Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 10, 2010

Ajali Mbaya Dar- Daladala lagongana na Treni

DEREVA wa daladala lililokuwa na namba za usajili T.542 ALR ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amefariki dunia na abiria wengine 26 kujeruhiwa baada ya daladala aliyokuwa akiendesha kuigonga injini ya treni eneo la Yombo Dovya, jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi mkoa Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), Liberatus Sabas, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana wakati daladala hiyo iliyokuwa ikitokea Tandika ilipokuwa inakatisha Reli ya Tazara kuelekea Yombo Dovya.Alisema, katika ajali hiyo abiria 26 waliokuwa kwenye daladala hiyo, ambapo wanaume 16, wanawake 7 na watoto watatu, walijeruhiwa na watano kati yao wamekimbizwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu kwa kuwa hali zao zilikuwa tata.Alisema majeruhi wengine 21 katika ajali hiyo walikimbizwa Hospitali ya Temeke na hali zao alidai zinaendelea vizuri. Alisema kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema kuwa, dereva huyo alipofika eneo hilo hakuweza kuangalia kushoto na kulia wakati alipokuwa akivuka reli hiyo na ndipo daladala hilo lilipoigonga injini ya treni hiyo iliyokuwa ikitokea Stesheni ya Tazara kuelekea Kurasini.Hata hivyo Kamanda Sabas alisema kuwa, treni iliyohusika katika ajali hiyo haikuweza kusimama.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote