Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 10, 2010

Dunia imefika mwisho? Kijana wa miaka 35 ambaka bibi wa miaka 85 Bagamoyo

AJUZA wa miaka 80, mkazi wa kitongoji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo amebakwa na kijana mwenye umri wa miaka 35 na kusababishiwa majeraha makali katika sehemu zake za siri. Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku wa kuamkia jana na kwamba kijana aliyehusika na tukio hilo (jina linahifadhiwa), ni mkulima wa Kiwangwa wilayani humu. Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma alidhibitisha tukio hilo na kusema kuwa bibi kizee huyo alibakwa wakati akiwa amelala nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuvunja mlango usiku huo na kuingia katika chumba cha ajuza huyo kisha kumbaka kwa nguvu. Mwakyoma alisema tukio hilo linasikitisha na kutia aibu vijana kutokana na ukweli kwamba bibi huyo anaishi kwa shida na taabu nyingi. "Inavyoonekana huyo jamaa, alikuwa anamvizia ajuza kwa muda mrefu na nadhani alikuwa akimfuatilia kwa karibu ili kujua mwenendo mzima,alipobaini analala mwenyewe ndipo alipotumia mbinu ya kumvizia muda huo na kuvunja mlango na hatimaye kumbaka hata imani za kishirikina zinaweza kuwa ni chanzo,"alisema Mwakyoma. Alisema mlalamikaji anaishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo na kwamba tayari mtuhumiwa alikamatwa na anaratajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara uchunguzi utakapokamilika, mlalamikaji anaendelea vizuri.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote