Kesi ya mauji ya kikatili ya watu 17 wa ukoo mmoja imechukua sura mpya baada ya mtu anayesadikiwa kuwa mganga wa kienyeji kuunganishwa kesi ya mauaji inayowakabili watuhumiwa wengine 18. Mganga huyo ambaye ni mwanamke pekee katika kesi hiyo, alitajwa kuwa ni Mariam Sivanus Masatu, anadaiwa kufanikisha mipango ya mauaji hayo. Masatu jana alipandisha kizimbani kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka la kushiriki katika mauaji hayo yaliotokea usiku wa Februari 16, mwaka huu katika eneo la Buhare, nje kidogo ya Manispaa ya Musoma. Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi, Gabriel Bonanza, alidai mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Husen Mushi, kuwa kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kunaongeza idadi ya kutoka 19 hadi 20, ingawa alisema mtuhumiwa mmoja kati yao amefariki dunia hivyo kubakia watuhumiwa 19. Alimtaja mtuhumiwa aliyefariki kuwa ni Daudi Nyamagati Makika huku akiitaarifu mahakama kuwa mtuhumiwa mwingine, Bundara Ikaka, alishindwa kufika mahakamani jana kutokana na kuwa mgonjwa na kwamba amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara. Wathumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote dhidi ya mashitaka 17 ya mauaji na matatu ya kujaribu kuua ambayo yanawakabili. Walirejeshwa rumande hadi Aprili 14, mwaka huu. Polisi wengi walimwagwa kuimarisha ulinzi ili kuepusha uwezekano wa watuhumiwa hao kushambuliwa na watu wenye hasira. Wakazi wengi wa manispaa ya Musoma walijitokeza kuwashuhudia watuhumiwa wakiingia mahakamani. Hati ya mashitaka iliyosomewa watuhumiwa hao, ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao waliwaua watu 17 kwa kukusudia wakati wakijua ni kosa. Watuhumiwa katika kesi hiyo ni Marwa Mau Mgaya (16), Matiko Mgasa, Juma Mgaya, Juma Kinonko, Daudi Nyamagati, ambaye ni marehemu, Aloyce Nyakumu, Bahati Simeo, Nyakangara Wambura na Nyakangara Masemere. Wengine ni Kumbata Alphonce, Alphonce Nyabugimbi, Sodaki Alphonce, Mikindo Mgendi, Mole Magesa, Vedastus Nyangeta na Sospiter Mbita, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Nsingi Kukirango Usiku wa Februari 16 mwaka huu katika mtaa wa Bugaranjabho watu wasiofahamika walivamia familia tatu za ukoo mmoja na kuwaua kwa kuwachinja na kuwaatakata mapanga watu 17 wakiwemo watoto wachanga kwa kile kilichadaiwa ni ulipizaji wa visasi.
Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Wednesday, March 31, 2010
Tahadhari kwa wanywaji wa Windhoek na Heineken
KAMPUNI bia ya Mabibo Beer inspirit ya jijini Dar es Salaam imetoa tahadhari kwa wananchi kwa kuwa na wimbi kubwa la uingizwaji wa bia bandia nchini aina ya Heineken na Windhoek. Kampuni hiyo imesema vinywaji hivyo huingizwa nchini kupitia wao lakini kwa sasa kuna watu binafsi wamejitokeza kuingiza bia hizo bandia na kuzisambaza wakitumia nembo hizo kinyume na sheria.
KOVA aamuru kufungwa kwa BAR zote zilizopo karibu na Vituo vya POLICE
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameagiza baa zote zilizopo karibu na vituo vya polisi katika jiji la Dar es Salaam zifungwe sizieneldee na biashara hiyo kwa usalama zaidi wa vituo. Kamanda Kova alitoa tamko hilo jana ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari.Amesema lengo la kufunga baa hizo ni kupisha usalama wa vituo na kupisha huduma hiyo muhimu ambayo baa imeonekana ni moja ya vikwazo inayoikabili vituo hivyo.Amesema baa hazina umuhimu kama vituo vya polisi na wanafanya mpango ubadilishwa kuendesha shughuli hizo na kupewa leseni za kuwa maduka ya bidhaa nyingine za kawaida. `Liyumba ana kesi ya kujibu`
Upande wa Jamhuri katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.1 dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, umeiomba mahakama kumuona ana kesi ya kujibu. Upande wa Jamhuri umetoa hoja hiyo kwa kubainisha kuwa Liyumba alihusika kupitisha malipo ya ujenzi wa ghorofa kabla ya kibali cha bodi ya BoT. Wakijibu hoja za upande wa utetezi, upande wa Jamhuri umedai kuwa Liyumba anadaiwa kufanya mabadiliko hayo katika mradi huo bila kwanza kuomba idhini ya bodi na badala yake aliomba kibali baada ya kufanya mabadiliko. Hoja hizo zimewasilishwa jana alasiri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Ilidaiwa kuwa katika ushahidi uliotolewa na mashahidi nane dhidi ya mshitakiwa huyo, ni rai ya upande wa Jamhuri kwamba mahakama imuone mshitakiwa ana kesi ya kujibu. Hata hivyo, mahakama baada ya kupokea hoja za pande zote mbili kwa njia ya maandishi, hatma ya Liyumba kujitetea au kuachiwa huru itajulikana Aprili 9, mwaka huu. Pia upande huo wa mashtaka umeeleza kwamba ushahidi huo na kupitia vielelezo 13 vinatosha kabisa kuishawishi mahakama kumuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu. Machi 22, mwaka huu, upande wa utetezi uliomba mahakama kumuona mshitakiwa hana kesi ya kujibu baada ya ushahidi uliotolewa kutokuwa na nguvu hivyo mahakama imuachie huru. Machi 15, mwaka huu upande wa mashtaka ulifunga ushahidi dhidi ya kesi hiyo ambapo mahakama iliamuru pande zote ziwasilishe hoja za kama mshtaka ana kesi ya kujibu au la, kwa njia ya maandishi.Chanzo: Nipashe
Mama Kikwete anusurika katika ajali Mara
MKE wa Rais Mama Salma Kikwete anusurika kifo kwa ajali mbaya baada ya msafara wake kuingia doa kwa kuvamiwa na lori na kugonga magari matatu ya msafara huo. Ajali hiyo ilitokea jana wilayani Rorya mkoani Mara wakati Mama Salma akiwa ziarani mkoani humo. Kamanda wa Polisi Tarime, Bw. Constantine Masawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alisema lori hilo lilisimamishwa na askari wa barabarani lisimame ili kupisha msafara huo na kukaidi na kuingia barabarani na kusababisha ajali hiyo.Amesema kuwa lori hilo liligonga magari matatu ya nyuma ya msafara huo na kusababisha ajali ambayo haikuwa ya lazima kwa muda huo.Amesema lori hilo lilikuwa linatokea nchini Kenya ambapo ilidaiwa pia lori hilo lilikuwa limebeba mali za magendo.Hivyo imedaiwa dereva huyo ameshikiliwa na jeshi hilo ili kujibu tuhuma hizo.Hata hivyo hakuna aliyeweza kupoteza maisha katika ajali hiyo.Ujerumani launda Jopo maalum kuchunguza malalamiko ya dhuluma za kijinsia
Baraza la mawaziri la Ujerumani limeunda jopo maalum litakalovichunguza visa vya madai ya dhuluma za kijinsia vilivyotokea tangu miaka ya 1950 katika shule za Kikatoliki na za binafsi.Jopo hilo litasimamiwa na wizara za Sheria, Masuala ya Jamii na Elimu. Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria Sabine Leutheusser-Schnarrenberger,wajibu wa jopo hilo ni kujaribu kuhakikisha kuwa madai mengine mapya yanaripotiwa kabla ya kumalizika muda uliowekwa wa kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu wa kijinsia.Waziri wa masuala ya Jamii wa zamani,Christine Bergmann ndiye aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa jopo linalochunguza visa vilivyotokea muda mrefu uliopita ambavyo haviwezi kuchunguzwa na polisi. Mpaka sasa watu 250 walioathirika wamejitokeza.Wakati huohuo Papa Benedict wa XVI alilikubali ombi la kujiuzulu la askofu mmoja wa Kanisa Katoliki la Ireland aliyekuwa msaidizi wa binafsi wa mapapa 3 waliomtangulia.Askofu John Magee wa Cloyne,Ireland alitajwa katika uchunguzi wa mwaka uliopita akidaiwa kuwa hakuchukua hatua mwafaka wakati visa vya dhuluma za kijinsia viliporipotiwa kutokea katika dayosisi yakeCCJ yapokea kigogo wa CCM
JANA mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Bw. Fred Mpendazoe ametangaza rasmi kujiengua CCM na kujiunga na Chama cha Jamii CCJ. Hivyo kutokana na maamuzi hayo chama hicho kipya cha jaamii kilichotangaza awali kuwa kuna vigogo wa CCM watakifata chama hicho hivyo imethibitisha kauli hiyo baada ya mbunge huyo kuwa wa kwanza kujiengua na CCM na kujiunga huko.Alisema amejiengua na CCM ili kuweza kutetea maslahi ya wananchi wanyonge ambapo ameona ndani ya CCM jambo ambalo halitaweza kutekelezwa kwa kuwa kila mtu anatetea masilahi yake binafsi na si kutazama wananchi wapiga kura.Alifafanua kuwa serikali inayoundwa na CCM inayumba kwa kushindwa kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo la Richmond ambalo lilihusisha serikali kuipa zabuni ya kufua umeme wa dharura kampuni hiyo bila kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma, kashfa ya mgodi wa Kiwira kuuzwa kwa bei nafuu na mkataba wa uendeshaji wa Shirika la Reli (TRL) ambao umezorotesha kabisa huduma za reli ya kati. Hivyo kwa kujiunga kwake ataweza kurekebisha mambo hayo kwa kujiunga na chama hicho.Alisema CCM imetekwa na wafanyabishara wanaojikita katika kuwania nyadhifa mbalimbali kwa lengo la kuficha maovu yao badala ya kuwatetea wananchi"Nimeishi kwa matumaini ndani ya CCM kwa muda mrefu na sasa natangaza wazi kuwa nakihama chama hicho na kuhamia chama mbadala ambacho ni CCJ," alisema Mpendazoe Monday, March 29, 2010
Mzee wa miaka 96 aoa binti wa miaka 30
kibabu cha umri wa miaka 96 wa nchini Taiwan kimekuwa gumzo nchini humo baada ya kufunga ndoa na mwanamke aliyemzidi miaka 66. Babu Lin Chung ameweka rekodi ya kuwa bwana harusi mwenye umri mkubwa kuliko wote nchini Taiwan baada ya kufunga ndoa na mwanamke mwenye umri wa miaka 30.Chung amekuwa gumzo kwenye kitongoji cha Tainan baada ya kumuoa mwanamke huyo anayetoka maeneo ya ukanda wa kati nchini China katika jimbo la Hunan.Chung ambaye hakuwahi kuoa katika ujana wake, ana watoto wawili aliojitolea kuwalea tangia walipokuwa wadogo ambao hivi sasa mmoja kati ya watoto hao ana umri wa miaka 68.Chung anadai kwamba miaka mitatu iliyopita, alipewa maelezo na Mungu aende kwenye jimbo la Hunan nchini China ili kumtafuta mwanamke anayekuja kuwa mke wake.Chung alifunga ndoa na mwanamke huyo hivi karibuni pamoja na upinzani mkali toka kwa mwanae huyo wa kujitolea ambaye alikuwa akimuona babu huyo kama amelaghaiwa."Inanibidi niwe na mwenza katika uzee wangu... sikuwahi kuwa na mke, kwanini hivi sasa hataki mimi nioe", alisema Mzee Chung.
Balaa lingine Mara!
AJUZA mwenye miaka kati ya 90-100 Sifia Makubo amenyofolewa miguu yake yote miwili kwa panga na sasa yupo hospitali akiwa mahtuti. Ajuza huyo alikumbwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki nyumbani kwake Ngerengere kata ya Sirari tarafa ya Inchugu wilayani Tarime Mkoani Mara. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya Costantine Massawe alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 27 mwaka huu na ajuza huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya Tarime. Imedaiwa kwamba ukatili huo amefanyiwa na Mkazi wa kijiji cha Kubiterere ambaye hakufahamika jina lake mara moja. Kamanda Massawe akielezea mkasa huo zaidi alisema mtuhumiwa huyo akiwa na panga alivamia nyumba ya bibi Huyo na kuanza Kumshambulia kwa Kumkata kata mapanga na kumwacha akivuja damu nyingi huku akilia kuomba msaada , Kamanda Massawe alisema kuwa Mjukuu wa Bibi huyo alisikia kilio cha bibi yake kuomba msaada na kuanza kupiga yowe ambapo wananchi Majirani walijitokeza mara moja na kumfukuza hadi walipomtia mikononi na kuanza kumpiga. Mtuhumiwa huyo alikatwa panga tumboni hadi utumbo wote kutoka nje. Polisi Kituo cha Sirari walifika waliwahi kufika kwenye kituo kumuokoa mtuhumiwa kwa kumfikisha hospitalini na ajuza huyo. Mtuhumiwa alifariki siku hiyo hiyo na ajuza huyo bado amelazwa Wodi namba 6 kwa matibabu ya miguu yake yote Miwili na majeraha ya mkono wa kushoto.
Subscribe to:
Posts (Atom)
VJN Super Motors
Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote



