Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, September 30, 2009

Mambo usiyoyajua Kuhusu Jose Chameleon

Jina halisi : Joseph Mayanja
Kazi : Mwanamuziki
Mke : Danniella Atim

Chameleon ni mmoja wa wanamuziki maarufu na waliotokea kutamba na kupendwa katika ulimwengu wa Muziki kwenye nchi za Afrika mashariki, pia ameonyesha kipaji cha kuimba nyimbo kwa kutumia lugha za nchi mbalimbali ikiwemo nje ya Afrika Mashariki na hii imeonekana pale alipotoa singo yake ya Maokao & Maoko aliyoiimba ya lugha ya kizimbabwe. Binafsi anazungumza kuwa muziki ni vile wewe unavyoupenda na kuukubali haijalishi hata kama huelewi maana halisi ya nyimbo ( nafikiri anamaanisha midundo)




Chameleon akiwa na Asali wa Moyo wake Danniella Atim siku ya harusi yao.Inasemekana siku ya Harusi Chameleon aliwasili kanisani akitumia usafiri wa ndege ndogo huku bibi harusi Danniella akiwa na msafara wa magari 7 aina ya Benz. Harusi yao ilifanyika Kampala Serena Hotel na inakadiriwa kuwa moja ya harusi maarufu zilizowahi kufanyika nchini Uganda. Nyepesi nyepesi zetu zimetujulisha kuwa watu walikunywa, walikula na kusaza na inakadiriwa kulikuwa na Krate za bia zaidi ya 500 bila kuhesabu vinywaji laini, mivinyo na pombe kali.



Baadhi ya picha zinachomuonyesha Chameleoan akiwa Kitandani baada ya kupata ajali mbaya ya gari 2008.



No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote