Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 4, 2010

Zuma Akiri kuwasaliti wake zake 3 na mchumba wake mpya

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amezithibitisha taarifa za vyombo vya habari kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti wa rafiki yake na amemzalisha mtoto wa kike.Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Zuma jana, Zuma amekiri kuwasaliti wake zake watatu na mchumba wake anayetegemea kumuoa hivi karibuni.Mbali na kukiri uhusiano huo, rais Zuma amepinga vikali tuhuma kuwa anaonyesha mfano mbaya wakati harakati za kupambana na ukimwi zikiendelea nchini Afrika Kusini.Asilimia 10 ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya ukimwi.Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti wiki hii kuwa Rais Zuma mwenye umri wa miaka 67 amezaa na binti wa rafiki yake wa karibu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini.Gazeti la Sunday Times la Afrika Kusini liliripoti kuwa Zuma alizisaliti ndoa zake na kuzaa na Sonono Khoza ambaye ni binti wa Irvin Khoza, mmiliki wa timu ya Orlando Pirates.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote