
MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema ametangaza kumfikisha Spika wa Bunge, Samuel Sitta, mahakamani kwa kuwa amemdhalilisha. Mrema alidai Sitta anamdhalisha kwa kumwambia amechanganyikiwa akili na amefilisika na kumtaka athibitishe kauli hizo kinyume na hapo atamfikisha mahakamani.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mrema alisema Spika ametumia lugha za matusi na kumdhalilisha kupitia vyombo vya habari kuwa amefilisika kisiasa na kifedha ndio maana anakifanyia kampeni Chama Cha Mapinduzi (CCM).Mrema alisema, suala la kufilisika halina ukweli kwa sababu anamiliki zaidi ya shilingi milioni 37 kiasi alichoeleza kuwa ni kikubwa kuliko anachomiliki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.“Mimi sijafulia wala kufilisika kisiasa… kwenye akaunti yangu ya NMB nina sh 37,751,451.79 ” alisema Mrema na kusisitiza nimemzidi hata Waziri Mkuu Na kuongeza kuwa yuko timamu kiakili, anao uwezo wa kuwasomesha watoto wake bila kuhitaji msaada wowote na kwamba amejipanga vema kunyakua ubunge wa Vunjo, hivyo kauli za Spika huyo aliyedai kukosa sifa za uongozi ni kumchafulia na kumdhalilisha.Mrema alisema ameshangazwa na Spika kwa kushindwa kumuelewa kwa kuwa yeye alimuonya kuachana na makundi ndani ya CCM huku akimkaribisha kujiunga na wapinzani endapo hakubaliani na viongozi wa chama chake.Alisema kuwa Ibara ya 5(d) ya kanuni ya maadili ya vyama vya siasa inasema wajibu wa vyama vya siasa ni kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni ya uongo kuhusu mtu yeyote au chama cha siasa chochote.Hivyo kutokana na Spika na pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM kwa makusudi amekiuka kanuni za maadili ya vyama vya siasa nchini.Awali spika Sitta alimtupia Mrema tuhuma za kuhongwa na CCM. Alisema CCM ina uwezo wa kushinda bila kupigiwa debe na Mrema huku akitolea mfano mwaka 1995; mwaka 2000 na 2005 kushindwa katika chaguzi mbalimbali bila ya kupigiwa debe na yeye.
No comments:
Post a Comment