Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, March 15, 2010

Amuua Mpenzi wake baada ya kumfumania na wanaume wawili kitandani!

Mwanaume mmoja nchini mkazi wa Brooklyn nchini Marekani mwenye umri wa miaka 50 aliingia kwenye nyumba ya mpenzi wake na bila kutarajia alimkuta mpenzi wake akifanya mapenzi na wanaume wawili kwa wakati mmoja.Mwanaume huyo alimuachia ujumbe wa sauti rafiki yake kuwa amemuua mpenzi wake mwenye umri wa miaka 51 baada ya kumfumania akifanya mapenzi na wanaume wawili kwa mpigo.Polisi walipewa ujumbe huo wa sauti na kuwahi kwenye nyumba ya mwanamke huyo na kumkuta mwanaume huyo akiizunguka maiti ya mpenzi wake.Mwanaume huyo alikiri mbele ya polisi kuwa alishikwa na hasira sana baada ya kumfumania mpenzi wake akifanya mapenzi na wanaume wawili, alimuua mpenzi wake na wanaume hao wawili na kisha kuikatakata vipande vipande miili ya wanaume hao na kwenda kuitupa kwenye vichaka.Jirani mmoja wa mwanaume huyo alisema kuwa mwanaume huyo hakuonekana kutetereka wala kujutia mauaji aliyoyafanya, aliinamisha kichwa chake chini wakati alipokuwa akipandishwa kwenye karandinga la polisi, liliripoti gazeti la New York Post.Polisi wanaendelea kumshikilia mwanaume huyo na uchunguzi wa kesi yake unaendelea.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote