Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, November 30, 2009

Je wajua?

Unywaji wa glass nane (8) za maji kwa siku unasaidia kukufanya uwe na afya zaidi pamoja na kupunguza uzito mwilini.

Kweli raha jipe mwenyewe ukingoja kupewa utachelewa!!!!!!!!!!!!!

Kwanini nisinunue gari ya ndoto yangu kisa sijajenga nyumba nzuri?

Kwani wenye magari mazuri ni wale wanaoishi kwenye nyumba nzuri?

Kwani ni lazima uwe na Bangaroo ndio ufunge setilaiti dishi ?

Uswahili kuna Vituko?

Umeona vyoo vya uswazi sharti kwa kupanda na ngazi uliyajua haya?

Kwa sasa nipo busy na Muziki shule baadae

Baada ya kutamba na single zake za ‘Tabasamu’ na ile inayotamba kwasasa ‘Tupo pamoja’ Dogo mwenye uwezo mkubwa wa kuishi kistaa, Heri Samir ‘Blu’ amesema kuwa hivi sasa kizungumzia ishu ya shule atakuwa anadanganya kwa sababu haipo kwenye programu yake. Blu, staa wa Bongo Flava asiyefunikika, alisema kupitia kipindi kimoja cha kinachorushwa na Radio moja jijini kuwa ana mambo mengi yanayomkip busy lakini ishu ya elimu haipo kwenye ratiba yake. Dogo huyo ambaye anajulikana pia kwa jina la Kabayser, alizungumza hivyo kama jibu la swali liloulizwa na presenta wa kipindi hicho. Mbali na ishu ya elimu, Blu alisema kuwa sasa hivi hayupo kwenye mikakati ya albamu, isipokuwa atakachokuwa anakifanya ni kudondosha singo kali kila mara ili kuwapa raha mashabiki wake.

D Banj awapagawisha Wabongo

Mwanamziki mahiri kutoka Nigeria anayetamba na kibao cha ‘FALL IN LOVE’, D Banj, jana amedhihirisha maana halisi ya jina la mwimbo anaotamba nao kwa sasa ‘FALL IN LOVE’, baada ya kuhakikisha ya kwamba mashabiki waliokuja kumtazama wame fall in love naye. Msanii huyo alikuwa anatumbuiza katika tamasha la Intercollege Special 2009 lililodhaminiwa na kampuni ya Sigara Tanzania TCC. Pamoja na msanii huyo, tamasha hilo lilitumbuizwa na wasanii lukuki. toka Tanzania TID, Marlaw, CPwaa, Quick Racker, Joh Makini, Ally Kiba na wengine wengi. Kutoka Kenya alikuwepo Nameless, Nonini na Juacali.

Mapenzi kizunguzungu - Afukua maiti ya Mkewe na kulala nayo kwa miaka 5 mfululizo

Mwanaume mmoja wa nchini Vietnam ambaye alikuwa na huzuni ya kuondokewa na mkewe, alifukua kaburi la mkewe na kuichukua maiti ya mkewe na kuanza kulala nayo kitanda kimoja kwa kipindi cha miaka mitano. Le Van aligubikwa na huzuni kubwa wakati mkewe alipofariki mwaka 2003 kiasi cha kwamba alianza kulala juu ya kaburi lake katika mji wa Quang Nam uliopo ukanda wa kati wa Vietnam.Gazeti la Vietnamnet liliripoti kuwa Van aliendelea kulala juu ya kaburi la mkewe usiku kwa kipindi cha miezi 20 mpaka alipoanza kuugua kutokana na hali ya hewa ya baridi.Ili kujikinga na baridi, Van aliamua kutengeneza handaki lililoenda kwenye jeneza lake na kuanza kulala pembeni ya maiti yake.Watoto wa Van waliligundua handaki hilo na waliamua kumzuia Van kulitembelea kaburi la mkewe.Mwezi novemba mwaka 2004, Van alilifukua kaburi la mkewe na kuichukua maiti ya mkewe hadi nyumbani kwake.Van alitumia udongo mfinyazi kuizunguka mifupa ya maiti ya mkewe na kisha aliivalisha maiti hiyo nguo za kike na kisha kuipaka vipodozi.Van mwenye umri wa miaka 55, baba wa watoto saba, alianza kulala pembeni ya maiti ya mkewe akiikumbatia kuanzia wakati huo hadi leo.Picha zinazomuonesha Van akiwa pembeni ya maiti ya mkewe zilichapishwa kwenye gazeti la Vietnamnet, ikiwemo picha moja ambayo iliionyesha mifupa ya mkono wa mkewe ikiwa imezungushiwa udongo.

Huu ni Uungwana? Watanzania washushwa ndege ya Precision Air na kupakizwa wazungu!!!!!

ZAIDI ya abiria 15 raia wa Tanzania waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision Air kutoka Arusha kuelekea Dar es Salaam wameshushwa na kupakizwa raia wa kigeni. Tukio hilo lilitokea jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kusababisha mtafaruku uliodumu kwa zaidi ya dakika 30 kabla ya walinzi wa uwanja huo kuingilia kati, ili kutuliza hali hiyo kutokana na abiria hao kugoma kushuka. Wakizungumza na Tanzania Daima uwanjani hapo, abiria hao wamedai kuwa, kitendo cha kuteremshwa katika ndege waliyopanda na kupakizwa abiria wengine ambao ni raia wa kigeni (Wazungu) bila kuelezwa sababu za msingi ni cha ubaguzi wa hali ya juu. Akizungumza na gazeti moja, mmoja wa abiria aliyekumbwa na kadhia hiyo, Pamela Msuya, mkazi wa Dar es Salaam, alisema dakika chache kabla ya ndege kupaa hewani, rubani alizima injini ya ndege na wahudumu kuwaeleza kuwa kumetokea dharura, hivyo hawataweza kupaa. Alisema kutokana na hali hiyo, waliombwa kusubiri hadi saa 5:40 asubuhi. Awali walikuwa waondoke na ndege hiyo saa 1:00 asubuhi. Abiria huyo alieleza kuwa, ilipofika saa 5:40 waliingia katika ndege na rubani kuiwasha, lakini ilizimwa tena na kuamriwa kuteremka kwa maelezo ndege hiyo ilipaswa kupakia abiria wa Zanzibar ambao ni raia wa kigeni. Pamela aliendelea kudai kuwa, wakiwa wanashushwa katika ndege hiyo, baadhi ya abiria waligoma na kusababisha kutokea kwa mtafaruku mkubwa wa zaidi ya dakika 30 kabla ya walinzi wa uwanja huo kuitwa na wahudumu wa ndege hiyo na kwenda kuwashusha huku wakiwaita wazamiaji. “Si siri, tumedhalilishwa sana, yaani tunaitwa wazamiaji mbele ya wageni, watatuelewaje? Tuna booking ya muda mrefu tofauti na hao (raia wa kigeni),” alisema Pamela. Baada ya kushushwa abiria hao, wengine ambao wengi ni raia wa kigeni, walionekana wakipanda ndege hiyo kuelekea Zanzibar. Abiria mwingine ambaye hakupenda kutaja jina litajwe, alisema alishangazwa na kitendo hicho kutokana na abiria hao (wazungu) kutokuwa na taarifa za usafiri (booking) na kwamba walifika muda huohuo na kupatiwa usafiri. Aliongeza kuwa, baadaye waliambiwa kuwa wasubiri ndege ya saa 11:00 jioni ambayo itawapeleka jijini Dar es Salaam. “Tulishushwa tukaambiwa tusubiri ndege ya saa tano, tukavumilia na muda huo ulipofika tena wakatuambia tusubiri ya saa 11. Huu si uungwana hata kidogo,” alisema abiria huyo. Baada ya jitihada za kupata uongozi wa shirika hilo kugonga mwamba, mmoja wa wafanyakazi wa Precision Air mkoani Arusha ambaye alikataa kutaja jina wala cheo chake, alisema kwa kifupi tatizo hilo linashughulikiwa, na alipoulizwa zaidi aliwataka waandishi wa habari waende katika Uwanja wa KIA.

Adai kuiona sura ya YESU kwenye Pasi

Mwanamke mmoja nchini Marekani anayejulikana kwa jina la Mary Jo Coady mkazi wa Massachusetts nchini Marekani, ambaye ndoa yake na mumewe ilivunjika hivi karibuni na kufuatiwa na mkosi wa kupunguziwa masaa ya kufanya kazi kazini kwake, ametangaza kuiona sura ya Yesu kwenye pasi ya umeme na amedai ana uhakika maisha yake yatakuwa mazuri baada ya kuiona sura Yesu.Mary alidai kuigundua picha ya Yesu kwa mara ya kwanza siku ya jumapili iliyopita wakati alipoingia kwenye chumba cha mtoto wake.Uchafu uliotokana na kuungua kwa nguo kwenye pasi ulionekana kama sura ya mtu mwenye nywele ndefu.Mary mwenye umri wa miaka 44 pamoja na watoto wake wawili, walikubaliana kuwa sura inayoonekana kwenye pasi ni ya Yesu na wamba Yesu anawasikiliza.Mary ambaye alilewa katika mazingira ya kikatoliki aliliambia gazeti la The Eagle-Tribune kuwa mkasa wake wa kuiona sura ya Yesu utakuwa changamato kwa watu wengine wakati huu krismasi ikikaribia.Mary alisema kuwa ana mpango wa kuificha pasi hiyo kwenye kabati na atanunua pasi nyingine.

Friday, November 27, 2009

Je ni haki Kampuni ya Famili ya Kingunge (Smart Holdings) kupewa Tenda ya kukusanya Mapato Machinga Complex baada ya kuharibu Ubungo Stand?

Vyama vya wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) kwa kushirikiana na Muungano wa Masoko ya Mkoa wa Dar es Salaam (Mumada), vimeandaa mkutano mkubwa, kujadili pamoja na mambo mengine, uhalali wa kampuni inayomilikiwa na familia ya Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru. Familia hiyo imepewa zabuni ya kukusanya mapato katika jengo la Machinga Complex, huku ikiwa imefanya vibaya katika kazi hiyo katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT). Vyama vilivyoandaa mkutano huo utakaofanyika wiki ijayo kwa kushirikiana na Mumada, ni pamoja na Asbo, Tamada, Vibindo pamoja na Umoja wa Wafanyabiashara Walemavu Mkoa wa Dar es Salaam (Uwawada). Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, David Nyendo, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa tayari wameshaunda kamati ya watu sita, ambayo ina mwakilishi kutoka katika kila chama kwa ajili ya kuratibu mkutano huo. Nyendo alisema mkutano huo utafanyika Desemba 5, mwaka huu, katika ukumbi wa Al-Muntazir (zamani Korea) na kwamba, wanatarajia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, kuwa mgeni rasmi. “Barua ameshapelekewa. Tulifika Ofisini kwake (Mkuu wa Mkoa), tukamkabidhi Msaidizi wake. Hivyo tunatarajia atakuwa mgeni rasmi katika mkutano wetu,” alisema Nyendo alipozungumza na na chombo kimoja cha habari. Alisema mkutano huo unatarajia kujadili kuhusu maendeleo ya Machinga Complex na mikakati ya kusukuma mambo, ambayo wamachinga wanahisi kuwa yana maslahi nao katika uendeshaji wa jengo hilo lililoko Ilala. Ajenda nyingine ni zabuni ya kukusanya mapato katika jengo hilo, pamoja na uhalali wa kampuni ya Smart Holdings iliyopewa zabuni hiyo ya kukusanya mapato katika jengo hilo. “Tutahoji pia, kwa nini Jiji wameharakia kutangaza zabuni kabla hata jengo halijaisha,” alisema Nyendo. Wakati mkutano huo ukisubiriwa kwa hamu kubwa, habari tulizozipata jana kutoka kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo, zinaeleza kuwa huenda mkutano huo ukapitisha azimio la kutotoa ushirikiano kwa kampuni hiyo, ikiwa ni pamoja na kugomea kuilipa chochote kwa lengo la kushinikiza zabuni waliyopewa Smart Holdings itangazwe upya. “Kama mtu kaharibu Ubungo hadi Waziri Mkuu akaagiza ukaguzi ufanyike, iweje apewe sehemu nyingine akaharibu?” alihoji kiongozi mmoja wa Asbo, ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake liandikwe magazetini kwa maelezo kuwa si msemaji wa chama. Licha ya kampuni hiyo ya mwanasiasa mkongwe nchini kufanya vibaya katika kazi ya ukusanyaji mapato ya serikali katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), kiongozi huyo alidai kuwa ushindi wa zabuni yake umegubikwa na utata. Alidai utata huo unatokana na moja ya makampuni yaliyoomba zabuni hiyo, kampuni ya Amma Consult Limited, kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kuwania zabuni hiyo, lakini ikanyang’anywa ushindi huo na zabuni hiyo kutolewa kwa Smart Holdings Limited katika mazingira ya kutatanisha. Kampuni nyingine iliyowania zabuni hiyo, lakini ikashindwa, ni Zing Company. “Aliyenyang’anywa ushindi ‘alitenda’ zaidi ya Sh. bilioni 1.2 na alionyesha uwezo wake na namna atakavyoweza kufanya kazi hiyo, lakini aliyepewa zabuni alitenda fedha kidogo,” alidai bila kufafanua. Aliongeza: “Kampuni ya Amma Consult Limited ndiyo iliyokuwa imeshinda mwanzo, lakini katika hali ya kushangaza afisa mmoja wa kitengo cha manunuzi cha Halmashauri ya Jiji akainyang’anya ushindi.” Alidai katika kutekeleza njama hizo, Bodi ya Usimamizi na Uendeshaji wa jengo hilo haikushirikishwa katika hatua yoyote ya mchakato wa kumpata mzabuni licha ya Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM) kuagiza suala hilo. Badala yake, bodi iliishia tu kualikwa kwenye ufunguzi wa kinyang’anyiro cha zabuni.

Hongera Babu Sikare

Save Albino Benefit Concert ilioandaliwa na Babu Sikare anayekwenda kwa jina la Albino Fulani ambaye ni msanii, muigizaji na CEO wa Afrobino.Inc. ( http://www.afrobino.org/) iliyofanyika huko Columbus, Ohio, ilifana kupita kiasi ambapo watu wengi walijitokeza kutumbuizwa na wasanii mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya na Zambia. Akiongea na mtandao mmoja wa habari, bwana Sikare alitoa shukurani za dhati kwa wote waliohudhuria na kutoa ushirikiano wa hali juu kufanikisha shughuli hiyo. Aliongeza kuwa imefika wakati kwa wasanii kutumia vipaji vyao kusaidia kwa namna moja ama nyingine watu wanaohitaji misaada katika jamii. Alitoa shukurani za dhati pia kwa kampuni ya Walgreens Pharmacy ya Marekani ambao walitoa bei poa ya mafuta ya kinga ya jua kwa watoto wenye ualbino yaliyonunuliwa. Mafuta hayo yatakwenda kusaidia watoto kuanzia miaka 5-10 na yatakabidhiwa kwa chama cha maalbino Tanzania hivi karibuni

Daznundaz kurudi tena?

Kama unalikumbuka ni kundi lililowahi kutamba sana miaka ya 90 ambalo lilikuwa likiundwa na wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wawili Ferouz na Daz Baba ambao ndio walichangia kwa kiasi kikubwa kundi hilo kujipatia umaarufu wametangaza rasmi kumaliza tofauti zao. wakizungumza kwa pamoja na mtandao mmoja wa habari , wasanii hao walidai kuwa kwa sasa wako tayari kufanya kazi pamoja na hata kulirejesha upya kundi lao la Daznundaz. “Unajua tofauti zetu zilikuwa ndogo tu, ingawa vyombo vya habari vilichangia sana kuzikuza,hivi sasa tuko pamoja na mimi niko tayari kufanyakazi na mshkaji Daz Baba,” alieleza Ferouz, ambaye anaonekana kufulia kinoma kimuziki na kimaisha tofauti na alipokuwa na kundi la Daz nundaz. “Mimi na msanii mwenzangu Larumba ambaye tulikuwa pamoja tulianzisha kundi letu la Tanzaniano , lakini hili halituzuii kukaa pamoja na Ferouz na washkaji wetu wengine ili kulirejesha kundi letu la Daznundaz. Ferouz ni mtu wangu na niko tayari kufanya naye kazi,” alisema Daz Mwalimu . Kundi la Daznundaz lilisambaratika siku chache baada ya baadhi ya wasanii wake wakiongozwa na Ferouz kumtimua kundini msanii mwenzao Dazbaba kwa madai kuwa alikuwa akitumia dawa za kulevya ‘teja.’

Je wajua?

Ulaji wa Kabichi unasaidia upunguzaji wa uzito katika miili ya binadamu kwa sababu inauwezo wa kubadilisha sukari na carbohydrate katika Mafuta

CHOKORAA apewa kadi ya Njano Twangapepeta

RAPA wa bendi ya Twanga International, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ amesimamishwa na uongozi wa bendi hiyo kutokana na sababu za kuchochea tabia ya utovu wa nidhamu ndani ya bendi. Habari za kusimamishwa kwa msanii huyo zilipatikana Jumatano usiku katika ukumbi wa Club Bilicanas ambapo msanii huyo anakabiliwa na shutuma za kuanzisha kundi la Mapacha Wanne ambako wamekuwa wakifanya kazi bila ya kupata idhini kwa mwajiri wao.Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya hiyo, Asha Baraka, alisema ndani ya ukumbi wa Club Bilicanas kwamba wamefikia hatua hiyo kwakuwa Chokoraa ndiye kinara na tayari uongozi ulimpa onyo la kuacha kuchochea mgomo kwa wasanii wengine ambao ni Charls Gabriel ‘Chalz Baba’ na Kalala Hamza Kalala ‘Kalala Junior’ kutoka African Stars ‘Twanga Pepeta’ na Jose Mara wa FM Academia

Tibaigana atengua hukumu ya kifungo cha maisha kwa OTHUMAN KAZI

MWENYEKITI wa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Alfred Tibaigana, amemfutia adhabu ya kufungiwa maisha mwamuzi Othman Kazi. Tibaigana alisema mchana huu kwamba, kamati yake imelizika na hoja ya utetezi kutoka kwa Kazi na sasa atafungiwa kwa muda wa miezi mitatu pekee.“Kamati imeona hana hatia ya kufungiwa maisha kutokana na utetezi wake, badala yake tumempa adhabu ya kutojihusisha na SOKA kwa miezi mitatu tu,”

Thursday, November 26, 2009

Wafanyakazi Watano wa Kampuni moja wafariki dunia kwa mpigo

WAFANYAKAZI watano wa Kampuni ya ujenzi ya SICU ya jijini Dar es Salaam, wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Leonard Paul, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea jana, majira ya saa moja usiku katika Kijiji cha Inokanoka, wilayani Ngorongoro na kulihusisha gari T 372 AFC Mitsubishi Canter. Kamanda Paul aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Letuyo Lembeu (38), Ngidadiya Paluny (38), Oleyumbayiguti Pasani (36), John Mgawa (50) na Mesikongi Silelian (25), wote wakazi wa Ngorongoro. Aidha, waliojeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ni pamoja na Ezekiel Habali (27), Brayson Bake (26) na Azizi Hassan (27). Alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo kilitokana na ubovu wa barabara, hatua ambayo ilisababisha dereva wa gari hilo kushindwa kulimudu na kuacha njia kabla ya kupinduka. Polisi wanamshikilia dereva wa gari hilo, Huchen Weni (28), ambaye ni raia wa China kwa uchunguzi zaidi. Kamanda Paulo alifafanua kuwa gari hilo ni mali ya Kampuni ya ujenzi ya SICU ya jijini Dar es Salaam na lilikuwa linatoka Campu likiwa limebeba wafanyakazi 17 wa kampuni hiyo kuelekea eneo la Sopa na lilipofika kwenye kona liliacha njia na kupinduka.

Hali ya Mjamzito aliyekataliwa Hospitali ya Mwananyamala bado ni tata

HALI ya mwanamke mjamzito ambaye kiumbe chake kimefia tumboni tangu wiki iliyopita, bado ni tete, huku ndugu zake wakijitahidi kutafuta tiba ili kunusuru maisha yake. Akizungumza na Tanzania Daima nyumbani kwao Mwananyamala A, dada mkubwa wa mgonjwa huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake kwa kuogopa kuendelea kukosa ushirikiano kutoka Hospitali ya Mwananyamala, alisema hali ya ndugu yao si nzuri. “Kusema kweli ndugu yetu bado hali yake si nzuri, maana hata hii (leo) jana tumerudi tena Hospitali ya Mwananyamala lakini hakuna tiba tuliyopata,” alieleza. Aliongeza kuwa hata jana walipokwenda na kumtafuta daktari wa wasaidia, aliwaeleza kuwa wasubiri muda wa wiki mbili waliopangiwa awali. Alisema kutokana na majibu hayo, waliamua kurudi nyumbani na mgonjwa huyo huku wakijaribu kuwasiliana na ndugu wengine, ili kutafuta fedha kwa ajili ya kumpeleka katika hospitali binafsi. “Kwa sasa hatuna njia nyingine, kwa muda huu tunajaribu kukusanyana na kufanya kikao ili tumpeleke katika hospitali binafsi, kwani hatuwezi kukaa kwa wiki mbili, kwani hali yake ni mbaya,” alisisitiza.

Wednesday, November 25, 2009

Mama na Mwana


Pichani Madonna na mtoto wake wa kusaili DAVID BANDA walipotemebelea Malawi

Liyumba aendelea Kusota lupango

Aliyekua Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu Tanzania Amatusi Liyumba,akirudishwa rumande,baada ya kesi yake ya matumizi mabaya ya Ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh221 bilioni katika ujenzi wa majengo pacha ya Benki hiyo,kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana

Same bado wafuta machozi

Wananchi wa Kijiji cha Goha wilayani same wakifukua kifusi cha mlima kilichoangukia nyumba wakitafuta mabaki ya vyombo baada ya mlima huo kuangukia nyumba na kuua watu zaidi ya 20 wilayani humo mkoa wa kilimanjaro wiki mbili zilizopita

Utata wa Makusanyo ya mapato Kituo cha Ubungo - Jiji yaiumbua familia ya Kingunge

Makusanyo ya mapato katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (UBT), yameongezeka maradufu, ikiwa ni wiki chache tangu mkataba wa kampuni binafsi inayomilikiwa na familia ya Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru, kumalizika na kazi hiyo kukabidhiwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilianza rasmi kusanya mapato kituoni hapo Novemba Mosi, mwaka huu baada ya kampuni hiyo ya familia ya Kingunge ya Smart Holdings, iliyokuwa imepewa zabuni hiyo kwa zaidi ya miaka mitano kumaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi uliopita. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi, alisema jana kuwa tangu Halmashauri ianze kazi hiyo, imekuwa ikikusanya mapato ya wastani wa Shilingi milioni nne kwa siku. Kingobi aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa katika kikao cha Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam. Kwa hesabu hiyo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa mwezi itakuwa ikikusanya Sh. milioni 120. Awali, kampuni ya Smart Holdings ililalamikiwa kuwa ilikuwa ikikusanya mapato makubwa katika kituo hicho, lakini ikiishia kuilipa serikali fedha kidogo Sh. milioni 1.5 tu kwa siku. Katika makusanyo hayo, kampuni hiyo ilikuwa ikiilipa serikali sh. milioni 46.5 kwa mwezi. Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, kufanya ukaguzi wa hesabu za mapato katika kituo hicho na katika Shirika la Masoko ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam na kisha kuwasilisha ripoti ofisini kwake. Pinda alitoa agizo hilo wakati akizungumza katika kikao cha majumuisho, baada ya ziara yake ya siku tatu, jijini Dar es Salaam, Machi 15, mwaka huu. Katika agizo lake, Pinda alisema bila kujali mmiliki halali wa kampuni hiyo, ukaguzi wa hesabu hizo unapaswa kufanyika kwa maslahi ya umma, kabla ya kuchukua hatua kwa mujibu wa mapendekezo yatakayotolewa na CAG. Katika ziara hiyo, Pinda alishangazwa na kushtushwa na utendaji mbovu wa uongozi wa UBT, mkataba uliofikiwa kati ya kituo hicho na kampuni hiyo na namna ilivyopatikana. Pinda alifikia hali hiyo, baada ya kupewa taarifa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Kingobi, kuhusu hali ya utendaji wa uongozi wa UBT, ukusanyaji wa mapato, mkataba wa mkandarasi na maendeleo ya kituo hicho. Katika taarifa yake, Meneja wa Kituo hicho, Fadhili Izumbe, alisema kwa mujibu wa mkataba, mkandarasi huyo huipa Halmashauri ya Jiji, Sh. milioni 1.5 kwa siku, taarifa iliyomshangaza Pinda na kumfanya ahoji: “Hata kama anakusanya Shilingi bilioni moja anatoa Sh. milioni 1.5? Na kwa nini mkataba utamke shilingi badala ya asilimia?”. Kwa siku mabasi zaidi 400 husafirisha abiria, teksi 100 na watu zaidi ya 2,000 huingia UBT. Pia, kuna maduka ya vinywaji (baa na grosari), maduka ya kawaida, hoteli, ‘vioski’, gereji, ambavyo vyote hulipa ada za viwango mbalimbali. Siku moja baada ya ziara hiyo ya Pinda, mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Smart Holdings, Hassan Khan, alisema viongozi wa Halmashauri ya Jiji waliokuwapo kwenye ziara hiyo, hawajui lo lote na ndio maana walishindwa kumueleza Waziri Mkuu ukweli kuhusu mkataba huo. Khan alisema katika mkataba huo, walikubaliana na Halmashauri ya Jiji kuwa wangekuwa wakiilipa asilimia 75 na kushangazwa kusema asilimia hiyo ni sawa na Sh. milioni 1.5. Alisema katika mkataba huo, pia walikubaliana wawe wanalipa kiasi hicho cha fedha kwa kila siku bila kujali hali ya mapato itakayokuwa na bila kujali pia kuwa siku za mwishoni mwa juma (wikiendi) na wakati madaraja yanapokatika, kampuni yao hupata hasara. Utouh alikabidhi ripoti ya UBT mjini Dodoma, Julai mwaka huu, wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge. Akijibu maswali ya papo kwa papo mwishoni mwa mwezi uliopita bungeni, Pinda alisema ripoti hiyo inapitiwa na Katibu Mkuu wa Tamisemi na yule wa Ofisi ya Waziri Mkuu na kuahidi kuwa itatolewa hadharani baada ya maofisa hao wa serikali kumaliza kazi ya kuipitia. Hata hivyo, kabla Pinda hajatoa kauli hiyo, wiki kadhaa zilizopita, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alidokeza kuwa serikali ingechukua kituo cha Ubungo kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwisho wa mwezi uliopita.

Rihhana akanusha kuwa na mahusiano ya mapenzi ya Jay - Z

Nyota wa muziki wa R&B wa Marekani aliyetamba na nyimbo yake ya "Umbrella" Rihhana ameelezea kuchukizwa na uvumi uliozagaa wakati alipoanza kuwika kwenye anga ya muziki kuwa alimhonga penzi Jay-Z ili ampe tafu kwenye masuala ya kimuziki. Ni kweli kuwa Kipaji changu kilivumbuliwa kwenye visiwa vya Barbados na Jay-Z ambaye na alinipa tafu katika kuandaa albamu yangu ya kwanza.Rihanna anasema kuwa hata marafiki zake wa karibu waliamini kuwa alilala na Jay-Z ili apewe tafu.Rihanna amekanusha uvumi huo na kusema kuwa hakuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na Jay-Z."Uvumi huu ulinifanya nijisikie vibaya wakati wote na nilishindwa hata kumuangalia machoni Jay-Z", alisema Rihanna.

Tuesday, November 24, 2009

Yanga yamtosa Ambani

Mabingwa watetezi Yanga hatimaye jana walitangaza rasmi kumtema mfungaji bora wa Ligi Kuu wa msimu uliopita, Boniface Ambani, na kuhitimisha uvumi uliotawala vyombo vya habari kwa muda mrefu kwamba mshambuliaji huyo kutoka Kenya hana nafasi tena kwenye kikosi cha kocha Mserbia Kostadin Papic. Mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Yanga msimu uliopita akitokea nchini India alikokuwa akicheza soka la kulipwa na kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wake wa pili mfululizo baada ya kuifungia mabao 18, hajafunga goli hata moja msimu huu hadi wakati timu zikienda mapumziko baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Afisa Habari wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema kuwa mchezaji huyo ameachwa kwa sababu ya kushuka kwa kiwango chake cha uchezaji. Mbali ya Ambani aliyebakiza muda wa miezi sita wa katika mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo, wachezaji wengine walioachwa kwa sababu za kushuka kwa viwango vyao huku bado wakiwa na mkataba na Jangwani ni beki mrefu kutoka Kenya Joseph Shikokoti, beki wa kati Hamis Yusuph na Vincent Barnabas aliyeuzwa kwa mkopo kwenye timu ya African Lyon.

Apata Mimba baada ya kufunga kizazi

Mama mmoja anayejulikana kwa jina la Debbie Amos mwenye umri wa miaka 43, mama wa watoto watatu, alifunga kizazi kwa kufanya upasuaji wa kuikata mirija ya kupitisha mayai na kisha kuikunja ili kumfanya asipate mimba tena.Miezi mitatu iliyopita, alishangaa kuona mabadiliko ya tumbo lake na alipofanyiwa uchunguzi aligundulika kuwa na mimba ya miezi sita.Wiki iliyopita ikiwa ni miaka 13 tangia alipofunga kizazi, Debbie alifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike aliyekuwa na uzito wa kilo 3.9."Sikuamini macho yangu, vipimo vilipoonyesha nina mimba, nilikaa chini kwa lisaa limoja nikiwa siamini, bado siamini mpaka sasa".Debbie na mumewe Melvyn mwenye umri wa miaka 57, walikuwa na matatizo ya kupata mtoto baada ya kufunga ndoa.Debbie alianza kutumia madawa ya kusaidia kupata mimba yanayoitwa Clomid wakati huo akiwa na umri wa miaka 19 na madawa hayo yalimsaidia kupata ujauzito wa mtoto wake wa kwanza ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 24.Aliendelea kutumia madawa hayo kwa miaka miwili zaidi na kufanikiwa kupata ujauzito wa mtoto wao wa pili wa kiume ambaye sasa ana umri wa miaka 19.Baada ya hapo waliamua kuwa watoto walionao wanatosha na Debbie aliacha kutumia madawa hayo lakini walishangazwa alipopata ujauzito wa mtoto wa tatu wa kike ambaye sasa ana umri wa miaka 16.Kwa kuhofia kupata watoto zaidi Debbie aliamua kufunga kizazi kwa operesheni ambayo ilifanyika kwenye hospitali kuu ya mji wa Colchester.Miaka 13 ikiwa imepita tangia alipofunga kizazi Debbie na mumewe walishangazwa kugundua kuwa wanatarajia mtoto wa nne."Mirija yangu yote miwili ya mayai ya uzazi ilikatwa na kukunjwa kwa hiyo ilikuwa ni vigumu sana kupata tena mimba", alisema Debbie."Na kwa umri wangu huu nilio nao ilikuwa vigumu zaidi kupata mimba tena".Madaktari walimwambia Debbie kuwa mirija yake ya mayai (fallopian tube) ilijiunda yenyewe tena baada ya kukatwa na hivyo kumfanya apate mimba tena.

Walimu 22 wafukuzwa kwa Ulevi Singida

Walimu 22 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ulevi na utoro kazini. Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na ofisa Elimu wa Wilaya ya Iramba, Leonard Ngaharo, kwenye mkutano wa viongozi uliofanyika katika kijiji cha Mwanga, Tarafa ya Nduguti. Mkutano huo uliitishwa na Mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai. Ngaharo alisema walimu hao wamesimamishwa kazi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ikiwa ni mkakati wa wilaya hiyo kuhakikisha taaluma inayotolewa kwenye shule zake za msingi, inakuwa na ubora unaostahili. Alisema walimu hao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa ya kukiuka mikataba ikiwemo ulevi na utoro kazini. Aidha, Ofisa Elimu huyo alisema ofisi yake itawahamisha walimu wote waliokaa kwenye kituo kimoja kwa muda mrefu ili kuleta ufanisi na upatikanaji elimu bora kwenye shule zake za msingi. Ngaharo alilazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia ombi la kiongozi wa serikali za mitaa kumwomba Msindai asaidie kuwahamisha walimu wa shule ya msingi waliotumika kwa miaka mingi kwenye Kata ya Mwanga. Kwa upande wake, Mbunge huyo aliwataka viongozi wa dini kufanya kazi kwa bidii na kujenga uhusiano mwema kati yao na waumini wanaowaongoza, huku akiiasa jamii kuheshimu mema yote wanayoelekezwa. “Naomba sana waongozeni waumini wenu kwa njia za haki, msikate tamaa na endeleeni kuwahimiza wafanye kazi zaidi, ikiwemo utoaji wa michango ya miradi mbalimbali ya maendeleo…ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu,” alifafanua Msindai. Mbunge huyo alikuwa kwenye ziara katika jimbo lake hususani Kata za Mwanga na Ilunda, ambapo aliwahimiza wananchi kushiriki kwenye miradi ya maendeleo na kutumia vizuri mvua zinazonyesha sasa ili washiriki fursa ya kilimo kwanza.

Busta Asifia Ukarimu wa watanzania

MSANII mkongwe wa Hip Hop kutoka Marekani, Busta Rhymes amesema kuwa ameridhishwa na ukarimu wa Watanzania hali inayomfanya afikirie kuitangaza Tanzania kwa wasanii wenzake wa nje kuja nchini.Busta Rhymes alikuwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mwaliko wa kuwa moja ya wasanii wa kutumbuiza katika tamasha la Fiesta la mwaka huu ililofanyika jumamosi katika viwanja vya Chuo cha Posta.Mara baada ya kupanda jukwaani na kutakiwa azungumze kidogo, Mwanahip hop huyo maarufu duniani alisema "Sikutegemea kuwa Watanzania wanapenda muziki, ni wakarimu, na hii inanifanya niwakumbuke zaidi na zaidi nikirejea Marekani".Alisema, atafanya kila analoliweza kuitangaza Tanzania kimuziki, na hata kuwavutia wanamuziki wenzake wakubwa, wakiwemo 50 Cent na Jay Z kuja kwa ajili ya nyesho, ikiwezekana katika onyesho lijalo la Fiesta.Licha ya msanii huyo kuchelewa kupanda jukwaani, aliweza kutumbuiza zaidi ya saa moja huku akiwa na wasaidizi wake na kuufanya umati uliofika hapo kumshangilia kwa nguvu.Busta alishangiliwa zaidi pale alipoimba vibao vyake ambavyo vimezoeleka katika masikio ya wapenda muziki kama `Make it Clap` na `Arab money'.

Monday, November 23, 2009

Mwanaume aliyepoteza fahamu kwa miaka 23 azinduka

Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Rom Houben mwenye umri wa miaka 46 amezinduka baada ya kupoteza fahamu kwa miaka 23 kutokana na ajali ya gari. Kwa sasa anaweza kusoma meseji na vitabu kupitia chombo maalumu akiwa bado hospitalini. Rom alisema napiga kelele lakini hakuna mtu ambaye anasikia sauti yangu muda wote huu nimekuwa nikiwaza maisha mazuri ila hakuna neno zuri linaloweza kumaanisha furaha yangu niliyonayo" Sitaweza kusahau siku niliyogundua tatizo langu ni sawa na kuzaliwa upya aliongeza Rom. Ninataka kusoma, kuongea na marafiki kupitia Computer na kuinjoi maisha kama mtu wa kawaida na ninafurahi kama ndugu na marafiki wamejua kuwa sijafa

Sisi mabingwa watarajiwa Chalenji atamba Maximo

Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Marcio Maximo, amesema kwamba kikosi chake kitapambana kwa nguvu zote katika mashindano ya Chalenji kwa sababu timu yetu ni miongoni mwa mabingwa watarajiwa. Maximo alisema kati ya nchi 12 zinazoshiriki mashindano hao, ni nchi sita tu ndio zenye uwezo wa kuibuka mabingwa na kwamba wengine "ni wasindikizaji". Alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na mabingwa watetezi, Uganda, Kilimanjaro Stars, Kenya, Rwanda, Zambia na Zimbabwe. Hata hivyo, Maximo ameonya kuwa Watanzania wasitarajie miujiza kwa sababu lolote linaweza kutokea katika soka. Maximo akiongea na vyombo vya habari juzi wakati timu yake ikiendelea na mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza Jumamosi hii nchini Kenya, kwamba mashabiki na wadau watarajie matokeo mazuri lakini sio miujiza. Alisema kwamba matokeo mabaya katika mechi tatu za kirafiki za kimataifa walizocheza hivi karibuni, yameamsha morari kwa vijana wake ambao wameahidi kucheza kufa na kupona. "Kila mmoja anafahamu nini anatakiwa kukifanya, na nawajenga wajiamini kwamba wanaweza. Nafikiri, kama hatutamaliza mashindano tukiwa washindi wa tatu, basi tutafanya vizuri zaidi ya hapo," alisema Maximo.

Mtoto wa ajabu azaliwa - LINDI

Mkazi mmoja wa Mtaa wa Rupiani katika Halmashauri ya Mji wa Lindi na ambaye hufahamika kwa jina la Salima Ally, 38, amejifungua mtoto wa ajabu na kuzua gumzo la aina yake kwa madokta na wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Lindi. Mtoto huyo ambaye ni wa kike, amekuwa gumzo kwani licha ya kuzaliwa na afya njema na uzito wake wa kilo 3.2, imebainika kuwa hana macho wala pua. Aidha, mtoto huyo ana mdomo wenye mpasuko mkubwa kiasi cha kumfanya ashindwe kunyonya mwenyewe, huku kwenye paji la uso akiwa na uvimbe usio wa kawaida. Mtoto huyo alizaliwa jana, mishale ya saa 11:30 asubuhi katika hospitali hiyo ya mkoa wa Lindi iitwayo Sokoine. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hospitalini hapo, Afisa Muuguzi wa zamu katika wodi hiyo ya wazazi namba nne aitwaye Bi. Zuhura Namkovera, amesema mtoto huyo alizaliwa salama lakini kinachosikitisha ni kwamba hadi sasa, maumbile yake ya ajabu yamemfanya aishi kwa shida mno. “Tangu azaliwe, mtoto huyu tumekuwa tukimnywesha maji, tena huwa anakunywa kwa shida sana kutokana na maumbile ya mdomo wake, ” amesema muuguzi huyo. Akieleza zaidi, Muuguzi huyo akasema kuwa huo ni uzazi wa sita wa mama huyo kwa mume aliyenaye. "Maendeleo ya afya ya mama (Bi. Salma) yanaendelea vizuri… na mtoto wake pia anaendelea vizuri, licha ya kwamba hajaanza kunyonya mwenyewe maziwa ya mama yake,” akasema Bi. Zuhura . Naye mganga aliyekuwa zamu katika hospitali hiyo, Dokta Jumanne Shija, amesema kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha hali hiyo, ikiwa ni pamoja na mama kuwahi kuathiriwa na magonjwa mbalimbali. “Ila mambo mengine yanakuwa ni maumbile tu… ni baada ya baadhi ya vichocheo vya mwili kushindwa kufanya kazi yake,” akasema Dk. Shija.

Wananchi Newala wazuia Msafara wa Waziri Mkuu

MSAFARA wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ulisimamishwa njiani baada ya wakazi wa kijiji cha Mkunya wilayani Newala, Mtwara, kuziba njia wakiwa na mabango wakitaka waziri huyo asimame asiendelee na safari zake awasikilize kwa dakika kadhaa. Tukio hilo lilitokea Jumamosi majira ya mchana wakati Pinda akielekea kwenye bonde la mto Ruvuma kukagua kituo cha maji cha Mkunya na kupokea taarifa ya kilimo cha umwagiliaji kwenye bonde la mto Ruvuma katika ziara yake.Mara baada ya kufika njiani hapo msafara huo ulikuta njia imefungwa na wananchi wakwia wamekaa kando ya barabara, na hatimaye Waziri Mkuu aliteremka kutoka kwenye gari yake na kuwasikiliza wananchi hao.Katika mazungumzo yao wakazi hao walisema wana kero ya kutopata maji safi na salama, kutolipwa malipo ya korosho na kutopatiwa pembejeo za ruzuku lakini uongozi wa wilaya umekuwa ukiwapuuza na kuficha taarifa badala ya kuwasaidia.Walisema kwamba tatizo la uhaba wa maji katika eneo lao limedumu kwa zaidi ya miaka 15 jambo ambalo linawafanya watumie muda mwingi kusaka maji badala ya kuutumia muda huo kwenye kilimo.Kuhusu mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani, wakazi hao walisema hawautaki kwa sababu hawalipwi fedha zote za Sh. 700 kwa kila kilo kama walivyoahidiwa.Pia waliiomba Serikali iwasaidie kuwapatia pembejeo na mbolea za ruzuku kwani bei ni kubwa na wengi wanashindwa kuzimudu.Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwaahidi wakazi hao kuwa kabla hajaondoka, atakuwa amepata ufumbuzi wa matatizo hayo na kukutana na wahusika mara moja.Kuhusu mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani, Waziri Mkuu alisema hauna tatizo ila una kasoro ambazo itabidi ziangaliwe upya na kumtaka Mkuu wa Mkoa huo, Kanali (mstaafu) Anatory Tarimo, kujipanga upya na kusambaza elimu ya mfumo huo kwa wakulima.Kuhusu pembejeo za ruzuku, Pinda alisema atahakikisha anafuatilia suala hilo ili katika mwaka wa fedha ujao, mikoa ya Lindi na Mtwara iingizwe katika programu hiyo.

Shoga aliyeleta Kizaazaa Italia Achomwa Moto na Kufa

Shoga wa kibrazili aliyesababisha maafisa wanne wa polisi nchini Italia kutiwa mbaroni na gavana wa mji wa Lazio kujiuzulu amefariki kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba yake. Shoga raia wa Brazili mkazi wa Italia ambaye alihusika katika skendo la ngono la nchini Italia ambalo lilisababisha gavana wa jiji la Lazio kujiuzulu, amefariki kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba yake katika mji wa Roma.Vyombo vya habari vya Italia, viliripoti kuwa chupa ya pombe kali aina ya whisky ilikutwa pembeni ya mwili wa shoga huyo aliyejulikana kwa jina la Brenda.Gavana wa Lazio, Piero Marrazzo, alijiuzulu nafasi yake mwezi uliopita baada ya video ya ngono akijivinjari na shoga huyo kuvuja kwenye vyombo vya habari.Mwanzoni mwa mwezi huu, Brenda aliwaita polisi na kutoa taarifa kuwa ameshambuliwa na kuporwa mali zake mtaani.Brenda na shoga mwingine wa kibrazili aliyejulikana kama Natalie walihusika kwenye skendo la ngono lililopelekea gavana Marrazzo ajiuzulu.Polisi wanne waliochukua video kwa siri wakati gavana huyo akijivinjari na mashoga hao, walijaribu kujipatia pesa toka kwa gavana huyo kwa kutishia kuiweka hadharani video hiyo lakini walikamatwa na kutiwa mbaroni.Gavana Marrazzo alijiuzulu huku akikiri kuwa na uhusiano na mashoga wanaofanya uhakaba.Mwanasheria wa gavana huyo amewataka polisi kumpa ulinzi shoga Natalie ili na yeye yasije yakamkuta kama yaliyomkuta rafiki yake.


Aliyemuua Mkewe akiwa Usingizini aachiwa huru

Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye alimyonga mkewe usingizini wakati alipoota ndoto anapigana na wezi, ameachiwa huru na mahakama. Brian Thomas, 59, aliota ndoto mwizi ameingia kwenye gari lao wakati alipokuwa amelala na mkewe usiku kwenye gari hilo, alimuua mkewe kwa kumkaba koo kwa nguvu akidhania anapigana na mwizi.Aliamka asubuhi na kugundua amemuua mke wake Christine Thomas na kuamua kuwapigia simu polisi ambapo alikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa kosa la mauaji.Akitoa hukumu jaji wa kesi hiyo alisema kwamba Brian alikuwa mume mwaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa mkewe na alikuwa hajijui wakati alipokuwa akifanya kitendo hicho.Mahakama iliambiwa kuwa hali aliyokuwa nayo Brian imewahi kuwatokea watu 50 tu dunia nzima.Brian alimnyonga mkewe usingizini mwezi julai mwaka jana wakati walipokuwa kwenye Mapumziko katika mji wa Aberporth, Wales.

Mahujaji 4 wafariki kwa mafua ya Nguruwe

Mahujaji wanne waliokuwa nchini Saudi Arabia kuungana na mamilioni ya mahujaji toka nchi mbali mbali duniani kwaajili ya hija kubwa, wamefariki dunia kutokana na mafua ya nguruwe.
Mwanaume mmoja toka India, mwanamke mmoja toka Morocco na mwanaume mwingine toka Sudan wote wenye umri zaidi ya miaka 75 pamoja na msichana mwenye umri wa miaka 17 toka Nigeria wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe walioambukizwa wakati wa hija."Wote walikuwa na matatizo mbali mbali ya kiafya kabla ya kukumbwa na mafua ya nguruwe, msichana wa Kinigeria alikuwa na matatizo ya kifua", alisema msemaji wa wizara ya afya ya Saudia, Khaled al-Marghlani."Pia hakuna hata mmoja wao aliyepiga sindano ya chanjo ya ugonjwa wa mafua ya nguruwe", aliongeza msemaji huyo wa wizara ya afya.Takribani waislamu milioni 2.5 wanatarajiwa kuhudhuria hija ya mwaka huu, ukiwa ni mkusanyiko mkubwa kuliko wote wa watu tangia ugonjwa wa mafua ya nguruwe ulipogunduliwa nchini Mexico mwezi aprili mwaka huu.Watu 20 wamegundulika kuambukizwa mafua ya nguruwe tangia hija zilipoanza katika miji ya Makka na Madina na 12 kati yao walipatiwa matibabu na kutolewa hospitali wakati watu wanne bado wamelazwa hospitali.Wataalamu wa masuala ya afya wamesema kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yamekuwa katika kiwango kidogo sana kuliko ilivyohofiwa kutokana na tahadhari zilizochukuliwa.Wataalamu wa afya 20,000 wamepelekwa kwenye miji ya Makka, Madina na Jeddah kuwa tayari tayari kupokea watu watakaoambukizwa ugonjwa huo huku hospitali zimewekwa mamia ya vitanda vya ziada.Mawe yatakayotumika kuipiga alama ya shetani wakati wa hija, nayo yamewekwa madawa kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.Watu wenye magonjwa sugu, wazee sana, watoto na wanawake wenye mimba wametakiwa kuahirisha safari zao za hija mwaka huu.

Thursday, November 19, 2009

Zoezi la kuchunguza chanzo cha maafa Same lasitishwa

Mbunge wa Same Mashariki,Anna Kilango Malecela akilia kwa uchungu huku akiwa amekalia sehemu ya kifusi kilichosababishwa na kuporomoka kwa mlima na kusababisha vifo vya wananchi wake wa kijiji cha Goha.

Sina mpango wa kugombea urais 2010 - Dr. Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, amevunja ukimya na kueleza kuwa hafikirii kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Dk Slaa ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Karatu, alisema "Ikulu si mahali pazuri kukimbilia na urais si mchezo wa kitoto." Alisema wakati alipojiundoa katika upadre na kujitumbukiza katika ulimwengu wa kawaida, aliahidi kuwatumikia wananchi wa Karatu na si kutafuta njia ya kuingia Ikulu, ambako alisema kuna matatizo mengi yanayoweza kumfanya mtu kukosa usingizi. Unajua Ikulu si lele mama, kunahitaji mtu mvumilivu hasa wananchi wake wanapohangaika na ugumu wa maisha ya kila siku, jambo ambalo linaweza kumfanya ashindwe kupata usingizi, kwa sababu ya mawazo,alisema Dk Slaa. Alisema kama mtu anataka kugombea nafasi hiyo anapaswa kukumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtu anayekimbilia Ikulu anapaswa kuogopwa kama ukoma. Alisema mtu wa aina hiyo mara nyingi anakusukumwa na maslahi binafsi kuliko maendeleo ya watu. Dk Slaa alisema maendeleo yanapatikana bila ya hata kuingia ikulu na kwamba la msingi ni viongozi kujipanga katika kupigania maendeleo ya wananchi. Alisema mkakati wake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Karatu wananufaika na uongozi wake kwa kuwatafutia maendeleo na kuwaondolea kero kama ya maji na kadhalika. Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi kwa Dk Slaa ana mpango wa kuwania kiti cha urais kupitia tiketi ya Chadema. Kwa mujibu wa habari hizo, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hana mpango wa kuwania tena nafasi hiyo na badala yake anakwenda kuwania ubunge katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.

Baba wa kijana Aliyedai Amebakwa na Michael Jackson Ajiua

Baba wa kijana Jordy Chandler ambaye alilipwa dola milioni 20 baada ya kudai Michael Jackson amembaka, amejiua mwenyewe kwa kujipiga risasi ya kichwa. Evan Chandler mwenye umri wa miaka 65 ambaye ni baba wa kijana Jordy Chandler ambaye alidai amebakwa na Michael Jackson, amejiua mwenyewe kwa kujipiga risasi.Evan na mwanae walilipwa dola milioni 20 na marehemu Michael Jackson ili kuimaliza kesi hiyo nje ya mahakama.Evan ambaye alikuwa ni daktari wa meno, alikutwa amefariki kwenye nyumba yake iliyopo New Jersey akiwa na jeraha la risasi kichwani mwake.Polisi walitoa taarifa baadae wakisema kuwa wanaamini Evans alijiua mwenyewe kwakuwa alikutwa akiwa ameishikilia bunduki ambayo aliitumia kujiua.Mwaka 1993, Evans alimfungulia mashtaka Michael Jackson kwa niaba ya mwanae ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 13.Evans alimtuhumu Michael Jackson kumbaka mwanae, na ilimbidi Michael Jackson atoe dola milioni 20 kuimaliza kesi hiyo nje ya mahakama.Pamoja na kukubali kutoa kiasi hicho cha fedha, Michael Jackson aliendelea kukanusha kufanya kitendo chochote kibaya kwa mtoto huyo.Baada ya kukabidhiwa pesa hizo, Evan na mwanae walifarakana na kila mtu alienda kuanza maisha yake kivyake kivyake.

Dunia Imefika mwisho - Mchungaji Kortin Singida kwa kubaka

POLISI mkoani Singida linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wa Usharika wa Igengu katika Dayosisi ya Kati, kwa tuhuma ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 18 na kumtelekeza . Ilidaiwa msichana huyo (jina kapuni) alibakwa na mchungaji huyo na kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Celina Kaluba, alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Japhet Kidindima (37) mkazi wa wilayani Iramba mkoani humo.Kamanda Kaluba alisema kuwa tukio hilo lilitokea Jumatatu ya wiki hii, katika majira ya saa 9:45 alasiri, kwenye vichaka vilivyopo kati ya vijiji vya Igengu na Ibaga katika tarafa ya Kirumi, wilayani Iramba.Kamanda Kaluba alisema kuwa, mtuhumiwa huyo alifanikisha njama zake za ubakaji baada ya kumdanganya msichana huyo kuwa anataka kumtafutia kazi za ndani jijini Dar es Salaam.Kamanda alisema licha ya kumuahidi kumtafutia ajira, pia Mchungaji huyo alimuahidi msichana kuyo kumsafirisha hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kufanya kazi hiyo.Alisema kuwa safari ya kwenda kijiji jirani cha Ibaga ilianza kwa miguu ambako ndipo ulipo usafiri wa basi, lakini walipofika katikati ya vijiji hivyo, Mchungaji Kidindima alimbaka msichana huyo kwenye vichaka.Alifafanua kuwa baada ya kumbaka, waliendelea na safari yao hadi kwenye kituo cha mabasi kilichopo kijiji cha Ibaga na hapo ndipo mtuhumiwa alifanikiwa kumtelekeza msichana huyo akiwa haelewi cha kufanya.Kamanda Kaluba alisema kuwa baadaye msichana huyo aliamua kuripoti tukio hilo katika kituo cha polisi kilichopo katika kijiji cha Ibaga kesho yake saa 7:30 mchana na jitihada za polisi kumsaka mtuhumiwa huyo zilianza.Alisema polisi walifanikiwa kumkamata Mchungaji Kidindima jana, majira ya saa tano asubuhi wakati akiwa masomoni kwenye chuo cha Biblia mjini Kiomboi.Hatua za awali zinachukuliwa ili mchungaji huyo aweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhmu hizo za ubakaji na kutelekeza binti huyo vichakani.

Kuweni makini na Urembo wa Madukani

Mwanafunzi mmoja wa kike wa nchini Uingereza ameharibika sura yake kabisa baada ya kutumia dawa ya kuzibadilisha rangi nywele zake ziwe nyeusi.Abigail Colbourne mwenye umri wa miaka 15, alitumia dawa za kupaka za kubadilisha rangi ya nywele kuwa nyeusi za kampuni ya Clairol ili kuzifanya nywele zake ziwe nyeusi lakini ghafla sura yake ilianza kuvimba na macho yake yalivimba kiasi cha kushindwa kuona.Sura yake iliharibika kabisa kiasi cha kushindwa kutambulika.Akiongea na gazeti la The Sun la Uingereza Abigail alisema "Macho yangu yalifunga kutokana na jinsi yalivyovimba na kichwa changu pia kilivimba... nilikuwa natisha sana".Abigail ambaye ni mkazi wa London alisema kwamba alishindwa kufanya vipimo vya aleji kabla ya kujipaka dawa hizo kama ilivyoshauriwa kwenye paketi ya dawa hizo.Aliwahishwa hospitali ambako alipatiwa matibabu na uvimbe huo kupungua kidogo. Bado anaendelea na matibabu ya kuirudisha sura yake katika hali yake ya awali.Mama yake Abigail, Joanna Leech alisema kuwa tukio hilo la kusikitisha lililompata mwanae liwe fundisho kwa wengine wanaotumia dawa kama hizo.

Monday, November 16, 2009

FIFA yamfungia Maradona Miezi miwili

Kocha wa Argentina Diego Maradona amepigwa marufuku kujishughulisha na shughuli zozote zinazohusiana na masuala ya soka kwa kipindi cha miezi miwili. Diego Maradona amepigwa faini ya faranga 25,000 za Uswizi (Takribani Tsh. Milioni 30) na kutakiwa akae mbali na shughuli za soka kwa miezi miwili kutokana na maneno yake ya kashfa aliyoyatoa kwa waandishi wa habari waliokuwa wakimkosoa kufanya vibaya kwa timu ya taifa ya Argentina kwenye michuano ya awali ya kuwania nafasi ya kushiriki kombe la dunia mwakani nchini Afrika Kusini.Hata hivyo Argentina ilifanikiwa kupata nafasi ya kuja barani Afrika mwakani baada ya kushinda mechi yao ya mwisho katika kundi la Amerika kusini.Hukumu hiyo ya Fifa ilitolewa mjini Zurich Uswizi na Fifa ilisema kuwa adhabu hiyo ya Maradona inaanzia novemba 15 mwaka huu hadi januari 15 mwaka 2010.Kutokana na adhabu hiyo Maradona atazikosa sherehe za mwezi januari mwakani ambapo makundi ya kombe la dunia yatapangwa.Maradona aliwasili Zurich kusikiliza kesi yake hiyo akitokea nchini Hispania ambako Argentina ilibamizwa na Hispania mabao 2-1 siku ya jumamosi.Maradona aliondoka kwenye kikao hicho cha FIFA bila kuzungumza na vyombo vya habari lakini aliomba radhi wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake kwa kitendo chake cha kuwatukana waandishi wa habari.

Auwawa kikatili na Mumewe kisa kutakaa kuokota EMBE usiku

MSICHANA Khadija Daudi (22), mkazi wa Mbagala Charambe aliuawa kikatili na mumewe kwa kuchomwa na kisu mgongoni kwa kile kilichodaiwa kuwa ni baada ya kukataa kuamka usiku kwenda kuokota embe. Tukio hilo la kusikitisha lilitoka mwishoni mwa wiki huko Mbagala jijini Dar es Salaam.Ilidaiwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni mume wa msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Shariff Kondo alimuamsha marehemu kumtaka aende nje ya nyumba yao majira ya saa kumi kasoro usiku, aende akaokote embe lakini marehemu aligoma na kudai kwa kuwa ni usiku asingeweza kwenda nje kufanya kazi hiyo.Inadaiwa kuwa kutokana na majibu hayo mumewe alikasirika na ndipo alipochukua kisu na kumchoma nacho mgongoni.Baada ya kuchomwa kisu hicho alipiga kelele na majirani walijitokeza kumpa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Temeke huku akiwaambia kilichomtokea kwa mumewe huyo.Kwa bahati mbaya msichana huyo alipoteza fahamu na kufariki mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo.Wakithibitisha tukio hilo baadhi ya majirani wa marehemu huyo, wamedai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada katika chumba cha mpangaji mwenzao na mara baada ya kuingia ndani kwake kujua kilichotokea ndipo walipokuta kitanda chake kimelowa damu na huku akiugulia maumivu.Majirani hao wamesema kutokana na hali hiyo walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na baadhi yao walijaribu kumtafuta mumewe lakini hakupatikana ndipo walipokwenda kumwamsha baba mzazi wa msichana huyo anayeishi Charambe na kumuelezea yaliyompata binti yake.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabasi, amesema kuwa, tayari mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo tayari ameshakamatwa yuko katika kituo cha polisi cha Chan’gombe na anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Friday, November 13, 2009

Mtandao wa wezi wa Magari wakamatwa Dar

MTANDAO mkubwa wa wezi wa magari uliokuwa ukiongozwa na mwanamke mwenye asili ya Mnyarwanda umekamatwa.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema, mtandao huo ulinaswa na polisi wanaoendesha msako mkali kuwasaka wahalifu hao kote nchini.Amesema mtandao huo ulikuwa ukiongozwa na mwanamke Meritha Mwanahawa (20), ambaye katika kumbukumbu zake imeonesha kuwa ni bingwa wa kuwalaghai wanaume kimapenzi ambapo huenda kufanya nao mapenzi kisha kuwanywesha dawa za kulevya na kuwaibia funguo na kutoweka na magari yao.Amesema kuwa kumbukumbu za magari mengi yaliyoibwa zimeonyesha kuwa msichana huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na baadhi ya madereva hao ambaod wealikiri wenyewe.Wengine walionaswa katika mtandao huo ni pamoja na Hamis Fumu (37), Arafat Juma (34), Samwel Mwamba (19), Yasmin Chuchu (20), Antipasi Kilawe (28) na Elias Moses (35).Kamanda Kova amesema kuwa jeshi lake bado linaendelea na msako mkali na litawafikisha mahakamani watuhumiwa baada ya upelelezi kukamilika.

Tyson Matatani kwa kumpiga Mpiga Picha ngumi ya uso na kumpasua

Polisi nchini Marekani wamesema kuwa bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu, Mike Tyson na mpiga picha mmoja wamefunguliana mashtaka kila mmoja baada ya ugomvi uliozuka kwenye uwanja wa ndege wa Los Angeles International Airport.Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Mike Tyson alikuwa safarini kuelekea Las Vegas kwa kupitia uwanja wa ndege huo akiwa pamoja na binti yake mwenye umri wa miezi 10 na mkewe wakati tukio hilo lilipotokea.Taarifa zinasema kuwa Tyson na paparazzi huyo walirushiana ngumi lakini alikuwa ni Mike Tyson aliyempachika ngumi moja mpiga picha huyo iliyompeleka moja kwa moja chini na kumpasua sehemu ya juu ya uso wake.Mpiga picha huyo alipelekwa hospitali kupatiwa matibabu kwa majeraha aliyopata kufuatia kipigo alichokitafuta mwenyewe kwa kumghasi mbabe huyo wa zamani wa uzito wa juu.Alishonwa nyuzi tano katika sehemu yake ya juu ya uso wake iliyopasuliwa kwa ngumi nzito ya Tyson.Mike Tyson alikamatwa baada ya tukio hilo na kutupwa selo kwa muda kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000.

Mbwa wahitajika zoezi la kutafuta Miili ya waliopoteza maisha Same

BAADA ya zoezi la kukamilika kwa kuzikwa kwa miili 20 iliyopatikana kwa kufunikwa na mlima, Serikali imeombwa kupeleka mbwa wa kunusa ili kusaidia kutafuta maiti nyingine ambao hazijapatikana. Inadaiwa kuwa maiti nyingine zaidi ya tano bado hazijapatikana na zoezi hilo kuwa gumu kwa kuwa maiti hizo zilifunikwa na tope baada yam lima huo kuporomoka.Jumla ya nyumba saba zilifunikwa katika maporomoko hayo na watu wote waliokuwamo katika nyumba hizo usiku wa manane wa kuamkia juzi walikufa.Ombi la kuomba kikosi cha mbwa, lilitolewa jana na Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa maelezo kwamba, juhudi pekee za wananchi hazitafanikiwa kupata miili iliyosalia bila kuopolewa. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega, aliwataka wananchi kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari kwa hali yoyote isiyokuwa ya kawaida katika eneo hilo na kuripoti maramoja.Katika tukio hilo walioopolewa kati yao kulikuwa na mama wajawazito wawili na miili ya vichanga hivyo vilitolewa tumboni mwa mama zao na kuzikwa tofauti, ambapo mama mmoja aliyefariki alishatimiza mimba ya miezi tisa.Maiti zilizotambuliwa na kuzikwa ni pamoja na Neema Shambi (70), Napenda Bakari (7), Namsemba Bakari (11), Sikudhani Elitabu (20), Nath John (12), Haika Charles (3) na Mariam Juma (4), Wemaeli Mhina (30), Ruth Mhina (6), Neema Bakari (8) na Christina Kiondo (32).Mingine ni Elitabu Shambi (30), Shambi Elineema (11), Ndimangwa Elineema (5), Amani Mhina (9), Kiondo Amani (37), Imani Kiondo (9) na Nikundiwe Kiondo (5), wote wakazi wa Goha.

Wednesday, November 11, 2009

Hatimaje Elizabeth kutua Dar Leo

Aliyekuwa mshiriki wa Tanzania kwenye Jumba la Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta ‘Queen’ anadaiwa kuwa ni mgonjwa na hiyo ndiyo sababu iliyomfanya atolewe mapema kwenye jumba hilo

Msiba mzito Same

Watu ambao idadi yao haijafahamika inasemekana wamepoteza maisha katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo katika jimbo linaloongozwa na Mheshimiwa Anne Kilango Malecela. Msiba huo umetokea baada ya mlima mmoja kumeguka na kufunika zaidi ya nyumba saba na inadaiwa watu wote waliokuwa wamelala ndani, wamepoteza maisha. Tukio hilo limetokea majira ya saa 7:00 usiku katika kata ya Miamba kitongoji cha Manka wilayani Same. Akizungumza na vyombo vya habari kwa njia ya simu leo asubuhi, Mbunge wa Same Mashariki, Mhe. Anne Kilango Malecela amesema chanzo cha maafa hayo ni mvua zilizonyesha mfululizo kwa siku tatu na kusababisha mlima kumeguka. "Mvua kubwa zimekuwa zikinyesha kwa siku tatu mfululizo, mbaya zaidi zinanyesha usiku tu, hali hiyo imesababisha udongo na miamba kumeguka na kufunika nyumba saba katika kitongoji cha Manka, huku watu wakiwa wamelala ndani, katika famila hizo hakuna aliyekwishaokolewa akiwa hai hadi sasa," amesema Mhe. Kilango. Kwa mujibu wa Mhe. Kilango hadi sasa miili kumi na moja imeshatolewa chini ya kifusi na juhudi zinaendelea. Hata hivyo amesema hali ya uokoaji nayo inakuwa ngumu kutokana na wapiga kura wake hao kuishi milimani ambako sio rahisi kufikika kirahisi na vyombo vya uokoaji. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'oboko amethibitisha kutokea kwa maafa hayo lakini hakutoa taarifa zaidi kwa madai kuwa alikuwa njiani kuelekea eneo la tukio. "Hapa nilipo niko njiani kwenda eneo la tukio huko Same Mashariki, taarifa zaidi nitatoa baadaye baada ya kufika na kuona madhara yaliyotokea," amesema Kamanda Ng'oboko.

Ahudhuria mazishi yake

Jamaa mmoja nchini Brazili ambaye alisemekana kuwa amefariki kwenye ajali mbaya ya magari, aliwashtua familia yake na waombelezaji wakati alipojitokeza makaburini wakati mazishi yake yakiendelea. Ademir Jorge Goncalves mwenye umri wa miaka 59 alitangazwa amefariki baada ya ndugu zake kuitambua maiti yake katika ajali mbaya sana ya magari katika jimbo la Parana nchini Brazili, taarifa ya polisi ilisema.Kama zilivyo taratibu za kitamaduni, mazishi yake yalifanyika siku iliyofuatia siku ambayo pia ilikuwa ni siku wabrazili hutembelea makaburi yao kuwakumbuka ndugu zao.Kitu ambacho familia yake haikujua ni kuwa, Goncalves alitumia usiku mzima kwenye maegesho ya malori akinywa pombe ya miwa inayoitwa "Cachaca" akiwa pamoja na marafiki zake.Goncalves hakusikia chochote kuhusiana na habari za kifo chake na alikuja kugundua asubuhi wakati huo waombelezaji wakiwa wameishalibeba jeneza kwenda kuzika na wakiwa wameishafika makaburini.Ilimbidi awahi makaburini kuwafahamisha familia yake kuwa yeye hajafa bado yupo hai, alisema msemaji wa polisi katika mji wa Santo Antonio da Platina."Maiti ya mwanaume aliyefariki katika ajali hiyo ilikuwa imeharibika vibaya sana lakini alikuwa amevaa nguo kama za Goncalves na hivyo kuifanya familia yake kuamini ndio yeye", aliendelea kusema msemaji huyo wa polisi."Watu wanaogopa kuangalia maiti kwa muda mrefu wakati wa kuzitambua maiti za ndugu zao na ndio sababu hali kama hii imetokea".Binamu wa Goncalves alisema kwamba baadhi ya ndugu wa familia yake waliitilia shaka maiti hiyo kama ni ya Goncalves lakini baada ya ndugu wengi kusisitiza ni maiti yake, taratibu za mazishi ziliendelea.Mazishi hayo hayakuendelea tena na ilibidi warudi nyumbani na kuwapa taarifa polisi ambapo maiti hiyo ilitambuliwa baadae kuwa ni ya mwanaume mwingine na ilizikwa jumatatu katika jimbo jingine.

Akata nyeti za baba yake wa kambo na kuzichoma moto

Brigitte Harris ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 29, alikuwa akinyanyaswa kijinsia na kubakwa na baba yake wa kambo Eric Goodridge tangia alipokuwa na umri wa miaka mitatu.Kwa kuhofia ataendeleza tabia yake hiyo kwa mabinamu zake wadogo na akiwa na dhamira ya kulipa kisasi, alimpiga kwa kitu kizito kichwani baba yake huyo wa kambo aliyekuwa na umri wa miaka 55 na kupelekea apoteze fahamu.Brigitte alimshindilia taulo mdomoni na kisha kuukata uume wake kwa kutumia kisu kikali na kukinyofoa kabisa kipande kikubwa cha uume wake.Ili kuhakikisha madaktari hawataweza kukiunga tena kipande hicho cha uume wake alichokinyofoa, alikiweka kwenye jiko na kukichoma moto.Baada ya kuhakikisha kimeteketea kwa moto, alipiga simu hospitali kuita ambulansi lakini mpaka watu wa ambulansi walipofika, Goodridge alikuwa ameishafariki kwa kukosa pumzi.Brigitte mkazi wa New York, alishikiliwa na polisi tangia alipofanya mauaji hayo mwaka 2007.Akitoa hukumu ya kesi hiyo, jaji Arthur J Cooperman alimhukumu Brigitte kwenda jela kwa mauaji aliyofanya ingawa baadhi ya watetezi wake walikuwa na imani angeachiwa huru.Jaji Arthur aliagiza Brigitte atumikie kifungo kisichopungua miaka mitano na kisichozidi miaka 15.Brigitte amepanga kukata rufaa.

Golikipa wa timu ya Taifa ya Ujerumani ajiua

Golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Ujerumani na timu ya Hannover inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Robert Enke amefariki dunia jana jumanne baada ya kugongwa na treni wakati aliposimama kwenye reli mbele ya treni lililokuwa kwenye spidi ya kilomita 160 kwa saa.Enke aliyekuwa na umri wa miaka 32 alifariki kwenye eneo la tukio ambalo haliko mbali na nyumba yake.Madereva wawili wa treni lililomgonga walisema kwamba walishangaa kumuona mtu akiwa amesimama kwenye reli mbele yao wakati treni likiwa spidi, walijaribu kufunga breki bila mafanikio.Rais wa timu ya Hannover, Martin Kind alielezea kusikitishwa kwake na habari za kufariki kwa golikipa wa timu yake ambaye alikuwa akitegemewa kulilinda lango la Ujerumani kwenye fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwakani.Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew na meneja wa timu ya taifa Oliver Bierhoff walisema "Tumeshtushwa sana, hatuna la kusema".Mtoto wa kike wa Enke aliyekuwa na umri wa miaka miwili alifariki miaka miwili iliyopita na mwezi mei mwaka huu Enke na mkewe walijitolea kumchukua na kumlea mtoto wa kike mwenye umri wa miezi miwili.Enke alipewa jezi namba moja ya Ujerumani baada ya kipa mkongwe wa Ujerumani Jens Lehmann kustaafu baada ya kombe la Euro 2008.Enke, alizaliwa katika mji wa Jena na wakati wa uhai wake alizichezea timu za Borussia Moenchengladbach ya Ujerumani, Benfica ya Ureno, Barcelona ya Hispania, Fenerbahce ya Uturuki na Tenerife ya Hispania.

Umeshawahi kuona keki ya Kuachana(Divorce keki)?


Tuesday, November 10, 2009

Kuweni makini na Mapenzi ya kwenye Mtandao

Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza amebatizwa jina la 'Speminator' baada ya kuwapachika ujauzito wanawake 12 aliofahamiana nao kwenye mtandao wa Facebook wawili kati yao aliwapachika mimba ndani ya usiku mmoja. Wanawake nchini Uingereza wanaotumia mtandao wa tovuti ya Facebook wameshauriwa kutofanya urafiki na Dominic Baronet, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni hatari sana katika kuwalaghai na kuwapachika ujauzito wanawake anaofahamiana nao kupitia mtandao wa Facebook.Katika kuthibitisha kuwa Dominic ni hatari sana kwa kuwapachika mimba wanawake, aliwapachika mimba wanawake wawili ndani ya usiku mmoja na kulifanya gazeti la News of The World la Uingereza limbatize jina la "Sperminator".Dominic hutumia siku chache kufanikiwa kuwalaghai wanawake anaofahamiana nao kwenye Facebook na kisha kufanya nao mapenzi.Wanawake watano tayari wameishajifungua watoto wake, wanawake watano wengine wanafikiria kuzitoa mimba zao na wanawake wawili wanatarajia kujifungua watoto wake hivi karibuni.Miongoni mwa wanawake waliokumbana na zahama la Dominic ni Kerry Martin, 24, ambaye aligundua kuwa Dominic ana wapenzi wengi baada ya kutembelea ukurasa wake kwenye Facebook na kukutana na ujumbe wa Baronet akijipongeza kumpachika ujauzito mwanamke mwingine aliyejulikana kama Stacy Jones mwenye umri wa miaka 24.Kerry alipounda urafiki na Stacy aligundua kuwa wote wawili walipata ujauzito siku moja ndani ya usiku mmoja isipokuwa nyakati tofauti."Dominic inabidi apigwe marufuku kwenye Facebook, anatumia tovuti ya Facebook kuwalaghai wanawake na kuwapachika mimba na kisha kuwatelekeza bila ya kujali matokeo yake", Stacy aliliambia gazeti la News of the World.Stacy ameutaka uongozi wa Facebook umfute Dominic kwenye mtandao huo na umpige marufuku kujiunga tena.

Thursday, November 5, 2009

Mbatia aibuka na kusema "Takukuru, Wabunge wote ni WAFISADI"

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR -Mageuzi, James Mbatia, amesema malumbano kati ya Bunge na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) yanatokana na ufisadi uliopo pande zote mbili. Mbatia alisema tafsiri ya malumbano baina ya Takukuru na Bunge, inaonyesha kuwa pande zote mbili zinatafutana nani fisadi zaidi ya mwingine. Alisema hali hiyo imetokana na nchi kuwa na mfumo mbovu wa Katiba kwa miaka mingi ambao hauendani na mazingira ya sasa. Mbatia alisema Takukuru imekuwa haina meno ya kupambana kikamilifu dhidi ya mafisadi na walarushwa kwa sababu, inasubiri kupewa maagizo kutoka Ofisi ya Rais. Pia, Mbatia alisema kutokana na tatizo hilo Takukuru imekuwa ikifanya kazi zake bila meno ya kung'ata mafisadi na walarushwa. Aliongeza kuwa malumbano hayo ni ishara inayoelekeza nchi kutafuta suluhu endelevu ambayo ni urekebishaji Katiba.Alisema kwa upande wa bunge, baadhi ya wabunge wamekuwa wakitumia kifungu namba 3 cha mwaka 1998 cha Bunge kujikinga. "Kwa kuwa sheria wameitunga wao lazima wakubali kuwa pindi wanapotakiwa kuhojiwa mahali popote wafanye hivyo, Endapo hawatatekeleza taratibu walizojiwekea wenyewe huo ni ufisadi,” alisema

Ahukumiwa kunyongwa na mwili wake Kuwekwa Msalabani

Mwanaume mmoja nchini Saudi Arabia ambaye aliwabaka watoto watano miongoni mwao akiwemo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu ambaye alimtelekeza jangwani afariki, amehukumiwa kunyongwa na kisha mwili wake kuwekwa kwenye msalaba. Mahakama nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanaume aliyewabaka watoto watano adhabu ya kunyongwa na kisha mwili wake kuwekwa kwenye msalaba na kisha kuwekwa hadharani watu waushuhudie.Mwanaume huyo mbali ya kuwabaka watoto hao watano, alimchukua mtoto mmoja wa kiume aliyembaka na kumtelekeza katikati ya jangwa ili afariki mwenyewe.Mahakama ya rufaa ya mjini Riyadh imethibitisha adhabu hiyo ambayo ilitolewa mwezi juni mwaka huu na mahakama moja ndogo ya mji wa Hail ambako mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 22 alifanya unyama wake huo,limeripoti gazeti la Okaz la Saudi Arabia.Baada ya kunyongwa mbele ya hadhara, mwili wake utawekwa kwenye msalaba na kuwekwa wazi kwenye hadhara watu waushuhudie.Mwanaume huyo ambaye hakutajwa jina lake, alikamatwa wiki chache zilizopita baada ya kujaribu kumlaghai mtoto mwingine kwa kumpa lifti ya baiskeli kutoka nyumbani kwao hadi shuleni kwao.

Watu 4 wakamatwa na Meno ya Tembo Dar

JESHI la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wanne wakiwa na meno ya Tembo vipande 33 kinyume na sheria za nchi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ASP Suleimani Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, nyara hizo zilikamatwa maeneo ya Mbagala Nzasa Wilayani Temeke wakijaribu kuzisafirisha nyara hizo nje ya nchi.Kamanda Kova alisema watu waliokamatwa walikutwa wakijiandaa kupeleka nje ya nchi nyara hizo wakati hawana nyaraka zozote za umiliki wa meno hayo.Alisema nyara hizo za serikali zina uzito wa kilo 102.9 zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 7, na kwamba zilikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Monday, November 2, 2009

Kitoto kichanga chaopolewa kutoka kwenye tundu la choo kikiwa hai

MTOTO mchanga wa siku moja ameopolewa akiwa hai akiwa ametupwa ndani ya shimo la choo huko maeneo ya Kimara King’ongo jijini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema kuwa, mtoto huyo alitupwa juzi chooni majira ya saa 12 asubuhi, huko Kimara King'ongo na mtu asiyefahamika.Amesema choo hicho kipo nje ya nyumba ya Justina Lema na kichanga hicho alikutwa ameviringishwa matambara ndani ya choo hicho.Amesema kuwa mtoto huyo aliokolewa na wananchi wa eneo hilo baada mmiliki wa choo hicho kutoa taarifa kwa majirani kuwa anasikia sauti ya kichanga inatoka kwenye tundu hilo.Mtoto huyo ameokolewa akiwa hai na amehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na hali yake inaendelea vizuri.Kamanda huyo alisema juhudi za kumtafuta na kumsaka mtuhumiwa zinaendelea kwa kasi ili kumkamata ili aweze kufikishwa mahakamani

Binti wa Miaka 11 ajifungua Siku ya Harusi Yake

Binti wa miaka 11 wa nchini Bulgaria Kordeza Zhelyazkova mwenye umri wa miaka 11 alijifungua salama wiki iliyopita mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.4 ambaye alimpa jina la Violeta lakini alitoroka hospitali na mtoto wake usiku huo huo aliojifungua mtoto wake ili awahi kumalizia sherehe za harusi yake.Kordeza ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi, alisema kuwa alikutana na mumewe mpya mwenye umri wa miaka 19 Jeliazko Dimitrov kwenye viwanja vya michezo vya shule yake baada ya Jeliazko kumuokoa kutoka kwenye kipigo cha wahuni wa mitaani.Kordeza anadai alianza kufanya mapenzi na Jeliazko bila kutumia kondomu na anakiri alikuwa hajui kondomu ni kitu gani wakati huo.Kordeza alipata mimba ndani ya wiki moja baada ya kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wake huyo.Kordeza anasema alikuwa hajui kama ana mimba mpaka bibi yake alipoona mabadiliko ya maumbile yake, tumbo lake likizidi kuwa kubwa."Nilifikiria labda nimekula burger nyingi sana ndio maana tumbo langu limekuwa kubwa", alisema Kordeza."Sitachezea tena madoli, ninalo doli langu jipya nalipenda sana", Kordeza alinukuliwa na gazeti la News of The World la Uingereza akisema."Sitarudi shule tena, nimeishakuwa mama",alisema Kordeza.Wakati huo huo kuna uwezekano wa mumewe kutupwa jela miaka sita kwa kufanya mapenzi na msichana mwenye umri chini ya miaka 14.Umri unaoruhusiwa kisheria kuanza mapenzi nchini Bulgaria ni miaka 14."Ninaogopa sana... nataka nimtunze mtoto wangu na mke wangu lakini kuna uwezakano nikatupwa jela", alisema Jeliazko."Nimefanya makosa lakini sitaomba msamaha kwa sababu nimepata mtoto mrembo Violeta", aliongeza Jeliazko.

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote