Mwanamme mmoja huko Afrika ya kusini kafunga ndoa na wanawake 4 kwa wakati mmoja . Mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Milton Mbhele mwenye umri wa miaka 44 aliingia kwa mbwembwe sehemu ya sherehe hizo huku akitumia usafiri wa gari ya kifahari aina ya limousine na kuwavisha pete na kuwabusu wake zake wote kwa zamu. Bwana harusi alisema harusi hii ya mara moja imemsaidia sana kubana matumizi kuliko angefunga harusi 4 tofauti. Serikali ya Afrika ya Kusini inatambua harusi za namna hii na imekuwa jambo la kawaida kwa watu wa jamii ya Wazulu alikotokea Raisi wa nchi hiyo Jacob Zuma ambaye nae ana wake 3.
