Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 25, 2010

Mwanaume mwenye nywele ndefu duniani afariki Dunia


Urefu halisi wa nywele zake ni mita 6.8. Kutokana na maelezo ya Mke wake Tran Van Hay's alianza kufuga nywele zake miaka 50 iliyopita , na hii ilisababishwa na kuumwa kila aliponyoa nywele hizo. Aliishi maisha ya kawaida sana kama tabibu wa tiba za asili, hakuna pikipiki iliyoweza kumbeba kutokana na kushindwa kuvaa Helmet na majira ya mchana alikuwa anaziviriga nywele zake na kuzibeba kichwani kama ndoo huku zikisaidia na kitambaa, Hay alifariki jana huko Kien Giang kusini mwa Vietnam akiwa na miaka 79

Rais wa Nigeria arudi kwao Buheri wa Afya

Rais wa Nigeria Yar’Adua, 58, jana alirudi kwao baada ya miezi mitatu ya matibabu ya moyo nchini Saudi Arabia .

Mkoa wa Morogoro kuwa na Majimbo mawili mapya?

BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya Morogoro limepitisha mapendekezo ya kuligawa jimbo la Morogoro mjini ili liweze kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi katika kurahisha huduma za maendeleo kwa wananchi. Akitangaza mapendekezo hayo katika kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Morogoro,meya wa Manispaa hiyo, Profesa Romanus Ishengoma alisema kutokana na mabadiliko hayo sasa kutakuwa na jimbo ya Bondwa na jimbo la Lupanga . Ishengoma alisema mabadiliko hayo yamelenga kuwarahisishia huduma za kijamii wananchi wa Manispaa ya Morogoro wanaokadiriwa kufikia 500,000. Alisema mbali na kupendekeza majimbo mawili pia baraza hilo la madiwani limependekeza kuongeza tarafa kutoka moja na kuwa mbili za Lupanga na Bondwa ikiwa ni pamoja na kuongeza kata za manispaa hiyo. Akisoma mapendekezo hayo katika kikao hicho,naibu meya wa manispaa hiyo, Amir Nondo alisema pia mapendekezo hayo yamelenga kuzigawa kata kutoka kata 19 hadi kufikia 26 kulingana na ukubwa wa baadhi ya kata. Nondo alizitaja kata zilizogawanywa kuwa ni pamoja na kata ya Mbuyuni ambayo itakuwa na kata mbili za Magadu na Mbuyuni,kata ya Mzinga itakayokuwa na kata ya Luhungo na Kauzeni na kata ya Mwembesongo itakayokuwa na kata ya Mafisa na Mwembesongo. Naibu meya huyo alizitaja kata zingine zilizopendekezwa kugawanywa kuwa ni kata ya Kihonda itakayokuwa na kata ya Kihonda na Mkundi,kata ya Kingulwira itakayokuwa na kata ya Tungi na Kingulwira na kata ya Mazimbu itakayokuwa na kata ya Mazimbu,Mindu na Magorofani.

Ajiua baada ya Mpenzi wake wa zamani kutuma picha zake za utupu kwenye mtandao wa Face book

Mwalimu wa Kike Emma Jones 24 raia wa UK ambae alikuwa mfanyakazi wa moja ya International School huko Abu Dhabi amejiua baada ya mpenzi wake wa zamani kutuma picha zake za utupu kwenye mtandao wa Facebook, Emma alihofia kufungwa kutokana na sheria kali za Chini za Kiarabu na hapo ndipo alipoamua kujiua mwenyewe kwa kunywa sumu.

Emma enzi za uhai wake
Boyfriend anayetuhumiwa kutuma hizo picha zilizopelekea kifo chake


Mwanamke Aliyesingizia Kubakwa Atupwa Jela

Biurny Peguero mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa jiji la New York nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu baada ya kukiri kumsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.Mwaka 2005, Biurny alimsingizia mwanaume huyo kuwa alimtishia na kisu kabla ya kumbaka. Mwanaume huyo alihukumiwa kwenda jela miaka minne.Mwaka jana Biurny alienda kutubu madhambi yake kanisani na kukiri mbele ya mchungaji kuwa alimsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.Hatua hiyo ilisababisha polisi wapewe taarifa ambapo mwanaume huyo aliachiliwa huru muda mfupi baadae.Akisomewa hukumu yake, Biurny alihukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu.

Ukweli kuhusu Irene Uyowa kurudi Bongo huu hapa!!

“Nahisi kuna watu wanataka nipewe talaka, wananiombea hivyo, lakini nataka watu wajue kuwa Ndikumana (Hamad) hawezi kuniacha, na siwezi kuachika,” alisema Irene na kuongeza: “Mimi najua kuolewa lakini sijui kuachwa, nimekuja hapa Bongo kwa sababu ni nyumbani kwetu, sikatazwi, lakini naona mambo yamezidi, kila nikirudi hapa naambiwa nimeachwa.”Irene alisema kuwa kwa sasa amekuja nchini kwa lengo moja tu kucheza filamu, kuhusu muda gani atautumia nchini alizungumza kwa msisitizo kwamba huo ni uamuzi wake hata kama atakaa mwaka.“Nitakaa mwaka, na Ndikumana hawezi kuniacha, au nikupe namba ya simu uzungumze naye?” Aliuliza Irene lakini mwandishi wetu alipokubali, alikata simu na kuingia mitini.

Kituko vya mwaka - Waumini wakesha wakisali ili Wachungaji wao wafufuke!!

Waumini wa kanisa moja la Pentekoste magharibi mwa Kenya wamegoma kuwazika wachungaji wawili wa kanisa hilo waliofariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita na wamekuwa wakisali mbele ya majeneza yao muda wote wakiamini kuwa watafufuka kama alivyofufuka YESU.Mchungaji Patrick Wanjohi na mchungaji Francis Kamau Ndekei, walifariki februari 15 mwaka huu kutokana na ajali mbaya ya gari lakini waumini wao wamekuwa wakiamini kuwa wachungaji hao wamelala tu na wala hawajafariki."Hatutawazika kamwe, kwakuwa hawajakamilisha misheni zao hapa duniani, tunawahitaji warudi duniani kumalizia majukumu yao kwani bila ya wao kanisa litakufa", alisema mmoja wa waumini hao.Awali uongozi wa kanisa hilo ulisema kuwa wachungaji hao watafufuka siku ya jumamosi na kuwafanya maelfu ya watu washinde kwenye mvua kubwa sana wakisubiria wachungaji wao wafufuke. Hata hivyo siku ya jumamosi ilimalizika bila wachungaji hao kufufuka.Mamia ya waumini bado wanaendelea kusali masaa yote mbele ya majeneza ya wachungaji hao wakisubiria miujiza ijitokeze na wachungaji hao wafufuke.

Mishi Bomba kuolewa?

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa yule mtangazaji maarufu wa kipindi cha miondoko ya Pwani kupitia Kituo cha Redio cha Magic FM, Mwanahamisi Bashir Mwenda a.k.a Mishi Bomba, anatarajia kufunga ndoa mwezi ujao na mwanaume ambaye kwasasa tunamuweka kapuni kwasababu maalum...

Lyon kuitibulia Simba rekodi?

AFRICAN Lyon imeungana na Kagera Sugar kutibua rekodi ya Simba ya ushindi wa mechi zote msimu huu baada ya kuibana na kutoka sare ya bao 1-1. Kwa matokeo hayo, Simba wamezidi kucheleweshewa hafla yao ya ubingwa ambayo ilihitaji ushindi wa mechi mbili pekee kabla ya mechi ya jana. Katika mchezo huo, Lyon, walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji Robert Ssentongo katika dakika ya 5 baada ya kupata krosi safi ya Hamis Shengo iliyomchanganya kipa Juma Kaseja wa Simba. wakati goli la Simba lilipatikana katika dakika ya 81, lilifungwa na Mgosi baada ya kupiga shuti kali lililompita kipa wa Lyon, Ivo Mapunda. Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 50 na kuiacha Yanga iliyo ya pili kwa pointi nane baada ya mwanzo wa wiki kuifumua Toto African kwa mabao 6-0.

Jaribio la ndege kulipuka lawashtua wengi Dar

Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, jana walipata mshtuko na kuanza kukimbia kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kungalia ndugu zao kama wapo hai baada ya kuwepo taarifa za kutokea ajali ya ndege katika uwanja huo na kuua abiria kadhaa.Mtafaruku huo uliotokea jana mchana na kusababisha vikosi vya ulinzi na usalama kutimua mbio huku vikiwa na ving'ora kuelekea uwanja huo kwa ajili kwenda kufanya kazi ya uokoaji.Hata hivyo, jambo la kushangaza baada ya vikosi hivyo kufika katika uwanja huo, viliambiwa kwamba hapakuwa na tukio lolote baya bali Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), iliamua kufanya maigizo yanayofanana na tukio la kweli la ajali.Akizungumza na vyombo vya habari, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Kenyela, alisema hata yeye alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kupata taarifa hizo.Hata hivyo, alisema baada ya kufika eneo la tukio, alishangaa kuona halikuwa tukio la kweli bali yalikuwa maigizo kwa lengo la kupima utayari wa mamlaka husika endapo ajali ya ndege itatokea."Ni kweli na mimi nipo hapa lakini hakuna tukio baya na nimeambiwa haya ni maigizo ya kawaida ili kuviweka tayari vikosi vya ulinzi na uokoaji," alisema.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Prosper Tesha, alisema zoezi hilo hufanyika mara moja kila baada ya miaka miwili.Alisema katika zoezi hilo wamegundua mapungufu makubwa katika upande wa usafiri kwa ajili ya kupitisha magari ya uokoaji kwenda Uwanja wa Ndege

Angelina na baba yake sasa shwari?

Inasemekana zile tofauti zilizopo kati ya Angelina Jolie na Baba yake(Voight) kwa miaka mingi zimeisha na hii imetokana na kupiga picha wakiwa pamoja jana huko mjini Venice . Jamani tunawatakia kila la heri

Ronaldo Kustaafu Mwakani?

Nyota wa Brazili, Ronaldo de Lima ametangaza mpango wake wa kustaafu kucheza soka mwakani. Ronaldo ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Corinthians ya jijini Sao Paulo nchini Brazili, ametangaza kustaafu kucheza soka la kulipwa ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao. Ronaldo ambaye aliwahi kuchaguliwa mara tatu kuwa mchezaji bora wa dunia hivi sasa ana umri wa miaka 33. Ronaldo alisema kuwa atastaafu kucheza soka lakini ataendelea kuiwakilisha Corinthians baada ya kustaafu kama balozi wake. "Nimeongeza mkataba wangu kwa miaka miwili natarajia ndio miaka miwili ya mwisho katika soka", alisema Ronaldo. Ronaldo ambaye aliibeba Brazili kutwaa kombe la dunia mwaka 1994 na 2002 hakuweza kuyaficha matumaini yake ya kuitwa kwenye kikosi cha Brazili kitakachoshiriki kombe la dunia baadae mwaka huu nchini Afrika Kusini. "Tutaona itakavyokuwa, bado nina nafasi ya kuitwa timu ya taifa" alisema Ronaldo na kuongeza "Kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazili itakuwa vigumu sana kwangu kushiriki kwani umri wangu utakuwa umesogea sana".

Wednesday, February 24, 2010

Mbaroni kwa Kumuhifadhi Mtuhumiwa

JESHI LA POLISI Dar es Salaam limewakamata watu watano kwa kosa la kumuhifadhi raia wa Uingereza Salim Maunga [35] aliyekamatwa Uwanja wa NDege akiwa na dawa za kulevya. Watu hao inadaiwa ni rafiki wa mtuhumiwa huyo na ilidaiwa walimuhifadhi nyumbani kwao Makumbusho jijini Dar es Salam na kumsaidia katika sakata kusafirisha dawa hizo.Salim alikamatwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kubeba kete 69 za dawa za kulevya aina ya Cocaine na bangi gramu 610.Alikamatwa akiwa katika hatua ya mwisho ya ukaguzi kabla ya kupanda ndege ya British Airways, pia rafiki wa mtuhumiwa huyo waliandaa dawa za kulevya bandia pamoja na Sh3 milioni kwa ajili ya kumpa mtunza stoo wa kituo cha polisi uwanja wa ndege.Mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba 109483453, Kamishna Msaidizi wa polisi wa viwanja vya ndege nchini, Mwajuma Kiponza alisema walimpekua na kubaini kuwa alificha kete 16 kwenye pindo la suruali yake sehemu ya kiunoni na kete 14 zilikutwa katika pindo ya chini ya suruali yake.Pia alipofikishwa kituoni kwa ajili ya kumhoji zaidi walipofungua begi lake walikuta pia vinyago vitatu ambavyo alivibeba kinyume na sheria. Hivyo watu hao wameshikiliwa na Jeshi hilo kwa kosa la kumuhifadhi raia huyo huku wakijua dhamira ya rafiki yao huyo kusafirisha madawa na kushirikiana nae katika kufanya uhalifu huo ili aweze kusafirisha madawa hayo.

Wapenzi wa 24 Jack Bauer arudi ulingoni baada ya Operesheni

Mwigizaji maarufu wa tamthilia ya 24 Kiefer Suthrland 43 anayefahamika kama Jack Bauer(pichani) amerudi ulingoni wiki 2 baada ya kufanyiwa upasuaji .

Diamondi Musical Interantional kutambulisha wanamuziki wapya Ijumaa, Mulemule ndani ya Nyumba?!!

Bendi ya muziki wa dansi ya Diamond Musica International Ijumaa ya tarehe 26 mwezi huu watafanya utambulisho wa wanamuziki wapya akiwemo mwimbaji mahiri wa bendi ya FM academia Mulemule ambaye amehamia kwenye bendi hiyo hivi karibuni. Utambulisho huo utafanyika ijumaa jioni katika ukumbi wa Vatican city sinza jijini Dar es Salaam. Akiongea kiongozi wa wanenguaji Baby Bus alisema kuwa wamejiandaa na shoo hiyo ambayo itakuwa ya kihistoria hapa nchini .Aliwataja wanenguaji wengine ambao watashirikiana kuwasha moto jukwaani hapo alisema safu yao itawakirishwa na Baby Full, Janeth Mrisho na Korando Mikololo.

Marekani yaiokoa Meli ya Tanzania

Meli I ya kivita ya Marekani imefanikiwa kuzuia shambulizi kwa meli ya Tanzania kutoka kwa maharamia wasiojulikana, na kuwadhibiti wanane waliokuwa katika mchakato huo,Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema. Meli hiyo ya kimarekani, USS Farragut ilirusha helkopta SH-60B Seahawk na kwenda kuiokoa MV Barakaale 1 baada ya kupokea ishara zikiashiria kuwa meli hiyo, iko kwenye hatari ya kushambuliwa na genge la maharamia, taarifa ya ubalozi huo imesema. "Helkopta hiyo ilifanikiwa kufyatua risasi za tahadhari juu ili kuidhibiti boti iliyokuwa ikiongeza kasi ya kuiendea meli ile" ilisema. "Timu ya wanajeshi toka USS Farragut walijotosa kwenye boti ile na kuwakamata maharamia wanane waliokuwepo na kuwasafirisha kwa the Farragut." Hata hivyo, taarifa hiyo iliyochapishwa na Shirika la Habari la Reuters haikusema lini na wapi tukio hilo limetokea na pia halikubainisha uraia wa maharamia hao. The USS Farragut ni maalum kwa ajili ya kufanya maangalizi na ni sehemu ya kikosi maalum namba 151 ambacho kinafanya doria katika rasi ya Aden na mashariki ya pwani ya Somalia. Kikosi hicho maalum, kilianzishwa mwaka 2009, kinahusisha jozi tatu za meli kutoka Australia, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Pakistan, Canada, Denmark, Uturuki, Marekani na Uingereza miongoni mwa nchi washirika. Pwani ya Somalia ni miongoni mwa eneo hatari sana duniani kwa meli kusafiri. Idadi ya mashambulizi ya maharamia duniani kote yamepanda kwa asilimia 40 mwaka jana, ambapo maharamia wenye silaha walioshindwa katika mataifa ya pembe ya Afrika yanafikia karibu nusu ya matukio 406 yaliyoripotiwa kwa mujibu wa the International Maritime Bureau.

Igeni na Hii


Hitima ya Mzee Kawawa Kufanyika Jumamosi

Siku ya Jumamosi ya tarehe 27 mwezi wa pili mwaka huu Taifa litafanya HITIMA maalumu kwa ajili ya Mzee wetu Mpendwa Marehemu Rashidi Mfaume Kawawa huko Nyumbani kwake Madale kuanzia saa 7 za mchana. Wote mnakaribishwa

Huu ni ujasiri wa hali ya juu

Ni jambo la Kijasiri ambalo linakatisha tamaa kama hukupata sapoti, Hii imemtokea mwanamichezo wa kuteleza kwenye barafu anayejulikana kama Joannie Rochette wa Canada baada ya kumpoteza mama yake mzazi massa 48 kabla ya mashindano hayo ya Olympic, lakini pamoja na uchungu wote mwadada huyu akipewa sapoti kutoka kwa Kocha na baba yake mzazi aliweza kushiriki ili kutimiza ndoto yake ambayo hata mama yake mzazi alikuwa anatamani mtoto wake atimize. Wakati mauti ikitokea inasemekena Marehemu Therese na Mumewe pichani chini walisafiki pamoja ili kumpa apoti mtoto wao
Baba Mzazi wa Rochette
Rochette akijiandaa kuanza shindano

Rochette akiwa katika mashindano

Tundaman aja na Video mpya - Kaeni mkao wa kula

Msanii kutoka TIP TOP Connection anayekwenda kwa jina la Tunda Man amefanya video yake mpya inayokwenda kwa jina la "Hali Yangu Mbaya." Tunda anasema wimbo huo umesimamiwa na Producer Marco Chali na amewashirikisha wakali weingine toka Temeke na Manzese, Chege na Madee.

Kioja cha Mwaka - Wavua nguo na kubaki uchi Mahakamani Temeke

WASHTAKIWA watano jumatatu walifanya kituko cha mwaka baada ya kuvua nguo katika mahakama ya Wilaya ya Temeke na kutembea uchi huku umati wa watu waliokuwepo mahakamani hapo ukibaki umeduwaa. Habari zilizolifikia jana na kuthibitishwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Helleni Liwa zilisema washtakiwa hao walifanya kituko hicho jana mchana ikiwa ni hatua ya kupinga kile walichokiita kubambikiwa mashtaka. Habari zaidi zilieleza kuwa awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha, lakini waliachiwa juma lililopita kabla ya kukamatwa tena siku hiyohiyo na kufunguliwa mashtaka mengine. Jana washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa lengo la kusomewa mashtaka upya, lakini walipoitwa kuingia mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka hayo walikataa, wakidai kuwa walikuwa wakimtaka Hakimu Mfawidhi ili wamwelezee malalamiko yao hayo. Chanzo chetu cha habari kilichoshuhudia kituko hicho kilisema kuwa baada ya askari kuwalazimisha kuingia mahakamani, ndipo washtakiwa hao walipoamua kuvua nguo zote na kubaki kama walivyozaliwa. Chanzo hicho kilidokeza zaidi kuwa baada ya kuvua nguo hizo walitoka mahabusu na kwenda kukaa nje karibu na mlango wa kuingilia mahakamani jambo ambalo liliwaacha vinywa wazi watu waliokuwepo mahakamani hapo. Akidhibitisha Hakimu Mfawidhia Liwa kuwa washtakiwa hao kufanya kituko hicho na kusema kwamba aliagiza washtakiwa hao wapandishwe kizimbani na kusomewa mashtaka mapya ya kuvua nguo hadharani. "Ni kweli kabisa tukio hilo limetokea leo muda wa saa 8 hivi mchana, nami nimewashuhudia,"alisema Hakimu Liwa. Alisema awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha, lakini walifuatiwa mashtaka na kuachiwa huru mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mapya. Kwa hiyo jana walifikishwa mahakamani hapo mapema tu kwa ajili ya kusomewa tena mashtaka hayo upya. Walifikishwa mapema tu lakini walipoitwa kuingia mahakamani kusomewa mashtaka walikataa wakidai kuwa wanataka kuonana na mimi, alisema Hakimu Liwa na kuongeza; "Ndipo nilipoamua kwenda kuwaona ili kuwasikiliza lakini nikawakuta wako uchi wa mnyama kama walivyozaliwa, na baada ya kuwakuta katika hali hiyo nikawambia siwezi kuzungumza nao wakiwa katika hali kama hiyo, hivyo wakawambeleza wakavaa nguo ndipo nikazungumza nao." Hakimu Liwa aliongeza kuwa washtakiwa hao walimlalamikia kuwa wamechoka na mashtaka wanayofunguliwa kwani wanakamatwa na kubambikiwa kesi na wanapelekwa mahakamani lakini hakuna ushahidi. "Lakini niliwaeleza wazi kuwa walichokifanya ni makosa kwani kwani walitakiwa watii kwanza kuingia mahakamani na kama wana malalamiko mengine ndio yangefuata na si kuvua nguo, alisema Hakimu Liwa, na kuongeza; "Hivyo kwa kuwa mimi nilikuwa ninaondoka kwenda Mahakama Kuu, nilimwagiza Hakimu Rose Kaliwa ambaye ndiye alikuwa awasomee mashtaka mapya ya leo, awasomee mashtaka ya kuvua nguo mbele ya hadhara"

Tuesday, February 23, 2010

Shakira kukutana na Rais Obama kujadili mambo ya Elimu kwa watoto

Shakira ambae ni Balozi wa UNICEF ana anayemilikia mfuko wake binafsi unaojulikana kama The Barefoot Foundation amekutana jana na Rais Obama kujadili masuala ya Elimu kwa watoto, inasemakana kuwa Shakira amekuwa mstari wa mbele katika kazi za jamii na kuzunguka sehemu nyingi duniani kusisitiza hayo na amesisitiza kuwa wamekubaliana na Obama kufanya kazi kwa karibu katika suala zima la kukuza uchumi, kupiga vita umaskini, na kuhakikisha usalama na Amani vinaongezeka.

Mfanyakazi wa Bima ya Afya ashinda Gari la Zain?


Kampuni ya simu za mikononi ya Zain Tanzania jana mchana imemkabidhi gari jipya pichani aina ya Toyota Land Cruizer Bw.Willfred Maleko (28) Mkazi wa Mbezi ambaye ni mfanyakazi wa Taifa Bima ya Afya,Willfred amezawadiwa gari hiyo baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya Ongea Uzawadiwe na Zain katika makao makuu ya Kampuni ya hiyo Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Manara aendelea Kusota Lupango

ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, ameendelea kusota rumande baada ya kushindikana kwa utaratibu wa kumwekea dhamana katika kesi inayomkabili ambapo anadaiwa kufanya utapeli uliohusisha magari ya kukodi. Kesi hiyo inasikilizwa katika Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Katika tukio la aina yake ndugu na jamaa wa Manara walizuia asipigwe picha kwa madai kuwa wanamdhalilisha ndugu yao.

Mauaji ya Musoma hadi sasa watu 17 Mbaroni

Hadi kufikia jana mchana, jeshi la polisi nchini limefanikiwa kukamata watu 10 mkoani Mara wanaohusishwa na mauaji ya watu 17 wa ukoo mmoja.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, amesema hadi sasa watu hao wameshakamatwa na msako mkali unaendelea ili kuhakikisha watu wote waliohusika katika kufanya unyama huo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.Kamanda Boaz alisema watu hao walikamatwa katika maeneo tofauti ndani na nje ya mkoa huo baada ya kupata taarifa za uhakika kutoka kwa raia wema ambazo zimekuwa zikifanyiwa kazi na jeshi lake.Pia amewataka wananchi kuzidi kutoa taarifa kwa siri kuhusiana na watu hao.Amesema timu kubwa ya askari wake wamesambazwa kila kona ya mkoa wa Mara na nje ya mkoa ili kuwasaka watu hao wauaji na kusema kazi hiyo itafanikiwa kwa jeshi hilo.Amesema utaratibu wa kisheria utakapokamilika watu hao wanatarajiwa kupandishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.

Monday, February 22, 2010

Mganga 'feki' aliyeua wanne ahukumiwa kunyongwa

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa, mganga wa kienyeji 'feki' Mabala Masasi, mwenyeji wa Shinyanga, baada ya kupatikana na hatia ya makosa manne ya mauaji ya kukusudia. Masasi mwenye wake wanane na watoto 32, alipatikana na hatia ya kuwaua kwa makusudi Shija Mihayo na mkewe Fatuma Makunja, Mustafa Masanja na Mohamed Makwaya wote wakazi wa kijiji cha Chamakweza Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kinyume cha kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu (Penal Code). Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 75 ya mwaka 2006, Ijumaa iliyopita, Jaji Raziah Sheikh alisema baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na ushahidi wa upande wa utetezi aliridhika kuwa upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa pasi na shaka yoyote. "Nimeridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha bila shaka na naunga mkono maoni ya wazee wawili wa baraza waliosema kuwa mshtakiwa ana hatia. Nimeridhika kuwa mshtakiwa wa kwanza (Masasi) pekee au na wenzake wasiokuwepo mahakamani waliwaua marehemu hao kama inavyodaiwa na upande wa mashtaka; Hivyo kwa maoni yangu mshtakiwa una hatia ya kuwaua marehemu (watu) wanne kinyume cha sheria kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu," alisema Jaji Sheikh na kumpa nafasi wakili wa mshtakiwa Oscar Msechu kusema jambo lolote kabla ya kutamka adhabu. Wakili Msechu aliomba mahakama imuonee huruma na kumpunguzia adhabu mshtakiwa kwa madai kuwa ana wake wanane na watoto 32 ambao wote wanamtegemea na kwamba hilo ni kosa lake la kwanza na muda aliokaa rumande (miaka takribani 7) ni mingi, utetezi ambao hata hivyo Jaji Sheikh aliutupilia mbali. "Ninavyofahamu kisheria adhabu kwa kosa la kuua kwa makusudi ni moja tu nayo ni kunyongwa. Hivyo nami ninatoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa. Mshtakiwa anayo haki ya kukata rufaa," alisema Jaji Sheikh na kunyanyuka kwenye kiti chake. Kabla ya hukumu hiyo ilidaiwa na upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa aliwaua watu hao kwa nyakati tofauti tofauti, kati ya mwezi Februari na mwezi Mei, mwaka 2004, kwa lengo la kuchukua mali walizokuwa nazo. Ilidaiwa kuwa kabla ya kuwaua watu hao mshtakiwa aliwadanganya kuwa yeye ni mganga wa kienyeji mwenye uwezo wa kuwatibu magonjwa mbalimbali na pia kuwapa dawa ya kupata utajiri, lakini baada ya kuwanywesha dawa hizo waliishiwa nguvu na kudhoofika ndipo akawapiga hadi kuwaua kabla ya kuwafukia ardhini. Upande wa mashtaka ulidai kuwa mshtakiwa huyo ambaye alikuwa ni mgeni kijijini hapo alifikia nyumbani kwa marehemu Shija na kuwadanganya kuwa yeye ni mganga wa kienyeji ana tibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia dawa za kienyeji na kwamba ana dawa za kuwafanya wawe matajiri. Ilidaiwa kuwa marehemu Shija na mkewe walimuamini akawanywesha dawa, lakini mara tu baada ya kunywa dawa hiyo waliishiwa nguvu na kulegea ndipo mshtakiwa alipowapiga kwa mchi wa kutwangia vichwani hadi wakafariki dunia. Baada ya kuwaua ilidaiwa kuwa mshtakiwa aliwazika kwenye kisima kilichokuwa kimekauka nyuma ya nyumba yao. Upande wa mashtka uliendelea kudai kuwa baadaye marehemu Masanja na marehemu Makwaya ambao walikuwa ni wafanyabiashara wa duka la pamoja walikwenda kwa mshtakiwa ili kupata dawa ya kuongeza utajiri wao ndipo mshtakiwa wa kwanza (Masasi) na mshtakiwa wa pili (aliyeachiwa baada ya kuonekana hana kesi), waliwaua na kisha kuwazika porini. Upande wa mashtaka uliita mahakamani mashahidi wanane ambao ni pamoja na mwenyekiti wa kijiji, maofisa wa polisi waliowatia mbaroni watuhumiwa na kupeleleza tukio hilo, mke wa marehemu Makwaya, daktari na mlinzi wa amani (Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Bagamoyo), ambaye mshtakiwa alitoa maelezo ya ungamo mbele yake. Mashahidi hao ambao maelezo yao yalifananafanana waliieleza mahakama kuwa mshtakiwa alikamatwa baada ya marehemu kupotea katika mazingira ya kutatanisha ambapo walianza kumfuatilia na kumkuta akiwa anaendesha baiskeli ya mmoja wa marehemu. Walisema mshtakiwa alipelekwa katika kituo cha polisi Chalinze ambako alihojiwa na kukiri kuwaua watu hao ndipo kesho yake alirudishwa kijijini pale akiwa na askari polisi pamoja na daktari na kwenda kuwaonyesha mahali alikokuwa ameizika miili ya marehemu wale, mbele ya viongozi wa kijiji. Walisema miili miwili ilikutwa imefukiwa katika shamba moja porini tofauti tofauti na kwamba mshtakiwa aliwapeleka sehemu nyingine ambako walikuta miili miwili iliyokuwa imefukiwa ndani ya kisima kilichokauka pamoja na mchi wa kutwangia. Walisema mwili mmoja wa mwanaume na mwingine wa mwanamke na kwamba miili yote hiyo ilikuwa na majereha kichwani. Mshtakiwa alipelekwa hospitalini kupimwa akili na baadaye akaandika maelezo yake ya onyo (Caution statement) mbele ya shahidi wa saba (ofisa wa polisi aliyepeleleza tukio hilo), kisha alipelekwa kwa mlinzi wa amani ambako aliandika maelezo ya ungamo (Confession Statement) ambako kote huko alikiri kuwaua watu hao. Mlinzi wa amani, Rehema Juma Salum ambaye ni shahidi wa nane aliileza mahakama kuwa mshtakiwa alitoa maelezo mbele yake kwa hiyari na kwamba alikiri kuwaua marehemu na kuwafukia, baada ya kuwapa dawa za kienyeji ili aweze kurithi mali zao kama vile mashamba, nyumba na biashara walizokuwa nazo kama vile duka. Hata hivyo, wakati akijitetea mahakamani mshtakiwa alikana mashtaka hayo na kwamba yeye si mganga wa kienyeji bali ni mkulima na mfugaji ambaye hufanya pia shughuli za biashara ya kuuza nyama. Alidai kuwa alikuja Chalinze Juni 2004 kutoka kwao Shinyanga ambako ameacha wake wanane na watoto 32, kwa ajili ya kununua ng'ombe ili awasafirishe kuja Dar es Salaam kwa njia ya reli na kwamba ndipo alipofuatwa na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mwenyekiti wa kijiji na kumwambia kuwa anahitajika katika ofisi ya kijiji. Alidai akiwa huko ndipo alipokamatwa na polisi na kuchukuliwa begi lake lililokuwa na pesa Sh72milioni za biashara, huku akidai polisi walimpiga kwa muda wa siku tano ndipo siku ya sita walipompeleka hospitalini kutibiwa majeraha kabla ya kufikishwa mahakamani kwa mashataka hayo. Alikana pia kuandika maelezo ya onyo kwa polisi na ya ungamo kwa mlinzi wa amani, kuwafahamu wala kuishi kama wageni kwa marehemu hao wala kukiri kufanya mauaji hayo na kuwapeleka mashahidi hao eneo la matukio, huku akidai kuwa polisi walimbambikizia kesi hiyo ili wamdhulumu pesa zake hizo Sh72milioni alizokamatwa nazo. Hata hivyo, Jaji Sheikh alipuuza utetezi wake na kusema kuwa hauna msingi wala si wa kweli. Alisema kuwa wakati akitoa ushahidi wake alikuwa akimwangalia sana na mshtakiwa huyo alionekana kuwa ni mjanjamjanja na mkwepaji ambaye hakutaka kuisaidia mahakama.

Apigania Atambulike Kuwa Yeye Ndiye Mtu Mfupi Duniani

Khagendra Thapa Magar ameanza safari za kutembelea nchi za ulaya kupiga kampeni za kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness kuwa yeye ndiye mtu mfupi kuliko wote duniani.Khagendra alituma maombi yake kwenye ofisi za London nchini Uingereza akitaka aingizwe kwenye rekodi za dunia pindi afikapo umri wa miaka 18 mwezi oktoba mwaka huu.Hata hivyo, Khagendra amesema kuwa hajapata majibu yoyote toka kwenye ofisi hiyo.Awali Khagendra alituma maombi yake ya kuingizwa kwenye rekodi za dunia alipokuwa na umri wa miaka 14 lakini maombi yake yalitupiliwa mbali kwasababu hajatimiza umri wa miaka 18 wa kumwezesha ahesabike kama mtu mzima huku ikihofiwa kuwa anaweza kurefuka.Madaktari nchini Nepal wameshindwa kuelezea sababu zinazomfanya Khagendra awe mfupi kiasi hicho."Tunaenda Italia kujaribu kuingiza jina lake kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness " alisema baba yake Rup Bahadur Thapa Magar, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari toka mjini Katmandu.Baada ya kutoka nchini Italia ambako watashiriki kwenye shoo moja kwenye Televisheni ya Italia, Khagendra na kambi yake wataamua nchi gani nyingine ya kwenda.Mamia ya wapenzi wa Khagendra walijitokeza jana kumuaga na kumkabidhi mashada ya maua.Hivi sasa He Pingping wa nchini China, ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia ya mtu mfupi kuliko wote duniani akiwa na urefu wa sentimeta 73.

Watu 40 wafa 120 wajeruhiwa kwa mafuriko huko Madeira, Ureno

Maafisa wa Uoakoaji nchini Ureno, bado wanaendelea kuwasaka walionusurika, baada ya mafuriko na maporomoko kukumba kisiwa cha kitalii cha Madeira, siku ya Jumamosi. Watu 42 wanakisiwa wamekufa, huku wengine 120 wakiripotiwa kujeruhiwa. Mamia ya wengine wameachwa bila ya makazi, baada ya upepo mkali kuharibu madaraja, barabara na nyumba katika kisiwa hicho maarufu kwa watalii. Timu za madaktari zimeondoka katika mji mkuu wa Lisbon kuelekea katika kisiwa hicho kilichopo katika bahari ya Atlantic, huku maafisa wa Ureno wakihofia idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka. Waziri Mkuu wa Ureno, Jose Socrates alitembelea eneo hilo la mkasa na kuahidi serikali itasaidia katika juhudi za msaada na ukarabati wa kisiwa hicho. Mafuriko hayo yanaripotiwa kuwa mabaya kabisa kuwahi kukumba kisiwa cha Madeira, tangu yale mafuriko ya mwaka 93, ambapo watu wanane walikufa.

Je tutafika?

Hii ni nyumba ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi,Mihuga,iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani.Wakati serikali iko kwenye mchakato wa kujenga shule za kata ili kuinua kiwango cha elimu nchini,nyumba za walimu katika shule za msingi nyingine ziko katika mazingira hatarishi .

Happy Birthday Mugabe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesherehekea siku yake ya kuzaliwa na kufikisha umri wa miaka 86 na kuwa rais mzee kuliko wote duniani. Vyombo vya habari vya Zimbabwe jana jumapili vilimwagia pongezi na sifa kibao rais Robert Mugabe kwa kutimiza umri wa miaka 86.Mashirika yanayomilikiwa na serikali, makundi ya kanisa na baadhi ya mashirika binafsi yaliweka matangazo ya kurasa nzima kwenye magazeti kumpongeza Mugabe na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.Mugabe ambaye amekuwa akiitawala Zimbabwe tangia mwaka 1980 alimiminiwa sifa kibao akitajwa kuwa yeye ndiye mtetezi wa kutokomeza fikra za kikoloni.Mugabe ambaye kwa sasa anapata upinzani mkubwa toka kwa kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai, aliitumia siku yake ya kuzaliwa kimya kimya akiwa na familia yake.Sherehe kubwa zitafanyika jumamosi ijayo mjini Bulawayo ambapo maelfu ya watu wataweza kujumuika na rais Mugabe kusherekea siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Friday, February 19, 2010

China yalaani mkutano wa Obama na Dalai Lama

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya China imelaani vikali mkutano uliofanyika kati ya Rais Barack Obama wa Marekani na kiongozi wa kidini wa jimbo la Tibet, Dalai Lama. Wizara hiyo imesema ilitarajia Marekani itachukua hatua za kuhakikisha inarejesha uhusiano wa nchi hizo mbili katika hali ya kawaida. Mazungumzo kati ya Rais Obama na Dalai Lama yalifanyika katika Ikulu ya Marekani-White House. China ilionya kuwa endapo mazungumzo hayo yatafanyika uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaathirika zaidi. Hata hivyo vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia katika mkutano huo. Rais Obama alielezea nia yake ya kuiunga mkono Tibet katika kutetea na kulinda haki za kidini na kitamaduni za watu wa eneo hilo. Dalai Lama yuko katika ziara ya siku kumi nchini Marekani na anatarajiwa kutoa mihadhara itakayozungumzia kuhusu huruma na amani ya dunia huko California na Florida.

ARV'S ZAZUIA MAAMBUKIZI YA HIV?

Utafiti uliofanywa miongoni mwa wanandoa elfu tatu mia tano wanaougua virusi hivyo barani afrika , ulionyesha kuwa uwezekano wa wagonjwa waliotumia sana dawa za ARV's kuwaambukiza wenzao, ni wa chini mno.Kwa kipindi cha miaka mitatu, zaidi ya watu mia moja waliopata maambukizi mapya ya HIV miongoni mwa waliokuwa wanafanyiwa utafiti huo, ni mtu mmoja tu aliyekuwa anatumia dawa hizo ndiye alieambukizwa.Waliofanya utafiti huo, wanasema huenda mtu huyo aliambukizwa kutokana na mabadiliko mwilini mwake yaliosababishwa na dawa hizo.

Manara akamatwa baada ya kutoroka

AMHAJJI MANARA, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, aliyekimbia baada ya kudhaminiwa katika Kituo cha Polisi Magomeni amekamatwa tena na anashikiliwa na Jeshi hilo kwa mahojiano . Awali, Manara alikamatwa Januari 28, mwaka huu baada ya kutuhumiwa kutapeli magari kwa kutumia jina la Chama Cha Mapinduzi.Baadaye alikimbia dhamana aliyowekewa na mama yake mzazi, hali iliyosababisha mama yake kukamatwa na kuswekwa rumande.Hivyo jeshi hilo lilifanya msako mkali na jana alikamatwa na kufikishwa tena katika kituo cha polisi cha Magomeni.Manara alidaiwa kukodisha magari zaidi ya 40 kutoka kampuni tofauti nchini za kukodisha magari kwa kutumia jina la CCM.Hata hivyo Jeshi hilo lilisema kutokana na kuwa Manara alishakiuka masharti ya dhamana na kuikimbia hawatamwachia tena hadi watakapompeleka mahakamani.

Kakobe, Tanesco Wazichapa Live

MTAFARUKU mkubwa ulizuka jana kati ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship na Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) baada ya walokole wa kanisa hilo kudaiwa kuvamia na kuwapiga wafanyakazi wa Kampuni ya TAKAOKA kutoka Japan na kujeruhi baadhi yao. Wakati TANESCO wakidai walokole hao waliwapiga wafanyakazi hao wa Kijapani ambao baadhi yao walilazwa hospitali, waandishi wa habari waliokuwapo na Askofu wa kanisa hilo, Zachary Kakobe walikanusha kipigo hicho. Meneja Uhusiano wa TANESCO, Badra Masoud, aliliambia Tanzania Daima kuwa tukio hilo lilitokea mita chache kabla ya wafanyakazi hao kufika kwenye kanisa hilo ambako kulikuwa na waumini zaidi ya 200 waliokuwa wametanda. “Ni kweli mafundi wa Kampuni ya TAKAOKA walikwenda eneo hilo kwa ajili ya kusafisha eneo la kuweka nyaya, lakini kabla ya kuanza zoezi lao walivamiwa na kundi la waumini wa kanisa hilo ambao walihisi kuwa wanataka kuanza kazi ya kutandaza nyaya…wakaanza kuwapiga na kuwarushia kila kilichokuwa mbele yao. “Bahati nzuri wale mafundi walikuwa wamevaa kofia maalumu za kulinda kichwa (helmet) ambazo ziliwasaidia kupata matatizo zaidi,” alisema. Alisema katika vurumai hiyo, wafanyakazi watatu walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Palestina iliyoko Sinza kwa ajili ya kupatiwa matibabu. “Wafanyakazi wetu walipigwa kwa nondo, lakini bahati nzuri polisi wakiwa na magari matano walifika kwenye eneo la tukio kutuliza hali hiyo,” alisema Masoud. Alisema kutokana na tukio, wafanyakazi hao waliamua kwenda kuripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mabatini kilichoko Mwananyamala. Hata hivyo, Kakobe aliwaambia waandishi wa habari kuwa baada ya wafanyakazi wa TANESCO kufika katika eneo hilo, waumini wake waliwatimua ili kuzuia upitishaji wa nyaya hizo. TANESCO inapanga kupitisha nyaya za umeme wa kilovolti 132 katika eneo hilo. Kakobe alisema waumini wa kanisa hilo wamechukizwa na hatua hiyo ya serikali kwa kuwa wameshachanga sh milioni 800 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha Televisheni ya Holiness ambacho wanadai kimeota mbawa kutokana na upitishwaji wa nyaya hizo. “Ni kweli waumini waliwatimua, lakini hawakuwa na silaha zozote za kuwapiga wafanyakazi hao…sasa nashangaa kusikia kuna watu eti wamepigwa,” alisema Askofu Kakobe. Alisema kilichotokea ni wafanyakazi hao kuingia ndani ya gari lao lenye namba za usajili T 346 ARR na kisha kuondoka katika eneo hilo baada ya kusikia ving’ora vya magari ya polisi yaliyosheheni askari kwa ajili ya kukabiliana na hali yoyote ya vurugu kama ingetokea. Askari hao walifika katika eneo hilo na kisha baadhi yao kuelekea ndani ya ofisi za Askofu Kakobe ili kupata maelekezo kuhusiana na mgogoro huo. Mnamo saa tano asubuhi, wafanyakazi hao walifika eneo hilo wakiwa kwenye gari maalum kwa ajili ya kupakia na kushusha vitu vizito. Waumini walihisi kuwa limepelekwa pale kwa ajili ya kuchomeka nguzo kubwa za umeme. Wakati wafanyakazi wakiendelea na kazi ya kushusha nguzo hizo, waumini walianza kupigiana simu na kutaarifiana kuhusu tukio hilo. Ghafla waumini kwa mamia walimiminika katika eneo hilo na kusababisha vurugu kubwa kati yao na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya TAKAOKA. Muda mfupi baadaye magari ya polisi yaliwasili katika eneo hilo huku yakipiga ving’ora, hali iliyosababisha wafanyakazi hao kuamua kupakia nguzo zao na kisha kutoweka. Askofu Kakobe alisema askari hao waliingia ndani ya ofisi za kanisa hilo ili kupata ufafanuzi wa hali iliyokuwa ikiendelea katika eneo hilo bila ya kukamata hata muumini mmoja. “Tuliwapa polisi maelezo kuhusu hali ya mambo iliyokuwa ikiendelea hapa,” alisema Askofu Kakobe. Hata hivyo, waandishi wa habari waliokuwa eneo hilo, walisema hawakuona tukio lolote la watu kupigwa. Alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hadi jana jioni ofisi yake haikuwa na taarifa yoyote kuhusiana na vurugu hizo. Alimtaka mwandishi wa habari hizi kuwasiliana na mtu aliyemtaja kwa jina la Masinde aliyeko katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kwa ajili ya ufafanuzi zaidi wa tukio hilo, lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokewa.

Thursday, February 18, 2010

Umewahi kukutana na Mbwa huyu?

Inabidi utumie busara ya hali ya juu kwa mtu kama huyu baada ya kukunyima lifti muda mfupi uliopita ( kama ni wewe ungefanyaje)?




Huu ni ukosefu wa Ajira au?

Kamanda wa Polisi wa viwanja wa vya ndege nchini,Kamishna msaidizi Mwajuma Kiponza(kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari jana madawa yakulevya yaliyokuwa yameifadhiwa kwenye vinyago.Madawa hayo yalikamatwa kutoka kwa mtuhumiwa anayejulikana kwa jina Halid Maunga juzi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa akijiandaa kuyasafirisha kwenda Uingereza.

Maunda Mjamzito ????

Asanteni Ufaransa

BALOZI wa Ufaransa nchini, Jacques de Labriolle, jana amekikabidhi msaada Chama Cha Msalaba Mwekundu tawi la Tanzania, wenye thamani ya takribani Sh milioni 100 za Tanzania kwa kuwasaidia waathirika wa mafuriko wilayani Kilosa katika mkoa wa Morogoro. Balozi Labriolle amesema, Serikali ya Ufaransa imetoa Euro 50,000 kuzisaidia zaidi ya familia 200 zilizokumbwa na mafuriko Kilosa. “Mwezi uliopita, mara moja baada ya maafa haya, Chama Cha Msalaba Mwekundu Ufaransa kimetuambia kwamba hali katika wilaya ya Kilosa ilikuwa mbaya sana na kimetupa ushauri kuitikia ombi la msaada wa dharura lililotolewa na Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania” amesema Balozi huyo katika hotuba aliyoitoa kwa lugha ya Kiswahili. Amesema, fedha hizo zimetumika kununua vifaa vya kuwasaidia waathirika wa Kilosa, vikiwemo vyandarua, vyombo vya kupikia, mahema, dawa za kusafisha maji ya kunywa, na pia kugharamia usambazaji wa maji safi kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.

Mchezaji anayelipwa Faranga kubwa kuliko wote duniani huyu hapa

Cristiano Ronaldo

Kuweni makini na Ombaomba

Pale salender Bridge ambapo anasimama trafiki akivuta magari, kuna mdada alikuwa ndani ya gari lake kwenye foleni akisubiri zamu yake ya kuruhusiwa na trafiki ifike apite. ndipo aliposogea kaka mmoja ombaomba, akasogea kwenye gari la yule dada na kuomba msaada. Dada huyo kwa kumhurumia akamsaidia. Alipompa pesa tu mkono wa yule dada ukaota manyoya ya paka, akachanganyikiwa alipokuwa anaendelea kushangaa trafiki akawa anaruhusu magari ya upande wake yule dada akawa hawezi kuendesha gari, ndipo trafiki akamsogelea na kuuliza kulikoni?! Yule dada akatoa mkono wake na kumuonyesha trafiki na kumsimulia kilichotokea na bahati nzuri yule kaka aliepewa pesa alikuwa mita chache pembeni anamuangalia yule dada. Ikabidi trafiki aende kumuuliza yule ombaomba kulikoni?Ndipo yule ombaomba akamwambia trafiki kuwa yule dada akimbusu tu atapona mkono utarudi kawaida. Basi ikabidi yule dada atelemke aende kumbusu yule kaka, alivyombusu wakapotea wote palepale, gari ya yule dada ikabaki barabarani ndipo trafiki alipoita watu wakaanza kuisukuma ile gari na kuiweka pembeni.Kuna dada mwingine alikuwepo leo kanisani baada ya ibada akawa anatusimulia, yeye alikuwa nyuma ya gari ya huyo dada alishuhudia hilo tukio anasema ni tukio la kweli kabisa ameshuhudia kwa macho yake.Hivyo jamani nawatahadharisha ndugu zangu mlio na moyo wa huruma msipende kutoa pesa zenu hovyo sababu umekutana na maskini.Biblia inasema maskini wapo na wataendelea kuwepo, mwombe Mungu kwanza kila unapotaka kutoa sadaka yako. Mwenye Masikio na Asikie

Askari mstaafu adaiwa kumuua mkewe

ASKARI mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Matiku Ng’enge (55), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kwamba, lilitokea jana saa 11 alfajiri nyumbani kwa wanandoa hao Mazizini Ukonga, Dar es Salaam. Kamanda Shilogile alisema Matiku alianza kuzozana na mkewe Rehema Matiku (42) na kuanza kumshambulia, akamchoma kisu katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo kichwani, tumboni na mikononi. Amesema, mwanamke huyo alipiga kelele na kuokolewa na majirani, lakini kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata, alidondoka na kupoteza fahamu baada ya kuvuja damu nyingi, hali iliyosababisha kifo chake. Shilogile amesema, chanzo cha ugomvi wa wanandoa hao hakijajulikana, ingawa inasadikiwa ni wa kifamilia. Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi ili kufahamu tatizo, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilala, Amana kwa uchunguzi zaidi. Shilogile amesema, mtuhumiwa huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Staki Shari, ingawa baada ya mke wake kufariki dunia, ghafla naye alipata mshtuko na kukimbizwa Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Taarifa zaidi zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinadai mwanamume huyo alikuwa akigombana na mkewe kwa mara kutokana na mwanamke huyo kutotaka kuuzwa kwa ardhi yao ambayo alidai ingeisaidia familia yao. Hata hivyo, kutokana na kikwazo hicho, jana alfajiri mumewe alimkumbushia tena suala hilo, lakini aliendelea kupinga na mume kushikwa na hasira na kuanza kumshambulia kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali.

Agongwa na Kufa akitoroka matibabu Hospital

KIJANA Musa anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-25, amegongwa na gari wakati akitoroka matibatu katika hospitali ya Temeke ya jijini Dar es Salaam. Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Faustine Shilogile, alisema jana kuwa, Alisema marehemu huyo ambaye alikuwa akisumbuliwa na malaria kali alikuwa akitibiwa hospitalini hapo na aligongwa na gari jana alfajiri katika Barabara ya Sokoine wakati akitoroka matibabu.Alisema mashuhuda walimuona Musa akitoka hospitalini hapo huku akikimbia na baadae wakapata taarifa kuwa amegonjwa katika barabara hiyo majira hayo ya alfajiri.Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini, na polisi wanaendelea kumtafuta dereva aliyesababisha kifo hicho.

Mamia wahudhuria mazishi Musoma

MKUU wa Mkoa wa Mara, Kanali Enos Mfuru jana aliongoza maelfu ya wakazi wa Musoma mjini katika mazishi ya watu 17 wa ukoo mmoja waliouawa kikatili na watu wasiojulikana kwa kile kilichodaiwa ni kulipiza kisasi juzi. Akizungumza muda mfupi kabla ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu hao katika Kata ya Butare wilayani humo, Mfuru aliwahakikishia waombolezaji na wananchi wote wa mkoa wa Mara kwamba serikali itawalinda waliobaki na kwamba watadhibiti vitendo hivyo. Alisema msaada huo utajumuisha udhamini katika masomo ya kijana mmoja aliyesalimika katika tukio hilo na madawa kwa ajili ya majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara. Mfuru aliwataka wananchi wa mkoa kushirikiana kwa pamoja na maofisa wa polisi kuhakikisha kwamba, wauaji hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka. "Nawahakikishia wananchi wote wa Mara kwamba, uongozi wenu wa mkoa utafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa mnapata ulinzi wa kutosha ili kuepukana na mauaji kama hayo pamoja na kukomesha kabisa matukio ya namna hii," alisema Mfuru. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Dk Benedicto Mwijarubi, alisema hali ya majeruhi mmoja kati ya watatu waliofikishwa hapo Maria Kawawa (18), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Buhare ni mbaya. "Anakabiliwa na maumivu makali kichwani, jicho lake la kushoto, shingoni na mkono wake wa kushoto umeondolewa moja kwa moja na wauaji hao," alisema Dk Mwijarubi. Alisema mwanafunzi huyo amepoteza zaidi ya lita mbili za damu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa tukio hilo na kwamba, waganga wa hospitali hiyo wanafanya juhudi kuokoa maisha yake. Alifahamisha kuwa hali ya majeruhi wengine wawili Moris Mgaya (40) na Maximillian Roba (20) inaendelea vizuri hospitalini hapo ambapo wamelazwa wakipatiwa matibabu. Miongoni mwa ndugu hao wa ukoo mmoja waliopoteza maisha juzi kwa kukatwakatwa kwa mapanga ni Nyasinde Moris, Mgaya Moris, Mage Moris, Maheri Moris, Alice Moris na Kado Moris. Wengine ni pamoja na Kawawa Kinguye, Angelina Kawawa, Kinguye Kawawa, Mengi Kawawa, Nyarukende Kawawa, Juliana Kawawa, Nyambona Kawawa, Nyanyama Kawawa, Dorika Mgaya, Umbera Mgaya na Sospeter Sopereti. Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Mara Robert Boaz, alisema maofisa wa polisi kwa kushirikiana na wananchi hadi jana jioni inawahoji watu watano ambao wanahusishwa na tukio hilo la kinyama.

Obama kukutana na Dalai Lama

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kukutana hii leo na kiongozi wa kidini wa jimbo la Tibet, Dalai Lama licha ya vitisho vya China kwamba mkutano huo utavuruga zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Rais Obama na Dalai Lama watakutana katika ikulu ya mjini Washington na hawatarajiwi kuonekana pamoja hadharani kama alivyofanya rais wa zamani wa Marekani Georg W Bush, wakati alipokutana na kiongozi huyo wa Tibet. China inamlaumu Dalai Lama kwa kuendeleza juhudi za kutaka jimbo la Tibet lijitenge na China. Rais Obama amesema anakutana na Dalai Lama anayeishi uhamishoni nchini India kwa kuwa ni kiongozi wa kiroho anayeheshimika kimataifa. Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Marekani Hillary Clinton atakutanapia Dalai Lama mjini Washington.

Wednesday, February 17, 2010

Miriam Gerald nje kwa dhamana?

HATIMAYE Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald ameachiwa kwa dhamana baada ya kukaa gerezani kwa siku tatu, kuanzia Ijumaa mchana kwa kukosa dhamana. Mrembo huyo wa mwaka jana, alipelekwa jela kwa kile kilichoelezwa kushambulia pamoja na kuharibu mali. Katika shtaka la kwanza, wanatuhumiwa kumshambulia Shaaban Moshi kwa vitu vyenye ncha kali shtaka lililosomwa na mwendesha mashtaka Inspekta wa Polisi, Nassor Sisiwahy, mbele ya Hakimu, Kwey Lusemwa. Shitaka la pili, watuhumiwa kufanya uharibifu wa mali yenye thamani ya Sh laki 720,000. Mali iliyoelezwa ni vifaa vya muziki. Ijumaa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kupelekwa Gereza la Segerea. Hata hivyo, jana alipata dhamana pamoja na rafiki yake, Kennedy Victor. Baada ya kuruhusiwa na mahakama, Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliwaomba radhi Watanzania kwa yanayotokea kwa washindi wa taji hilo. Lundenga aliyasema hayo jana nje ya Mahakama ya Kinondoni baada ya kumwekea dhamana mrembo wake na kusema: "Hayo ni mambo ya kimaisha na yanaweza kumtokea yeyote." Mrembo huyo aliwasili mahakamani hapo saa 5.15 asubuhi akiwa kwenye gari aina ya Land Cruizer STK 4253 ambalo liliingia Mahakamani hapo kwa kasi akiwa na wenzake wawili na Miriam alishuka akiwa amejifunika mtandio usoni. Baada ya hapo, saa 11.30 washtakiwa hao walipandishwa kizimbani na Hakimu Richard Kabate ambaye aliwaachia kwa dhamana kwa niaba ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kwey Lusema. Wote walitimiza masharti ya dhamana yao na kuwataka kurudi tena mahakamani Februari 25 .

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake Chatangazwa

Adolf Rishard, Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars itakayoshiriki katika michuano ya awali ya kufuzu kushiriki fainali za Afrika za wanawake nchini Afrika Kusini, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 kitakachopambana na timu ya taifa Ethiopia.Mechi hiyo itachezwa Machi 6 mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.Adolf alitangaza majina hayo kwa niaba ya kocha mkuu Charles Boniface ambaye yupo nje ya jiji la Dar es Salaam.Wachezaji hao tayari wameingia kambini jana katika Hosteli ya Lamada iliyopo Ilala jiji Dar es Salaam.Adolf akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Mpira wa miguu nchini TFF alisema kuwa yeye kwa uhakika haifahamu timu ya Ethiopia lakini anacho jua ni timu nzuri na watahakikisha yeye na kocha wake mkuu wanafanya kila liwezekanalo katika kuwaandaa vijana wao Twiga stars wanaoendelea na mazoezi katika Uwanja wa Karume uliopo katika ofisi za TFF.Aliwataja wachezaji watakaoiwakilisha Tanzania kuwa ni Fatma Omari ,Pulkeria Chalaji, Sofia Mwasikila, Mary Masatu, Estar Chabuluma, Fatuma Mstafa, Zena Juma na Fatuma Bushiri.Wengine ni pamoja na Neema Kuga, Hindu Muharami, Aisha Rashidi, Fadhila Kilele, Mwanahamisi Omary, Fatuma Hatibu, Mwanaidi Temba, Zena Hamisi na Hellen Peter.Katika orodha hiyo pia wamo Pridian Daud Ettoo Mlezi, Fadhia Hamadi, Maimuna Said, Nasiria Ashri Abdallah, Mwajuma Abdalaah, Hakima Mwasilimu Hamis ,Warda Khalid Abdallah, Musimu Suluhu Hussan na Anita Elias.

Haya ni mauaji ya kinyama - Watu 17 wa Ukoo mmoja wauawa kwa Sime Musoma

WATU 17 wa familia tatu za ukoo mmoja, wamefariki dunia na wengine watano kunusurika baada ya kushambuliwa usiku wa manane na kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi. Habari zilizolifikia jana zimeeleza kuwa tukio hilo lillitokea saa 6:00 usiku wa kuamkia jana katika kitongoji cha Mgarajabo Buhare Musoma mjini mkoani Mara. Kwa mujibu wa habari hizo zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Robert Boaz, mbali na mauaji hayo, wauaji hao pia waliua ng'ombe wa jamaa za marehemu hao. Kamanda Boaz alitaja moja ya familia zilizofikwa na mkasa huo kuwa ni ya Kawawa Nyarukende ambako watu wanane waliuawa ndani ya nyumba hiyo na yeye mwenyewe kujeruhiwa vibaya na amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara. Kwa mujibu wa kamanda huyo, familia nyingine iliyovamiwa ni ya Mgaya Nyarukende ambayo watu wawili waliuawa na yeye kujeruhiwa. Familia ya Morisi Mgaya ambako waliuawa watu saba. "Watu wote waliouawa ni wa ukoo mmoja na ndio maana unaona majina yanafanana," alisema Kamanda Boaz na kuongeza: "Ndani ya nyumba ya Morisi Mgaya waliuawa watu saba na yeye kujeruhiwa vibaya. Wauaji hao walikuwa wanatumia vitu vyenye bapa kali kama mapanga na sime". Kamanda Boaz aliwataja waliouawa kuwa ni Nyasinde Morisi, Mgaya Morisi, Mage Morisi, Maheri Morisi, Allice Morisi na Kado Morisi. Wengine ni Kawawa Kinguye, Angelina Kawawa, Kinguye Kawawa, Mengi Kawawa, Nyarukende Kawawa, Juliana Kawawa, Nyambona Kawawa, Nyanyama Kawawa, Dorika Mgaya, Umbera Mgaya na mwanafunzi wa sekondari ya Mkirara, Sospeter Sopereti ambaye alikuwa mgeni wa familia hiyo. "Nadhani walikuwa watu wengi maana nyumba zile zimetawanyika sana moja iko umbali wa kama mita 300, hivyo isingewezekana wamalize kufanya unyama hapa halafu waende kwingine,"alisema kamanda. Alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba, baada ya mauaji hayo hakukuwa na tukio lolote la wizi hali inayoonyesha kuwa huenda mauaji hayo yamefanyika ili kulipiza kisasi. Hata hivyo baadaye jana kamanda Boaz alilieleza kuwa polisi inawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo huku wakiendelea na msako wa kuwatafuta wengine. Kamanda Boaz :"Hivi sasa ni mapema kuwataja watuhumiwa. Kwanza kazi bado inaendelea na kufanya hivyo itakuwa ni kuharibu upelelezi". Muuguzi Mkuu wa hospitali ya mkoa wa Mara, Benedictor Mwijarubi alikiri kupokea majeruhi wanne wa tukio hilo na kufahamisha kuwa majeruhi mmoja alikufa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo. Alibainisha kuwa Dorika Siti (70) alifia hospitalini hapo kwa sababu ya kuvuja damu nyingi kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata sehemu mbalimbali mwilini. Muuguzi huyo aliwataja majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo kuwa ni Morisi Mugaya (40) Maximilliani Roba (20) na Maria Kawawa (18), alisema hali za majeruhi hao sio nzuri na madaktari wanaendelea na jitihada kuokoa maisha yao. Akinukuu maelezo ya majeruhi hao, muuguzi huyo alisema tukio hilo lilitokea kwa wauaji hao kuvunja milango ya wenyeji wakiwa wamelala. Alisema watoto wawili wadogo walipona baada ya kulala katikati ya maiti na hivyo kudhaniwa kuwa wamekufa. Alisema majeruhi hao walipona baada ya kupiga kelele na watu kuanza kujitokeza kutoa msaada kulikowafanya wauaji kukimbia. Wakizungumza na gazeti hili kutoka eneo la tukio, baadhi ya mashuhuda walisema mauaji hayo yamefanyika kulipa kisasi kufuatia tukio linalodaiwa kutokea mwaka 2006 ambapo watu wawili wa kabila la Wazanaki waliuawa katika jaribio la wizi wa mifugo kwenye familia hizo. Kwa mujibu wa mashuhuda hao ambao hawakutaka kutajwa , ndugu wa marehemu hao walilaani mauaji hayo na kusema ndugu zao hawakuwa wezi wa mifugo bali wawindaji wa nungunungu na nguruwe pori. Inadaiwa kuwa katika tukio hilo la mwaka 2006, Kawawa ambaye jana alivamiwa nyumbani kwake, alikamatwa akihusishwa na tukio la mwaka huo , lakini baadaye aliachiwa huru. Kabla ya kuvamiwa jana, akiwa mahabusu kwa tuhuma za tukio la mwaka 2006, watu wasiojulikana walifika nyumbani kwake na kufanya mauaji ya watu wawili kisha wakaondoka. Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Enock Mfuru alisema limetokana na kulipizana visasi na akaliagiza jeshi la polisi kuhakikisha linawasaka na kuwatia mbaroni wahusika wote aliosema wameuchafua mji wa Musoma. Tukio hilo limeufanya mji mzima wa Musoma kuzizima kwa simanzi huku wengi wakidai kuwa wahusika watakuwa wanafahamika kwa kuwa tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya tangu mwaka 2005 walipouawa watuhumiwa wa wizi wa mifugo.

Hatimaje Mama mkwe wa Rais Obama ahamia White House

Inasemekana kuwa mama mzazi wa Mke wa Rais wa Marekani Mrs. Robinson (pichani) amehamia kwa muda Ikulu ya Marekani ili kuwasaidia Wajukuu zake kutokana na ukweli wa Kuwa Obama na Mkewe hutumia muda mwingi kusafiri katika shughuli zao za kazi.

Sherehe za Valentine zampeleka Ahera

HAMIS Said (22), mkazi wa Ukonga Stakishari, amekufa baada ya kuzidiwa na maji wakati akiogolea katika bwawa la Pub iliyojulikana Kiota. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 4 usiku, huko maeneo ya Ukonga Stakishari.Amesema kuwa kijana huyo alikuwa ni mteja katika baa hiyo na alikwenda kwa ajili kupata vinywaji katika baa hiyo na baadae kuhitaji huduma hiyo ya uogeleaji.Amesema ilidaiwa kijana huyo wakati akiogelea alizidiwa na maji hayo na baadae maiti yake kukuta ikiogelea majini humo.Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Amana na polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Tuesday, February 16, 2010

Hatimaye Wamarekani wamkamata Kamanda Mkuu wa Taliban

Kamanda mkuu wa kundi la Taliban,Mullah Abdul Ghani Baradar amekamatwa na maafisa wa ujasusi nchini Pakistan. Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la New York Times, maafisa wa Marekani wamethibitisha kwamba Mullah Abdul Ghani Baradar alikamatwa na maafisa wa ujasusi wa Marekani wakishirikiana na wenzao wa Pakistan. Mtu huyo anazuiliwa na maafisa wa Pakistan, Mullah Baradar ndiye anayeongoza harakati za kundi la Taliban nchini Afghanistan. Kamanda huyo ni mmoja wa viongozi katika baraza kuu la kundi hilo akishikilia wadhifa wa naibu kiongozi wa Taliban . Kiongozi mkuu wa Taliban Mullah Muhammad Omar ameendelea kuwa mafichoni.

TID atangaza ndoa ???

TID akiwa katikati ya perfomance Platinum Club Mikocheni, aliamua kuwashangaza watu alipozima muziki na kutangaza kuwa yuko tayari kuoa, kuhangaika tena sasa baaaaasi. TID alikiri mbele ya umati mkubwa wa watu waliopo hapo ukumbini kuwa KINANA ndie mwanamke aliemchaguliwa kuwa mke kama inavyoonekana pichani

Hapi bethidei Kalunde band

Deo Mwanambilimbi alikiongoza kikosi kizima cha Kalunde Band kusherehekea kwa mpigo siku ya wapendanao pamoja na hepi besdei ya nne ya kuzaliwa bendi hio ukumbi wa Rainbow Club Mbezi Beach jijini Dar usiku wa tarehe 14.

Hispania kuwachukua wafungwa kutoka jela ya Guantanamo?

Waziri wa mambo ya nje wa Uhispania Miguel Angel Moratinos amesema nchi yake iko tayari kuwapokea wafungwa watano kutoka jela ya Marekani ya Guantanamo Bay iliyoko katika kisiwa cha Cuba.Hata hivyo waziri huyo amekataa kusema wafungwa hao ni raia wa nchi gani . Kiasi cha nchi 10 wanachama wa Umoja wa Ulaya hadi sasa zimeridhia kuwapokea wafungwa kutoka jela hiyo.Mara ya kwanza Uhispania ilikubali kuwapokea wafungwa kutoka jela ya Guantanamo mwaka uliopita wakati uhusiano kati yake na Marekani ulipoanza kuimarika kufuatia ziara ya waziri mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero katika ikulu ya Marekani kwa mara ya kwanza tangu Uhispania ilipowaondoa wanajeshi wake nchini Iraq mwaka 2004. Uhusiano huo hata hivyo uliingia dosari mwezi huu baada ya rais Obama kusema hatohudhuria mkutano kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya unaotarajiwa kuandaliwa mjini Madrid mwezi Mei.

SMZ yamwaga Ajira 500 kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), inatarajia kuajiri walimu 500 ili kupunguza upungufu wa watalaam hao katika shule za msingi na sekondari visiwani. Hayo yalielezwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amal, Haroun Ali Suleiman, baada ya kujitokeza upungufu wa walimu kwa baadhi ya shule. Alisema walimu hao wapya wanataaluma ya cheti na Stashahada na kazi hiyo itafanyika katika wilaya tatu ambazo zimeonekana kuwa na upungufu wa walimu Zanzibar. Waziri Haroun, alisema serikali imo katika mikakati ya kuimarisha sekta ya elimu kwa vile ina umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Serikali wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini kwa wananchi wake. Wilaya zitakazonufaika na mpango huo ni Micheweni na Mkoani Kisiwani Pemba na Wilaya ya Kaskazini A Kisiwani Unguja. Aidha alisema serikali inaendelea na mpango wake wa kujenga nyumba za walimu ili waishi karibu na vituo vya kazi.Hata hivyo, alisema mpango wa kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar pia utazingatia maslahi ya walimu kama vile mishahara na posho ili kuwawekea mazingira mazuri ya kazi. Tayari serikali imeamua kurejesha posho la asilimia 25 la kufundishia kwa walimu ili kuwapunguzia ukali wa maisha, kama ilivyokuwa imeamuliwa na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani mwaka 2007. Hata hivyo, shule nyingi hivi sasa Zanzibar zinakabiliwa na uhaba wa walimu wa sayansi na hisabati na kuathiri maendeleo ya wanafunzi wengi visiwani katika masomo

Je wajua Unywaji wa maji ni dawa?

Unywaji wa glass 8 za maji kila siku unasaidia kufanya mwili kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito usiohitajika

Kilio TEGETA

Wanafunzi na walimu wa Shule ya sekondari Tegeta nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakiangalia masalia ya vifaa mbalimbali vilivyoteketea kwa moto baada ya bweni lao kuwaka moto juzi usiku. Hakuna mwanafunzi aliyeungua na chanzo cha moto huo bado hakijajulikana hadi sasa.

Bi Kidude bado yumo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Machinga watunishiana Misuli na Mgambo wa jiji


Mgambo wa jiji na Mfanyabiashara wa mifuko ya plastiki wakiwa wamekunjana baada ya mfanyabiashara huyo kukutwa akiendelea na biashara yake katika eneo la Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam jana ambalo haliluhusiwi kwa wafanyabiashara hao.

TBL kuongeza bei ya Bia?????!!!!!!!!!

KAMPUNI ya Bia nchini (TBL) imetangaza kupandisha bei ya bia rejareja na jumla kuanzia leo Jumanne. TBL imeagiza kwamba, nyongeza ya bei ya chupa moja kwa mnywaji isizidi sh 100. Kampuni hiyo imesema, bei imeongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya malighafi, kupanda gharama za uzalishaji, usafiri, mafuta, na mabadiliko ya kiwango cha kubadilisha fedha. Baadhi ya bia zenye ujazo wa mililita 500 zilizokuwa zikiuzwa mtaani sh 1,300 sasa zitakuwa sh 1,400 ambazo ni Safari lager, Kilimanjaro, Bingwa, Ndovu special Malt na balimi. Kwa baadhi ya bia zenye ujazo wa mililita 330 ambazo zitauzwa sh 1,200 kwa rejareja ni Safari Lager, Kilimanjaro, na Tusker Lager.

Vichaa,wafu watumika kwenye ufisadi wa kuiba bilioni 6.8 za ruzuku ya pembejeo za kilimo

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay, yupo tayari kujiuzulu endapo mamlaka za uteuzi zitamtaka awajibike kutokana na kashfa ya ufisadi wa fedha za ruzuku ya pembejeo za kilimo inayowakabili viongozi mkoani humo. Njoolay amewaeleza waandishi wa habari kuwa, yupo tayari kujiuzulu ikiwa hana budi kufanya hivyo. Ametoa msimamo huo baada ya kupokea taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza kashfa ya matumizi mabaya fedha za ruzuku ya pembejeo za kilimo kupitia mfumo wa vocha. Inadaiwa kuwa,viongozi mkoani humo wametumia visivyo Sh bilioni 6.8,za ruzuku. “Uongozi wa Mkoa wa Rukwa unaiomba radhi sana serikali kwa kashfa hii iliyotokea mkoani na tutakuwa tayari kuwajibika kisiasa kama hapana budi,” imesema sehemu ya taarifa ya Njoolay aliyoitoa kwa waandishi wa habari. Taarifa ya tume hiyo ya watu tisa iliyofanya uchunguzi kwa takribani mwezi mmoja, imebainisha kuwa waliohusika na ufisadi huo ni watendaji 43 wa vijiji, mawakala 23, watumishi wanne wa kilimo ambao wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa mujibu wa Njoolay,wenye nyadhifa za kisiasa waliobainika kuhusika na kashfa hiyo wakiwemo madiwani na wakuu wa wilaya watafikishwa kwenye vyama vyao vya kisiasa ili washughulikiwe huko. Taarifa ya Njoolay imeeleza kuwa, uchunguzi wa tume umebaini mambo mengine kadhaa ikiwa ni pamoja na mkoa, wilaya na vijiji kutokuwa makini kusimamia na kufuatilia kwa karibu usambazaji wa ruzuku ya pembejeo ya kilimo kwa wakulima. Kwa mujibu wa taarifa hiyo,'wajanja' walitumia mwanya huo wa Serikali kutofuatilia kwa makini kuiibia Serikali mabilioni hayo ya fedha. Kazi ya kufanya hesabu haijakamilika,lakini kiasi kilichokuwa kimechukuliwa benki ni Sh bilioni 6.8 na kilichobaki ni Sh bilioni 1.6 tu. Kati ya hizo kiasi kilichotumika vizuri, asilimia 25 zimetumika Sumbawanga, asilimia 30 Nkasi na asilimia 80 80 wilayani Mpanda. Waliohusika kuiba fedha hizo za Serikali walitumia mbinu kadhaa ikiwa ni pamoja na kughushi sahihi za wakulima, kuandikisha wakulima hewa, wafu, watoto,na vichaa. Mbinu zingine ni pamoja na kuwahonga wakulima fedha kidogo kati ya Sh 2,000 na 7,000 ili watie saini vocha bila kupata mbolea na pia kuwapatia wakulima idadi ndogo ya mbolea kuliko kiasi halisi walichosainishwa. Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa imeagiza hatua kadhaa zichukuliwe zikiwemo za kuipongeza Wilaya ya Mpanda kwa kusimamia kwa ufanisi suala hili na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Serikali waliolegalega kufuatilia kwa ukaribu zoezi hili. Hatua nyingine ni pamoja na mawakala wote na watendaji walioibia Serikali wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na tume iendelee na uchunguzi kuwabaini wengine, kuna uwezekano idadi ya watuhumiwa ikaongezeka. Tume ya kuchunguza uozo huo uliokuwa ukipigiwa kelele na wakulima wengi waliolalamika kukosa pembejeo za kilimo msimu huu, iliundwa Januari 11, mwaka huu na mkuu wa mkoa huyo.

Mambo usiyoyajua kuhusu Flora Mbasha

Jina Halisi : Frola Henry Mayallah
Kuzaliwa: 1983
Jina la Baba : Henry Mayallah
Jina la Mama : Caroline Moses Kulola
Kabila : Msukuma
Ndugu : Benjamini, Dorcus, Suzy & Esther
Shule aliyosoma : Taqwa Secondary school Mwanza
Mume : Emmanuel Mbasha
Mtoto : Eliza
kikundi cha kwanza kuimba : Bugando Divine Singer Mwanza
Vitu anavyopenda : Kuimba na kuchati na marafiki
Flora aliolewa na Emmanuel Mbasha tarehe 22/09/2002 katika kanisa la E. A. G. T Mwanza na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anayejulikana kwa jina la Eliza, na tumegundua kuwa Flora ni mjukuu wa mchungaji maarufu nchini Moses Kulola ( yaani ni babu yake mzaa Mama)

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote