Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, March 8, 2010

Richa Adhia aula tena?

MISS Tanzania 2007, Richa Adhia kwa mara nyingine tena ataipeperusha bendera ya Tanzania katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia mwenye asili ya Asia 'Miss World 'itakayofanyika Machi 27 kwenye ukumbi wa International Convention Centre mjini Durban, Afrika Kusini. Shindano hilo ambalo ni la 19 kufanyika tangu kuanzishwa kwake, Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza ikiwa imedhaminiwa na Kampuni ya Samsung na kuzinduliwa usiku wa kuamkia jana kwenye ukumbi wa hoteli ya New Afrika, jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mratibu wa Miss India Tanzania, Sati Gadhvi alisema shindano hilo linatoa fursa kwa wanawake wa kitanzania wenye asili ya Kihindi kuweza kushindana kuonyesha urembo na vipaji vyao na mshindi ataiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Miss World India. "Mshindi wa Samsung Miss Tanzania India mbali na kuitangaza Tanzania kimataifa pia atajihusisha na shughuli za kijamii ikiwa na pamoja na kuchangisha fedha zitazotumika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya Kitanzania." alisema Sati Gadhvi "Kwa vile tumeanza mwaka huu tumeamua kumteua Richa akaiwakilishe Tanzania katika mashindano hayo, lakini kuanzia mwakani tutakuwa na mchakato wa kumsaka mrembo kuanzia ngazi ya chini mpaka taifa, kadri siku zitakavyoenda tutafanya kwa nchi nzima."

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote