Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, March 8, 2010

Mtoto mdogo kuliko wote azaliwa Germany

Mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wake ambaye alikuwa mwepesi sana kiasi cha kwamba kopo dogo la cocacola lilikuwa zito kulinganisha na uzito wake, amemaliza miezi minane akiwa hai pamoja na hofu ya madaktari kuwa asingeweza kuishi siku nyingi. Mtoto huyo alizaliwa nchini Ujerumani akiwa na umbile dogo sana na uzito wa gramu 275 tu kiasi cha kwamba aliingia kwenye rekodi za kuwa mtoto wa kiume aliyezaliwa akiwa na uzito mdogo kuliko wote.Kwa jinsi alivyokuwa na umbile dogo karatasi ya daftari yenye ukubwa wa A4 iliweza kumfunika kuanzia kichwani hadi miguuni.Uzito wake ulikuwa ni robo tatu ya uzito wa kopo la Cocacola ambalo huwa na uzito wa gramu 350.Awali madaktari walisema kuwa ni vigumu sana kwa mtoto anayezaliwa akiwa na uzito chini ya gramu 350 kuishi muda mrefu.Lakini mtoto huyu amefanikiwa kumaliza miezi kadhaa akiwa hai kutokana na matunzo ya kitaalamu aliyokuwa akipewa.Habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo hazikutangazwa kutokana na hali mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo wakati alipozaliwa.Madaktari wameamua kutoa taarifa za kuzaliwa kwa mtoto huyo baada ya kuthibisha sasa kuwa afya yake imekuwa njema na maisha yake hayako hatarini tena.Mtoto huyo alizaliwa mwezi juni mwaka jana wakati mimba ya mama yake ilipokuwa imetimiza wiki 25.Alitumia miezi sita akipewa huduma maalumu hospitalini kabla ya wazazi wake kuruhusiwa kuondoka naye mwezi disemba mwaka jana wakati uzito wake ulipoongezeka na kufikia kilo 3.7.Taarifa ilisema kuwa madaktari wa Ujerumani walizipitia rekodi za watoto wa kiume waliozaliwa kabla ya muda wao katika nchi mbali mbali duniani lakini hakupatikana mtoto hata mmoja aliyezaliwa akiwa na uzito mdogo kama wa mtoto huyo.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote