Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, October 1, 2009

Mjue Pipi kutoka THT(Tanzania House of Talent)


Safari yake ya Muziki
Pipi alianza Muziki kwenye miaka ya mwaka 2004 akiwa anasoma
kidato cha kwanza, na mgunduzi wa kipaji chake ni mama yake
mzazi aliyekuwa akimpata moyo baada ya kumsikia akiimba nyimbo
mbalimbali za wanamuziki wa nje kama Celion Dion na Kelly Clerkosn.

Album
Kuhusu Album binafsi hadi sasa Pipi hajafanikiwa kutoa ila binafsi
anasema hilo wazo lipo na muda ukifika ataingia uwanjani.

Anaongeleaje kuhusu Muziki wa Tanzania
Kwa sasa muziki wa Kitanzania unapanda chati kwa sana
ila haulipi sana, anadai Promota wanabana ila ana imani ipo
siku wataachia

Wanamuziki anaowapenda
Kwa Tanzania anamzimia sana Nakaaya na Barnaba na kwa
nje ya nchi Alicia Keys na Lil Wayne.

Shughuli nje ya Muziki
Anasoma Chuo

Mahusiano
Kwa sasa hana
Pipi anawashukuru washabiki wake wote kwa kumpokea kwa mikono miwili anasema hakutegemea kama ingejulikana hivi amekubalika na kupendwa sana ingawa wimbo haukuwa wake alishirikishwa tu na Barnaba , Pia aliwaasa wasanii chipukizi wawe macho na mafataki kwani wakishajuwa unajina watakufuatia sana . Pipi katoa shukrani za pekee kwa Mungu kwa kila kitu, mashabiki wake wote, THT bila kumsahau mama yake kipenzi na familia yake kwa kuwa nae wakati wote.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote