Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, March 9, 2010

Amuua Mkewe kwa kumchinjwa

Philippe Cousin mwenye umri wa miaka 53 alimchinja mkewe wa ndoa ya miaka 21 Nicole Cousin mwenye umri wa miaka 47 baada ya Nicole kuendelea kukataa kufanya naye mapenzi kwa kuhofia kupata watoto.Nicole alikutwa amefariki kwenye nyumba yao katika mji wa Calais kaskazini mwa Ufaransa.Philippe aliwaambia polisi kuwa mkewe alikataa kufanya naye mapenzi kwa kipindi chote cha ndoa yao akisema kuwa anahofia watoto watakaozaliwa watarithi ugonjwa sugu wa multiple sclerosis (ugonjwa unaosababisha madhara kwenye ubongo na uti wa mgongo) ambao umekua ukimsumbua baba yake Nicole.Uchunguzi wa maiti ya Nicole ulithibitisha kuwa hadi wakati anafariki Nicole alikuwa kweli ni bikira ingawa alikuwa kwenye ndoa kwa miaka 21.Siku ya tukio hilo ugomvi ulizuka kati ya Philippe na mkewe ambapo Philippe alichukua kisu na kumwekea mkewe shingoni kabla ya kukikata na kukinyofoa kabisa kichwa chake.Baada ya tukio hilo Philippe aliwapigia simu polisi na kuwaambia "Samahani kwa kuwasumbua, nimemuua mke wangu".Phillippe alipandishwa kizimbani jana kwa mauaji hayo aliyoyafanya mwezi aprili mwaka juzi.Wakili wa Philippe alisema kuwa Philippe alifanya mauaji hayo kutokana na kuchanganyikiwa kimawazo kwa kushindwa kuwa baba.Philippe ambaye hivi sasa anapatiwa matibabu ya kisaikolojia ndani ya jela huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote