Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, October 6, 2009

Je unataka kuwa Richard au Kanumba wa Bongo?????? Kazi kwenu

Mchakato wa kutafuta na kuibuwa vipaji vya waigizaji chipukizi unaojulikana kama IBUA Film Star Tanzania utaanza rasmi tarehe 30 -10- 2009 na litahusisha mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam. Mchakato huu wa aina yake ambao utawahusisha watu wote wasiowahi kushiriki katika uigizaji filamu au tamthilia yoyote utaangalia vigezo vifuatavyo:-

1) awe Mtanzaniawatanzania
2) umri wa miaka 16 na kuendelea
3)awe na akili timamu
4) ajue kusoma na kuandika
Usaili utaanza kwa mikoa husika ambapo 10 bora wa kila mkoa ataingia kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta msanii chipukizi wa filamu Tanzania. Mwaka huu kampuni mbali mbali yameonyesha nia ya kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa hapo baadaye Mshindi wa IBUA Film Star Tanzania atajinyakulia zawadi ambayo itatangazwa baadae na pia atapata mkataba wa kushiriki filamu mbali mbali za wasanii wa ndani na nje ya nchi. Mshindi wa shindano hili atapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kupitia kipindi maalumu kitakachoonyeshwa hapo baadae kama ilivyo kwa Big Brother au Bongo Star Search.
Fomu za kushiriki shindano la IBUA Film Stars Tanzania zinapatikana mikoa husika kama ifuatavyo Arusha (Club Silk), Mwanza (Salma Cone), Mbeya (CPMTL Stationery mkabala na ofisi ya mkuu wa mkoa), Dodoma (Zunny Ice Cream Parlour), Zanzibar (Ofisi za Zenj FM), Dar es Salaam (TCC Chang’ombe, Shear Illusions mlimani City, Royal Salon Sinza, Zizzou Fashions). Fomu zitaanza kupatikana tarehe 10 Oktoba 2009. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30 Oktoba 2009 .

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote