Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 11, 2010

Si utani Jamaa katushika

Ukikumbuka alivyoanza utadhani ni utani au utadhani kama kubahatisha fulani vile kifupi namwongelea Diamond anayetamba na ngoma yake Nenda kamwambie iliyofanyika katika studio za Sharobaro. Mpaka hivi sasa huyu dogo amekamilisha album ambayo ina ngoma kama kumi na mbili. Ameipa jina la Nenda kamwambie ambayo itasambazwa na 'FM Wasambazaji'. Ndani ya hiyo album kuna ladha tofauti tofauti ambazo amewashirikisha vichwa vya bongofleva akiwemo Ngwair na Geez Mabovu kwenye ngoma inaitwa Jisachi, Mzee wa Kabaisa Mr. Blue, Chid Benz, Rommy, Fatuma, Hemedy na dogo flani ambaye nayeye siku za karibuni atakuja kutushika ile mbaya anaitwa Hawa na ngoma ameipa jina la Nitarejea. Ameamua kufanya kwenye studio tofauti ili aweze kutoa vionjo vyenye fleva mbalimbali zikiwemo Sharobaro, 41, J-SIK na Fish crab. Baadhi ya hizo ngoma ni Nenda kamwambie, I hate you, Moyo wangu, Nalia na mengi na Toka mwazo. Albam Itaanza kusambazwa rasmi siku ya Wapendanao maarufu kama "Valentine day"

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote