Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, March 12, 2010

Serikali ya Uholanzi yapitisha Sheria ya kujiua?


Serikali ya Uholanzi inategemea kupitisha sheria yenye utata itakayowaruhusu watu wenye umri kuanzia miaka 70 kujiua wenyewe kwa msaada wa madaktari iwapo watahisi kuwa wametosheka na maisha duniani. Watu wenye umri zaidi ya miaka 70 wataruhusiwa kujiua kwa kusaidiwa na madaktari iwapo wataona wameishatosheka na maisha yao hapa duniani. Watu ambao hawana ujuzi wa udaktari watapewa mafunzo jinsi ya kuwasaidia wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 kujiua kwa kutumia sindano za sumu hospitalini.Bunge la Uholanzi linatarajia kuujadili muswada wa sheria hiyo baada ya watu wanaoipigia kampeni sheria hiyo kukusanya sahihi za watu 112,500 wanaounga mkono sheria ya kuruhusu watu kujiua.Watetezi wa sheria hiyo wamesema kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo kutawawezesha wazee kuamua kufariki kimya kimya kwa utulivu pindi watakapoona wamechoka kuishi na wanataka kuepukana na pilikapilika za dunia.Wasaidizi wa madaktari watakaokuwa wakichanganya dawa ya sumu itakayotumika kuwaulia wazee watakaojitokeza.Hata hivyo mashirika ya kidini yameelezea kupinga kwake kuruhusu watu kujiua eti kwasaabu ya kuyachoka maisha.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote