Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, March 9, 2010

Basi lawaka Moto 21 wanusurika

ABIRIA 21 waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Scandinavia kutokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya wamenusurika kufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuungua moto. Ajali hiyo imetokea eneo la Melela Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro katika barabara kuu ya Iringa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. Kamanda Polisi mkoani hapa Thobias Andengenye alisema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 4:30 asubuhi. Alisema ajali hiyo imehusisha basi lenye namba za usajili T 641 AGA lililokuwa likiendeshwa na John Steven. Hata hivyo Andengenye alisema ingawa hakuna kifo kilichotokea ipo hasara ya mizigo na abiria kupata majeraha madogo

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote