Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote

Sunday, January 17, 2010

Je huu ni uungwana?

Zayed al-Nahayan(pichani) ambaye ni kaka wa mtawala wa falme za kiarabu UAE, akishirikiana na polisi kumtesa jangwani raia wa Afghanistan imezua mtafaruku duniani baada ya sheikh huyo kuachiwa huru na mtu aliyeitoa video kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano.

Saturday, January 2, 2010

Ajali ya gari yaua Dar na kujeruhi Tisa

Mfululizo wa matukio ya ajali yanayogharimu maisha ya watu na kujeruhi kadhaa hasa kipindi cha mwisho wa mwaka, umeendelea kuliandama Jiji la Dar es Salaam ambapo jana huko Mbagala, mtu mmoja amefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa vibaya baada gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Lwambano Masino amesema, tukio hilo lilitokea mishale ya saa 11:00 jioni huko Mbande Mzambarauni, Mbagala Charambe. Kamanda amesema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 713 ATB aina ya Fuso, lililokuwa likiendeshwa na Mohamed Haji, 27, mkazi wa Magomeni kutokea Mbagala kuelekea Mbande. Kaimu Kamanda Masino amesema dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu gari lake na hivyo kuacha njia na kisha kupinduka. Amemtaja mtu aliyefariki katika tukio hilo kuwa ni Omari Mandunguru, 27, mkazi wa Chamazi. Amesema majeruhi wawili kati ya tisa waliojeruhiwa, walitibiwa katika hospitali ya Temeke na kuruhusiwa ambapo wengine saba wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Amewataja waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Abdul Noli, 17, Sultan Rajab, 17, Musa Yusuph, 15, MohamedYusuph, 16, Bakari Said, 17, Omari Juma, 14 na Miki Evenus, 20. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke.

Miaka 20 jela kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wake

Ashley Jo Beach, mwalimu mwanamke mwenye umri wa miaka 38 (pichani) ambaye ni mama wa watoto watatu, alikamatwa akifanya mapenzi kwenye kichaka na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.Mwalimu huyo pia anatuhumiwa kula uroda na mtoto huyo ndani ya darasa lake huku milango yote ikiwa imefungwa.Wakati alipokuwa akifanya nae mapenzi, mtoto huyo wa kiume alikuwa na umri wa miaka 12."Alianza kutembea nae kimapenzi wakati alipokuwa darasa la sita na yeye akiwa ndio mwalimu wake", alisema mwendesha mashtaka Jean Fisher.Ili kufanikisha azma yake ya kumteka kimapenzi mwanafunzi wake, mwalimu huyo alikuwa akimnunulia zawadi mtoto huyo na wakati mwingine akimtaka awaangalie watoto wake.Mwalimu Beach alikiri makosa yake na kuongeza kuwa anatafuta tiba ya makosa aliyofanya."Imani ambayo nimeivunjia familia yangu na jamii yangu inanisumbua kila siku", mwalimu Beach aliiambia mahakama.Katika hali ya kushangaza zaidi, mume wa mwalimu huyo naye alikamatwa wakati wa uchunguzi wa kesi hiyo kwa kuwapiga picha wafungwa wanawake wakiwa uchi.Alikuwa na ruhusa ya kuingia kwenye jela ya wanawake kutokana na kazi yake aliyokuwa akifanya kwenye ofisi ya mkuu wa polisi.Mume wa mwalimu huyo alimtumia mkewe picha za wafungwa wanawake wakiwa uchi ili kumfanya aone wivu, mahakama iliambiwa.Naye amefunguliwa mashtaka kuhusiana na picha hizo na hivi sasa anasubiria hukumu yake.

Amuua mama yake kwa kukataza kuuza nyumba ya urithi

Mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam, Cristabela Mtondo ,60, ameuawa kwa kuchinjwa shingo na mtu anayedaiwa kuwa ni mwanae. Imedaiwa mama huyo alifanyiwa ukatili huo baada ya kukataa kuuza nyumba ya urithi. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile, aliongea na gazeti moja kuwa, mwili wa marehemu uligundulika juzi saa 9:00 alasiri ukiwa ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi. Kwa mujibu wa Kamanda Shigolile, polisi wanamshikili kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Amani Mtondo. “Polisi walipokwenda kwenye nyumba hiyo walimkuta mtuhumiwa ambaye inadaiwa mara kwa mara alikuwa akimlazimisha mama yake kuiuza nyumba hiyo,”amesema Kamanda. Hata hivyo amesema akasema marehemu (Cristabela), alikuwa akikataa kuiuza nyumba hiyo iliyoachwa na marehemu mumewe. Kamanda Shilogile amesema hadi sasa haijafahamika silaha iliyotumika kumchinja mwanamke huyo na kwamba upelelezi wa tukio unaendelea.

Simba wa Vita kuzikwa leo

MAZISHI ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo kuanzia majira ya saa 7 za alasiri huko nyumbani kwake Madala Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Marehemu Kawawa alifariki juzi, majira ya saa 3:20 za asubuhi, katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako juzi alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia afya yake.Akiongea na waandishi wa habari kwa huzuni Ikulu, Raisi Kikwete alisema Mzee Kawawa alifika hospitalini hapo juzi kwa ajili ya kwenda kupima malaria kwa kuwa alikuwa na safari na alienda hapo ili aweze kujitambua kama angekuwa na malaria ajitibie kabla ya kwenda safari yake hiyo.Alisema alipofika hospitalini hapo alipima malaria na kukutwa kuwa hakuwa nayo, na alianza safari ya kurudi nyumbani kwake, kabla hajafika nyumbani kwake hali ilibadilika na waliongozana nae walimrudisha hospitalini hapo na jopo la madaktari walianza kumpima kutambua alikuwa akisumbuliwa na nini.Katika vipimo vya haraka haraka madaktari hao waligundua kuwa sukari yake ilikuwa imeshuka sana na kufikia 0.6 hali ambayo iliwafanya madaktari wafanye jitihada kubwa kumshughulikia kurudisha hali yake ikae sawa.Mbali na kumshughulikia sukari, pia waliweza kugundua kuwa figo zote mbili zilikuwa hazifanyi kazi na pamoja na jitihada zote mwenyezi mungu alichukua uamuzi wa kumchukua majira hayo.Kufuatia kifo hicho Kikwete amesema wamempoteza kiongozi shupavu aliyepigania uhuru wetu wa Tanganyika enzi za mwalimu na kusema alikuwa ni kiongozi mshauri wa karibu katika kuweka hali ya nchi sawa na walikuwa wakimtegemea kwa ushauri wa hapa na pale enzi za uhai wake.Marehemu aliweza kushika nyadhifa nyingi enzi za uhai wake kama vile Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri Mkuu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na vyeo vingine kadhaa.Marehemu Kawawa alizaliwa mkoani Ruvuma Wilaya na Namtumbo, Februari 27, mwaka 1926. Alifariki jana akiwa na umri wa miaka 83.

Waoana baada ya kupeana Talaka

Ndoa ya miaka 20 ilikuwa ni chungu sana kuvunjika kiasi cha kwamba Lee na Jan Jones waliamua kurudiana na kufunga harusi kwa mara nyingine ikiwa ni wiki chache tu baada ya kupeana talaka kila mtu aanze maisha yake kivyake.Kwa mujibu wa gazeti la Dail Mail, Lee na Jan walikuwa wakikutana wakati wa taratibu za kuivunja ndoa yao mahakamani lakini ghafla walifikiria kuwa wamefanya uamuzi mbaya sana na kuamua kufunga ndoa tena.Wanandoa hao ambao wana umri wa kwenye miaka ya 40 na ushee wamezaa watoto 10 pamoja.Walioana kwa mara ya kwanza mwaka 1990 na walifunga ndoa tena kwa mara ya pili siku ya mkesha wa krismasi.Watoto wao ambao waliwaona wazazi wao ni wapumbavu kwa kuachana kwao ndio waliokuwa wapambe wakati wa harusi hiyo ya pili."Tulijiona tumefanya makosa kuachana", alisema bi Jones.Wanandoa hao walikuwa wakiwasiliana kwa kutumia ujumbe wa simu wakati taratibu za kuivunja ndoa yao ya mwanzo zikiendelea.Bwana Jones alilalamikia matatizo mbali mbali kwenye familia ndiyo yaliyopelekea ndoa yao ya mwanzo ivunjike.
There was an error in this gadget

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote