
Ndoa ya miaka 20 ilikuwa ni chungu sana kuvunjika kiasi cha kwamba Lee na Jan Jones waliamua kurudiana na kufunga harusi kwa mara nyingine ikiwa ni wiki chache tu baada ya kupeana talaka kila mtu aanze maisha yake kivyake.Kwa mujibu wa gazeti la Dail Mail, Lee na Jan walikuwa wakikutana wakati wa taratibu za kuivunja ndoa yao mahakamani lakini ghafla walifikiria kuwa wamefanya uamuzi mbaya sana na kuamua kufunga ndoa tena.Wanandoa hao ambao wana umri wa kwenye miaka ya 40 na ushee wamezaa watoto 10 pamoja.Walioana kwa mara ya kwanza mwaka 1990 na walifunga ndoa tena kwa mara ya pili siku ya mkesha wa krismasi.Watoto wao ambao waliwaona wazazi wao ni wapumbavu kwa kuachana kwao ndio waliokuwa wapambe wakati wa harusi hiyo ya pili."Tulijiona tumefanya makosa kuachana", alisema bi Jones.Wanandoa hao walikuwa wakiwasiliana kwa kutumia ujumbe wa simu wakati taratibu za kuivunja ndoa yao ya mwanzo zikiendelea.Bwana Jones alilalamikia matatizo mbali mbali kwenye familia ndiyo yaliyopelekea ndoa yao ya mwanzo ivunjike.
No comments:
Post a Comment