Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, March 31, 2010

Mauaji Musoma mganga aongezwa

Kesi ya mauji ya kikatili ya watu 17 wa ukoo mmoja imechukua sura mpya baada ya mtu anayesadikiwa kuwa mganga wa kienyeji kuunganishwa kesi ya mauaji inayowakabili watuhumiwa wengine 18. Mganga huyo ambaye ni mwanamke pekee katika kesi hiyo, alitajwa kuwa ni Mariam Sivanus Masatu, anadaiwa kufanikisha mipango ya mauaji hayo. Masatu jana alipandisha kizimbani kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka la kushiriki katika mauaji hayo yaliotokea usiku wa Februari 16, mwaka huu katika eneo la Buhare, nje kidogo ya Manispaa ya Musoma. Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi, Gabriel Bonanza, alidai mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Husen Mushi, kuwa kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kunaongeza idadi ya kutoka 19 hadi 20, ingawa alisema mtuhumiwa mmoja kati yao amefariki dunia hivyo kubakia watuhumiwa 19. Alimtaja mtuhumiwa aliyefariki kuwa ni Daudi Nyamagati Makika huku akiitaarifu mahakama kuwa mtuhumiwa mwingine, Bundara Ikaka, alishindwa kufika mahakamani jana kutokana na kuwa mgonjwa na kwamba amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara. Wathumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote dhidi ya mashitaka 17 ya mauaji na matatu ya kujaribu kuua ambayo yanawakabili. Walirejeshwa rumande hadi Aprili 14, mwaka huu. Polisi wengi walimwagwa kuimarisha ulinzi ili kuepusha uwezekano wa watuhumiwa hao kushambuliwa na watu wenye hasira. Wakazi wengi wa manispaa ya Musoma walijitokeza kuwashuhudia watuhumiwa wakiingia mahakamani. Hati ya mashitaka iliyosomewa watuhumiwa hao, ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao waliwaua watu 17 kwa kukusudia wakati wakijua ni kosa. Watuhumiwa katika kesi hiyo ni Marwa Mau Mgaya (16), Matiko Mgasa, Juma Mgaya, Juma Kinonko, Daudi Nyamagati, ambaye ni marehemu, Aloyce Nyakumu, Bahati Simeo, Nyakangara Wambura na Nyakangara Masemere. Wengine ni Kumbata Alphonce, Alphonce Nyabugimbi, Sodaki Alphonce, Mikindo Mgendi, Mole Magesa, Vedastus Nyangeta na Sospiter Mbita, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Nsingi Kukirango Usiku wa Februari 16 mwaka huu katika mtaa wa Bugaranjabho watu wasiofahamika walivamia familia tatu za ukoo mmoja na kuwaua kwa kuwachinja na kuwaatakata mapanga watu 17 wakiwemo watoto wachanga kwa kile kilichadaiwa ni ulipizaji wa visasi.

Tahadhari kwa wanywaji wa Windhoek na Heineken

KAMPUNI bia ya Mabibo Beer inspirit ya jijini Dar es Salaam imetoa tahadhari kwa wananchi kwa kuwa na wimbi kubwa la uingizwaji wa bia bandia nchini aina ya Heineken na Windhoek. Kampuni hiyo imesema vinywaji hivyo huingizwa nchini kupitia wao lakini kwa sasa kuna watu binafsi wamejitokeza kuingiza bia hizo bandia na kuzisambaza wakitumia nembo hizo kinyume na sheria.

KOVA aamuru kufungwa kwa BAR zote zilizopo karibu na Vituo vya POLICE

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameagiza baa zote zilizopo karibu na vituo vya polisi katika jiji la Dar es Salaam zifungwe sizieneldee na biashara hiyo kwa usalama zaidi wa vituo. Kamanda Kova alitoa tamko hilo jana ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari.Amesema lengo la kufunga baa hizo ni kupisha usalama wa vituo na kupisha huduma hiyo muhimu ambayo baa imeonekana ni moja ya vikwazo inayoikabili vituo hivyo.Amesema baa hazina umuhimu kama vituo vya polisi na wanafanya mpango ubadilishwa kuendesha shughuli hizo na kupewa leseni za kuwa maduka ya bidhaa nyingine za kawaida.

`Liyumba ana kesi ya kujibu`

Upande wa Jamhuri katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.1 dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, umeiomba mahakama kumuona ana kesi ya kujibu. Upande wa Jamhuri umetoa hoja hiyo kwa kubainisha kuwa Liyumba alihusika kupitisha malipo ya ujenzi wa ghorofa kabla ya kibali cha bodi ya BoT. Wakijibu hoja za upande wa utetezi, upande wa Jamhuri umedai kuwa Liyumba anadaiwa kufanya mabadiliko hayo katika mradi huo bila kwanza kuomba idhini ya bodi na badala yake aliomba kibali baada ya kufanya mabadiliko. Hoja hizo zimewasilishwa jana alasiri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Ilidaiwa kuwa katika ushahidi uliotolewa na mashahidi nane dhidi ya mshitakiwa huyo, ni rai ya upande wa Jamhuri kwamba mahakama imuone mshitakiwa ana kesi ya kujibu. Hata hivyo, mahakama baada ya kupokea hoja za pande zote mbili kwa njia ya maandishi, hatma ya Liyumba kujitetea au kuachiwa huru itajulikana Aprili 9, mwaka huu. Pia upande huo wa mashtaka umeeleza kwamba ushahidi huo na kupitia vielelezo 13 vinatosha kabisa kuishawishi mahakama kumuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu. Machi 22, mwaka huu, upande wa utetezi uliomba mahakama kumuona mshitakiwa hana kesi ya kujibu baada ya ushahidi uliotolewa kutokuwa na nguvu hivyo mahakama imuachie huru. Machi 15, mwaka huu upande wa mashtaka ulifunga ushahidi dhidi ya kesi hiyo ambapo mahakama iliamuru pande zote ziwasilishe hoja za kama mshtaka ana kesi ya kujibu au la, kwa njia ya maandishi.
Chanzo: Nipashe

Mama Kikwete anusurika katika ajali Mara

MKE wa Rais Mama Salma Kikwete anusurika kifo kwa ajali mbaya baada ya msafara wake kuingia doa kwa kuvamiwa na lori na kugonga magari matatu ya msafara huo. Ajali hiyo ilitokea jana wilayani Rorya mkoani Mara wakati Mama Salma akiwa ziarani mkoani humo. Kamanda wa Polisi Tarime, Bw. Constantine Masawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alisema lori hilo lilisimamishwa na askari wa barabarani lisimame ili kupisha msafara huo na kukaidi na kuingia barabarani na kusababisha ajali hiyo.Amesema kuwa lori hilo liligonga magari matatu ya nyuma ya msafara huo na kusababisha ajali ambayo haikuwa ya lazima kwa muda huo.Amesema lori hilo lilikuwa linatokea nchini Kenya ambapo ilidaiwa pia lori hilo lilikuwa limebeba mali za magendo.Hivyo imedaiwa dereva huyo ameshikiliwa na jeshi hilo ili kujibu tuhuma hizo.Hata hivyo hakuna aliyeweza kupoteza maisha katika ajali hiyo.

Ujerumani launda Jopo maalum kuchunguza malalamiko ya dhuluma za kijinsia

Baraza la mawaziri la Ujerumani limeunda jopo maalum litakalovichunguza visa vya madai ya dhuluma za kijinsia vilivyotokea tangu miaka ya 1950 katika shule za Kikatoliki na za binafsi.Jopo hilo litasimamiwa na wizara za Sheria, Masuala ya Jamii na Elimu. Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria Sabine Leutheusser-Schnarrenberger,wajibu wa jopo hilo ni kujaribu kuhakikisha kuwa madai mengine mapya yanaripotiwa kabla ya kumalizika muda uliowekwa wa kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu wa kijinsia.Waziri wa masuala ya Jamii wa zamani,Christine Bergmann ndiye aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa jopo linalochunguza visa vilivyotokea muda mrefu uliopita ambavyo haviwezi kuchunguzwa na polisi. Mpaka sasa watu 250 walioathirika wamejitokeza.Wakati huohuo Papa Benedict wa XVI alilikubali ombi la kujiuzulu la askofu mmoja wa Kanisa Katoliki la Ireland aliyekuwa msaidizi wa binafsi wa mapapa 3 waliomtangulia.Askofu John Magee wa Cloyne,Ireland alitajwa katika uchunguzi wa mwaka uliopita akidaiwa kuwa hakuchukua hatua mwafaka wakati visa vya dhuluma za kijinsia viliporipotiwa kutokea katika dayosisi yake

Magardener kazi kwenu




CCJ yapokea kigogo wa CCM

JANA mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Bw. Fred Mpendazoe ametangaza rasmi kujiengua CCM na kujiunga na Chama cha Jamii CCJ. Hivyo kutokana na maamuzi hayo chama hicho kipya cha jaamii kilichotangaza awali kuwa kuna vigogo wa CCM watakifata chama hicho hivyo imethibitisha kauli hiyo baada ya mbunge huyo kuwa wa kwanza kujiengua na CCM na kujiunga huko.Alisema amejiengua na CCM ili kuweza kutetea maslahi ya wananchi wanyonge ambapo ameona ndani ya CCM jambo ambalo halitaweza kutekelezwa kwa kuwa kila mtu anatetea masilahi yake binafsi na si kutazama wananchi wapiga kura.Alifafanua kuwa serikali inayoundwa na CCM inayumba kwa kushindwa kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo la Richmond ambalo lilihusisha serikali kuipa zabuni ya kufua umeme wa dharura kampuni hiyo bila kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma, kashfa ya mgodi wa Kiwira kuuzwa kwa bei nafuu na mkataba wa uendeshaji wa Shirika la Reli (TRL) ambao umezorotesha kabisa huduma za reli ya kati. Hivyo kwa kujiunga kwake ataweza kurekebisha mambo hayo kwa kujiunga na chama hicho.Alisema CCM imetekwa na wafanyabishara wanaojikita katika kuwania nyadhifa mbalimbali kwa lengo la kuficha maovu yao badala ya kuwatetea wananchi"Nimeishi kwa matumaini ndani ya CCM kwa muda mrefu na sasa natangaza wazi kuwa nakihama chama hicho na kuhamia chama mbadala ambacho ni CCJ," alisema Mpendazoe

Monday, March 29, 2010

Mzee wa miaka 96 aoa binti wa miaka 30

kibabu cha umri wa miaka 96 wa nchini Taiwan kimekuwa gumzo nchini humo baada ya kufunga ndoa na mwanamke aliyemzidi miaka 66. Babu Lin Chung ameweka rekodi ya kuwa bwana harusi mwenye umri mkubwa kuliko wote nchini Taiwan baada ya kufunga ndoa na mwanamke mwenye umri wa miaka 30.Chung amekuwa gumzo kwenye kitongoji cha Tainan baada ya kumuoa mwanamke huyo anayetoka maeneo ya ukanda wa kati nchini China katika jimbo la Hunan.Chung ambaye hakuwahi kuoa katika ujana wake, ana watoto wawili aliojitolea kuwalea tangia walipokuwa wadogo ambao hivi sasa mmoja kati ya watoto hao ana umri wa miaka 68.Chung anadai kwamba miaka mitatu iliyopita, alipewa maelezo na Mungu aende kwenye jimbo la Hunan nchini China ili kumtafuta mwanamke anayekuja kuwa mke wake.Chung alifunga ndoa na mwanamke huyo hivi karibuni pamoja na upinzani mkali toka kwa mwanae huyo wa kujitolea ambaye alikuwa akimuona babu huyo kama amelaghaiwa."Inanibidi niwe na mwenza katika uzee wangu... sikuwahi kuwa na mke, kwanini hivi sasa hataki mimi nioe", alisema Mzee Chung.

Balaa lingine Mara!

AJUZA mwenye miaka kati ya 90-100 Sifia Makubo amenyofolewa miguu yake yote miwili kwa panga na sasa yupo hospitali akiwa mahtuti. Ajuza huyo alikumbwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki nyumbani kwake Ngerengere kata ya Sirari tarafa ya Inchugu wilayani Tarime Mkoani Mara. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya Costantine Massawe alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 27 mwaka huu na ajuza huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya Tarime. Imedaiwa kwamba ukatili huo amefanyiwa na Mkazi wa kijiji cha Kubiterere ambaye hakufahamika jina lake mara moja. Kamanda Massawe akielezea mkasa huo zaidi alisema mtuhumiwa huyo akiwa na panga alivamia nyumba ya bibi Huyo na kuanza Kumshambulia kwa Kumkata kata mapanga na kumwacha akivuja damu nyingi huku akilia kuomba msaada , Kamanda Massawe alisema kuwa Mjukuu wa Bibi huyo alisikia kilio cha bibi yake kuomba msaada na kuanza kupiga yowe ambapo wananchi Majirani walijitokeza mara moja na kumfukuza hadi walipomtia mikononi na kuanza kumpiga. Mtuhumiwa huyo alikatwa panga tumboni hadi utumbo wote kutoka nje. Polisi Kituo cha Sirari walifika waliwahi kufika kwenye kituo kumuokoa mtuhumiwa kwa kumfikisha hospitalini na ajuza huyo. Mtuhumiwa alifariki siku hiyo hiyo na ajuza huyo bado amelazwa Wodi namba 6 kwa matibabu ya miguu yake yote Miwili na majeraha ya mkono wa kushoto.

Serikali yafikiria kuitanua barabara ya Morogoro?


SERIKALI ipo katika mazungumzo na wahisani ili kuweza kupanua barabara ya Morogoro kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze, kwa kiwango cha njia mbili zitakazosaidia kurahisisha usafiri na kuondokana na ajali zisizo za lazima. Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari Ruvu mkoani Pwani, kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ruvu iliyopo Ruvu Darajani. Alisema ajali nyingi zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembamba wa barabara hiyo kama inavyofikiriwa, bali zinatokana na uzembe wa madereva ambapo wengi wao wameonekana wakiendesha kwa kukiuka kanuni za usalama barabarani ikiwemo kwenda mwendo kasi kupita kiasi, kulewa na madereva wengine hupitiwa na usingizi wakiwa waneendesha magari. Dk Kawambwa amezungumza hayo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea ajali mbaya katika eneo la Kibamba Darajani jijini Dar es Salaam, ambako watu 10 akiwamo mama mjamzito aliyepasuka tumbo, walifariki dunia papo hapo baada ya lori la mafuta kuiangukia daladala. Wembamba wa eneo ilipotokea ajali ya juzi na kuua watu wote kwenye daladala ni changamoto kwa serikali kutanua barabara hiyo, lakini ajali zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembbama wa barabara, kwani ajali zinazotokea katika eneo hilo zinatokana na uzembe wa madereva,alisema Dk Kawambwa. Akizungumzia kuhusiana na mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo, Dk Kawambwa alisema mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka huu na utaanzia kutanua eneo la Mwenge hadi Tegeta kwa ngazi ya njia mbili za kuingia na kutoka ili kusaidia kuondokana na msongamano wa magari katika barabara hiyo. Tunajua tutapata changamoto kubwa kwa wananchi waliojenga kandokando ya barabara hizo tunazotaka kuzitanua, lakini tutajitahidi kwenda na wakati kwa kuendelea na ujenzi huo huku mazungumzo na wananchi hao katika maeneo mengine ambayo yatakuwa bado hatujayafikia yakiendelea ili kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa kwa kiwango cha njia mbili,alisema Dk Kawambwa. Pia Dk Kawambwa alisema ili kuondokana na tatizo kubwa la msongamano wa magari ndani ya jiji la Dar es Salaam, kupitia mradi wa kutanua barabara 10 za jiji hilo la Dar es Salaam utafanyika kwa lengo la kurahisisha usafiri katikati ya jiji hilo. Alisema mradi huo utafanya kazi kwa kutumia barabara tofauti na zilizo zoeleka katika usafiri wa daladala kama barabara ya Morogoro na Mandela. Tunatarajia kutumia njia nyingine na hazitamlazimisha dereva kutumia barabara moja ya Morogoro ili afike Posta ama Ubungo bali ataweza kupita ya kutokea Kigogo na kumuwezesha kufika ubungo ama Posta hiyo ikiwa ni malengo ya kuondokana na msongamano wa foleni katika barabara hizo. Aliongeza kuwa mradi huo pia utasaidia kuondoa mrundikano wa malori kuwa katika foleni moja na magari madogo hasa katika barabara ya Jangwani, ambapo imeonekana malori yakiitumia pamoja na magari mengine madogo ambapo mradi huo ukianza malori na magari mengine hayatakuwa katika barabara moja.

Ajali ya Kibamba yaacha Yatima

Mtoto Mwanaidi Ibrahim (4) (kulia), ambaye wazazi wake wote wawili walifariki dunia katika ajali ya gari, Kibamba akiwa amebebwa na Mama yake mdogo, Sharifa Ally wakati wa maombolezo ya msiba wa wazazi wake hao, Kibamba, Dar es Salaam jana.

Watoto wa Sayansi na Tekelinalokujia ndio hawa!

Mahakama yasomewa waraka kesi ya mauaji

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepokea waraka ambao inadaiwa uliandikwa na Benson Urio kabla ya kutenda kosa baada ya kushtakiwa kwa jaribio la mauaji. Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2008, Benson anadaiwa kujaribu kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Omega Leweta ambaye ni mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam baada ya kumvizia akiwa usingizini na kuanza kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili. Pia mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa baada ya kumkatakata mpenzi wake, Benson pia anadaiwa kujikatakata shingoni kwa panga kwa lengo la kujiua sambamba na mpenzi wake huyo. Waraka huo ambao unadaiwa kuandikwa na mshtakiwa huyo kwenda kwa mama yake mzazi, Felister Urio ulisomwa juzi mahakamani hapo na shahidi wa tano katika kesi hiyo D/Sgt. Gotard Ipande wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo. Waraka huo unaonyesha dhamira ya mshtakiwa huyo kumuua mpenzi wake na baadaye kujiua. Katika waraka huo, Benson anaeleza jinsi mama yake alivyomlea na kumtakia maisha mema, lakini baadaye anaanza kueleza jinsi alivyopendana na mpenzi wake hadi wakati anaondoka kwenda Ulaya. Anaeleza jinsi alivyokatisha maisha yake ya barani Ulaya na jinsi ambavyo mpenzi wake hakufurahia kurejea kwake mapema na baadaye kueleza jinsi mpenzi huyo alivyobadilika baada ya kurejea. "Hali niliyokukuta nayo haikuwa nzuri kama nilivyokuzoea. Nilikuuliza una tatizo gani ukajibu hakuna tatizo. Nilikuuliza au umepata mpenzi mwingine ukasema hakuna. Nilivyokufahamu siyo ulivyokuwa na siku zilivyozidi kwenda nilikuuliza kila tulivyozoeana," anasema katika waraka huo. Hadi leo uhusiano wangu kwake hauko, hata ya kusema anachonisemesha ni salamu tu, habari za asubuhi na za saa hizi atokapo kazini. Hata wakati wa kula ni mende tu ndio wanamfukuza chumbani na kumwambia nenda kakae na mwenzako umemwacha; Hata nikimsemesha anaitikia tu sasa jamani naomba kuuliza, ni mapenzi gani haya? Je ni kwa sababu ya kusafiri kwangu? Je, ni kwa sababu ya umaskini wangu jamani kwa vile sina pesa, anahoji. "Uhusiano kwangu si mzuri, isitoshe kashfa na dharau na kejeli zimezidi;Nimegundua Omega ana kiburi kwa sababu ana pesa, siku hizi anajuana na watu wengi, lakini kazi anayofanya katafutiwa na dada yangu Happy lakini leo hata Happy hamthamini." Anaendelea kueleza katika waraka huo kuwa anahisi mpenzi wake alipata bwana wakati akiwa Ulaya na anamshangaa kwa jinsi asivyojielewa kwa kuwa alikuwa mpishi wa chakula, maarufu kama "Mama Ntilie". Anaeleza jinsi alivyomsomesha mwanae Grace tangu darasa la nne hadi sekondari. Anaeleza jinsi alivyotuma dola za Kimarekani 250 na baadaye Sh5.5 milioni kwa ajili ya ubarikio wa Grace na zawadi nyingi zenye thamani ya dola 300 za Kimarekani wakati aliporejea nchini, lakini bado anadharaulika na anamaliza waraka wake kwa kueleza kuwa hana deni bali yeye ndiye anayewadai watu aliowataja na kwamba vitu vyote apewe mama yake.

Chanzo Mwananchi

Friday, March 26, 2010

Mrema adai Sh 1 bilioni kwa Spika Sitta

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party(TLP) taifa, Augustine Mrema amemfungulia kesi ya madai Spika wa Bunge la Tanzania Samuel Sitta kwa kile alichodai kuwa ni kumkashfu na kumvunjia heshima. Kesi hiyo ya madai yenye namba 32 ya mwaka 2010ilifunguliwa Mahakama Kuu juzi baada ya kumalizika kwa muda wa siku saba alioutoa kwa Spika Sitta ili aweze kuuomba radhi kutokana na kashfa alizomtolea. Katika kesi hiyo Mrema anamtaka Sitta kumlipa fidia ya Sh 1 bilioni za kitanzania katika kipindi cha siku saba tangu alipopokea barua yake. Hivi karibuni Sitta alinukuliwa na gazeti hili akimwelezea Mrema kuwa amekwisha kisiasa, na kipesa (amefulia) hali ambayo Mrema alisema ni kuvunjia heshima hivyo, kumpa notisi ya siku saba ili aweze kumuomba radhi, lakini Sitta hakutekeleza. Mrema ambaye hivi karibuni alionekana kumtetea Rais Kikwete kwa kiasi kikubwa alisema, kitendo alichokifanya Sitta hakikuwa cha heshima na kuwa lengo lake lilikuwa ni kumuundia njama kwa polisi ili wamkamate kwa kuwa anakula rushwa. Hii yote ni njama ya Sitta aliyotaka kuniundia kwa mapolisi ili waje wanikamate kwa kuwa eti natumiwa na CCM katika kukipigia kampeni, mimi sipokea wala sitoi rushwa jamani, kwanini nipigie kampeni chama kingine wakati nina chama changu, alihoji Mrema. Mrema alisema, Sitta hajatumia madaraka yake vizuri kwa kuwa amekiuka misingi anayotakiwa kuwa nayo Spika wa Bunge lolote, na kuwa anaongoza moja kati ya mihimili mitatu ndani ya nchi.
Spika ni mhimili na kiongozi muhimu katika nchi anatakiwa kuongoza kwa haki tena bila kubagua, lakini yeye anaongoza kwa makundi kwa nini, alihoji. Mrema aliongeza kuwa madaraka aliyoyatumia Sitta yamemvunjia heshima yake aliyokuwa nayo kwa sababu tangu amtolee kashfa hizo baadhi ya wananchi wameanza kumdharau. Watu wote wameshanza kunidharau sasa, hivyi kweli heshima yangu niliojijengea tangu uongozi wangu wote nilipokuwa Serikalini mpaka hapa nilipo leo hii Mwenyekiti wa Chama Taifa halafu natupiwa matusi na kashfa kiasi hicho, mbona amenidhalilisha sana huyu Sitta jamani, alisema Mrema. Mrema aliendelea kuwa, bado anahofia maisha yake kwa kukamatwa na polisi kwa kuwa Sitta yuko katika kamati kuu na ni mjumbe hivyo anaweza kuaminika na mtu yeyote. Aidha Mrema alimtaka Sitta kuacha kutumia jina lake katika kupiga kampeni za kumchafua Rais Kikwete na kuwa kama ana malengo ya kumchafua Rais amfuate moja kwa moja. Hizi ni kampeni chafu, Kama Sitta anataka kumkashfu Kikwete asinitumie mimi apite moja kwa moja akamweleze alisema Mrema. Alisema yeye hawezi kuipigia kampeni CCM kwa kuwa hata yeye ana chama chake na kuwa kama CCM ilipata ushindi wa kishindo katika miaka ya nyuma bila yeye kufanya kampeni iweje iwe mwaka 2010. "Tangu mwaka 1995 hadi 2005 CCM ilipata ushindi wake kwa nguvu bila kupigiwa debe na mrema iweje iwe mwaka huu, mimi ni mtu mdogo sana kwa nafasi hizo" alisema Mrema.
Chanzo: Mwananchi

Vilio, Simanzi vyatanda katika mji mdogo wa Kibamba Dar es salaam

Vilio, simanzi na majonzi, vilitawala jana katika eneo la Kibamba nje kidogo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, wakati miili ya abiria 11, ukiwamo wa mama mjamzito, ikinasuliwa kutoka kwenye vyuma vya daladala na lori la mafuta ya taa, baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso na watu hao kufariki dunia papo hapo. Miili ya watu hao ilinasa katika vyuma hivyo baada ya lori hilo aina ya IVECO lenye namba za usajili T 189 ABP kuligonga daladala hilo aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 615 AJW na kisha kulisukuma kwenye mtaro na kulilalia hivyo kufanya kazi ya kuinasua miili hiyo kutoka kwenye vyuma vya magari hayo kuwa ngumu. Daladala hilo linalofanya safari kati ya Mlandizi na Ubungo, lilikuwa likitokea Kibamba wakati lori hilo linalomilikiwa na Mahmoud Mohamed lilikuwa likisafirisha lita 30,000 za mafuta ya taa kutoka Dar es Salaam kwenda Isaka, Shinyanga. Ajali hiyo inayotajwa kuwa moja ya ajali mbaya zilizowahi kutokea jijini Dar es Salaam katika siku za karibuni, ilitokea saa 10:30 alfajiri jana, baada ya lori hilo kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na kwenda upande wa pili wa barabara ya Morogoro na kuligonga daladala hilo. Kutokana na ajali hiyo, daladala hilo liliharibika vibaya kiasi cha kukutofaa tena kwa matumizi na watu wote 11, wanaume wakiwa wanane na wanawake watatu waliokuwamo walifariki dunia papo hapo na miili yao iliharibika vibaya. Baadhi ya maiti zilishuhudiwa zikiwa zimepasuka vichwa na nyingine viungo vya miili vikiwa vimekatika vipande vipande. Miongoni mwa waliokuwamo kwenye daladala hilo, ni pamoja mama mjamzito, aliyefahamika kwa jina la Zainabu Ally, ambaye pembeni ya mwili wake kulikutwa mkoba uliokuwa na vifaa vinavyotumika wakati wa kujifungua. Haikufahamika mara moja iwapo mama huyo safari yake ya jana kabla ya kukumbwa na umauti, alikuwa akienda hospitali kujifungua au la. Maiti mwingine aliyetambuliwa ni dereva wa daladala hilo, Faraji Ismail Ngalamba, ambaye alikutwa akiwa amenasa kwenye vyuma vya lori hilo. Alinasuliwa baada ya askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Chama cha Msalaba Mwekundu pamoja na polisi kukata vyuma vya lori hilo. Mwingine, ni abiria Shukuru, ambaye alitambuliwa na baba yake mzazi, Hussein Saleh Mwagilo, mkazi wa Kibamba katika eneo la ajali na mwingine alitambuliwa kwa jina la Abutwalib Twaibu. Ajali hiyo ilivutia maelfu ya wakazi wa maeneo ya katikati na nje ya Jiji la Dar es Salaam, ambao walifurika katika eneo la ajali kushuhudia miili ya watu iliyonasa kwenye vyuma vya magari hayo kwa takriban saa 8; kuanzia saa 10:00 alfajiri hadi saa 6:10 mchana. Askari polisi wa kawaida na wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), usalama barabarani pamoja na askari kanzu wenye silaha za moto, wakiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Askari wa Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, walifika saa 1:00 asubuhi na kudhibiti eneo lote la ajali. Hatua hiyo ilichukuliwa na polisi, baada ya baadhi ya watu kuvamia eneo hilo muda mfupi baada ya ajali kutokea na kuanza kuiba mafuta kutoka kwenye tanki la lori hilo. Kazi ya kuinasua miili kutoka kwenye vyuma vya magari hayo, ilianza rasmi saa 4:30 asubuhi baada ya gari la kampuni ya Effco Crane la kunyanyua vitu vizito kufika eneo hilo. Kazi hiyo iliyochukua zaidi ya saa mbili; kuanzia saa 4:30 asubuhi hadi saa 6:10 mchana, ilisababisha barabara ya Morogoro kufungwa kwa muda huo. Hata hivyo, awali kazi hiyo ilichelewa kuanza baada ya askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kufika mapema, lakini wakashindwa kufanya lolote kutokana na kuwa na vifaa duni. Hali hiyo ilidhihirika pia, wakati kazi ya kunasua miili hiyo ikifanyika, kwani askari wa kikosi hicho walishuhudiwa wakibeba miili ya watu hao huku wakiwa wamevaa mifuko ya plastiki ya rangi nyeusi badala ya glovu. Maiti mbili; moja ya Shukuru Hussein, nyingine ya mwanamke, ambaye hajatambuliwa pamoja na mguu, baada ya kunasuliwa zilichukuliwa na Land Rover ya polisi na kupelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani. Maiti nyingine tisa, ambazo hadi tunakwenda mitamboni zilikuwa hazijatambuliwa, zilipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam. Wakati kazi ya kuinasua miili hiyo ikiendelea, watu waliofika eneo la ajali, walianza kushangilia baada ya mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Fred Nicodemus, mkazi wa Kibamba, kuangua kilio ghafla katika eneo, ambako lori na daladala hilo zilikuwa zimeanguka. Fred aliangua kilio baada ya kuitambua maiti ya mama yake mzazi, Ester Christiano, aliyekuwa mfanyabiashara wa Kariakoo, jijini Dar es Salaam. Baada ya kusikia sauti ya Fred ikitoka katika eneo yalikokuwa magari hayo, umati wa watu hao walianza kushangilia wakidhani kijana huyo alikuwa miongoni mwa abiria aliyetolewa akiwa hai katika vyuma vya magari hayo baada ya kunusurika katika ajali hiyo. Awali, mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Rashid Mfaume, alisema daladala lililopata ajali, lilianza safari Kibaha na inakisiwa walikuwamo abiria kati ya saba hadi 10. Shuhuda mwingine, Frank Msemwa, ambaye ni dereva wa gari la wanafunzi, alisema aliona lori lililosababisha ajali likitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na baada ya dakika chache ikatokea ajali hiyo. Baba mzazi wa marehemu Shukuru, Hussein Saleh Mwagilo, alisema mwanaye mauti yamemfika alipokuwa njiani akienda kuchukua gari kwa tajiri yake kwa ajili ya kufanya kazi. Naye Sajenti Solomon Mwangamilo, ambaye anaishi karibu na eneo ilikotokea ajali hiyo, alisema akiwa nyumbani kwake saa 11:00 alafajiri, alisikia kishindo kikubwa. Alisema aliposikia hivyo, alijua pengine ni ajali ya kawaida, hata hivyo, hakupuuza, bali alivaa sare kisha akatoka na kwenda kwenye eneo la ajali na kuona watu wakiwa wamekandamizwa na magari hayo. Kamanda Mpinga akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ajali, alisema walifanikiwa kudhibiti eneo la ajali baada ya baadhi ya watu kutaka kuiba mafuta kutoka kwenye tangi la lori lililopata ajali. Alisema lori hilo lilikuwa limebeba lita 30,000 za mafuta ya taa na kwamba kazi ya kunasua maiti za watu waliokufa ilichelewa kuanza kutokana na magari matatu ya kunyanyua vitu vizito yaliyofika mapema kushindwa kufanya kazi hiyo kutokana na kuwa na vifaa duni. “Hii ni changamoto kubwa inayoikabili serikali,” alisema Kamanda Mpinga, ambaye alisema taarifa za awali alizopata zilieleza kuwa waliokufa ni watu wanane.

Vituko Mahakamani

Washtakiwa watatu wanaokabiliwa na kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha, jana walimmwagia kinyesi askari na kutoroka wakati wakiwa kwenye chumba cha mahabusu. Mahabusu hao walikimbia wakiwa uchi huku wakiwa wamejipaka kinyesi mwilini, kabla ya askari kuwakamata na kuwarudisha katika Mhakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Washtakiwa hao ambao waliachiwa huru baada ya Hakimu Richard Kabate wa Mahakama hiyo kuwaondolea shitaka hilo, walifikia hatua hiyo baada ya kuwekwa tena chini ya ulinzi na askari kwa ajili ya kurudishwa kituo cha polisi cha Magomeni kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka mengine mapya ya unyang'anyi wa kutumia silaha. Tukio hilo lilitokea mchana wakati askari wakijiandaa kuwatoa washtakiwa chumba cha mahabusu ili wawapandishe kwenye gari wawapeleke kituoni, ndipo washtakiwa walipotoroka wakiwa uchi. Katika sakata hilo, mmoja wa askari ambaye ni askari magereza mwenye namba A 7690 koplo Peter alimwagiwa kinyesi hicho kwenye sare yake na washtakiwa hao. Askari baada ya kuona hali hiyo walifyatua risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwepo mahakamani ili wapate nafasi ya kuwafukuza washtakiwa ambao tayari walikuwa wakitokomea mitaani. Hata hivyo askari waliwakamata washtakiwa wawili, ambao walikuwa wakikimbia uchi eneo laKinondoni Bwawani, wakati mshtakiwa mmoja ambaye alikuwa na nguo alikamatwa na wananchi na kupata kipigo kabla ya askari kufika na kumchukua. Washtakiwa hao ambao walikuwa wamechoka kwa kipigo walichukuliwa kwenye gari la polisi lenye namba T213 AMV kupelekwa kituo cha polisi cha Magomeni kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka mapya. Washtakiwa hao waliotoroka ni Rashid Salum, (25), Hamza Abdallh (27) na Juma Mathis (24).

Thursday, March 25, 2010

Picha za Ajali ya Kibamba kwa Hisani ya The Global Publisher





Mzungu wa Hilton Hotel Dar atupwa selo kwa kumpiga na kumtusi mfanyakazi wake

Kuna Tetesi kuwa General Manager wa Hoteli moja ya Kitalii iliyoko ufukweni ya Hilton the Double Tree ambaye ni Mzungu ameswekwa Rumande kwa kosa la kumpiga mfanyakazi na kumtusi eti sura yake inafanana na Nyani.Taarifa zaidi zimebainisha kuwa mpaka sasa mzungu yuko selo baada ya kukosa mdhamini.

Ajali Mbaya - Kibamba

Kuna habari za kuaminika kuwa kuna Hiace lenye no ya usajili T615 AJW lililokuwa linatokea Ubungo kwenda Mlandizi imegongwa uso kwa uso na Lori la mafuta aina ya Scania lenye no za usajili T192ABP iliyoandika kwa nyuma maandishi yanayosomeka (Yarabi salama)majira ya saa 1 asubuhi ya leo eneo la Kibamba - Morogoro Rd, Dar es Salaam. Ni ajali mbaya na ya kutisha , mmoja wa mashuhuda kashuhudia maiti zisizopungua saba kwenye Hiace na kaongeza kwa kasema kuwa "Scania imeilalia hiace kabisa yaani scania iko juu hiace iko chini hata kuokoa haiwezekani..na sidhani kama kuna mtu atakuwa amepona ila kwenye scania dereva na konda anaweza akawa amepona..sikuwa na kamera ningeweka kupiga picha, Zimamoto wameelekea eneo la tukio . Taarifa zaidi na za kuaminika tutawaletea baadae . Mungu atupe subira na Uvumilivu

Ukatili kama huu hadi lini?

Mtoto mwenye jumla ya vidole 31 afanyiwa Operation



Mtoto mmoja wa Kiume nchini China ambaye amezaliwa akiwa na jumla ya Vidole 31 amefanyiwa operation wa kutolewa vidole vya ziada , Inasemekana kuwa operation hiyo iliyodumu kwa masaa 6 1/2 ilifanyika katika Hospitali ya Shengjing huko Shenyang China, katika Operation hiyo Madaktari walifanikiwa kutoa vidole 11 vya ziada ambavyo baadhi ya vidole vya mikono vilikuwa vimeungana .Kutokana na maelezo ya mama wa mtoto huyo , mwanawe alipachikwa jina la "Monster" na watoto wenzake darasani (chekechea) na inasemekana kuwa akawa mtu wa kwanza kuwa na Vidole vingi duniani kwa madai ya Gazeti la Daily Mail. Moja ya mguu wake ulikuwa na vidole 7 na mwingine 8, mkono mmoja ulikuwa na vidole 3 vilivyoungana na mwingine ukiwa na 4 vilivyoungana pia.

23 Wanusurika kwenye ajali ya basi la HEKIMA

WATU 23 wamenusurika kupoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika kijiji cha Tanangozi, mkoani Iringa. Ajali hiyo ilitokea jana saa tano asubuhi, baada ya basi la Hekima kulipita gari ndogo lililokuwa limebeba pombe ya kienyeji aina ya ulanzi kisha kuserereka na kupinduka. Basi hilo lililokuwa na abiria zaidi 70 lilikuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam. Akizungunza na vyombo vya habari kwa njia ya simu, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk George Kabona alisema kati ya majeruhi hao, 13 ni wanaume na kumi ni wanawake na kwamba hali ya majeruhi mmoja ikiwa ni mbaya. "Majira ya saa 6 mchana leo (jana), tulipokea majeruhi 23 kutoka katika ajali ya basi iliyotokea katika kijiji cha Tanangozi. Kati ya hao 13 ni wanaume na kumi ni wanawake na hali zao zinaendelea vizuri, lakini mmoja kati yao hali yake ni mbaya na amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi," alisema Dk Kabona. Dk Kabona alisema kuwa kwa mujibu wa majeruhi hao, ajali hiyo ilitokea kutokana na barabara katika eneo hilo kuwa na utelezi uliosababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa na mikoa mingine katika Nyanda za Juu Kusini. Alisema kwamba baada ya basi kulipita gari dogo lililokuwa limebeba pombe aina ya ulanzi na dereva kutaka kurudi katika njia yake ndipo liliposerereka na kupinduka. Mmoja wa majeruhi hao alipouliza alisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya basi (Hekima) kulipita gari dogo lililokuwa limebeba pombe ya ulanzi na kuserereka kutokana na barabara kuwa na utelezi uliosababishwa na mvua," alibinisha Dk Kabona.

Mvua Kubwa yatishia Mwanza

MVUA kubwa iliyonyesha jana alfajiri jijini hapa kwa saa mbili imezikosesha makazi zaidi ya kaya 24 za mtaa wa Mabatini Kusini na 10 za Mabatini Kaskazini. wakazi wa kaya hizo walionekana katika harakati za kukusanya vyombo na mali zao zingine zikiwa zimelowa maji na baadhi ya nyumba zikiwa zimebomoka. Akizungumza katika mtaa wa Mabatini Kusini, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Yohana Nono, alisema msaada wa haraka wa mahema, vyakula na nguo unahitajika kuwasitiri baadhi ya wananchi ambao vitu vyao vilisombwa na mafuriko ya maji. “Baada ya kufanya tathmini na wananchi wa mtaa wangu, tumebaini kuna jumla ya watu 100 wa kaya 24 ambao nyumba zao zimebomolewa na mafuriko, “ alisema Nono na kuongeza kuwa wanafanya juhudi ya kuwasiliana na uongozi wa wilaya ili kuona uwezekano wa kuwasaidia wananchi hao. Kati ya watu walioathiriwa na mafuriko hayo ni pamoja na Stella Robert (6), ambaye kwa mujibu wa mjumbe wa nyumba 10 shina la Mabatini Kusini mtaa wa Benjamin, Anthony Msafiri, alishtuka saa 10.45 alfajiri na kusikia kelele za watu wakiomba msaada. “Kwanza nilifikiri tumevamiwa na majambazi, maana nilikuwa usingizini, lakini baada ya kuamka nilishuhudia nyumba zote zimejaa maji huku vitu vikielea, nilimkuta Mama Nyanjige - mama mzazi wa Stella aliyesombwa maji, akilia akiniomba kumwokoa Stella,” alisema Msafiri. “Nilichukua tochi na kufuatilia mkondo wa maji, nikawatoa baadhi ya watoto walionasa kwenye baadhi ya nyumba na kuelekea kambi ya Polisi Mabatini, ambako tulikutana na maaskari na tulipowauliza, wakasema Stella aliokolewa na mwanamke. “Alikuwa akielea huku akipiga kelele za kuomba msaada kwa maaskari hao, ndipo walipochungulia dirishani wakamwona na kuokolewa na mke wa askari,” alisema na kuongeza kuwa walimpeleka kituo cha afya na hatimaye hospitali ya mkoa ya Sekou Toure alikolazwa. Wakizungumza kwa uchungu mbele ya wananchi waliofurika eneo hilo, waathirika Issa Mauba, Tatu Ally na Hassan Babu, walidai kuwa chanzo cha mafuriko ya mara kwa mara Mabatini ni ujenzi usiozingatia mipango. Hii ni mara ya pili katika kipindi kifupi, Jiji la Mwanza kukumbwa na mafuriko huku ya hivi karibuni yakisababisha watu sita kupoteza maisha na zaidi ya 200 makazi. Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, alisema tayari timu ya wataalamu imefika mitaa hiyo ya mafuriko ingawa hakukuwa na athari za kutisha. “Timu yangu ya wataalamu imefika maeneo yaliyopata mafuriko na tutatoa taarifa baadaye na tuone nini cha kufanya juu ya waathiriwa wa mafuriko, baada ya mvua ya jana,” alisema Kabwe.

Mwanamke aenda jela Miaka 7 kwa kufanya mapenzi na mtoto wa Miaka 15 Moshi

MWANAMKE ambaye ni mke wa mtu mwenye watoto watatu, amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 15. Mwanamke huyo, Sophia Philemon (44) mkazi wa kambi namba tisa katika kiwanda cha sukari cha TPC, wilaya ya Moshi vijijini kuhukumiwa kifungo hicho, pia ameamriwa kumlipa mwanafunzi huyo fidia ya Sh1 milioni. Hukumu hiyo, ilitolewa jana mjini Moshi na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro, John Nkwabi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka. Nkwabi alisema ushahidi wa mashahidi hao, akiwemo mwanafunzi huyo wa sekondari ya Langasani, umeithibitishia mahakama kwamba mwanamke huyo, alimlazimisha mtoto huyo kufanya naye tendo la ndoa. Kitendo hicho ni kosa chini ya kifungu namba 138B (1) (d) cha kanuni ya adhabu kinachosimamia makosa ya kimapenzi kwa watoto baada ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho mwaka 2002. Hakimu Nkwabi alisema mahakama imeridhika na ushahidi kuwa Februari 28, mwaka jana, saa 1:00 usiku huko kambi namba tisa, mshitakiwa alimlazimisha mwanafunzi huyo kufanya naye mapenzi katika chumba anachoishi na mumewe. Muda huo, mwanafunzi huyo alikuwa ametoka dukani alikokuwa ametumwa na wazazi wake na mwanamke huyo, alimwita na kumshawishi aingie ndani ya nyumba yake na baadaye kumlazimisha kufanya naye tendo la ndoa. Baada ya kutiwa hatiani, wakili wa serikali, Hellen Moshi aliyeendesha kesi hiyo, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwani vitendo vya ubakaji vinazidi kuongezeka nchini hususani kwa watoto wadogo na wanafunzi. Katika utetezi wake, Sophia alisema ni mke wa mtu na hakubahatika kupata mtoto na mwanaume huyo, lakini kabla kuolewa alikuwa tayari amezaa watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume. Mshitakiwa alikataa kufanya tendo la ndoa na mtoto huyo, licha ya kumfahamu kuwa ni jirani yake. Utetezi wake ulitupiliwa mbali na mahakama hiyo.

Mshindi wa Miss Universe 2009 alamba BINGO

MREMBO wa Tanzania, Miss Universe Tanzania 2009, Illuminata James, amepata fursa ya masomo scholarship nchini Marekani kutoka kwa Kampuni ya New York Film Academy. Mbali na kutoa nafasi hiyo ya masomo, pia kampuni hiyo imejitolea kudhamini mashindano hayo mwaka huu na kuahidi pia kutoa fursa ya masomo kwa mshindi atakayemrithi Illuminata. Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communication, ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo taifa, Maria Sarungi, aliwaambia waandishi wa habari jana wameamua kuboresha mashindano hayo zaidi ikiwa ni sambamba na kutafuta udhamini wa nje ya nchi ili kuongeza chachu ya mashindano. Alisema kuwa hiyo itakuwa ni nafasi ya pekee kwa warembo wa Tanzania kujitokeza ili kuwania nafasi hiyo nyeti na nyingine nyingi ambazo wadhamini wa hapa nchini watatoa. "Tunatarajia kufanya usaili wa warembo hao katika mikoa mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha ili kupata warembo 20 ambao wataingia kambini kwa ajili ya kuchuana hadi kumpata mshindi. "Katika usaili huo tutaangalia zaidi vigezo ili kumpata mrembo bomba ambaye atatuwakilisha vema kimataifa na hatimaye kuibuka na ushindi" alisema Sarungi. Wadhamini wengine kwenye mashindano hayo ni Kampuni ya Precision Air, Serengeti Breweries, PSI, Movenpick Hotel, Hugo Domingo, Choice FM, Prime Time Promotions pamoja na Midland Hotel.

Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii It Must be Love





Wednesday, March 24, 2010

Mapenzi yampeleka Kaburini yeye na mtoto wake

Katika hali ya kusikitisha, mwanaume aliyetambuliwa kuwa ni Mwidadi Hamisi,(32) mkazi wa Bombambili mjini Songea, mkoani Ruvuma, amemnyonga mtoto wake wa umri wa miaka minne na baadaye naye kujinyonga huku akiwa ameacha ujumbe kuwa uamuzi huo umetikana na shida alizokuwa akipata kutoka kwa mke wake wa zamani.Tukio hilo lilisikitisha wengi hasa kwa kitendo cha kumnyonga mtoto Mulla, ambaye hakuwa na hatia, lilitokea saa 5:00 asubuhi wiki iliyopita katika maeneo ya Mlima wa Chandamali,nje kidogo wa mji wa Songea.Kabla ya kuamua kujinyonga, marehemu ambaye wakati wa uhai wake alikuwa mwendesha pikipiki zinazosafirisha watu,alimpiga simu kwa tajiri wake akimtaka afuate pikipiki yake katika maeneo ya mlimani huo.Habari zilisema katika simu hiyo marehemu alimwambia tajiri yake kuwa yeye ameamua kwenda kupumzika kaburini na mtoto wake, ili kuepuka shida alizokuwa akizipata kutoka kwa mke wake wa zamani.Kabla ya kujinyonga, Mwadadi, aliacha ujumbe huku akiambatanisha na orodha ya namba za simu za ndugu zake na kutaja sehemu anakotoka kuwa Newala mjini mkoani Mtwara.Katika ujumbe huo, marehemu alisema ameamua kujinyonga yeye na mtoto wake kufuatia kashfa alizokuwa akizipata kutoka kwa mama watoto wake.Katika ujumbe huyo marehemu alimtuhumu mama huyo kuwa amekuwa akimweleza mpenzi wake, siri za maungoni mwake.Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio tajiri wa marehemu huyo,Hussein Msafiri, alisema siku kadhaa zilizopita, marehemu aliwahi kumweleza matatizo yake yeye na mke wa zamani."Mara nyingi alionekana mtu ambaye hana amani moyoni mwake," alisema

Nafasi ya Kazi

The EC Delegation in Tanzania wanahitaji mfanyakazi wa muda kwa nafasi ya Receptionist / Telephone Operator, ili kuziba nafasi ya mtu anayeenda kwenye Likizo ya Uzazi kuanzia 15 April hadi 30 July 2010. Maombi yote yatumwe kwa :Ms May Kazuka Admin Assistant / Personnel EC Delegation Tanzania Umoja House, Garden Avenue Dar es Salaam Simu: +255 22 2117473-6 Fax:+255 22 2113277 Email: May.KAZUKA@ec.europa.eu

Tuesday, March 23, 2010

Wanafunzi IFM wagoma kupinga ongezeko la ada

WANAFUNZI wa Shahada ya kwanza na ya pili katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha [IFM] jana waligoma kuendelea na masomo kutokana na ongezeko la ada lililopanda ghafla. Wanafunzi hao jana waliamua kuweka mgomo baada kupinga ongezeko la ada zaidi ya asilimia 50% .Walionekana kuandamana kwenda kutaka kumuona mfadhili wa chuo hicho ambae ni Waziri wa Fedha ili wamueleze tatizo hilo kama ana taarifa nalo.Wanafunzi hao waliweka mgomo huo baada ya kutopata majibu ya matokeo ya mitihani baada ya kuambiwa hadi wamalize ada na kushangazwa na kauli hiyo.Wanafunzi hao walidai kuwa ada zimepanda kutoka shilingi milioni moja hadi kufika milioni moja na laki sita jambo ambalo limewashangaza kupanda kwa ada hizo bila ya kupewa taarifa rasmi.

Gari inauzwa (Pichani)

Toyota Mark 2 gx 1102004 Modelmetalic color1990CC75,000 Odometersports rims, CD changer, TV, airbag, ABS, PS, PW, Bumper iligongwa kidogo ila imerudishiwa vizuri na ukitaka unawekewa mpya kabisa,BEI tsh 10,000,000 tu!!Haraka ! wa kwanza ndo ataouziwa!! Kwa Mawasilino 0713 744 144 abdul

Kashfa Kubwa yaikumba Afrika ya Kusini - Yamfunga Mwanamke Jela ya Wanaume Kwa Miezi Sita

Skendo limeikumba kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini ambapo mwanamke aliyakamatwa kwa makosa ya ujambazi anadaiwa kufungwa kwenye jela ya wanaume kwa kipindi cha miezi sita na kupelekea mwanamke huyo abakwe na kulawitiwa na wafungwa wa kiume.Denise Wilson au maarufu kwa jina la Abbah wa mji wa Isipingo nchini Afrika Kusini amekifungulia mashtaka kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini kwa kumweka kwenye jela ya wanaume kwa miezi sita wakati alipokuwa akisubiria kufikishwa mahakamani kwa makosa ya ujambazi, kujaribu kuua na kuteka watu.Denise anadai fidia ya rand 100,000 kwa madhila aliyoyapata wakati alipokuwa kwenye jela ya wanaume.Katika nyaraka za mahakama, Denise alisema kuwa alikamatwa septemba 24 mwaka 2002 na kupelekwa kwenye jela ya wanaume.Alisema kuwa kitendo chake cha kupinga kuwekwa jela moja na wanaume kilisababisha avuliwe nguo mbele ya wanaume huku akizomewa na kuchekwa.Wakati wa kipindi chake cha miezi sita kwenye jela ya wanaume, Denise anadai kuwa walinzi wa jela walikuwa wakimlazimisha afanye matendo ya ngono bila ya idhini yake.Alidai pia kuwa wafungwa wa kiume walikuwa wakimpapasa mara kwa mara kwenye sehemu zake za siri bila ya idhini yake.Denise pia hakusita kusema kuwa alibakwa na kulawitiwa katika kipindi cha miezi sita kwenye jela ya wanaume.Alisema kuwa ingawa maafisa wa jela walikuwa wakijua kuwa yeye ni mwanamke, waliendelea kumweka jela moja pamoja na wanaume.Alisema kuwa hata daktari wa wilaya alipomfanyia uchunguzi wa kuthibitisha jinsia yake, aliendelea kuwekwa kwenye jela hiyo.Kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini kimeamua kukaa kimya kikisubiria kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani.

Hatima ya LIYUMBA Ni April 9 ,Mahakama yaombwa kutupilia mbali kesi inayomkabili

JOPO la mawakili wanne wanaomtetea, Mkurugenzi wa zamani wa Utawala na Fedha wa BoT, Amatus Liyumba wamewasilisha hoja za majumuisho za mwisho wakiitiaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuone mteja wao hana kesi ya kujibu dhidi ya mashtaka yanayomkabili. Kigogo huyo wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba anakabiliwa na kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh 221. Ilielezwa kuwa Aprili 9, mwaka huu, hatma yake itajulikana kama hana kesi ya kujibu ama la. Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka Machi 15, mwaka huu kufunga ushahidi wao mbele ya jopo la mahakimu watatu lililokuwa likiongozwa na Hakimu Edson Mkasimongwa. Wakili wa Serikali Juma Mzarau alifunga ushahidi huo baada ya mashahidi wao nane kutoa ushahidi dhidi ya kesi hiyo kati ya mashahidi 15 waliotarajia kuwaita. Wakiwasilisha hoja hizo za mwisho za majumuisho kwa njia ya maandishi, mawakili wa Liyumba, Hilary Mkate, Majura Magafu, Hudson Ndusyepo na Onesmo Kyauke waliiomba mahakama imwone mteja wao hana kesi ya kujibu kwa madai kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi nane wa upande wa mashtaka hautoshelezi kuithibitishia mahakama kwamba Liyumba alitumia vibaya madaraka yake kinyume na sheria, chini ya kifungu cha sheria cha 96 (i) cha kanuni ya adhabu. Walidai katika majumuisho hayo Shahidi wa nane na wa saba wa upande wa mashtaka walieleza katika ushahidi wao kuwa ni vigumu kuthibitisha hasara inayodaiwa kusababishwa na Liyumba kwa sababu ripoti kamili ya utekelezaji wa mradi wa Mtemi Mirambo unaojulikana kama Majengo Pacha hadi sasa bado haijaandaliwa. Kutokana na ushahidi huo, Mawakili hao, waliitaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imwone Liyumba kuwa hana kesi ya kujibu kwa sababu hakuna uthibitisho wowote ambao unaonyesha kuwa serikali imepata hasara katika mradi huo. Mawakili hao wa Liyumba waliongeza kudai kuwa ni mapema sana kudai kuwa serikali imepata hasara katika mradi wa majengo Pacha bila ya kuandaliwa kwa ripoti kamili ya mradi huo. Walidai kuwa licha ya upande wa mashtaka kushindwa kuithibitishia mahakama kuwa Liyumba alifanya maamuzi yenye madhara katika mradi wa majengo pacha, pia umeshindwa kuthibitisha kwamba Liyumba alifanya maamuzi hayo kwa nia ovu. Mawakili hao walisisitiza mahakama imwone mteja wao hana kesi ya kujibu na iliomba iyatupilie mbali mashtaka yanayomkabili mteja wao huyo.
Chanzo : Mwananchi

Kwa issue hii lazima wanawake waheshimike

Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote duniani
Mmmm jaribu kufikiri haya
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana . Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu! HIVI INGEKUWA WANAUME
WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Monday, March 22, 2010

Namibia wamkumbuka Nyerere

SERIKALI ya Namibia imemtunuku Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere nishani ya heshima. Nishani hiyo alikabidhiwa mkewe, Mama Maria ikiwa ni utambuzi na kuthamini nafasi yake katika harakati za kupigania uhuru wa Afrika ikiwemo nchi yao . Alikabidhiwa nishani hiyo juzi pamoja na watu wengine sita mashuhuri waliotoa mchango mkubwa kwa Namibia na kufanikisha ipate Uhuru Machi 21, 1990 kutoka kwa Afrika Kusini. Walipewa tuzo hizo wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais Hifikepunye Pohamba kwa ajili ya marais wote na wageni wengine waalikwa waliofika nchini hapa, akiwemo Rais Jakaya Kikwete kushuhudia sherehe za miaka 20 ya Uhuru pamoja na kuapishwa kwa Rais na Waziri Mkuu nchini hapa. Akielezea umuhimu wa Namibia kumtunuku Mwalimu Nyerere, Msimamizi wa Itifaki katika hafla hiyo, Martin Anyamba alisema kuwa mamilioni ya Waafrika, jina la Nyerere litaendelea kuwa kwenye kumbukumbu zao na wataendelea kumheshimu. Alisema Nyerere alikuwa mwanafalsafa, kiongozi na kiunganishi cha watu na mtu mwenye busara aliyefanya kazi kubwa ya kufungua mipaka ya nchi yake kwa ajili ya kupigania uhuru wa nchi mbalimbali barani. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Rais Jakaya Kikwete, ilielezwa kwamba ushirikiano na umoja wa Namibia uliowezesha kupata uhuru, ulitokana na mchango mkubwa wa Tanzania ambayo ilijitoa mhanga kwa ajili yao . “Wanachama wengi wa SWAPO walipata mafunzo huko Kongwa ( Dodoma )…Mwalimu Nyerere alikuwa muumini mzuri wa umoja,” alisema Anyamba kabla ya kumuita Mama Maria aliyekuwa wa kwanza kati ya watu saba kutunukiwa, kitendo kilichoshangiliwa kwa makofi na vigelegele na umati uliohudhuria. Wengine waliokabidhiwa nishani hizo kutokana na mchango wao katika uhuru wa Namibia ni Rais Mstaafu wa Zambia , Kenneth Kaunda aliyekwenda kuipokea kwa mbwembwe akitembea kwa mwendo wa haraka. Wakati huohuo Umoja wa Wanawake Watanzania waishio Namibia kupitia kwa Mwenyekiti wao, Chiku Mnubi, juzi walimpa Mama Nyerere zawadi ya ramani ya nchi hiyo ikiwa ni utambuzi wa mchango wake katika uhuru na pia kumshukuru kufika nchini humo kuhudhuria sherehe za Uhuru na kuapishwa kwa Rais Pohamba.

Thursday, March 18, 2010

Dalili za Mvua ni Mawingu! Hatimaye Mishi Bomba afanyiwa Kitchen Party

Haya haya kuolewa Mishi usirudi nyumbani kut.......
Mishi akiwa makini kusikiliza mambinu ya ndoa

Hawakuwa nyuma kuchangamsha sherehe!

Shostito nae alikuwepo

Milindimo ya pwani haikuwa nyuma

Haya ni baadhi ya mambo yaliyokuwepo

Mambo ya kibao cha Nazi mmmmh

Wednesday, March 17, 2010

Mchungaji adaiwa kuua mwanaye kwa kumuibia Sh. 50,000

Mchungaji wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Jonathan Sabuni (60), Mkazi wa kijiji cha Kasamwa wilayani Geita, Mkoa wa Mwanza, ameua mwanaye Amos Jonathan (16), kwa kipigo kwa tuhuma za kumwibia Sh. 50,000. Marehemu Amos alikuwa anasoma darasa la saba katika Shule ya Msngi Nyampa. Inadaiwa kuwa siku mbili kabla ya kutenda ukatili huo, mtuhumiwa aliikusanya familia yake ya watu wanne na kuwataka waombe baada ya kupotea kwa fedha hizo alizokuwa amepanga kuzifanyia ukarabati wa nyumba ya familia. Mbali na marehemu, wanafamilia wengine ni Baraka Jonatan (18) anayesoma kidato cha pili na mkewe, Esther Jonatahan. Inadaiwa kuwa mchungaji huyo mkewe na kuwataka waombe kuhususiana na upotevu wa fedha hiyo iliyokuwa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya familia. Imedaiwa kuwa Machi 13, siku mbili baada ya mtuhumiwa kutoa muda kwa marerehemu kurejesha fedha hiyo na kufanya Ibada maalum aliyowakutanisha wanafamilia baada ya marehemu kukiri kuwa ndiye aliyeiba fedha hizo na kuahidi kuzirejesha lakini hakufanya hivyo. Akizungumzia tukio hilo, Esther Jonathan, mama mzazi wa marehemu Amos alisema jana kuwa siku iliyofuata marehemu kwa woga aliamka alfajiri na kuondoka nyumbani kukwepa hasira ya baba yake lakini ilipofika saa nne alimtuma kaka yake Baraka kumrejesha nyumbani. Alisema wakiwa nyumbani saa tano ndipo mtuhumiwa alipoanza kumpiga marehemu kwa fimbo, rungu na mateke akidai marehemu alikuwa ameficha fedha hizo. Mama huyo alisema kuwa alijaribu kuingilia kati kumzuia mumewe kumpiga marehemu, lakini hakumsikiliza. Alisema ilipofika saa moja jioni marehemu alionekana kuzidiwa na ndipo mtuhumiwa alipoacha kumpiga na kwamba hali ya marehemu ilizorota ghafla na ilipofika saa 4:45 usiku mtuhuiwa alimwita Mchungaji Charles Mpanduji wa AIC kumuombea. Hata hivyo, kabla ya kumwita mchungaji mwenzake kumuombea marehemu, mtuhumiwa alimwosha marehemu mwili wote kumuondoalea uchafu kabla ya kukata roho. Kwa mujibu wa Ester, baada ya kugundua kuwa marehemu amekata roho, ndipo mtuhumiwa alipotoka nje na kisha kumuaga mkewe kuwa alikuwa anatoka kuelekea kusikojulikana, lakini yeye Ester) alimshtukia na kumzuia Kwa kumkaba shati asiondoke huku akipiga kelele kutaka msaada wa majirani, lakini baadaye alizidiwa nguvu na kumponyoka na ndipo mtuhumiwa alipotoroka. Kamanda wa Polsisi wa Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

Tuesday, March 16, 2010

Bongo Noma Kiswahili Kigumu ama?

Trawu, wafanyakazi TRL kutoa tamko leo

CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu) kitakutana na wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ili kutoa tamko la pamoja baada ya serikali kutangaza azma ya kuchukua hisa za mwekezaji ambaye ni Rites ya India. Tamko hilo linakuja wakati zikiwa zimepita siku chache tangu serikali kutangaza azma hiyo ya kuchukua hisa zake ambazo ni asilimia 51 kutoka Rites ambayo ilitakiwa iwekeze dola 8 milioni za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh10 bilioni za Kitanzania) katika mkataba wake wa miaka 25 ulioanzia mwaka 2007. Katibu mkuu wa Trawu, Sylvester Rwegasira aliiambia Mwananchi jana kuwa hatua hiyo itaweka sawa suala hilo kutokana na wafanyakazi kuwa na mawazo tofauti tangu serikali itangaze azma hiyo. Kesho tutakutana na wafanyakazi ili kupata tamko la pamoja ambalo litakuwa limebeba mawazo na maoni ya wafanyakazi wote wa TRL hasa baada ya serikali kuamua kununua hisa, alisema Rwegazira. Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote ya muda au chochote, tutafahamishana lakini ni lazima tukutane na kutoa tamko la pamoja. Tangu serikali itangaze azma yake, wafanyakazi wa TRL waliokuwa wakizungumza na vyombo vya habari walikuwa wakitoa maoni tofauti, hali ambayo Rwegasira alisema inatakiwa imalizwe kwa wafanyakazi wote kukutana. Ili serikali iachane na Rites haina budi kutoa taarifa ya miezi mitatu kwa kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali ya India na itatakiwa imlipe mwekezaji huyo Sh54 bilioni kama fidia za gharama mbalimbali na matumizi ambayo kampuni hiyo iliingia wakati wa kipindi cha uwekezaji na fedha nyingine Sh56 milioni ambazo zinatakiwa zilipwe kwa kampuni binafsi ya ulinzi ya Ultimate Security. Rites imekuwa ikidai kuwa haistahili kubebeshwa lawama kutokana na TRL kushindwa kuendeshwa kwa ufanisi kwa kuwa serikali ndiyo iliyoshindwa kutekeleza wajibu wake kwenye mkataba. Mkurugenzi mtendaji wa TRL, Hundi Chaundhary aliwaambia waandishi wa habari mwaka jana kuwa serikali inashindwa kuwaeleza wananchi yaliyomo kwenye mkataba ndio maana kampuni hiyo kubwa ya uendeshaji wa huduma za reli inalaumiwa.
Chanzo: Mwananchi

Hatima ya Liyumba kujulikana April 9

Upande wa mashtaka katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.1 za mradi wa majengo pacha ya Benki Kuu Tanzania (BoT), umefunga ushahidi wake dhidi ya kesi hiyo inayomkabili Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki hiyo, Amatus Liyumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake Mahakama hiyo imesema, itatoa uamuzi kama Liyumba ana kesi ya kujibu au la Aprili 9, mwaka huu. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Juma Ramadhani, alidai jana mbele ya jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Muingwe, wanaosikiliza kesi hiyo, kuwa baada ya upande wa Jamhuri kuita mashahidi wanane na kuwasilisha vielelezo 13 mahakamani hapo, umeamua kufunga ushahidi. Ramadhani alidai kuwa ili kesi iendelee kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai, kifungu cha 131 cha sheria ya mwaka 2002, upande wa mashitaka umefunga ushahidi wao dhidi ya kesi hiyo. Hata hivyo, wakili wa utetezi, Majura Magafu, aliomba mahakama hiyo kusikiliza majumuisho ya mwenendo wa kesi kwa maneno ili iweze kuona kama mshitakiwa ana kesi ya kujibu au la. Kadhalika, upande wa Jamhuri ulitoa pingamizi la kufanya majumuisho hayo jana kwa maneno na uliomba mahakama hiyo kuruhusu hoja za majumuisho zitolewe kwa maandishi ili kusaidia mahakama kutoa uamuzi. “Kwa sababu kesi hii ni ya Jamhuri, tunaomba tupewe nafasi ya kutoa hoja zetu kwa maandishi ili tuweze kuishahiwishi mahakama kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma zinazomkabili,” alisema Ramadhani. Hata hivyo, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama hiyo iliamuru ziwasilishwe kwa maandishi. Upande wa utetezi utawasilisha hoja zao Machi 22, mwaka huu na upande wa mashitaka utajibu Machi 29, mwaka huu. Hatima ya Liyumba kama ana kesi ya kujibu ama la itajulikana Aprili 9, mwaka huu baada ya mahakama kutoa uamuzi. Mapema Januari 10, mwaka jana, Liyumba na aliyekuwa Meneja Mradi huo, Deogratius Kweka, walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo wakikabiliwa na mashitaka ya kutumia madaraka vibaya na kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha. Hata hivyo, mahakama hiyo Aprili mwaka jana, iliwafutia mashtaka hayo, lakini Liyumba alifikishwa tena mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo. Awali, shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo, Mpelelezi Seif Mohamed (49), aliiambia mahakama kwamba Liyumba alikuwa akifanya mabadiliko ya kuongeza gharama za mradi na baadaye kuijulisha bodi ya BoT. Kadhalika, alidai kuwa Liyumba alifanya mabadiliko hayo baada ya kutoa maelekezo kwa njia ya barua kwa Mhandisi mshauri wa mradi huo. Shahidi wa pili, Meneja wa musuala ya bodi Yusto Tolola (45) kutoka BoT, alidai mahakamani kwamba bodi ilipokea maombi ya nyongeza ya mabadiliko ya fedha za mradi wakati tayari matumizi yameshafanyika. Pia, shahidi huyo alidai kuwa kurugenzi iliyokuwa ikiongozwa na Liyumba ilikuwa ikiomba kibali cha kufanya mabadiliko ya mradi wa ujenzi wakati tayari matumizi ya fedha yamekwisha kufanywa. Shahidi wa tatu, Julius Angelo (49) ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Fedha BoT, alimtetea Liyumba kwamba aliidhinisha malipo madogo ya nyongeza katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha kulingana na cheo alichokuwa nacho. Aidha, Mkurugenzi huyo aliiambia mahakama kwamba malipo makubwa ya nyongeza ya mradi huo, yaliidhinishwa na aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Balali. Shahidi wa nne, aliyekuwa Mkurugenzi wa bodi ya BoT, Michael Shirima (66), alidai kuwa alitaka kujiuzulu, baada ya kumjulisha aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati huo, Basil Mramba, kuhusu matumizi makubwa ya mradi wa majengo pacha, yaliyofanyika bila kibali cha bodi hiyo ambapo alijibiwa kwamba asingeweza kuingilia uamuzi wa Balali kwa kuwa anawajibika kwa Rais aliyemteua. Kadhalika, alidai kuwa alifikia maamuzi ya kujiuzulu baada ya kuona hakuna mchango anaoutoa kwa bodi hiyo ambayo ilipelekewa kuidhinisha mapendekezo ya matumizi ya fedha za mradi wakati tayari malipo yamefanyika bila mamlaka ya bodi hiyo. Katika kesi hiyo, Liyumba anadaiwa kuwa akiwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, alipindisha mkataba wa BoT kuhusu mradi wa ujenzi wa maghorofa pacha na hivyo kuongeza kiasi cha fedha zilizokuwa zikihitajika katika ujenzi. Ilidaiwa kuwa kutokana na Liyumba kupindisha mkataba huo, aliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 153,077,715.71 ambazo ni sawa na Sh. 221,197,299,200.96 kwa sasa.

Aona kwa kutumia ulimi

TATIZO la upofu sasa linaweza kuwa historia baada ya wanasayansi kuanza kumfundisha mwanajeshi wa Uingereza ambaye alipofuka vitani, kuona kwa kutumia ulimi wake. Craig Lundberg, 24( pichani), ambaye alipoteza uwezo wake wa kuona baada ya kupigwa na kombora la roketi miaka mitatu iliyopita, ni mwanajeshi wa kwanza kujaribishiwa teknolojia hiyo inayoitwa mfumo wa BrainPort, kwa mujibu wa Skynews. Kifaa hicho kinachotumika kumuwezesha mtu kuona kinahusisha teknolojia ya hali ya juu ya 'lollipop' ambayo imewekwa kwenye ulimi wa Craig. Kifaa hicho kinabadilisha picha kutoka kwenye kamera ya video, ambayo inavaliwa kwenye miwani, kuwa ishara ambayo huchangamsha seli zilizo kwenye lollipop. Kifaa hicho cha thamani ya Pauni 10,000 za Kiingereza kinatumia kanuni ya hisia mbadala. Ubongo hutambua kuwa ishara hizo zinazousisimua ulimi, hazina uhusiano na ladha na hivyo kuzielekeza kwenye sehemu ya picha katikati ya akili kwa ajili ya kuitengeneza taswira hiyo. Akili huweza kutafsiri picha hiyo na hivyo kumpa Craig uwezo wa kuona. Craig anaeleza kifaa hicho kuwa ni "kizuri cha aina yake". "Kila kitu ambacho kamera inaangalia, nahisi picha kwenye ulimi wangu," alisema. Mfumo huo pia unamuwezesha kutambua herufi. Alisema: "Naweza kuhisi kwa kutumia ulimi wangu kuwa herufi ya kwanza ni A na baadaye naelekea kwenye herufi inayofuata. Ni kitu cha ajabu. "Baadaye natembea kwenye varanda na naweza kwenda milangoni, ukutani na kuona watu wanaokuja kwangu." Teknolojia hiyo ya Lundberg ya BrainPort imefadhiliwa kwa pamoja na Wizara ya Ulinzi na taasisi ya hisani ya askari vipofu. "Mimi ni mkweli," alisema. "Najua hii haitanirejeshea kabisa uwezo wangu wa kuona, inaweza kuwa kitu kizuri kinachofuata."

Maiti ya Dereva Taxi yakutwa na Tundu

UTATA umezidi kuzingira kifo cha dereva teksi anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa na polisi wa kituo cha Chang'ombe jijini Dar es Salaam, baada ya familia kudai kuwa maiti ya kijana wao imekutwa ikiwa na tundu na uvimbe kichwani. Familia hiyo pia imesema maiti ya kijana wao, Mussa Juma, 27, pia imekutwa ikiwa imebabuka sehemu za siri, jambo ambalo linawatia mashaka ndugu. Familia ilitoa madai hayo mara baada ya kuuchukua mwili wa dereva huyo kutokana na madaktari kumaliza uchunguzi wao wa kutaka kubaini sababu ya kifo cha kijana huyo ambaye polisi imedai kuwa alifariki wakati akipelekwa Hospitali ya Temeke baada ya kulalamika hajisikii vizuri wakati akihojiwa. Akizungumza na gazeti hili jana Mwijuma Mzee, ambaye pia ni mjomba wake marehemu Mussa, alisema: Mimi kama mwanafamilia ninachoweza kukueleza ni kwamba mwili huo umekutwa na tundu sehemu ya mguu wa kushoto... sielewi limetokana na nini; uvimbe kichwani na amebabuka sehemu za siri. Hiki ndicho nilichoshuhudia na ninachoweza kukueleza." Mzee alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo familia hiyo ina hofu kuwa ndugu yao aliteswa kabla ya kufikwa na mauti, lakini akasisitiza kuwa majibu ya awali yatakayotolewa na daktari aliyefanyia uchunguzi maiti hiyo, yatasaidia kupata ukweli wa tukio hilo. Alisema wanatarajia kupata majibu hayo ya daktari leo na kwamba vipimo zaidi vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya utambuzi zaidi. Alisema sababu za kitaalamu za kupeleka vipimo hivyo kwa mkemia mkuu ni baada ya mwili huo kukutwa umejaa hewa na uvimbe, jambo alilosema linasababisha utata katika kupata ukweli halisi wa kifo chake. Tumeambiwa na mganga wetu kuwa vipimo zaidi vya mwili wa marehemu vinatarajia kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali ambaye atatoa majibu ya mwisho ya ukweli wa kifo hicho,alisema Mzee. Akizungumzia taratibu za msiba huo, Mzee alisema familia hiyo leo inatarajia kuupokea mwili huo rasmi na kuusafirisha hadi Bagamoyo mkoani Pwani kwa maziko. Alisema msafara huo utaanza majira ya saa 4:00 asubuhi ukitokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako maiti hiyo imehifadhiwa baada ya kuhamishwa kutoka Hosptali ya Manispaa ya Temeke. Kabla ya kufanyika kwa uchunguzi wa mwili huo familia hiyo ilikataa mwili huo kuchunguzwa ukiwa Hospitali ya Temeke ukidai kuwa wataalamu wa suala hilo wanapatikana Muhimbili na pia kuhofia polisi wa Chang'ombe kuingilia kazi hiyo. Kauli hiyo ya ndugu wa marehemu imekuja siku moja kabla ya mganga aliyefanya kazi ya kuupima mwili wa marehemu hajatoa majibu yake. Sakata la kifo cha dereva huyo liliibuliwa na wanafamilia Machi 10 baada ya kufuatilia kukamatwa kwake kwenye kituo hicho cha polisi na kueleza kuwa amefariki dunia. Inadaiwa kuwa dereva huyo aliuawa na askari hao wakati wakimuhoji kuhusu tukio la ujambazi lililotokea hivi karibuni. Familia inadai kuwa kijana huyo alikamatwa Machi 8 saa 3:00 usiku eneo la Mivinjeni wakati akielekea nyumbani kwake Mtoni Mtongani baada ya muda wa kazi kumalizika. Familia pia inadai kuwa kijana huyo aliuawa siku aliyokamatwa, yaani Machi 8, lakini kamanda wa polisi wa kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema kijana huyo alifariki Machi 10 wakati akikimbizwa hospitalini.
Chanzo: Mwananchi

Ali Ameir kung`atuka ubunge

Mwanasiasa mkongwe Zanzibar, Ali Ameir Mohammed, ametangaza kung’atuka kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu ujao. Ali Ameir ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Donge, Kaskazini Unguja, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Muungano pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM). Amesema ameamua kutogombea tena ubunge ili apumzike. Alisema uamuzi huo ni wake binafsi na kwamba hakuna kituo chochote kilichotaka aendelee kuwa mbunge wao.Alisema wananchi wa Donge bado wana imani na utumishi wake na hata kama wangejitokeza wanachama 100 kupambana naye angeweza kushinda. Alisema tayari wazee wa Donge wamekubali uamuzi wake wa kutogombea ingawa kwa kinyongo. Hata hivyo alisema uamuzi wake wa kustaafu huuna nia ya kuwashawishi wazee wengine kufuata nyayo zake kwa kuwa suala hilo ni hiari ya mtu. Miongoni mwa nyadhifa alizowahi kushikilia Mbunge wa jimbo hilo ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mshauri wa Rais wa Zanzibar wa masuala ya siasa, Waziri wa Habari na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Ameir ni mwanasiasa wa pili mkongwe kutangaza uamuzi kama huo Zanzibar. Mwingine ni Mbunge wa Makunduchi, Abdusalami Isaa Khatib, ambaye ameshasema kuwa hatagombea mwaka huu. Khatib hivi sasa ni Mbunge wa Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Chanzo: Nipashe

MV Serengeti yateketea kwa Moto

Meli ya MV Serengeti imeteketea kwa moto siku ya jumapili na mabaharia wanane wamenusurika kufa, wakati ikiwa imetia nanga nje ya bandari ya Malindi mjini Zanzibar. Moto huo ulianza kuwaka majira ya saa 6:30 mchana na kusababisha wasiwasi mkubwa katika eneo hilo lenye ukanda wa hoteli nyingi za kitalii, baada ya umati wa watu kuvamia maeneo hayo wakitaka kushuhudia moto huo. Mrajisi wa Meli Zanzibar, Abdallah Mohammed, alisema kwamba moto huo hadi juzi mchana ulikuwa unaendelea kuzimwa kwa kutumia Tagi ya Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC), pamoja na vifaa vya uokoaji kwenye majanga ya moto vilivyomo ndani ya meli hiyo. Hata hivyo, alisema ni mapema kueleza mabaharia wangapi walikuwemo ndani ya meli hiyo na chanzo cha moto huo, hadi hapo uchunguzi wa kitaalam utakapofanyika. Mohamed alisema meli hiyo inamilikiwa na kampuni ya JAK Enterprises L.T.D iliyosajiliwa Zanzibar na kwamba kwa mara ya mwisho ilifanyiwa ukaguzi kati ya Januari na Desemba mwaka jana. “Ukaguzi wa mwisho ulionyesha meli ni nzima na ndiyo maana ikaruhusiwa kutoa huduma ya kubeba abiria na mizigo” alisema Mrajisi huyo wa meli. Alieleza kwamba leseni ya meli hiyo inaruhusu kubeba abiria 550 na tani 100 za mizigo na ilikuwa ifanye safari jana usiku kuelekea kisiwani Pemba. Alisema hilo ni tukio la pili la meli za abiria kuungua moto zikiwa zimeshusha nanga nje ya bandari ya Malindi, ambapo hivi karibuni meli za MV Aziza I na Aziza II ziliteketea kwa moto wakati zikifanyiwa matengenezo katika eneo la Mtoni, nje kidogo ya Bandari ya Malindi. Hata hivyo, alisema kwa mujibu wa sheria abiria wote waliokuwa wasafiri na meli hiyo jana usiku wanapaswa kurejeshewa fedha zao au watafutiwe usafiri mwingine wa kuwafikisha. Kwa upande wake, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar, alisema ni mapema kuelezea chanzo cha moto huo na mabaharia waliokuwemo hadi hapo kazi ya uokoaji itakapokamilika. “Ni mapema kusema chanzo cha moto isipokuwa hatua za uokoaji zinaendelea na sehemu kubwa ya moto imekwisha dhibitiwa”, alisema Mkuu huyo wa Opereshen.

Mtu Mfupi kuliko wote Duniani afariki

He Pingping ambaye aliyekuwa akitambulika kama mwanaume mfupi kuliko wote duniani akiwa na urefu wa sentimeta 74.61 amefariki dunia jumamosi kutokana na matatizo ya moyo. He Pingping, amefariki dunia nchini Italia akiwa na umri wa miaka 21.He alikuwa nchini Italia kwa ajili ya kushiriki kwenye shoo ya kwenye luninga lakini alisumbuliwa na maumivu makali kwenye kifua na alipowahishwa hospitali wiki mbili zilizopita alifariki siku ya jumamosi kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni matatizo ya moyo.He alizaliwa nchini China akiwa na ugonjwa unaomfanya awe mfupi sana. Baba yake He Yun aliwahi kusema kuwa He alipozaliwa alikuwa mdogo sana kiasi cha kuenea kwenye viganja vyake vya mikono.He alitambulika rasmi kama mtu mfupi duniani na kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia, Guinness mnamo mwaka 2008.Akiwa na taji lake hilo, He alisafiri nchi mbalimbali duniani kutangaza rekodi yake hiyo akiwa na watu wengine waliovunja rekodi za dunia.Mwezi septemba mwaka 2008, He alienda mjini London, Uingereza na kupiga picha na mwanamke mwenye miguu mirefu kuliko wanawake wote duniani, Svetlana Pankratova.Mwanzoni mwa mwaka huu, He alisafiri kwenda Istanbul,Uturuki ambapo alikutana na mtu mrefu kuliko wote duniani Sultan Kosen mwenye urefu wa sentimeta 246.5.Guinness World Records wamesema kuwa mrithi wa taji la He atatangazwa katika siku zijazo.

KenolKobil kununua mali za BP Tanzania

Kampuni ya KenKobil ambayo hujishughulisha na biashara ya uuzaji mafuta, inakusudia kununua mali ya Kampuni ya BP Tanzania Limited ambayo hivi karibuni imetangaza kuachana na biashara ya mafuta katika nchi tano za Afrika ambazo ni Tanzania, Zambia, Namibia, Botswana na Malawi. Taarifa iliyotolewa na mmoja wa mameneja wake, Patrick Kondo, imeeleza kwamba KenolKobil, imevutiwa kuchukua nafasi ya masoko ambayo BP Tanzania Limited inataka kuachia kwa sababu kampuni hiyo ilikuwa na uendeshaji mzuri wa biashara zake na ilikuwa na masoko ya uhakika katika nchi zote tano. “Pia BP Tanzania inayo miundombinu mizuri na iliyojengeka vizuri katika nchi zote hizo ambayo inaachia, vile vile ilikuwa na inadhibiti sehemu kubwa ya soko miliki na uendeshaji thabiti wa shughuli zake,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Pia meneja huyo alisema KenolKobil imevutiwa zaidi na masoko hayo na nafasi kubwa ya kibiashara inayotoa kwa uwezekano mkubwa wa kukua kwa kampuni hiyo barani Afrika, hasa ikizingatiwa na “Mkakati Kuelekea Kusini” kama ilivyotangazwa mwaka jana. “Masoko haya yote yako katika maeneo ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika ambako masoko ya KenolKobil ambayo Bodi ya KenolKobil imeyaridhia kwa lengo la kuwekeza. KenolKobil inaouweza wa kifedha kununua sio mali hizo tu, bali hata nyinginezo,” alisema. Alisema miongoni mwa masoko hayo, Tanzania na Zambia, KenolKobil tayari ina makampuni yake tanzu na inao mpango wa upanuzi na kuimarisha biashara zake kwenye masoko hayo kwa kulingana na madhumuni na malengo ya kutaka kuwa kiongozi katika kila soko na mfanyabiashara mkubwa barani Afrika. Alisema KenolKobil inatambua kuwa masoko yote ambayo BP imetangaza kujitoa, kuna mwelekeo mzuri wa ukuaji wa biashara ambao utatoa fursa nzuri kwa kampuni yetu kuweza kuongeza biashara kulingana na malengo yetu.
Chanzo: Nipashe

Monday, March 15, 2010

Pengo azindua hospitali Kibangu

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amezindua Hospitali ya Misheni ya Kibangu na kuwahimiza waumini wenye uwezo kujitolea kuchangia katika ujenzi wa Hosptali hiyo ili kusaidia kufikisha huduma za afya kwa jamii. Hospitali hiyo ambayo ina ghorofa mbili na tayari imesajiliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii namba yake ikiwa 071350 tayari imeanza kuanza kuhudumia wagonjwa huku ujenzi wake uliosimamiwa wa Kanisa hilo Parokia ya Kibangu hadi sasa umeghalimu zaidi ya Sh 482.6 milioni. Katika hotuba yake ya uzindizi Pengo aliwahimizi waumini na watu wenye uwezo kuwa na moyo wa kujitolea katika michango ya ujenzi wa hospitali hiyo kwa kufanya hivyo kutawafanya washiriki kazi ya uponyaji iliyofanywa na Yesu Kristu. Tunapojenga hospitali kama hii tunawalenga watu ambao uwezo wao ni pungufu hasa akinamama, ili waweze kupata huduma hizi muhimu kwa ustawi wa maisha yao. Ninasema hivi kwa sababu watu wenye uwezo mkubwa huweza kuzipata huduma hizi kokote , kwa gharama yoyote na wakati mwingine huzifuata hata nje ya nchi kama Afrika ya kusini Ulaya na sehemu nyingine,alisema Pengo. Alisema watu wenye uwezo ni vyema wajitolee katika kuchangia huduma na ujenzi wa hospitali hiyo akiongeza kuwa huduma zake hazibagui dini, kabila wala rangi na kusisitiza kwamba ina lengo la kusaidia watu eneo hilo ambao kwa muda mrefu walikuwa wakimihaha kupata huduma hizo. Naye mwenyekiti wa Parokia hiyo Adrian Mpande alisema, ukosefu wa hospitali katika eneo hilo uliodumu kwa muda mrefu aliwalazimu watu kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya wanapougua. Mpande alifafanua kuwa mradi wa hospitali hiyo ulibuniwa mwaka 2003 na ambapo gharama za ujenzi wake zilikadiriwa kuwa Sh305 milioni lakini, baaaye zilipanda hadi kufikia sh 461 milioni katika mwaka 2008 na sasa hadi kukamilika kwake kutumika sh 500 milioni. Alisema hospitali hiyo hadi sasa inauwezo wa kulaza wagonjwa 50 kwa wakati mmoja na inatoa vipaumbele kwa wakinamama wajawazito,watoto na kiliniki za kwa jili ya kupima virusi vya Ukimwi.

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote