke huyo.Mume huyo aliamua kuingia kwenye baa hiyo kumsaka mkewe na ndipo alipomfumania mkewe akila uroda na mmiliki wa baa hiyo.Katika tukio hilo lililotokea kwenye mji wa Caltanissetta, Sicily, mwanaume huyo aliingia kwenye mzozo mkubwa sana na mkewe kabla ya kumshushia kipigo cha nguvu mwanaume aliyekuwa akimla uroda mkewe.Polisi waliitwa kuamua ugomvi huo na mmiliki wa baa hiyo alipelekwa hospitali akiwa ameharibiwa sura yake kwa mkong'oto aliopewa.Polisi walisema kwamba hakuna hatua yoyote waliyoichukua dhidi ya mwanaume aliyempiga mmiliki wa baa hiyo kwa kumchukulia mkewe. Hadi tunaingia Mitamboni inasemekena Mume huyo ameamua kuwasiliana na wanasheria wake na ameamua kumuacha mke huyo mkware.

Mauaji ya Albino yanaendelea- Mtoto albino auwawa kwa kukatwa shingo

MWANAFUNZI wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Nyawilimilwa, wilayani Geita, Mwanzamwenye ulemavu wa ngozi, Gasper Elikana (10) ameuawa kwa kukatwa shingo na mguu wake kunyofolewa. Mbali na kumuua albino huyo saa 2:30 usiku juzi, wauaji hao walimjeruhi vibaya kwa mapanga, baba yake mzazi, Elikana Ngelela (44). Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi limetangaza zawadi ya sh 1,000,000 kwa yeyote atayetoa taarifa za kukamatwa kwa wahusika, kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Bw. Elias Kalinga alipozungumza na Majira jana jioni baada ya kufika eneo la tukio. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Abbas Kandoro alisema kuwa alipokea taarifa za tukio hilo kwa masikitiko makubwa na kwamba kitendo hicho lazima kikemewa na kila Mtanzania anayejali maisha ya binadamuwenzake. Bw. Kandoro alisema utajiri haupatikani kwa kukata viungo vya albino bali ni watu kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo. Alisema kuwa serikali inatoa wito kwa jamii kutoa ulinzi kwa walemavu wa ngozi mkoani Mwanza na si kuiachia serikali pekee katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kinyama. Bw. Kandoro alisema ameagiza timu maalumu kutoka mkoani Mwanza, ikiongozwa na Bw. Kalinga kwenda wilayani Geita kufanya uchunguzi kuungana na Kikosi Kazi kinachoongozwa na Mkuu wa Wilaya yaGeita, Bw. Philemon Shelutete. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dkt.Cassian Kabuche alisema kuwa majeruhi ambaye amelazwa wodi namba nane hospitali hapo hali yake si ya kuridhisha kutokana na majeraha aliyopata kichwani. "Alifikishwa hapa jana (juzi) usiku akiwa hajitambui kiasi kwamba iwapo hali ingeliendelea hivyo hadi leo (jana), tungempeleka katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, lakini kutokana na juhudi zilizozifanya hali yake angalau inatia moyo kidogo," Alisema Dkt.Kabuche.Habari zilizopatikana kijijini hapo, zinasema wauaji hao wakiwa na mapanga, walifika nyumbani kwa Bw. Ngelela na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kisha kumuua mwanaye. Mkazi wa kijiji hicho, Bw. Makami Nkilijiwa, alisema majirani walisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa mama wa mtoto huyo, nawalipofika walikuta wauaji wamekwishatoweka na mguu wa kulia wa mtoto huyo, huku mwili wake ukiwa umekatwa shindo huku baba yake akiwa ajitambui. Baada ya kuona hali hiyo, wakazi wa kijiji hicho walimchukua majeruhi na mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Wilaya ya Geita ambako maiti imehifadhiwa na majeruhi akiendelea na matibabu.

Haya Mambo bado yapo? Mtoto afa kwa kukeketwa!!

POLISI mkoani Manyara wanamshikilia Bw. Danieli Shauri (37) kwa kosa la kumkeketa binti yake, Debora Daniel (4) na kumsababishia kifo.Mtoto huyo alikeketwa Oktoba 11, mwaka huu na kuendelea kuvuja damu sehemu za siri hadi Oktoba 18 alipofariki dunia.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Parmena Sumary alisema kuwa tukio hilo lilitokea siku hiyo saa 10.00 jioni katika Kijiji cha Imbilili wilayani Babati.Kamanda Sumary alisema kabla ya kifo chake, mtoto huyo alikuwa akiishi na mtuhumiwa baada ya mama yake mzazi, Bi. Chatherine Daniel (29) kupata kichaa na kumtelekeza akiwa mdogo.Kutokana na hali hiyo mtoto huyo alikosa afya na kupata na homa za mara kwa mara kwa sababu ya kukosa maziwa ya mama, hali iliyosababisha wazazi wa mtuhumiwa kushauri akeketwe ili kuondokana na matatizo hayo.Kamanda alisema kuwa mtuhumiwa alitekeleza ushauri potofu wa wazazi wake, lakini alishangazwa na hali ya mtoto huyo kuendelea kuwa mbaya hadi alipofariki dunia kwa kupoteza damu nyingi.Baada ya kifo hicho kutokea, mtuhumiwa alitaka kuuzika mwili wa mtoto huyo bila ya watu kujua lakini wasamaria alitoa taarifa kwa Mtendaji wa Kijiji hicho, Patizumu Jeseph ambaye alifika nyumbani kwa mtuhumiwa na kukuta maandalizi ya mazishi na kuwaamuru kusimamisha shughuli hiyo hadi hatua za kisheria zitakapofuatwa.Baada ya amroi hiyo mwili huo ulichukuliwa hadi Hospitali ya Wilaya ya Babati kwa uchunguzi zaidi na ndipo iligundulika kuwa marehemu alipatwa na mauti hayo baada ya kukeketwa na kuvuja damu nyingi.Kwa mujibu wa kamanda huyo, ngariba aliyehusika kumkeketa mtoto huyo, Mama Mangiza, alitoroka baada ya hali ya mtoto inakuwa mbaya na polisi wanaendelea kumsaka kujibu shtaka hilo.

Karibu Kundini - Frederick Werema

Picha Ya Mwanasheria Mkuu mpya Frederick Werema Baada ya Kuapishwa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete akimuapisha, Frederick Werema, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mpigie Kura Elizabeth

Eliza, Binti wa Kitanzania ameingia kikaangoni tena wiki hii katika jumba laBBA, kumnusuru asitolewe piga kura mara nyingi iwezekanavyo, kwani kura yako ndio salama yake ndani ya jumba hili na hatimaye kuibuka mshindi na kuiletea sifa Tanzania kama alivyoiletea Richard. Andika neno: VOTE ELIZA kisha tuma kwenda namba 15726. Hii ni kwa watu wote wenye mitandao ya Voda, Tigo na Zain.

Wednesday, October 21, 2009

Tulikupenda sana ila Mungu alikupenda zaidi - Buriani Masanja

Masanja Enzi za Uhai wake

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera akiweka shada la maua katika jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu masanja mara baada ya kutoa heshima za kwenye uwanja wa uhuru.

Waombolezaji wakiwa wameibeba mwili wa aliyekuwa meneja wa uwanja wa Uhuru, Celestine Charles Masanja wakati wa kutoa heshima za mwisho zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru

Huu ni Ukatili kupitiliza ukomeshwe

JESHI la polisi mkoani Mwanza, limefanikiwa kuipata mifupa ya albino kufuatia kumtia mbaroni mtuhumiwa wa kesi ya mauaji, aliyekuwa akisakwa tangu Juni mwaka huu.Kukamatwa kwake kumesaidia kupatikana kwa ushahidi wa mifupa ya marehemu, Jesca Charles iliyokuwa imefichwa kichakani baada ya kuuawa Juni 21 mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Elias Kalinga alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo (jina linahifadhiwa) kuliwezesha kupatikana kwa mifupa sita ya miguu na mikono ya marehemu Jesca.Kalinga alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa kulitokana na maendeleo ya upelelezi wa kesi ya mauaji namba 28/2009 ya Jesca Charles aliyeuawa kwa kukatwa mapanga mikono na miguu Igoma jijini Mwanza na wauaji wake kutoweka na baadhi ya viungo vyake.

First Lady Apewa TUZO ya Mama wa Upendo

Leo tarehe 21/10/2009 Mke Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya Mama wa upendo na wanafunzi wa shule za Sekondari za Mvomero mkoani morogoro ikiwa ni ishara ya shukrani za wanafunzi hao kwa jinsi anavyowajali na kuwasaidia watoto wenye shida. kufundishia, kuweka matanki ya maji na kufunga umeme wa jua katika Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo jana na Mariam Kaima ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Adrian Mkoba kwa niaba ya wanafunzi wenzake wakati wa tamasha la wanafunzi wa shule za Sekondari wa wilaya ya hiyo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu cha Mzumbe. Akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake Mariamu alisema kuwa Mama Kikwete ni mama na kiongozi wa kwanza hapa Tanzania kuhimiza watu wote kuwapenda watoto wa wenzao kama wanavyowapenda watoto wao, kuwasomesha watoto zaidi ya 300 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, kutoa misaada ya vifaa vya shule za Sekondari. Aidha Mama Kikwete kupitia Taasi yake ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatoa misaada ya vifaa vya afya ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto, kuendeleza kampeni za kutokomeza mimba za utotoni na kutumia muda mwingi wa kuzungumza na wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili. Kwa upande wake Mama Kikwete aliwashukuru wanafunzi hao kwa kuona umuhimu wa kazi anazozifanya kupitia Taasisi yake ya WAMA na kuwataka kukazana katika masomo yao ili weweze kupata elimu ya kutosha itakayowasaidia maishani mwao. "Nafasi ya kusoma mliyoipatamuitumie kwa kusoma kwa bidii na kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma ili wale wanaowasomesha wapate moyo wa kuwasomesha zaidi kwani kuna wenzenu wanatafuta nafasi kama hii lakini haipati", alisema Mama Kikwete.

Ndoa ya Monaliza Chinda yafikia Kileleni

Nyota wa Filamu za Kinegeria Monalisa Chinda, Ijumaa iliyopita alitoa kauli rasmi kuhusu kufa kwa ndoa yake iliyodumu kwa miaka mitano , katika wakala wake Monalisa mama wa mtoto mmoja wa kike (Tamar Kirejesu) amesema ndoa yake ni sawa na ndoa nyingine yoyote na ilikuwa na matatizo sawa na ndoa yoyote, aliongeza kwa kusema alimpenda na kumthamini mume wake kama ilivyotakiwa lakini anahisi kuwa kuna baadhi ya sehemu walikuwa na tofauti kama binadamu wa kawaida na ndizo zilizowapelekea wasipate suluhu na kusababisha kuachana, licha ya kuachana Monalisa amesisitiza atachukua jukumu la kumlea mtoto wao na kuendelea kumuheshimu baba mtoto wake na anamtakia kila la heri katika maisha yake mapya.

Zain yaja na Huduma Mpya ya Pamoja Plus (+)

Katika kuwapa ahueni wateja wake kimawasiliano katika wakati ambao teknolojia imekua, Kampuni ya simu za mikononi ya Zain imeleta tena huduma mpya ijulikanayo kama Pamoja Plus (+) itakayoanza kufanya kazi kuanzia sasa.
Akifanya uzinduzi huo jana asubuhi kwenye ukumbi wa Kibo katika Hoteli ya Kilimanjaro (Kempinski) hapa Dar es Salaam mbele ya Wanahabari, Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Bwana Khaled Muhtadi amesema kwa sasa wateja wake watapata huduma nafuu kwa kupewa punguzo la hadi asilimia hamsini (50%) kwa simu za Zain pamoja na mitandao mingine watakazopiga. Ameeleza kuwa mteja atakayejiunga na huduma hiyo (Pamoja Plus), atapata nafasi ya kusajili namba za watu kumi (10) wa mtandao wa Zain atakazopata, kisha ataongeza tena namba moja kutoka mtandao mwingine wowote aupendao ambayo nayo itafaidi punguzo hilo huku akiweza kubadilibadili namba hizo hadi mara tatu kwa mwezi apendavyo. Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Zain nchini amesema zile simu za Zain zitakazopigwa na ambazo haziko katika chaguo la namba alizozisajili katika Pamoja Plus nazo zitapata punguzo la asilimia ishirini (20%) na pia zile za mitandao mingine ambazo nazo hazijasajiliwa zitapata punguzo la asilimia kumi na saba (17%).

Kumbe mambo ya Limbwata hadi Majuu yapo !!!!!!!Cristiano Ronaldo apigwa JUJU

Mganga mmoja wa nchini Hispania ametamba kumpiga juju nyota wa Real Madrid asifurukute ndani ya Real Madrid na aandamwe na majeraha mpaka msimu utakapoisha. Uongozi wa club ya Real Madrid umepokea barua toka kwa mganga Jose Ruz, mwenye umri wa miaka 58 mkazi wa mji wa Malaga, ambaye ni maarufu kwa jina la "Pepe" akiwataarifu kuwa amemroga nyota huyo wa Ureno asifurukute kabisa uwanjani wakati akiichezea klabu ya Real Madrid. Pepe amedai kwamba Ronaldo ataandamwa na majeraha msimu mzima na kiwango chake cha soka kitashuka. Pepe alisisitiza kwamba hana nia mbaya na Real Madrid isipokuwa anatimiza wajibu wake kama mganga baada ya kutakiwa na mteja wake ampige juju Ronaldo."Nafanya kazi yangu kwa mujibu wa matakwa ya mteja wangu ambaye pia mtu maarufu na anajuana vyema na Ronaldo".Mganga huyo alidai kwamba mmoja wa wapenzi wa zamani wa Cristiano Ronaldo ndiye aliyemtaka ampige juju Ronaldo kutokana muda aliompotezea baada ya kuwa naye na kisha kumtosa.."Ronaldo atajeruhiwa vibaya sana uwanjani, siwaahidi lini ataumia, lakini subirini muone", alitamba Pepe.Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji ghali kuliko wote duniani baada ya kuhama kutoka Manchester United ya Uingereza kuhamia Real Madrid ya Hispania kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa paundi milioni 80.

Tuesday, October 20, 2009

Majuu wamedata - Bibi Huyu auza picha zake za utupu ili kuganga njaa

Bibi Marianne L. mwenye umri wa miaka 75 mkazi wa mji wa Berlin, Ujerumani amelazimika kuuza picha zake za utupu alizopiga akiwa kijana ili aweze kupata pesa za kuganga njaa na kulipia bili zake

Maajabu ya Kweli jitahidi na wakwako awe kama huyu

Adora Svitak (11) pamoja na umri wake mdogo amezidi kuwashangaza watu duniani kwa mambo yake anayoendelea kuyafanya.Mtoto huyo kama watoto wengine hupelekwa na wazazi wake shule lakini kinachowatenganisha na watoto wengine ni kwamba yeye hupelekwa shule kama mwalimu akiwa na nguo zake za kawaida tofauti na wenzake wanaokuwa kwenye unifomu.Mtoto huyo alianza kusoma alipokuwa na umri wa miaka miwili na alipotimiza miaka saba alitoa kitabu chake alichokiandika mwenyewe kwa mawazo yake mwenyewe.Adora sasa akiwa na umri wa miaka 11 amekuwa mwalimu na katika masomo yake amekuwa akielezea matatizo ya kiuchumi duniani,vita mbali mbali duniani na mambo mengi mengine makubwa kuliko umri wake.

Kipigo chamsababisha abakie nusu kichwa

Picha ya Steve Kabla ya kuumizwa

Picha ya Steve baada ya kuumizwa

Steve akiwa na Mama yake mzazi

Fuvu la mbele la kijana Steve Gator mwenye umri wa miaka 26 ilibidi liondolewe ili kuokoa maisha yake baada ya kushambuliwa kwa ngumi na mateke yaliyomfanya aende chini na kukipigiza kichwa chake kwenye kiambaza cha barabara.

Mtoto wa Ajabu awashangaza Wanasayansi Duniani

Wanasayansi na madaktari nchini Urusi wamestaajabishwa na mtoto mwenye umri wa miezi tisa ambaye mwili wake umekuwa ukitoa maandishi katika lugha ya kiarabu yakinukuu vipande vya maneno katika Quran.
Wanasayansi nchini Urusi wameshindwa kujua ni nini kinapelekea mtoto anayeitwa Ali mwenye umri wa miezi tisa, mwili wake uwe unatoa maandishi tofauti tofauti ya kiarabu mara kwa mara.Televisheni ya Vesti news ya nchini Urusi ilionyesha video ya mtoto huyo na picha ambazo wazazi wake wamekuwa wakimpiga kila maandishi mapya yanapotokea.Kwa mujibu wa wazazi wake wanaoishi kwenye mji wa Dagestan, siku mbili baada ya Ali kuzaliwa herufi za kiarabu zilianza kujitokeza kwenye miguu yake na baada ya siku kadhaa zilianza kutengeneza maneno kamili.Maandishi tofauti tofauti ya kiarabu hutokea zaidi kila siku ya jumatatu na ijumaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake.Awali kulikuwa na alama za maandishi yaliyofifia kwenye kidevu chake na baadae maandishi hayo yalijitokeza wazi yakisomeka "Allah", alisema mama wa mtoto huyo Madina Yakubova.Miongoni mwa maneno ambayo yamesomeka wazi ni yale yanayosema "Waonyesheni watu dalili za kuwepo kwangu".Kwa kushangaza zaidi kwenye mguu mmoja wa Ali yalijitokeza maandishi yaliyosemeka "Allah (Mungu) ndiye muumba wa vitu vyote".Ali alipozaliwa aligundulika kuwa na matatizo makubwa ya moyo wake na ugonjwa unaoathiri zaidi ubongo unaoitwa "cerebral paralysis" lakini alipopimwa tena baada ya maandishi hayo ya kiarabu yalipoanza kujitokeza aligundulika hana matatizo yoyote na afya njema.Madaktari nchini Urusi hawajui ni nini kinaendelea kwenye mwili wa mtoto huyo na wamekiri hawajawahi kwamba hawana jibu la kutoa kwa taaluma za kisayansi.

Mtoto amnyang'anya Baba yake Mke!!!!!!!!!!!!!!

Kijana mwenye umri wa miaka 18 wa nchini Uingereza amemchanganya kimapenzi mama yake wa kambo kiasi cha kusababisha avunje ndoa yake na baba yake na kisha kutoroka naye.
Kijana mwenye umri wa miaka 18 wa nchini Uingereza ametoroka na mama yake wa kambo mwenye umri wa miaka 34 baada ya kumchanganya kimapenzi na kupelekea avunje ndoa yake.Benjamin Smith alisababisha ndoa ya baba yake, Andrew Smith na mama yake wa kambo Dawn Smith ivunjike ikiwa ni miezi michache baada ya kukutana naye kwa mara ya kwanza tangia alipomtelekeza alipokuwa mtoto miaka 17 iliyopita.Benjamin Smith alikutana na baba yake mwaka jana na alihamia kwenye nyumba yake kuanza maisha mapya akiishi na baba yake.Lakini muungano huo wa baba na mwana uligeuka kuwa chachu kwa baba wa kijana huyo.Mke wake alianza kufanya mapenzi na kijana huyo na haikuchukua muda mrefu ndoa yao ilivunjika.Kijana huyo na mama yake wa kambo walitoroka na kuhamia mji mwingine jirani wa Lincoln kuanza maisha mapya pamoja.Kutokana na kwamba Benjamin alikuwa na mojawapo ya funguo za nyumba ya baba yake, alirudi nyumbani kwa baba yake kisiri na kumuibia pesa sawa na paundi 150.Benjamin alikamatwa na polisi na kufikishwa kizimbani ambako alikiri kosa lake na kuhukumiwa kufanya kazi bila malipo kwa masaa 60 pamoja na kumrudishia baba yake pesa alizomuibia.Si baba, mwana wala mama wa kambo ambaye alikuwa tayari kuzungumzia mkasa huu ambao umewavutia watu wengi nchini Uingereza.

Monday, October 19, 2009

Simba Yaigeuza asusa JKT Ruvu 4 -1

AUNGURUMAPO Simba mcheza nani?, ndiyo hali inayoendelea kwa sasa katika Ligi Kuu ya Vodacom baada ya vinara hao kuichakaza JKT Ruvu kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana. Maafande hao wa JKT wanaosifika kwa kutandaza soka ya kuvutia walishindwa kuhimili vishindo vya mnyama huyo aliyepania kutwaa ubingwa msimu huu na kujikuta wakiruhusu mabao mawili katika dakika mbili. Mshambuliaji Uhuru Selemani aliifungia Simba bao la kwanza katika dakika ya 29, kwa kumalizia mpira uliotemwa na kipa Shaaban Dihile aliyekuwa akijaribu kuzuia shuti. Dakika moja baadaye beki wa kimataifa wa Kenya, Joseph Owino alifunga bao la pili kwa vinara hao akimalizia pasi ya Mussa Mgosi kwa kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni. Kabla ya kiungo Ramadhani Chombo, 'Redondo' kufunga bao la tatu na Mgosi (78) kushindilia msumali wa mwisho kwa maafande hao. Hadi sasa Simba inashikilia rekodi ya kuwa timu pekee Duniani ambayo haijafungwa na wala haijatoa sare yoyote baada ya vinara wa Hispania, Barcelona kuharibu rekodi yao mwishoni mwa wiki walipolazimishwa sare na Valencia. Baada ya mabao hayo JKT walijirekebisha na kupata bao katika dakika ya 43 kupitia kwa Damac Makwaya aliyepiga mpira wa adhabu uliomshinda kipa Juma Kaseja aliyeudharau akifikiri unatoka na kufanya matokeo kuwa 2-1hadi mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hadi dakika ya 50 ambapo kiungo wa Simba, Ramadhani 'Redondo' alifunga bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi ya Salum Kanoni. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, aliyeteuliwa kwenye kikosi cha wachezaji bora wa CHAN, Mgosi alipachika bao la nne kwa vijana hao wa Msimbazi akimalizia pasi ya Okwi. Kwa matokeo hayo Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 24 baada ya michezo nane ikifutiwa na Mtibwa Sugar (15) inayolingana pointi na Azam na Yanga lakini kuna tofauti ya mabao ya kufunga. (Habari toka Mwananchi)

Vita Ya Ufisadi yageuka Shubiri

VITA ya ufisadi iliyotangazwa na baadhi ya wabunge waliojipambanua kuwa ni wapambanaji wa ufisadi na kuungwa mkono na baadhi ya watu hivi sasa inaonekana kuwa shubiri kutokana na baadhi ya maamuzi yaliyofanywa kwa hofu ya ufisadi kuonekana kuigharimu nchi kiasi cha kuhatarisha ustawi wa kiuchumi na kijaami.
Uhasama baina ya wabunge na mawaziri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulioonekana katika Bunge lililopita kiasi cha kuilazimisha Halmashauri Kuu ya chama hicho kuunda kamati maalum ya kutafuta suluhu ni miongoni mwa mambo yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na vita hiyo ambayo hivi sasa imeacha majeraha makubwa nchini.
Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili pamoja na mahojiano iliyofanya na baadhi ya viongozi mbalimbali imeonyesha baadhi ya maamuzi nyeti yanashindwa kupata baraka za viongozi wa kisiasa ambao hivi sasa wamekuwa wakitaka kushindana na kukomoa pasi na kuangalia athari za maamuzi yao.
Kukomoa huko ndiko kunakomtikisa Rais Jakaya Kikwete pamoja na kamati aliyoiunda chini ya Rais mstaafu, Alli Hassan Mwinyi, ambayo imeshaanza kuonyesha kutokuwa na uwezo uliotarajiwa kutatua suala hilo linaloonekana kuizidi kimo CCM.
Chuki miongoni mwa wabunge na mawaziri wa CCM sasa imeonekana si kukitafuna chama bali hata mgawo wa umeme uliopo ambao baadhi ya watendaji shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) walishatoa mapendekezo kadhaa serikalini ili kuinusuru nchi kuingia katika janga hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, ni mmoja wa watendaji waliosimama kidete kuelezea mipango yao ya kuboresha uzalishaji wa umeme ikiwemo kununua mitambo mipya, kununua ya Dowans na mingine ambayo ilikumbana na vikwazo vikali.
Baada ya Dk. Idris kupata upinzani huo alitangaza kuwa TANESCO imejitoa kununua mitambo ya Dowans huku akionya kuwa shirika hilo lisije likalaumiwa kwa mgawo ambao ungejitokeza Oktoba na Novemba mwaka huu.
Onyo hilo la Dk. Idris lipokewa kwa shutuma nzito na baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ilidai bora nchi iingie gizani kuliko kununua mitambo hiyo.
Mgawo wa umeme ulioanza wiki iliyopita wa saa 14 kwa siku ndiyo umewafanya baadhi ya wananchi, wanasiasa, wafanyabiashara kukumbuka onyo la Dk. Idris na kuwalaumu viongozi walioshiriki kwa namna moja au nyingine kukwamisha mipango ya TANESCO.
Wakati mgawo wa umeme ukionekana kushika kasi Kamati ya Nishati na Madini, chini ya Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM), itangaza kufanya uchunguzi ili kuona kama mgawo huo umesababishwa na watendaji wa TANESCO ili kutimiza mipango yao hasa ya kununua mitambo ya Dowans.
Kamati hiyo ilizungumza na watendaji wa TANESCO na baadaye ilisalimu amri kuwa mgawo huo ulitokana na kuharibika kwa mashine kadhaa pamoja na upungufu wa maji kama ambavyo shirika hilo lilivyotangaza.
Baadhi ya wafanyabiashara wenye viwanda wameingiwa na hofu ya kuendelea kufanyabiashara hasa kutokana na mgawo huo ambao umeathiri kwa kiwango kikubwa uzalishaji.
Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) ni miongoni mwa wadau waliojitokeza kutaka nchi isiendelee kuwa gizani kwa kuendekeza maamuzi yenye athari ilhali kuna mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme lakini inashindwa kutumika.
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ni miongoni mwa taasisi za serikali zinazoathirika na mgawo huo kwa kuwa imekuwa ikipoteza mapato mbalimbali iliyokuwa ikiyapata kutokana na uzalishaji mali.
Wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wameweka bayana kuwa nchi ipo hatari kuporomoka zaidi kiuchumi kama serikali haitochukua hatua za haraka kutafuta vyanzo vya kudumu vya kuzalisha nishati ya umeme ambayo hutegemewa na viwanda mbalimbali.
Wakati wachambuzi hao wakitoa tahadhari hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, ambaye siku za nyuma alijitokeza hadharani kulitaka Bunge na serikali kufikiria upya juu ya mitambo ya Dowans na ikiwezekana wainunue ili nchi isiingie gizani ameibuka tena kuitaka serikali itaifishe mitambo hiyo.
Zitto alisema uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo ni mgumu lakini kwa hali ilivyo hivi sasa ni lazima viongozi wakubali kufanya umuzi huo hata kama watasakamwa na wahisani kwa kukiuka sheria.
Hoja hiyo ya Zitto kwa kiasi kikubwa imeonekana kuungwa mkono na kada mbalimbali za wananchi huku serikali kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akikataa kufanya hivyo kwa madai ni kukiuka sheria za nchi.
Kauli hiyo ya Ngeleja imeonekana kupingwa na baadhi ya watu wakiwemo wanasheria ambao wameweka bayana kuwa serikali imekuwa ikikiuka sheria mbalimbali ambapo wakati mwingine si kwa manufaa ya walio wengi hivyo ni vema kufikiria upya wazo la Zitto.
Tindu Lissu ni mmoja wa wanasheria aliyeweka wazi kuwa serikali haiwezi kuwa na kesi ya kujibu kama ikifikia hatua hiyo kwa kuwa sheria ya kimataifa ya uwekezaji pamoja na namna mitambo hiyo ilivyoingia hapa nchi imegubikwa na mizengwe.
Mwanasheria ameweka bayana kuwa hofu hiyo ya serikali haipaswi kupewa nafasi katika kipindi hiki ambacho nchi ipo hatarini kuporomoka kiuchumi kutokana na kushuka kwa uzalishaji viwandani.
Mgawo wa umeme umeonekana kuibua upya sakata la vita ya ufisadi ambalo lilishika kasi baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kutokana na kuhusishwa katika kashfa ya kuipa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharula kampuni ya Richmond ambayo ilibainika kutokuwa na uwezo.
Sakata la Richmond ndilo kwa kiasi kikubwa lililozaa ufa na makundi yenye kuhasimiana vikali ndani na nje ya Bunge kiasi cha kuhatarisha mustakabali wa CCM ambao katika siku za hivi karibuni umekumbwa na kashfa mbalimbali.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona serikali itakuwa na wakati mgumu wa kuamua kipi cha kufanya kumaliza tatizo la mgawo wa umeme ambalo kwa namna moja au nyingine lilisababishwa na utendaji usio makini pamoja na tamaa za watu waliopewa jukumu la kuongoza nchi.
Moja kati ya sababu inayowafanya wachambuzi hao kuiona serikali kuwa iko njia ni ukweli kuwa wabunge walio katika mstari wa mbele kupinga baadhi ya mambo ni kutoka CCM ambacho ndicho chama kilichoshikilia dola.
Wachambuzi hao pia hawakusita kueleza wakati mgumu itakaokumbana nao Kamati ya Mzee Mwinyi iliyopewa jukumu la kutatua uhusiano mbovu baina ya wabunge na mawaziri ulioshamiri hivi sasa.
Ugumu wa Kamati ya Mzee Mwinyi unadaiwa utachagizwa zaidi na joto la uchaguzi mkuu ambapo kila mbunge anataka kuonekana anawajibika kwa wananchi wake hivyo kuwawia vigumu viongozi wa serikali. (Habari toka Mtanzania Daima)

Thursday, October 15, 2009

Zitto hakuwa nyuma siku Ya fainali ya BSS

Zitto kabwe alionekana kufuatilia kwa makini fainali za Bongo Star Search

Huyu ndie Michael Jackson wa Tanzania!!!!

Mzee wa Mavocal aondoka na Milioni 25

Hatimaye kile kitendawili cha nani atajiondokea na mzigo mzima wa Tsh 25,000,000/- za kitanzania ulitatuliwa usiku wa juzi pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee mara baada ya Pascal Cassian a.k.a Mzee wa Vocal au BabaRita kuondoka na kitita hicho. Diamond Jubilee ilifurika kiasi cha kukosa nafasi ya kupitisha mguu pale washabiki wengi walipojitokeza kushuhudia fainali hiyo ambayo ilirushwa Live katika mtando wa Dar411 na kituo cha televisheni cha ITV. Kabla ya kuanza kwa fainali Chief Judge Madame Rita alipanda jukwaani kutoa shukrani zake kwa wote waliofanikisha kwa namna moja au nyingine kuweza kuifikisha Bongo Star Search katika fainali hiyo. alitoa shukrani kwa wadhamini wakuu ambao ni Vodacom Tanzania, Kilimanjaro na wengine wote waliofanikisha toka mwanzo wa safari mpaka hapa tulipofika, bila kuwasahau wafanyakazi wote wa Benchamark”

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Amekua muda mrefu akihisi mke wake anamuibia kwa kutembea nje yandoa. Akaamua aandae safari feki na kurudi ghafla bila mkewe kutarajia. Akarudi na Taxi usiku wa manane na aliamua dreva Taxi aweshahidi, akamlipa 100,000 ili waende wote kufumania. Akanyanyua Bastola, wakanyatia ndani mpaka chumba chakulala, akaingia yeye na dereva taxi kwa kupanda kwa kamba,akawasha taa na dreva akafunua blanketi alilojifunikia mke wake....wapo wawili!Mke wa jamaa yu kitandani na mwanaume mwingine!!!Jamaa akaweka bastola kichwani kwa yule mwanaume mgoni wake, ghafla mke wake akapaza sauti, “Usimuue!Huyu bwana ametusaidia sana! Nlikudanganya niliposema nimerithi fedha. Ni yeye alinunua lile LandCruiser VX niliyokununulia, alilipia hii nyumba tunayomiliki sasa, alinipa zile pesa tulikuwa tunadaiwa na benki na analipia tiketi zetu zotetunavyoendaga maonyesho. Ndiye pia anayelipia ada za watoto wetu, hata hiyo suti uliyovaa na nyingine. Pia analipa kodi zetu za kilamwezi!”Huku akiyumbayumba kwa kutoamini, MME AKASHUSHA BASTOLACHINI, akamtazama dereva, akamuuliza, UNGEFANYA NINI UNGEKUWA NI WEWE? Dreva Taxi akamwambia; “Mfunike bwana, mfunike na hilo blanketi kabla hajasikia baridi”

Tuesday, October 13, 2009

Mwanamuziki wa Kundi la Boyzone Stephen Gately amefariki Dunia akiwa katika mapumziko huko Majorca


Chanzo cha habari kimesema Stephen mwenye umri wa miaka 33 alienda kulala kama kawaida lakini hakuweza kuamka asubuhi. Mwanamuziki mmojawapo wa Band Ronan Keating amesema kundi limepata pigo kubwa kutokana na kifo hiki. Stephen kakutwa umauti akiwa na partner wake wa miaka mingi ambaye walifungua ndoa ya watu wenye jinsia moja 2006 anayejulikana kama Andrew Cowles. Wanamuziki 4 waliosalia katika kundi la Boyzone wamesafiri asubuhi ya leo kuelekea"Majorca .

Monday, October 12, 2009

Kutana na Mama Bora na wa Mfano

Haya kivazi hicho wabongo!!!!!!!!!!!!!!!! Mtaweza?

Unaona Madhara ya Opereshani za Urembo?

Angalia Picha za Mastaa mbalimbali waliojaribu kutengeneza sura zako kwa visu.

Jaji wa Marekani Aliyewalawiti Wafungwa Kufungwa Maisha akipatikana na Hatia

Jaji 'Basha' wa nchini Marekani ambaye alikuwa akiwamendea wafungwa wanaume na kuwalawiti baadhi yao ili awapunguzie adhabu zao huenda akahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupandishwa kizimbani.
Jaji Herman Thomas, jaji ambaye alikuwa akiheshimika sana kiasi cha kwamba alikuwa akitabiriwa kuwa jaji mkuu wa kwanza mweusi wa Alabama Kusini, huenda akahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwalawiti wafungwa wanaume ili awapunguzie adhabu zao.Jaji Thomas anakabiliwa na tuhuma za makosa 78 ya kukiuka misingi ya kutoa haki, kulawiti wafungwa, kuwateka wafungwa na kuwashambulia waliokataa kulawitiwa.Jaji huyo mwenye umri wa miaka 48, alijitetea kwamba hakufanya kitendo hicho na kwamba alikuwa akikutana na wafungwa ili kuwapa miongozo bora.Wakili wa jaji huyo alidai kwamba mteja wake amebabimbikiwa kesi hiyo na wafungwa ili kumchafulia jina lake kwa kazi nzuri ya ujaji aliyoifanya kwa miaka 20.Jaji Thomas na wakili wake walidai kwamba kesi aliyofunguliwa ni njama za wanasiasa ambao hawapendi mafanikio yake.Lakini mahakama iliambiwa kwamba Jaji Thomas alianza kufuatiliwa mienendo yake baada ya kuibadilisha hukumu ya binamu yake mwaka 2006 ingawa hukumu ya kesi hiyo ilikuwa imetolewa na jaji mwingine.Mahakama iliambiwa pia kwamba jaji Thomas alizichukua kesi walizopewa majaji wengine bila ya kufuata taratibu husika.Baadhi ya wafungwa wanaume walielezea jinsi walivyotolewa jela na kupelekwa kukutana na Thomas kwenye gari lake au ofisini kwake.Awali kulikuwa na taarifa za wafungwa kuvuliwa nguo zao za ndani na kisha kuchapwa bakora halafu ndipo zilipojitokeza taarifa za kulawitiwa kwa wafungwa na wafungwa wengine kulazimishwa wajipigishe punyeto mbele yake.Wafungwa wote waliolawitiwa na jaji huyo walikuwa ni wafungwa weusi hakukuwa na mfungwa mzungu kati yao.Alama za bakora kwenye matako ya baadhi ya wafungwa na pia alama ya majimaji ya mbegu za kiume za mfungwa aliyelazimishwa apige punyeto kwenye zulia la ofisi ya jaji huyo ni miongoni mwa vielelezo vya ushahidi dhidi ya jaji huyo.Wafungwa waliotoa ushahidi waliweza kuelezea vizuri kabisa jinsi ilivyo ofisi ya jaji huyo ambayo haina madirisha.Thomas alijiuzulu nafasi yake mwaka 2007 baada ya tuhuma za wafungwa kuchapwa bakora kwenye makalio yao kusambaa.Waendesha mashtaka walisema kwamba kuna wafungwa 15 wapya na wa zamani ambao wako tayari kutoa ushahidi wa kulawitiwa na jaji huyo.Ushahidi huo utachukua wiki kadhaa na jaji Thomas huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.

Nani atakuwa Star wa Bongo mwaka huu?

Mdhamini mkuu wa shindano la Bongo Star Search, Kampuni ya Vodacom, juzi imetangaza zawadi ya washindi watakaoibuka katika kinyanganyiro hicho.Akitangaza zawadi hizo Meneja wa Udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna alisema kuwa fainali za shindano hilo zitafayika katika ukumbi wa Diamond Jubilee mnamo tarehe 13 mwezi huu.Katika fainali hizo mshindi wa kwanza ataibuka na zawadi nono ya shilingi Milioni 25, mshindi wa pili atajinyakulia shilingi Milioni 5, mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi Milioni 3 ambazo ni fedha taslimu pamoja na zawadi ya shilingi laki tano kutoka kwa Shear Illusion ambao ni moja ya wadhamini.Mshindi wa nne ataondoka na shilingi milioni moja na nusu na mshindi wa tano ataondoka na shilingi milioni moja.Kwa upande wa burudani, safu ya burudani itaongozwa na Shaa, Feisal Ismail, baby Madaha, Abubakar Mzuri na wasanii wengine kibao aliseama Ritta.Washindi waliofanikiwa kuingia katika tano bora ambao watagombania nafasi ya kuwa supa staa mpya wa Bongo ni Paschal Cassian wa Mwanza, Beatrice William wa mwanza, Peter Maechi toka mkoa wa Kigoma, Jackson George anayewakilisha mkoa wa Tanga na Kelvin Mbati toka Mkoa wa Dar es Salaam.

Je Wajua kama Zombe aachia ngazi jeshi la Polisi?


ALIYEKUWA Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe ameandika barua ya kuacha kazi katika jeshi hilo baada ya Serikali kukata dhidi yake. Jeshi la Polisi limethibitisha kupokea barua ya Zombe inayoeleza kutotaka tena kuendelea na ajira ya jeshi hilo.Maamuzi ya Zombe yamekuja kwa kudai kuwa baada ya kuona amefikia hatua hiyo ya hofu ya kwa kutengenezewa kesi nyingine na kulazimika kuandika barua ya kuomba kuacha kazi.Kamishna wa utawala na rasilimali watu wa Jeshi la Polisi, CP Clodwig Mtweve, amesema barua hiyo imepokelewa na imekabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ambaye kiutaratibu ndiye mwajiri wa Zombe.Mtwere alisema kuwa katibu huyo ndiye mwenye mamlaka ya kujibu barua hiyo ya kuacha kazi ama kuendelea nay eye ndiye atakayekuwa na mamlaka juu ya maombi hayo.Hatua ya Zombe imekuja baada Juzi Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) alikata rufani dhidi ya Zombe na wenzake wanaotuhumiwa kwa mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro, na dereva teksi mmoja.Rufani hiyo ina sababu 11 zinazopinga kuachiwa huru kwa washitakiwa hao wanaodaiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara hao.Sababu hizo zilizowasilishwa na DPP ni pamoja na Jaji Salum Massati, ambaye ndiye alikuwa akisikiliza kesi hiyo na kutoa hukumu ya kuwaachia huru washitakiwa hao, kufanya makosa katika kujielekeza, kujenga na kutoa tafsiri katika kanuni za kosa.Rufani hiyo inadai kuwa Jaji Massati alifanya makosa katika kumwachia huru mshitakiwa wa kwanza, ambaye ni Zombe, pamoja na kuwapo ushahidi wa kutosha wa kimazingira ambao ungeweza kumtia hatiani.Rufani hiyo pia inadai kuwa Jaji alishindwa kutoa sababu za washitakiwa wa WP Jane na D.2300 D/CPL Sarro kwa kuathirika kwao kimazingira kama alivyoeleza kwenye hukumu yake.

Thursday, October 8, 2009

"Hakuna Marefu yasiyo na Ncha" Hatimaye Usher na Tameka waachana

Hatimaje mwanamuziki wa Marekani Usher Raymond amefikia uamuzi wa kuachana na mkewe aliyeishi nae kwa Miaka 2 Tameka Foster. Kutokana na singo ya Usher aliyoitoa hivi karibu iliyoandikwa na Sean Garrett inaonyesha wazi kuwa kulikuwa na mzozo mkubwa kati ya wanandoa hao ( Nyepesi inawapa pole katika kipindi hiki kigumu)
There was an error in this gadget

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote