Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, March 9, 2010

Hali ya Maalim Seif yaimarika


Hali ya Afya ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, aliyelazwa katika hospitali binafsi ya Hindu Mandal, jijini Dar es Salaam, kutokana na kupatwa na matatizo ya shinikizo la damu, imezidi kuimarika, ingawa amesema bado anasumbuliwa na kifua. Maalim Seif, ambaye aliugua ghafla wakati akijiandaa kupanda ndege kwenda Mascut, Oman, Ijumaa wiki iliyopita katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na kukatisha safari hiyo, alisema jana kuwa hali aliyonayo hivi sasa imeimarika na kuwa tofauti na ile aliyokuwa nayo wakati anapelekwa hospitalini hapo. “Nawashukuru sana madaktari. Tangu nifike hapa hali ya afya yangu imekuwa tofauti kabisa na ilivyokuwa kabla. Imedhibitiwa kwa muda mfupi kabisa,” alisema Maalim Seif alipozungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana. “Vipimo vyote nilivyofanyiwa, sasa pressure (shinikizo la damu) ni nzuri sana, moyo unafanya kazi vizuri na sukari ni ya kawaida,” aliongeza. Hata hivyo, alisema bado anasumbuliwa na kifua na kwamba, anahisi huenda tatizo hilo likawa ni ‘athma’, lakini akasema si kubwa na ana matumaini ya kuruhusiwa na daktari kati ya jana au leo. Aliwataka Watanzania waondoe wasiwasi juu ya afya yake na akawashukuru kwa kuonyesha kumjali hadi kufikia wengine kupatwa na mshituko baada ya kusikia taarifa za kuugua kwake. “Mungu awajaalie awape moyo wa kupendana. Sina cha kuwalipa, lakini Mungu atawalipa,” alisema Maalim Seif. Alisema anasubiri kupata ushauri wa madaktari kuhusu muda wa kupumzika baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali kabla ya kuendelea na shughuli zake. Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, jana alifika hospotalini kumjulia hali Maalim Seif na Rais Jakaya Kikwete alituma ujumbe wakati Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi kumpa pole. Taarifa za kiongozi huyo kuugua ghafla na kuazwa zilisababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi wa Zanzibar ambao walionekana wakiwa wamekaa katika vvikundi mitaani wakijadili kuhusiana na taarifa hizo. Daktari wake, Dk. Ramaiya Kaosheki, alisema uchunguzi wa mwisho utakaofanyika kabla ya kuruhusiwa kutoka wodini ndio utakaoamua kama aendelee na shughuli zake au apumzike.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote