Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, March 9, 2010

Soko La Feri Kujengwa tena!

Wakati tathmini halisi ikilendelea kufanyika juu ya mali na vifaa vilivyoungua moto katika soko kuu la kuuzia samaki Feri Dar es Salaam, halmashauri ya Manispaa ya jiji inaandaa sehemu mbadala ya kuwapa Wafanyabiashara wa samaki. Akielezea suala hilo , Naibu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Lawrence Malangwa amesema halmashauri inaandaa mara moja eneo la dharura kuwawezesha wakaanga samaki kuendelea na kazi wakati mkakati wa kuliimarisha soko hilo ukiendelea. Amesema uchunguzi bado unaendelea kufanyika juu ya chanzo cha moto huo katika wakati ambao pia tathmini inaendelea kufanyika kujua ni hasara kiasi gani iliyoitokea mahali hapo. Soko kuu la Samaki Feri liliwaka moto na kuunguza sehemu kubwa ya eneo hilo huku chanzo cha moto huo kikiwa bado kiza kutokana na kutoeleweka ulikotokea

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote