Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, April 23, 2010

Maisha kusaidiana!!

Baba na Mama wakiwa mzigoni

Waziri Mkuu wa Ubelgiji awasilisha barua ya kujiuzulu

Ubelgiji inaonekana kuingia tena katika mzozo wa kisiasa, baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Yves Leterme kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kufuatia mgogoro wa lugha. Mgogoro huo ni kati ya jamii inayozungumza Kifaransa na ile inayozungumza Kiflemish. Chama cha kiliberali katika serikali ya Leterme, kimejiondoa katika serikali ya muungano kutokana na sheria za uchaguzi katika vitongoji vya mji mkuu wa nchi hiyo, Brussels. Kiasi jamii ya watu 1,000 wanaozungumza Kiflemish waliingia mitaani kudai mipaka ya wilaya za uchaguzi iwekwe kulingana na lugha. Mfalme Albert wa Pili kwa sasa amekataa hatua ya kujiuzulu Bwana Leterme, akisema kuwa hatua hiyo itatishia ustawi wa Wabelgiji na pia nafasi ya nchi hiyo barani Ulaya. Ubelgiji inajitayarisha kuchukua nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Ulaya mwezi Julai, mwaka huu.

Tuesday, April 20, 2010

Maimatha kudhamini shindano la uchezaji wa Kiduku!

MAKUNDI matano kati ya nane yamefanikiwa kuingia fainali ya mashindano ya kutafuta bingwa wa kucheza kiduku kwa mwaka huu,baada ya kushinda katika nusu fainali iliyofanyika katika ukumbi wa Traventain uliopo magomeni. Mashindano hayo ambayo,yameandaliwa na Manywele Entertaiment,ambayo ipo chini ya Maimartha,yaliwakutanisha makundi nane kutoka sehemu mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam. Katika shindano hilo ambalo wakazi wengi kutoka sehemu mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam,walihudhuria na kuujaza ukumbi na kusababisha baadhi ya watu wakose viti vya kukalia na kukaa chin. Vikundi vilivyofanikiwa kuingia fainali ni Vidaleki kutoka Magomeni Makuti,ambao walikuwa wa kwanza kwa kujikusanyia kura 830 na kufutiwa na Stavanga kutoka Mwananyamala waliopata kura 790,washindi wa tatu walikuwa Mazombi kutoka kwa Alimaua A ambapo walipata kura 660,waliofanikiwa kushika nafasi ya nne na tano ni Vsquer kutoka Yombo waliopata kura 650 na Wanaume Fight kutoka Makumbusho waliojikusanyia kura 560. Katika shindano hilo la kumtafuta mkali wa kucheza kiduku,fainali yake inatarajiwa kufanyika Mei 2 mwaka huu,ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha Dola 250 za Kimarekani. Hata hivyo Msimamizi wa Shindano hilo Maimartha,hakutaja ukumbi ambao utatumika siku hiyo ya fainali,na kuwatangazia mashabiki waliojitokeza katika shindano hilo,kuwa sehemu ambayo itafanyikia fainali itatangazwa siku zijazo,kabla ya fainali hiyo.

'ChemChem' ya Pesa Mkoani Ruvuma Yavuta Wengi

WAKAZI wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamekuwa wakikesha wilayani humo usiku na mchana wakisubiria pesa zinazotoka chini ya mti mithili ya chemchem. Baadhi ya Wakazi wa mji huo inasemekana waligundua maajabu hayo kwenye mti huo na baada ya wakazi hao kuanza kujizolea pesa toka kwenye mti huo habari ghafla zilisambaa mkoani Ruvuma kuwa kuna mti una chemchem ya pesa.Ilidaiwa kuwa wakazi hao walipokuwa wakipita chini ya mti huo waliona pesa zikitoka chini ya mti na pamoja na kustaajabishwa na tukio hilo wakazi hao waliamua kuzichukua pesa hizo.Taarifa zaidi zilisema kwamba kwa muda wa siku mbili mfulululizo wakazi wa wilaya ya Songea waliendelea kuziokota pesa zilizokuwa zikitoka kwenye mti huo.Pesa hizo inadaiwa zilikuwa zikitoka mithili ya chemchem zikiwa ni noti tofauti tofauti zikiwemo na noti za shilingi elfu kumi, tano na kadhalika.Baadhi ya watoto waliowahi kuhojiwa na mwakilishi wetu wa nifahamishe kutoka eneo la tukio, watoto hao walidai kuwa walishajizolea pesa hizo na walizipeleka kwa wazazi wao nyumbani.Walidai kuwa pesa hizo zilikuwa zikitoka chini ya ardhi na mamia ya watu toka sehemu mbalimbali za mkoani Ruvuma walikuwa wakizigombania kila zilipoanza kuchomoza.Watu wazima waliohojiwa na Nifahamishe nao pia walithibitisha kujizolea noti hizo zilizodaiwa kutoka kwenye chemchem hiyo.Kwa kuwa pesa pesa hizo zilikuwa zinatumia muda mrefu kutoka kwenye chemchem hiyo, maelfu ya watu kutoka wilaya tofauti wamekuwa wakiweka kambi eneo hilo kusubiria pesa hizo.Tukio hilo limethibitishwa na polisi mkoani humo na walisema wanafanya uchunguzi wa kina kubaini kuwa pesa hizo zinakuwa zinatoka wapi.

Tuesday, April 13, 2010

Baba ashikiliwa kwa tuhuma za kumkanyaga mtoto wake kwa gari na kusababisha kifo

MKAZI wa Makumbusho, Gharibu Ayubu (35) anashikiliwa kituo cha polisi Kinondoni jijini hapa kwa kumkanyaga kichwani kwa gari lake hadi kufa, mtoto wake, Ayubu Gharibu aliyekuwa na mwaka mmoja na miezi mitano wakati alipokuwa akirudi nyuma ili kutoka katika nyumba yake wakati akitaka kuelekea Sinza. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elius Kalinga aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2.00 asubuhi katika nyumba ya Gharibu iliyopo barabara ya New Bagamoyo eneo la Makumbusho katika Wilaya ya Kinondoni. Kalinga alisema tukio hilo lilitokea baada ya mtoto huyo kutaka kwenda na baba yake asubuhi hiyo, lakini baba yake akamkabidhi kwa mkewe ambaye alirudi naye ndani, lakini baada ya muda mtoto huyo alitoka tena nje na kulifuata gari hilo bila mama yake kujua. Alisema mtoto huyo alipolifikia gari hilo aina ya Toyota Folona alikwenda kusimama nyuma yake na Gharibu alipokuwa akirudi nyuma ili aweze kupata mwelekeo wa kutoka katika nyumba yake kuelekea Sinza ghafla akamkanyaga mtoto huyo kichwani na kumsababishia kifo kwa kuwa aliumia sana kichwani. Kamanda Kalinga alisema Gharibu anashikiliwa na jeshi lake na atafikishwa mahakamani huku uchunguzi wa kesi yake ukiendelea kufanyika.

Ajuza wa miaka 102 aanza darasa la kwanza

Bibi mmoja nchini China amekuwa mwanafunzi mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani baada ya kuamua kuanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 102. Ma Xiuxian, kutoka Jinan, katika jimbo la Shandong alifanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuanza elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka 102.Ma alianza kufanya kazi kwenye kiwanda cha nguo tangia alipokuwa na umri wa miaka 13 na kwa miaka yote aliendelea kufanya kazi huku akiwa na ndoto ya kuwa na angalau elimu ya shule ya msingi.Ma aliolewa akiwa na umri wa miaka 18 na alifanikiwa kupata watoto tisa, saba kati yao ni wahitimu wa shahada ya kwanza ya chuo kikuu.Ma alipewa nafasi ya kusoma kwenye shule hiyo baada ya kulieleza gazeti moja la mjini mwake kuwa alikuwa na ndoto ya muda mrefu sana ya kwenda shule."Nina furaha sana nimeweza kutimiza ndoto yangu ya kwenda shule ingawa katika umri huu", alisema Ma.Ma alienda shuleni akisindikizwa na mwanae wa mwisho wa kiume Yi Fengxin mwenye umri wa miaka 58.Katika somo lake la kwanza katika shule yake ya Weishan Road Primary School, Ma alisema "Nawashukuru walimu wangu, nawashukuru wanafunzi wenzangu nawaahidi nitajisomea kwa nguvu zote na nikimaliza shule nitasaidia kulijenga taifa".Ma anatumia kifaa cha kumsaidia kusikia vyema ili aweze kuwasikia walimuwa wake vizuri na huwatumia wanafunzi wenzake kumsaidia kusoma vitabu vya masomo yake.Ma ameingia kwenye rekodi za dunia kwa kuwa mwanafunzi mzee kuliko wanafunzi wote duniani.

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote