Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Saturday, January 2, 2010

Simba wa Vita kuzikwa leo

MAZISHI ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo kuanzia majira ya saa 7 za alasiri huko nyumbani kwake Madala Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Marehemu Kawawa alifariki juzi, majira ya saa 3:20 za asubuhi, katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako juzi alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia afya yake.Akiongea na waandishi wa habari kwa huzuni Ikulu, Raisi Kikwete alisema Mzee Kawawa alifika hospitalini hapo juzi kwa ajili ya kwenda kupima malaria kwa kuwa alikuwa na safari na alienda hapo ili aweze kujitambua kama angekuwa na malaria ajitibie kabla ya kwenda safari yake hiyo.Alisema alipofika hospitalini hapo alipima malaria na kukutwa kuwa hakuwa nayo, na alianza safari ya kurudi nyumbani kwake, kabla hajafika nyumbani kwake hali ilibadilika na waliongozana nae walimrudisha hospitalini hapo na jopo la madaktari walianza kumpima kutambua alikuwa akisumbuliwa na nini.Katika vipimo vya haraka haraka madaktari hao waligundua kuwa sukari yake ilikuwa imeshuka sana na kufikia 0.6 hali ambayo iliwafanya madaktari wafanye jitihada kubwa kumshughulikia kurudisha hali yake ikae sawa.Mbali na kumshughulikia sukari, pia waliweza kugundua kuwa figo zote mbili zilikuwa hazifanyi kazi na pamoja na jitihada zote mwenyezi mungu alichukua uamuzi wa kumchukua majira hayo.Kufuatia kifo hicho Kikwete amesema wamempoteza kiongozi shupavu aliyepigania uhuru wetu wa Tanganyika enzi za mwalimu na kusema alikuwa ni kiongozi mshauri wa karibu katika kuweka hali ya nchi sawa na walikuwa wakimtegemea kwa ushauri wa hapa na pale enzi za uhai wake.Marehemu aliweza kushika nyadhifa nyingi enzi za uhai wake kama vile Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri Mkuu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na vyeo vingine kadhaa.Marehemu Kawawa alizaliwa mkoani Ruvuma Wilaya na Namtumbo, Februari 27, mwaka 1926. Alifariki jana akiwa na umri wa miaka 83.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote