Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, October 5, 2009

Rais Kikwete aelemewa na Uchovu

Picha ikimuonyesha Rais Kikwete akiwa ofisini siku ya kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa 4 wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 16 Jan 2006

Rais wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete jana amelazimika kukatiza hotuba yake ghafla akionekana mchovu, na kuomba kuhutubia akiwa amekaa, jambo ambalo hata hivyo alilikatiza na baadaye kuondolewa kwenye jukwaa katika uwanja CCM kirumba mjini Mwanza na kwenda chumba maalum kwa ajili ya mapumziko mafupi. Hali hiyo imetokea wakati Rais Kikwete akihutubia maelfu ya waumini wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania katika madhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kanisa hilo nchini. Rais Kikwete alikatisha hotuba yake baada ya kutojisikia vizuri huku sauti yake ikisikika kudhoofu kama mtu ambaye amepatwa na matatizo. Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu DAR ES SALAAM kwa vyombo vya habari imesema Rais Kikwete alilazimika kupumzika kutokana na kuzidiwa na uchovu kufuatia shughuli nyingi mfululizo katika siku za karibuni. Hata hivyo baada ya mapumziko ya muda aliendelea kushiriki katika shughuli hizo hadi mwisho.
“Nguvu imerudi…napenda sasa kuchukua nafasi hii kuzindua rasmi uchangiaji wa shughuli za Kanisa lenu na mimi naanza na mchango wa sh. 1,000,000,” Rais Kikwete aliwaambia maelfu ya waumini wa AICT huku wakimshangilia kwa nguvu mara aliporejea jukwaani. Pia Rais alisema “Kwa kweli mshituko huu wa leo ni matokeo ya ubishi wangu. Nilishauriwa na wasaidizi wangu nipumzike baada ya kurejea nyumbani kutoka Marekani. Niliambiwa nisiende Arusha ama kuja hapa. Lakini nikakataa. Siku nyingine nitawasiliza zaidi.”

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote