Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, March 9, 2010

Bibi wa China Aota Mapembe

Bibi Zhang Ruifang (pichani) mwenye umri wa miaka 101 wa kijiji cha Linlou katika jimbo la Henan nchini China alianza kuota pembe moja kwenye kichwa chake mwaka jana.Hadi sasa pembe hilo lililoota kwenye upande wa kushoto wa paji lake la uso limekua na kufikia urefu wa sentimeta sita. Upande wa kulia wa paji lake la uso kuna pembe jingine ambalo ndio kwanza linaanza kujitokeza.Familia yake imepagawa na mapembe hayo na haijui kwanini yanajitokeza kwenye kichwa chake.Mtoto wa mwisho wa bibi huyo anayeitwa Zhang Guozheng mwenye umri wa miaka 60 alisema kuwa wakati mapembe hayo yalipoanza kujitokeza mwaka jana hawakujali sana walidhania ni makunjamano ya ngozi tu."Lakini siku zilivyozidi kwenda pembe lilijitokeza kwenye kichwa chake na sasa limefikia sentimita sita" alisema Zhang ambaye kaka yao wa kwanza ana umri wa miaka 82."Hivi sasa kuna kitu kinajitokeza kwenye upande wa kulia wa paji lake la uso bila shaka ni pembe jingine", aliendelea kusema Zhang.Madaktari walisema kuwa mapembe hayo yanaweza kuondolewa kwa operesheni lakini sababu ya kujitokeza kwa mapembe hayo bado haijulikani.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote