Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Saturday, January 2, 2010

Ajali ya gari yaua Dar na kujeruhi Tisa

Mfululizo wa matukio ya ajali yanayogharimu maisha ya watu na kujeruhi kadhaa hasa kipindi cha mwisho wa mwaka, umeendelea kuliandama Jiji la Dar es Salaam ambapo jana huko Mbagala, mtu mmoja amefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa vibaya baada gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Lwambano Masino amesema, tukio hilo lilitokea mishale ya saa 11:00 jioni huko Mbande Mzambarauni, Mbagala Charambe. Kamanda amesema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 713 ATB aina ya Fuso, lililokuwa likiendeshwa na Mohamed Haji, 27, mkazi wa Magomeni kutokea Mbagala kuelekea Mbande. Kaimu Kamanda Masino amesema dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu gari lake na hivyo kuacha njia na kisha kupinduka. Amemtaja mtu aliyefariki katika tukio hilo kuwa ni Omari Mandunguru, 27, mkazi wa Chamazi. Amesema majeruhi wawili kati ya tisa waliojeruhiwa, walitibiwa katika hospitali ya Temeke na kuruhusiwa ambapo wengine saba wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Amewataja waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Abdul Noli, 17, Sultan Rajab, 17, Musa Yusuph, 15, MohamedYusuph, 16, Bakari Said, 17, Omari Juma, 14 na Miki Evenus, 20. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote