WATU watano wamefariki dunia papo hapo jana, baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakiwa wanachimba kokoto huko katika kijiji cha Ntyuka, mkoani Dodoma Waliofariki katika tukio hilo ni wanawake watatu na watoto wawili ambao walikuwa na mama zao eneo la tukio.Wanawake hao ni Monica Chizumi na mwanawe Porina Chizumi mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, Mwajuma Mnubi na mtoto wake, Jonas Mnubi wa mwaka mmoja na miezi 8 na Mbeleje NdingomoMbali na waliokufa dunia watu wengine wawili ambao ni Beatrice Chizumi na Noel Lazaro alijeruhiwa na walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kunusurika katika tukio hilo.Tukio hilo la kusikitisha lililotokea jana majira ya saa 7 mchana kijijini humo.
Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Tuesday, February 16, 2010
Hela za Fidia Kiwapa zataka kumtokea puani!!!!!!
KIJANA mmoja aliyetambulika kwa la Mbegu Moto amejikuta matatani baada ya kubambwa akijaribu kutaka kuchukua fidia kwa kutumia jina la marehemu baba yake bila kufungua kesi ya mirathi. Sakata hilo liliibuka jana baada ya mtoto huyo kwenda kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa unaotumika kuwalipa fidia wakazi hao akiwa na kitambulisho chenye jina marehemu baba yake, lakini akiwa amebandika picha yake. Akizungumzia hilo mmoja wa wajumbe wa kamati ya malipo alisema nyumba yenye namba KP 996 ilikuwa ikimilikiwa na marehemu Mbegu Moto Bothi ambaye alishafariki na kwamba taarifa za kifo chake zinajulikana kwenye kamati hiyo. Alisema mara baada ya kuwasili kwake Jumatano ya wiki iliyopita kamati hiyo ilimtilia mashaka na kumtaka arudi nyumbani kwake akachukue vielezo vingine na ndipo alipopotokea jana akiwa na katibu wa iliyokuwa serikali ya mtaa ili amtambulishe kwetu. Kutokana na utambulisho aliokuwa nao kamati iliamua kumweka chini ya ulinzi ili kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukua mkondo wake. "Wakati wa uthamini wa nyumba za Kipawa mzee huyo alikuwa hai ndiyo sababu ya jina huyo marehemu kuingia kwenye kitabu cha malipo na kutengenezewa hundi, baada ya kufariki kwake, serikali ilipata taarifa kamati inalijua hilo na ndio maana ilisita kumpatia hundi kijana huyo,"alisema mmoja wa wajumbe wa kamati. Alisema jambo hilo liliishitua kamati hali iliyowalazimu kuhoji sababu za kijana huyo kwenda kuchukua hundi hiyo ambayo baadaye ilifahamika kuwa ni ya baba yake mzazi aliyefariki muda mrefu uliopita. Akizungumzia hilo katibu wa iliyokuwa serikali ya mtaa wa Kipawa Said Hangahanga alisema yeye anaifahamu familia hiyo, lakini hakujua kama kijana huyo alikwenda kuchukua fidia hizi bila ya kufungua kesi ya mirathi. Alisema yeye alipoitwa na kamati alijua kuwa anakwenda kufanya kazi ya kuelezea namna anavyomfahamu kijana huyo kama watu wengine wanavyofanyiwa pindi kunapokuwa na ugumu wa kamati kuwatambua. "Mimi ninaifahamu familia ya mzee Mbegu ina watoto watatu na huyu ndiye mkubwa, kimsingi sielewi ni kwani hakufungua kezi ya mirathi labda aliona apite njia ya mkato ili apate fida hizo,"alisema Hangahanga na kuongezea "yeye ndiye anayetegemewa na familia yake ukisema anaiba anamuibia nani au anajiibia?"alihoji. Alisema yeye alikwenda kutoa taarifa ya namna anavyomfahamu, lakini ahakuwa anajua kama kijana huyo kapitia njia ya mkato kiasi hicho katika madai yake.
Monday, February 15, 2010
Je unataka kuwa mweupe wa ngozi bila madhara kwa kutumia vitu vya asili?
Fanya hivi , tengeneza mchanganyiko wa
1. Kijiko kimoja cha asali
2 Kijiko kimoja cha Maziwa ya unga
3. Kijiko kimoja cha Juice ya ndimu
4. Nusu kijiko cha Mafuta ya almond
Paka mchanganyiko huo usoni au sehemu yoyote ya ngozi na uache kwa dakika 10 hadi 15 kama mara 3 kwa wiki utafanya ngozi yako iwe ung'ae na kuwa nyeupe
1. Kijiko kimoja cha asali
2 Kijiko kimoja cha Maziwa ya unga
3. Kijiko kimoja cha Juice ya ndimu
4. Nusu kijiko cha Mafuta ya almond
Paka mchanganyiko huo usoni au sehemu yoyote ya ngozi na uache kwa dakika 10 hadi 15 kama mara 3 kwa wiki utafanya ngozi yako iwe ung'ae na kuwa nyeupe
JK awapa shavu wasanii wa Bongo?
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete, ametangaza juhudi zake za kulinda maslahi ya wasanii nchini kwa kuunda kikosi maalumu cha kulinda haki zao na pia amewafungulia studio ya kisasa kwaajili ya kazi zao. Rais Kikwete alitoa ahadi hizo juzi alipoungana na wasanii mbalimbali nchini katika tamasha la Zinduka, kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchini.Katika tamasha hilo ambalo lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, majira ya jioni, liliweza kuteka umati wa mashabiki, kufuatia kuwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini.Wasanii zaidi ya 20 kutoka Tanzania na nje ya Tanzania waliweza kukonga nyoyo mashabiki hao kwa jinsi walivyoliumudu jukwaa.Rais aliwatoa hofu wasanii na kuwapongeza kwa jinsi walivyoweza kujipanga na kufanya jambo la msingi la kuelimisha umma, “Ningependa mjue kuwa, mimi nyimbo na kazi zenu zote nazifuatilia, nyimbo za Bongo fleva mimi ni msikilizaji mzuri sana, Zamani mimi nilikuwa nacheza Sikinde, Soboso na Lumba, kwa nyimbo za Bongo fleva ya sasa mnanikosha sana nawapa hongera” alisema JK.Wakati akisoma hotuba ya uzinduzi huo, Kikwete aliwataka wasanii wote nchini kujithamini na kuthamini kazi zao ili ziweze kuwanufaisha. “Kilio chenu, nimekisikia siku nyingi juu ya kunyonywa kwa mapato ya kazi yenu, najua mnavuja jasho lakini hamfaidiki matunda yake naahidi kuendelea kulishughulikia” alisema Kikwete.Rais aliwataka wasanii kujipanga na kutimiza malengo waliyojipangia, huku akiwataka kuitumia mitambo mipya na ya kisasa ya studio ambayo aliwaahidi kipindi cha nyuma kuwaletea ambapo alitimiza ahadi hiyo.“Kilio chenu cha studio ya kisasa mlichokuwa mnalia muda mrefu nimewatimizieni, mshindwe wenyewe na kwa swala la kuibiwa kazi zenu na kuwafanya kukosa mapato naahidi kulitokomeza kabisa hilo kwa kuunda kikosi maalum cha kushugulikia kero zote” Aliendelea kusema kuwa, kwa wasanii wa filamu na muziki ndiyo wanoongaza kwa kudhulumiwa kazi zao, huku akiwataka kusubiri neema kwa uundwaji wa kikosi kazi ‘Task force’ maalum kitakachokuwa chini ya Wasanii wenyewe, COSOTA, TRA, BASATA, Jeshi la Polisi na wizara yenye dhamana kuhakikisha kero hizo zinapotea kabisa nchini.Nyota wa Muziki wa Pop wa kundi la "No Angels" wa Ujerumani hatiani kwa kuwambukiza Ukimwi Wanaume Watatu
Waendesha mashtaka wa Ujerumani jana ijumaa walimuona msanii maarufu wa kundi la "No Angles" Nadja Benaissa mwenye umri wa miaka 27 ana hatia ya kuwaambukiza ukimwi wanaume watatu aliofanya nao mapenzi bila kinga. Nadja anadaiwa kufanya mapenzi na wanaume hao kati ya mwaka 2000 na 2004 bila kuwataarifu kuwa yeye ni muathirika.Nadja alikuwa akijitambua fika kuwa yeye ni muathirika tangia mwaka 1999, nyaraka za mahakama zilisema."Alikuwa akijua wazi kuwa kwa kufanya mapenzi bila kinga atawaambukiza maradhi yake wanaume hao", alisema mwendesha mashtaka katika mji wa Darmstadt ulio jirani na Frankfurt.Mmoja wa wanaume hao watatu ameishathibitishwa kuwa ameambukizwa virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi.Kundi la No Angeles liliibuliwa na mashindano ya vipaji kwenye luninga mwaka 2000 na baada ya kujipatia umaarufu mkubwa walifanya ziara nyingi sana barani ulaya kabla ya kundi hilo kuvunjika mwaka 2003.Rais Kikwete atangaza Malaria Janga la Taifa
RAIS Jakaya Kikwete ameutangaza ugonjwa wa malaria kuwa ni Janga la Taifa na kuwaambia Watanzania kuwa Serikali yake imeanza safari ya kuutokomeza ugonjwa huo nchini. Malaria ndiyo ugonjwa unaoua Watanzania wengi zaidi kuliko mwingine wowote. Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa marais wanaopambana na malaria barani Afrika alisema kwamba, ugonjwa wa malaria ni vita ambavyo ni lazima Watanzania wavishinde kwa vile nia ipo, sababu ipo na uwezo upo. Aliongeza kusema kuwa, lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa malaria inakuwa ugonjwa wa historia kwa Tanzania kwa kuwa hata nchi nyingine zimefanikiwa kuutokomeza. Alisema kuwa kila siku ya Mungu, kiasi cha watu kufikia 291 hufariki kwa ugonjwa wa malaria, wengi wao wakiwa watoto wadogo, vifo ambavyo alivielezea kuwa vinaweza kuzuilika na kutibika. "Kila siku ya Mungu, hapa nchini, wanakufa watu hadi 291 kwa ugonjwa wa malaria. Kwa maneno mengine, kila saa inayopita, wanakufa watu zaidi ya 10 kwa ugonjwa wa malaria." Rais Kikwete aliliambia taifa usiku wa kuamkia jana. "Hawa ni watu wengi mno. Hivyo, malaria ni Janga la Taifa letu. Lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba malaria ni ugonjwa unaoweza kuzuilika na kutibika. Ndiyo maana tumeamua kuwa wakati tunaendelea kushughulikia kutibu wagonjwa wa malaria, tuelekeze nguvu zetu katika kuzuia kwa kuanza juhudi za kutokomeza malaria nchini." Rais Kikwete alikuwa akizungumza moja kwa moja na taifa wakati anazindua Kampeni dhidi ya Malaria katika burudani maalumu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club mjini Dar es Salaam juzi usiku.Google Kutoa Simu Zinazotafsiri Lugha Tofauti Tofauti
Kampuni ya teknolojia ya Google inatarajia kutoa simu zinazotafsiri lugha zaidi ya 6000 zinazozungumzwa duniani ili kuwawezesha watu wanaozungumza lugha tofauti kuelewana.Google ambao awali walijiingiza kwenye biashara za simu kwa kutoa simu zao zinazoitwa Nexus One, tayari wanatamba na programu yao waliyoitoa ambayo inatafsiri maandishi katika lugha tofauti tofauti.Wiki iliyopita lugha ya Haiti "Creole" iliongezwa katika programu hiyo na hivyo kuzifanya lugha ambazo zinawezwa kutafsiriwa maandishi yake na programu ya Google kufikia 52.Hadi sasa Google imeishawawezesha watumiaji wa simu kutumia mfumo wa kutambua sauti kusachi vitu kwenye google kwa kuvitamka badala ya kuviandika.Google itaziunganisha teknolojia zake hizo mbili ili kuweza kutoa simu zitakazokuwa zinafanya kazi kama mkalimani.Kama ilivyo kwa watu wanaofanya kazi ya ukalimani, Simu hizo pia zitakuwa zikisiliza sentensi nzima mtu anayoongea ili kuelewa kinachosemwa kabla ya kuanza kuitafsiri.Mkuu wa huduma ya ukalimani ya Google, Franz Och, amesema kuwa wanachohangaikia kwa sasa ni kuuongeza usahihi wa kutambua sauti na kuweza kutafsiri kwa usahihi.Simu hizo mpya za Google zinatarajiwa kuingia madukani ndani ya miaka michache ijayo.
Friday, February 12, 2010
Papic kumrithi Maximo?
KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic jana aliwasilisha rasmi barua ya maombi ya kazi Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwania nafasi ya kumrithi Mbrazil Marcio Maximo anayemaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars mwezi Julai. Papic ambaye aliweka bayana dhamira yake hiyo ya kuwania kuifundisha Taifa Stars pale tu TFF ilipotangaza kuanza mchakato wa kumtafuta kocha mpya, aliwasili katika ofisi za shirikisho hilo majira ya saa 5:30 asubuhi akisindikizwa na katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi barua yake, Papic alisema amefikia uamuzi huo kutokana na kuamini kuwa ana vigezo vyote vinavyomwezesha kuwa kocha wa Taifa Stars.Nguza, Papii Kocha ndo basi tena uraiani???????? Francis ana Mbangu huru
VILIO na majonzi jana vilitawala katika Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam wakati mahakama hiyo ilipomuamuru mwanamuziki maarufu, Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya, na mwanawe, Papii Nguza (Papii Kocha) waendelee na vifungo vya maisha jela. Kwa mujibu wa taratibu za mahakama Tanzania, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ni wa mwisho, hivyo Babu Seya na Papii Kocha watakaa jela maisha yao yote. Mahakama hiyo imewaachia huru watoto wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza. Tangu Juni mwaka 2004 Babu Seya na wanawe watatu walikuwa jela kutumikia kifungo cha maisha kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam iliona wana hatia ya kubaka ya kulawiti. Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Babu Seya na Papii wamekutwa na hatia katika baadhi ya makosa, lakini Francis na Nguza Mbangu hawana hatia katika kosa lolote. Baada ya Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Neema Chusi, kusoma hukumu hiyo ya rufaa, watu walianza kulia, sauti ya Francis ilisikika zaidi pengine kutokana na uchungu wa kumuacha baba na kaka jela,sanjari na furaha ya kuachiwa huru. Wakati Francis akiendelea kulia, watu wakiwemo waaandishi wa habari walimzunguka hivyo kusababisha wananchi wengine waliokuwa pembeni kulia, askari wakawa wanabubujikwa machozi. Baada ya hukumu hiyo,wanamuziki hao walitolewa katika chumba cha mahakama na kupelekwa katika chumba kingine kilichozungukwa na watu wengi wakiwemo wasanii waliokwenda kusikiliza hukumu hiyo. Wakati wakielekea katika chumba hicho Papii Kocha alisikika akisema “Kikwete atatusaidia, Kikwete atatusaidia”. Chusi amesema, mahakama imeshindwa kuwatia hatiani Francis na Nguza Mbangu kwa sababu upande wa mashitaka umeshindwa kudhibitisha makosa dhidi yao. Mahakama imetoa mfano kuwa, baadhi ya mashahidi waliopelekwa mahakamani na upande wa mashitaka waliweza kuwatambua Papii Kocha na Babu Seya lakini hawakuwatambua hao wengine hata kwa majina. Awali Babu Seya na wanawe watatu walihukimiwa katika mashitaka 23, Mahakama ya Rufaa imeyaondoa mashitaka 11 ya kuingiliwa kinyume kwa maumbile kwa sababu hakuna mashitaka kama hayo chini ya sheria za kujamiiana. Mahakama ilikubaliana na Wakili Mabere Marando kuwa ushahidi uliotolewa ulichukuliwa bila kiapo kwa vile hakimu hakujiridhisha kama watoto waliohusika walikuwa na uelewa wa kutambua kile walichokuwa wanakisema ni cha kweli na hivyo ushahidi huo ulitakiwa kuungwa mkono. Mahakama hiyo imebaini kwamba,kulikuwa na ushahidi wa kutosha wa kuunga mkono ule wa watoto, ukiwemo unaoelezea namna chumba kilivyo ambacho kilikuwa kinatumika kwenye ubakaji na pia kitendo cha Babu Seya kuongeza sauti ya redio wakati wa kutenda kosa ili watu waliokuwa nje wasifahamu kilichokuwa kikiendelea ndani. Juni 25, 2004, Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Hakimu Addy Lyamuya, aliwatia hatiani Babu Seya na wanawe watatu kwa makosa 23 ya ubakaji na ulawiti, akawahukumu kifungo cha maisha. Wasanii hao walibainika kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam. Waliwasilisha rufaa kwenye jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania akiwemo Mbarouk Salim, Salum Massati na Nathalia Kimaro. Katika rufaa hiyo, wakili wa wasanii hao,Mabere Marando, alidai kuwa,Hakimu Lyamuya, aliingiza maslahi yake binafsi na hakuwa akizingatia ushahidi uliokuwa ukitolewa na upande wa washitakiwa. Marando amedai kuwa, hakimu huyo alitoa kipaumbele kwa mashahidi wa upande wa Jamuhuri na kupuuza mashahidi wa upande wa washitakiwa hivyo kuwanyima haki. Kwa mujibu wa Marando, watoto wote waliokwenda mahakamani kuthibitisha kwamba walibakwa au kulawitiwa na washitakiwa walitoa ushahidi bila kiapo isipokuwa mmoja kati ya 10 waliotoa ushahidi. Amedai kwamba, watoto hao pia hawakurekodiwa ushahidi wao kabla ya kutoa ushahidi mahakamani jambo ambalo linakiuka sheria. Marando amedai kuwa,baadhi ya watoto waliotoa ushahidi walikiri kutomtambua Babu Seya na washitakiwa wengine na kwamba, ripoti ya Daktari ilionyesha kwamba miongoni mwa watoto hao walikuwa ni bikira hivyo kumaanisha kwamba walikuwa hawakufanya kitendo chochote kilichohusiana na mashitaka hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
VJN Super Motors
Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote

