Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, March 12, 2010

Kikwete aongoza mazishi ya Mke wa Balozi Daraja

RAIS Jakaya Kikwete jana aliongoza mamia ya waombolezaji wakiwemo wanadiplomasia, katika kuuaga mwili wa mke wa Balozi mstaafu aliyeuawa wiki iliyopita, kabla ya kuusafirisha kwenda Muheza, Tanga kwa maziko. Shughuli ya kuuaga mwili wa Anna Mbago (65), aliyekuwa mke wa Balozi Andrew Daraja ilifanyika nyumbani kwake, Kimara Temboni, Dar es Salaam. Mke wa Rais, Mama Salma alikuwa pia miongoni mwa waombolezaji. Wengine waliohudhuria ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda, Balozi mpya wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere na Balozi Mstaafu, Paul Rupia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, walikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika nyumbani hapo jana. Rais Kikwete aliwasili saa 7 mchana nyumbani hapo na kusaini kitabu cha wageni na kuwasalimia wafiwa. Akiendesha Ibada, Padri Kiongozi wa Kanisa Anglikana la Mtakatifu Albano, Dar es Salaam, Aidan Mbulinyingi alisema hakuna binadamu atakayeepuka kifo. Aliwaasa waombolezaji kumshukuru Mungu kwa kila jambo, wasimkufuru Mungu na wajue kuwa maisha ni kama zawadi kwa kuwa wanadamu wote lazima wapitie kifo. Akisoma wasifu, Julius Mbaga alisema Anna ni Mwalimu Mstaafu. Alizaliwa Agosti 15, 1946 wilayani Muheza. Alianza shule ya msingi mwaka 1956 na kusomea shule mbalimbali Kilimanjaro na Morogoro kabla ya kujiunga na Sekondari ya Tabora mwaka 1964 hadi 1967 na kisha Chuo cha Ualimu Marangu mwaka 1968 hadi 1969. Alifundisha shule ya msingi wilayani Kisarawe, Jamhuri na Oysterbay kabla ya kumfuata mumewe nje ya nchi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na Marekani kwa nyakati tofauti. Ameacha watoto wanne ambao ni Lydia, Juliano, Blandina na Harrieth. Anna aliuawa Jumamosi iliyopita kwa kuchomwa visu vitatu mwilini. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Kalinga aliiambia vyombo vya habari jana kwamba wanaendelea kumsaka aliyekuwa mfanyakazi wa bustani nyumbani kwa Balozi, James Mabakuri (22) kwa tuhuma za mauaji hayo. “Bado tunamshikilia mmoja. Huyo mwingine hatujampata tunaendelea kumsaka,” alisema Kamanda Kalinga. Anayeshikiliwa kwa sasa ni mfanyabiashara Majiga Masaga (27) anayedaiwa kwamba ndiye aliyempeleka Mabakuri kufanya kazi nyumbani kwa Balozi Daraja.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote