Kuna habari za kuaminika kuwa kuna Hiace lenye no ya usajili T615 AJW lililokuwa linatokea Ubungo kwenda Mlandizi imegongwa uso kwa uso na Lori la mafuta aina ya Scania lenye no za usajili T192ABP iliyoandika kwa nyuma maandishi yanayosomeka (Yarabi salama)majira ya saa 1 asubuhi ya leo eneo la Kibamba - Morogoro Rd, Dar es Salaam. Ni ajali mbaya na ya kutisha , mmoja wa mashuhuda kashuhudia maiti zisizopungua saba kwenye Hiace na kaongeza kwa kasema kuwa "Scania imeilalia hiace kabisa yaani scania iko juu hiace iko chini hata kuokoa haiwezekani..na sidhani kama kuna mtu atakuwa amepona ila kwenye scania dereva na konda anaweza akawa amepona..sikuwa na kamera ningeweka kupiga picha, Zimamoto wameelekea eneo la tukio . Taarifa zaidi na za kuaminika tutawaletea baadae . Mungu atupe subira na Uvumilivu
Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Thursday, March 25, 2010
Mtoto mwenye jumla ya vidole 31 afanyiwa Operation


Mtoto mmoja wa Kiume nchini China ambaye amezaliwa akiwa na jumla ya Vidole 31 amefanyiwa operation wa kutolewa vidole vya ziada , Inasemekana kuwa operation hiyo iliyodumu kwa masaa 6 1/2 ilifanyika katika Hospitali ya Shengjing huko Shenyang China, katika Operation hiyo Madaktari walifanikiwa kutoa vidole 11 vya ziada ambavyo baadhi ya vidole vya mikono vilikuwa vimeungana .Kutokana na maelezo ya mama wa mtoto huyo , mwanawe alipachikwa jina la "Monster" na watoto wenzake darasani (chekechea) na inasemekana kuwa akawa mtu wa kwanza kuwa na Vidole vingi duniani kwa madai ya Gazeti la Daily Mail. Moja ya mguu wake ulikuwa na vidole 7 na mwingine 8, mkono mmoja ulikuwa na vidole 3 vilivyoungana na mwingine ukiwa na 4 vilivyoungana pia.23 Wanusurika kwenye ajali ya basi la HEKIMA
WATU 23 wamenusurika kupoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika kijiji cha Tanangozi, mkoani Iringa. Ajali hiyo ilitokea jana saa tano asubuhi, baada ya basi la Hekima kulipita gari ndogo lililokuwa limebeba pombe ya kienyeji aina ya ulanzi kisha kuserereka na kupinduka. Basi hilo lililokuwa na abiria zaidi 70 lilikuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam. Akizungunza na vyombo vya habari kwa njia ya simu, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk George Kabona alisema kati ya majeruhi hao, 13 ni wanaume na kumi ni wanawake na kwamba hali ya majeruhi mmoja ikiwa ni mbaya. "Majira ya saa 6 mchana leo (jana), tulipokea majeruhi 23 kutoka katika ajali ya basi iliyotokea katika kijiji cha Tanangozi. Kati ya hao 13 ni wanaume na kumi ni wanawake na hali zao zinaendelea vizuri, lakini mmoja kati yao hali yake ni mbaya na amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi," alisema Dk Kabona. Dk Kabona alisema kuwa kwa mujibu wa majeruhi hao, ajali hiyo ilitokea kutokana na barabara katika eneo hilo kuwa na utelezi uliosababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa na mikoa mingine katika Nyanda za Juu Kusini. Alisema kwamba baada ya basi kulipita gari dogo lililokuwa limebeba pombe aina ya ulanzi na dereva kutaka kurudi katika njia yake ndipo liliposerereka na kupinduka. Mmoja wa majeruhi hao alipouliza alisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya basi (Hekima) kulipita gari dogo lililokuwa limebeba pombe ya ulanzi na kuserereka kutokana na barabara kuwa na utelezi uliosababishwa na mvua," alibinisha Dk Kabona.
Mvua Kubwa yatishia Mwanza
MVUA kubwa iliyonyesha jana alfajiri jijini hapa kwa saa mbili imezikosesha makazi zaidi ya kaya 24 za mtaa wa Mabatini Kusini na 10 za Mabatini Kaskazini. wakazi wa kaya hizo walionekana katika harakati za kukusanya vyombo na mali zao zingine zikiwa zimelowa maji na baadhi ya nyumba zikiwa zimebomoka. Akizungumza katika mtaa wa Mabatini Kusini, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Yohana Nono, alisema msaada wa haraka wa mahema, vyakula na nguo unahitajika kuwasitiri baadhi ya wananchi ambao vitu vyao vilisombwa na mafuriko ya maji. “Baada ya kufanya tathmini na wananchi wa mtaa wangu, tumebaini kuna jumla ya watu 100 wa kaya 24 ambao nyumba zao zimebomolewa na mafuriko, “ alisema Nono na kuongeza kuwa wanafanya juhudi ya kuwasiliana na uongozi wa wilaya ili kuona uwezekano wa kuwasaidia wananchi hao. Kati ya watu walioathiriwa na mafuriko hayo ni pamoja na Stella Robert (6), ambaye kwa mujibu wa mjumbe wa nyumba 10 shina la Mabatini Kusini mtaa wa Benjamin, Anthony Msafiri, alishtuka saa 10.45 alfajiri na kusikia kelele za watu wakiomba msaada. “Kwanza nilifikiri tumevamiwa na majambazi, maana nilikuwa usingizini, lakini baada ya kuamka nilishuhudia nyumba zote zimejaa maji huku vitu vikielea, nilimkuta Mama Nyanjige - mama mzazi wa Stella aliyesombwa maji, akilia akiniomba kumwokoa Stella,” alisema Msafiri. “Nilichukua tochi na kufuatilia mkondo wa maji, nikawatoa baadhi ya watoto walionasa kwenye baadhi ya nyumba na kuelekea kambi ya Polisi Mabatini, ambako tulikutana na maaskari na tulipowauliza, wakasema Stella aliokolewa na mwanamke. “Alikuwa akielea huku akipiga kelele za kuomba msaada kwa maaskari hao, ndipo walipochungulia dirishani wakamwona na kuokolewa na mke wa askari,” alisema na kuongeza kuwa walimpeleka kituo cha afya na hatimaye hospitali ya mkoa ya Sekou Toure alikolazwa. Wakizungumza kwa uchungu mbele ya wananchi waliofurika eneo hilo, waathirika Issa Mauba, Tatu Ally na Hassan Babu, walidai kuwa chanzo cha mafuriko ya mara kwa mara Mabatini ni ujenzi usiozingatia mipango. Hii ni mara ya pili katika kipindi kifupi, Jiji la Mwanza kukumbwa na mafuriko huku ya hivi karibuni yakisababisha watu sita kupoteza maisha na zaidi ya 200 makazi. Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, alisema tayari timu ya wataalamu imefika mitaa hiyo ya mafuriko ingawa hakukuwa na athari za kutisha. “Timu yangu ya wataalamu imefika maeneo yaliyopata mafuriko na tutatoa taarifa baadaye na tuone nini cha kufanya juu ya waathiriwa wa mafuriko, baada ya mvua ya jana,” alisema Kabwe.
Mwanamke aenda jela Miaka 7 kwa kufanya mapenzi na mtoto wa Miaka 15 Moshi
MWANAMKE ambaye ni mke wa mtu mwenye watoto watatu, amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 15. Mwanamke huyo, Sophia Philemon (44) mkazi wa kambi namba tisa katika kiwanda cha sukari cha TPC, wilaya ya Moshi vijijini kuhukumiwa kifungo hicho, pia ameamriwa kumlipa mwanafunzi huyo fidia ya Sh1 milioni. Hukumu hiyo, ilitolewa jana mjini Moshi na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro, John Nkwabi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka. Nkwabi alisema ushahidi wa mashahidi hao, akiwemo mwanafunzi huyo wa sekondari ya Langasani, umeithibitishia mahakama kwamba mwanamke huyo, alimlazimisha mtoto huyo kufanya naye tendo la ndoa. Kitendo hicho ni kosa chini ya kifungu namba 138B (1) (d) cha kanuni ya adhabu kinachosimamia makosa ya kimapenzi kwa watoto baada ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho mwaka 2002. Hakimu Nkwabi alisema mahakama imeridhika na ushahidi kuwa Februari 28, mwaka jana, saa 1:00 usiku huko kambi namba tisa, mshitakiwa alimlazimisha mwanafunzi huyo kufanya naye mapenzi katika chumba anachoishi na mumewe. Muda huo, mwanafunzi huyo alikuwa ametoka dukani alikokuwa ametumwa na wazazi wake na mwanamke huyo, alimwita na kumshawishi aingie ndani ya nyumba yake na baadaye kumlazimisha kufanya naye tendo la ndoa. Baada ya kutiwa hatiani, wakili wa serikali, Hellen Moshi aliyeendesha kesi hiyo, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwani vitendo vya ubakaji vinazidi kuongezeka nchini hususani kwa watoto wadogo na wanafunzi. Katika utetezi wake, Sophia alisema ni mke wa mtu na hakubahatika kupata mtoto na mwanaume huyo, lakini kabla kuolewa alikuwa tayari amezaa watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume. Mshitakiwa alikataa kufanya tendo la ndoa na mtoto huyo, licha ya kumfahamu kuwa ni jirani yake. Utetezi wake ulitupiliwa mbali na mahakama hiyo.
Mshindi wa Miss Universe 2009 alamba BINGO
MREMBO wa Tanzania, Miss Universe Tanzania 2009, Illuminata James, amepata fursa ya masomo scholarship nchini Marekani kutoka kwa Kampuni ya New York Film Academy. Mbali na kutoa nafasi hiyo ya masomo, pia kampuni hiyo imejitolea kudhamini mashindano hayo mwaka huu na kuahidi pia kutoa fursa ya masomo kwa mshindi atakayemrithi Illuminata. Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communication, ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo taifa, Maria Sarungi, aliwaambia waandishi wa habari jana wameamua kuboresha mashindano hayo zaidi ikiwa ni sambamba na kutafuta udhamini wa nje ya nchi ili kuongeza chachu ya mashindano. Alisema kuwa hiyo itakuwa ni nafasi ya pekee kwa warembo wa Tanzania kujitokeza ili kuwania nafasi hiyo nyeti na nyingine nyingi ambazo wadhamini wa hapa nchini watatoa. "Tunatarajia kufanya usaili wa warembo hao katika mikoa mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha ili kupata warembo 20 ambao wataingia kambini kwa ajili ya kuchuana hadi kumpata mshindi. "Katika usaili huo tutaangalia zaidi vigezo ili kumpata mrembo bomba ambaye atatuwakilisha vema kimataifa na hatimaye kuibuka na ushindi" alisema Sarungi. Wadhamini wengine kwenye mashindano hayo ni Kampuni ya Precision Air, Serengeti Breweries, PSI, Movenpick Hotel, Hugo Domingo, Choice FM, Prime Time Promotions pamoja na Midland Hotel.Wednesday, March 24, 2010
Mapenzi yampeleka Kaburini yeye na mtoto wake
Katika hali ya kusikitisha, mwanaume aliyetambuliwa kuwa ni Mwidadi Hamisi,(32) mkazi wa Bombambili mjini Songea, mkoani Ruvuma, amemnyonga mtoto wake wa umri wa miaka minne na baadaye naye kujinyonga huku akiwa ameacha ujumbe kuwa uamuzi huo umetikana na shida alizokuwa akipata kutoka kwa mke wake wa zamani.Tukio hilo lilisikitisha wengi hasa kwa kitendo cha kumnyonga mtoto Mulla, ambaye hakuwa na hatia, lilitokea saa 5:00 asubuhi wiki iliyopita katika maeneo ya Mlima wa Chandamali,nje kidogo wa mji wa Songea.Kabla ya kuamua kujinyonga, marehemu ambaye wakati wa uhai wake alikuwa mwendesha pikipiki zinazosafirisha watu,alimpiga simu kwa tajiri wake akimtaka afuate pikipiki yake katika maeneo ya mlimani huo.Habari zilisema katika simu hiyo marehemu alimwambia tajiri yake kuwa yeye ameamua kwenda kupumzika kaburini na mtoto wake, ili kuepuka shida alizokuwa akizipata kutoka kwa mke wake wa zamani.Kabla ya kujinyonga, Mwadadi, aliacha ujumbe huku akiambatanisha na orodha ya namba za simu za ndugu zake na kutaja sehemu anakotoka kuwa Newala mjini mkoani Mtwara.Katika ujumbe huo, marehemu alisema ameamua kujinyonga yeye na mtoto wake kufuatia kashfa alizokuwa akizipata kutoka kwa mama watoto wake.Katika ujumbe huyo marehemu alimtuhumu mama huyo kuwa amekuwa akimweleza mpenzi wake, siri za maungoni mwake.Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio tajiri wa marehemu huyo,Hussein Msafiri, alisema siku kadhaa zilizopita, marehemu aliwahi kumweleza matatizo yake yeye na mke wa zamani."Mara nyingi alionekana mtu ambaye hana amani moyoni mwake," alisema
Nafasi ya Kazi
The EC Delegation in Tanzania wanahitaji mfanyakazi wa muda kwa nafasi ya Receptionist / Telephone Operator, ili kuziba nafasi ya mtu anayeenda kwenye Likizo ya Uzazi kuanzia 15 April hadi 30 July 2010. Maombi yote yatumwe kwa :Ms May Kazuka Admin Assistant / Personnel EC Delegation Tanzania Umoja House, Garden Avenue Dar es Salaam Simu: +255 22 2117473-6 Fax:+255 22 2113277 Email: May.KAZUKA@ec.europa.eu
Subscribe to:
Posts (Atom)
VJN Super Motors
Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote






