Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 18, 2010

Askari mstaafu adaiwa kumuua mkewe

ASKARI mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Matiku Ng’enge (55), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kwamba, lilitokea jana saa 11 alfajiri nyumbani kwa wanandoa hao Mazizini Ukonga, Dar es Salaam. Kamanda Shilogile alisema Matiku alianza kuzozana na mkewe Rehema Matiku (42) na kuanza kumshambulia, akamchoma kisu katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo kichwani, tumboni na mikononi. Amesema, mwanamke huyo alipiga kelele na kuokolewa na majirani, lakini kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata, alidondoka na kupoteza fahamu baada ya kuvuja damu nyingi, hali iliyosababisha kifo chake. Shilogile amesema, chanzo cha ugomvi wa wanandoa hao hakijajulikana, ingawa inasadikiwa ni wa kifamilia. Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi ili kufahamu tatizo, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilala, Amana kwa uchunguzi zaidi. Shilogile amesema, mtuhumiwa huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Staki Shari, ingawa baada ya mke wake kufariki dunia, ghafla naye alipata mshtuko na kukimbizwa Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Taarifa zaidi zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinadai mwanamume huyo alikuwa akigombana na mkewe kwa mara kutokana na mwanamke huyo kutotaka kuuzwa kwa ardhi yao ambayo alidai ingeisaidia familia yao. Hata hivyo, kutokana na kikwazo hicho, jana alfajiri mumewe alimkumbushia tena suala hilo, lakini aliendelea kupinga na mume kushikwa na hasira na kuanza kumshambulia kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote