Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, May 25, 2010

Watu 5 wa familia moja wateketea kwa moto

WATU watano wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketezwa kwa moto uliodaiwa kuwashwa kimakusudi kuteketeza familia hiyo huko Vijibweni Wilayani Temeke.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya usiku, huko maeneo ya Vijibweni Temeke ambapo ajali hiyo imetokana na ugomvi wa kimapenzi kutoka kwa mmoja wa wanafamilia hiyo.Watu hao wote kwa pamoja waliweza kupoteza maisha usiku huo baada ya nyumba hiyo kuteketea kwa moto wakiwa ndani kwao katika chumba kimoja kwa pamoja.Wanafamilia hao walioteketea kwa moto ni baba wa familia, John Onesmo (32) ambaye ni mfanyabiashara wa samaki eneo la Feri, mke Catherine John (25), watoto wao wawili ambao ni Joyce John (5) na Oliver John na Esther Amos (20) ambaye ni mdogo wa Catherine. Moto huo uliolipuliwa majira ya saa 6 usiku, ulidaiwa kulipuliwa na mchumba wake Ester aliyetambulika kwa jina la Shemsa Mpelela (22), kutuhumiwa kuchoma moto nyumba hiyo kwa kutumia mafuta aina ya petroliKwa mujibu ya maelezo ya majirani usiku huo walisikia mlipuko mkali na walidhani kuwa pikipiki imepasuka tairi ama mlio wa risasi na kuamka na kuona nyumba hiyo inawaka moto. Majirani waliweza kuamka kwa kushirikiana kutaka kuwaokoa watu hao lakini ilishindikana kwa kuwa moto ulishapamba kuzingira nyumba hiyo na juhudi zilishindikana na watu hao kumaliza maisha ndani humoHata hivyo zimamoto lilichelewa kufika eneo hilo kutokana na ubovu wa barabara na gari lilikwama njiani. Askari walipofika eneo la tukio na baada ya moto huo kuzimwa walipoingia ndani tayari watu hao walishapoteza maisha na John alikutwa amekumbatia watoto wake kitandani.Tukio hilo ambalo moja kwa moja linahusishwa na ugomvi kati ya Ester na Shemsi majirani walidai kuwa mwaka jana Esther alipomaliza darasa la saba Manyoni, Singida, alikuja kwa dada yake huyo kuishi nae. Ilidaiwa na majirani hao kuwa Ester alianza tabia ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume mahali hapo hali ambayo dada yake alikuwa akigombana nae hadi ilifikia hatua dada yake huyo kumrudisha kijijni kwao kutokana na tabia zake hizo.Ilidaiwa kuwa Ester alirudi tena jijini kwa kurudishwa na nauli aliyotumiwa na Shemsi na kwenda kuishi nae Kigamboni nyumbani kwa Shemsi na alirudi na kuja tena kwa dada yake baada ya kutokea ugomvi wa kimapenzi ambao haujafahamika chanzo chake hali iliyopelekea Shemsi kumchoma kisu Ester shingoni na tumboni. Na dada yake kwa kushirikiana na mume wake walijaribu kumtafuta Shemsi na hawakuweza kumpata na hawakujua yuko wapi. Na usiku wa kuamkia jana baada ya tukio hilo kutokea dumu ambalo lilikuwa na mafuta hayo lilionekana pembezoni mwa nyumba hiyo ambayo ilikuwa haijaisha na kumalizika chumba hicho na kuhamia.Polisi Mkoani Temeke limethitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari linafanyia kazi tukio hilo la kusikitisha.

Hukumu ya Liyumba ni kama Mazingaombwe!

MAHAKIMU kuwa katika jopo hakumaanishi kuwa katika kufikia uamuzi watafanana katika fikra, welewa na mtazamo na hilo limedhihirika katika hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba. Jopo hilo jana lilitofautiana na kuweka rekodi ambayo itakuwa ya mfano hata kwa wasomi wa sheria, baada ya Hakimu Edson Mkasimongwa kutofautiana na mahakimu wenzake Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa. Wote walikuwa wameunda jopo la kusikiliza kesi ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Liyumba, ambaye mahakimu Mlacha na Mwingwa walimwona ana hatia na hivyo kumhukumu kifungo cha miaka miwili jela. Lakini kwa upande wa Mkasimongwa, alimwona Liyumba kuwa hana hatia kwa kuwa mahakama ilishindwa kuthibitishiwa kama kweli alitumia madaraka yake vibaya katika ujenzi wa jengo pacha la BoT. Hata hivyo Mkasimongwa alisema kwa kuwa wengi wape, hukumu ambayo itahesabika kuwa ndio uamuzi wa mahakama itaanza kusomwa na kufuatia yake ambayo itabakia kuwa kumbukumbu ya mahakama na kuhifadhiwa katika jalada la kesi hiyo. Mkasimongwa katika uamuzi wake alisema mshitakiwa hana kesi ya kujibu kwa sababu mashitaka dhidi yake hayakuthibitishwa bila kuacha shaka yoyote kama sheria inavyotaka kwa kuwa kuna maswali mengi yalikosa majibu. Akisoma hukumu yake ambayo aliiita mbadala, alisema katika barua zilizoletwa mahakamani na upande wa mashitaka kama vielelezo zikidaiwa kusainiwa na mshitakiwa, hazina majibu kwamba ni kweli alifanya mabadiliko hayo na kama alikuwa na mamlaka hayo, vile vile haikuelezwa na upande wa mashitaka kuwa menejimenti nayo ilikuwa ikijibu nini. “Kuna uwezekano mabadiliko yale yaliridhiwa na Gavana na menejimenti yote, isingeleta swali kama kungekuwa na majibu au maelekezo tofauti,” alisema Mkasimongwa akiongeza kuwa ilitakiwa barua zilizokuwa zikimjibu mshitakiwa ziletwe, ili kujua na Utawala na Gavana walikuwa na uamuzi gani. Hivyo aliridhika kusema hakuna matumizi mabaya ya ofisi aliyotenda mshitakiwa. Hakimu Mlacha ambaye alisoma hukumu halisi alianza kwa kumkumbusha mshitakiwa mashitaka aliyofikishwa nayo mahakamani hapo ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 221. Hata hivyo mashitaka hayo yalifutwa na mahakama baada ya kukosa hatia wakati upande wa mashitaka ulipofunga ushahidi wake, pamoja na ya matumizi mabaya ya ofisi aliyokuwa amebaki nayo. Mlacha alisema katika hukumu hiyo aliyoanza kuisoma saa 3.50 hadi saa 7.20 mchana, kwamba bila shaka ushahidi ulionesha mshitakiwa alikuwa mtumishi wa umma katika kipindi chote cha mwaka 2001 hadi mwaka juzi kwenye Mradi wa 10 Mirambo (majengo pacha) anaodaiwa kubadili sura yake wakati ukitekelezwa, kwa mujibu wa mashahidi wanane walioletwa na upande wa mashitaka na wawili wa utetezi. Aidha alisema, mahakama inapingana na ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi ambao ulitolewa na mshitakiwa na Bosco Kimela ambaye alikuwa Katibu wa Bodi ya BoT ambao walidai kuwa Liyumba hakuhusika na mabadiliko ya sura ya mradi na badala yake kuutupa mpira kwa Gavana wa wakati huo Daudi Ballali na Meneja wa Mradi, Deogratius Kweka. Katika ushahidi wao, walidai kuwa ingawa mradi ulikuwa chini ya kurugenzi yake, lakini mshitakiwa hakuhusika kutoa uamuzi. Vile vile mahakama haikubaliani na ushahidi wao kuwa Gavana alimteua mshitakiwa kwa mdomo, kusaini barua kwa niaba ya BoT, kwa kile walichodai kuwa Kweka hakuwa mwajiriwa wa kudumu wa benki hiyo. Hata hivyo, katika uamuzi wa mahakimu hao walikubaliana na ushahidi wa upande wa Serikali kwamba mawasiliano yoyote ya ndani ya ofisi za BoT yalifanyika kwa njia ya maandishi na si kwa mdomo kama Liyumba alivyodai kupewa jukumu la kusaini barua kwa mdomo huku kukiwa na ushahidi mwingine kwamba Gavana naye hakuwa na uamuzi wa mwisho bali Bodi ya Wakurugenzi. “Katika mradi huo uliolengwa kutekelezeka kwa mujibu wa mkataba, inakubalika kuwa haukutekelezeka kama ilivyotakiwa, yalikuwapo mabadiliko makubwa, ushahidi ulionesha kwamba katika matumizi yote ya maendeleo Bodi ndiyo ilikuwa na mamlaka ya mwisho, lakini katika mradi huu, kanuni hiyo haikufuatwa, fedha zililipwa bila utaratibu,” alisema Mlacha. “Mahakama inasema mshitakiwa alisaini barua zote zilizokuwa zikitoa maelekezo ya kubadili mradi na alifanya hivyo bila mamlaka kinyume cha sheria matumizi yaliyoongezeka na kuathiri BoT na bila shaka Taifa kwa jumla,” aliongeza. Baada ya mshitakiwa kuondolewa mahakamani, ndugu zake walilia huku wakidai kutoridhishwa na uamuzi huo. Hata hivyo wakili Majura Magafu anayemtetea Liyumba, alisema jana wangewasilisha notisi Mahakama ya Rufaa ili kuonesha nia yao ya kukata rufaa kwani ni imani yao kuwa ushahidi katika kesi hiyo haukuchambuliwa ipasavyo. Mtuhumiwa huyo alikaa rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitatu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kutoa Sh bilioni 110. Akiwa katika basi linalobeba washitakiwa lenya namba STK 4373, saa 7.41 mchana Liyumba alianza safari yake akitokea Kisutu kuelekea makazi yake mapya ambako atatumikia kifungo hicho cha miaka miwili jela.
Chanzo:Habari leo

Je kulikuwa na umuhimu wa kupiga hii picha?

Monday, May 3, 2010

Ajira inapokuwa ngumu

Obama ndani ya jinamizi la kashfa ya ngono


Rais Barack Obama wa Marekani anadaiwa kuisaliti ndoa yake na Michelle Obama kwa kujirusha na mrembo wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Vera Baker.Mwaka 2004 wakati Obama akipiga kampeni za useneta ilidaiwa kuwa alijivinjari chumba kimoja hotelini na mrembo Vera Baker ambaye wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 29.Wakati huo Vera alikuwa mdau wa karibu wa Obama kwenye kuchangisha fedha za mfuko wa kampeni na alifanikiwa kuchangisha mamilioni ya dola.Miaka sita ikiwa imepita bila ya ushahidi hata wa picha kutolewa, jarida maarufu la Marekani National Enquirer limeliibua upya soo hilo likisema kwamba lina ushahidi wa video kuthibitisha kuwa Obama aliisaliti ndoa yake.Jarida hilo ambalo lilijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya kuibua skendo la mgombea urais John Edwards kuwa anajivinjari kwa siri na mrembo Rielle Hunter na kwamba amezaa naye mtoto mmoja.Hivi sasa National Enquirer linasema kwamba lina ushahidi wa video za kamera ya ulinzi kwenye hoteli ya jijini Washington D.C ambayo Obama na Bi Vera wanadaiwa kupumzika kwenye chumba kimoja.Jarida hilo limesisitiza kuwa iwapo watu wataziona video walizo nazo basi wataamini kuwa rais Obama aliisaliti ndoa yake na Michelle Obama.Obama hajasema chochote tangia National Enquirer lilipoliibua tena skendo hili ingawa Vera alishawahi kukanusha kuwepo kwa uhusiano wowote wa kimapenzi kati yake na Obama.Wafuasi wa chama cha Democratic cha rais Obama wanaamini kuwa skendo hili ni njama za Republican kummaliza kisiasa rais Obama

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote