Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, March 15, 2010

Rais Kikwete achangisha zaidi ya Milioni 700 Josiah Kibira


Kiongozi wa Kanisa la Kikristo la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dk. Alex Malasusa, ameusifia na kuupongeza uongozi wa Rais Jakaya Kikwete kwa dhamira, vitendo na mafanikio makubwa katika sekta ya elimu yaliyopatikana chini ya uongozi huo. “Tunaipongeza sana Serikali yako, Mheshimiwa Rais, inavyojali umuhimu wa Watanzania wengi zaidi kuzidi kupata elimu. Ni nia ya KKKT kuendelea kushirikiana na Serikali yako katika kuendelea kutoa huduma za elimu nchini,” Askofu Malasusa amemwambia Rais Kikwete. Askofu Malasusa alikuwa anazungumza kwenye chakula cha jioni cha kuchangisha fedha za kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Josiah Kibira mjini Bukoba, shughuli iliyofanyika Dar es Salaam, juzi. Rais Kikwete aliongoza uchangishaji fedha wakati wa chakula hicho na kiasi cha sh 706, 560, 000 zilichangwa kwa ajili ya uanzishaji wa chuo hicho kitachokuwa chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini kinachomilikiwa na KKKT. “Tunathamini sana mchango mkubwa wa KKKT katika utoaji wa huduma mbalimbali za jamii kwa wananchi, na hasa elimu.”Rais Kikwete pia alirudia ahadi ya Serikali yake kuwa itamwajiri kila mwalimu, na hasa walimu wa masomo ya sayansi, wanaohitimu elimu ya ualimu kutoka vyuo mbalimbali, ili kukabiliana na tatizo la walimu katika shule nchini, hasa za sekondari. “Sisi katika Serikali tutamwajiri kila mwalimu…yeyote atakayehitimu elimu ya ualimu anaweza kujihesabu kuwa tayari ameajiriwa. Hii ndiyo ahadi yetu. Ninayo ahadi na walimu katika kuwapatia ajira. Yeyote anayehitimu tutamchukua,”alisema Rais Kikwete. Rais Kikwete pia alilipongeza Kanisa hilo kwa kuamua kukipa chuo hicho kikuu jina la Josiah Kibira ambaye alikuwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kuongoza shirika la makanisa duniani la World Federation of Churches. Wakati wa mnada wa picha kwenye uchagishaji huo wa fedha za kujenga chuo hicho, picha ya Rais Kikwete ilinunuliwa kwa kiasi cha sh milioni 16.5, picha ya Askofu Kibira ilinunuliwa kwa sh milioni 6.3, picha ya Mwalimu Nyerere ilinunuliwa kwa sh mil. tatu.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote