Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 24, 2010

Kioja cha Mwaka - Wavua nguo na kubaki uchi Mahakamani Temeke

WASHTAKIWA watano jumatatu walifanya kituko cha mwaka baada ya kuvua nguo katika mahakama ya Wilaya ya Temeke na kutembea uchi huku umati wa watu waliokuwepo mahakamani hapo ukibaki umeduwaa. Habari zilizolifikia jana na kuthibitishwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Helleni Liwa zilisema washtakiwa hao walifanya kituko hicho jana mchana ikiwa ni hatua ya kupinga kile walichokiita kubambikiwa mashtaka. Habari zaidi zilieleza kuwa awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha, lakini waliachiwa juma lililopita kabla ya kukamatwa tena siku hiyohiyo na kufunguliwa mashtaka mengine. Jana washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa lengo la kusomewa mashtaka upya, lakini walipoitwa kuingia mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka hayo walikataa, wakidai kuwa walikuwa wakimtaka Hakimu Mfawidhi ili wamwelezee malalamiko yao hayo. Chanzo chetu cha habari kilichoshuhudia kituko hicho kilisema kuwa baada ya askari kuwalazimisha kuingia mahakamani, ndipo washtakiwa hao walipoamua kuvua nguo zote na kubaki kama walivyozaliwa. Chanzo hicho kilidokeza zaidi kuwa baada ya kuvua nguo hizo walitoka mahabusu na kwenda kukaa nje karibu na mlango wa kuingilia mahakamani jambo ambalo liliwaacha vinywa wazi watu waliokuwepo mahakamani hapo. Akidhibitisha Hakimu Mfawidhia Liwa kuwa washtakiwa hao kufanya kituko hicho na kusema kwamba aliagiza washtakiwa hao wapandishwe kizimbani na kusomewa mashtaka mapya ya kuvua nguo hadharani. "Ni kweli kabisa tukio hilo limetokea leo muda wa saa 8 hivi mchana, nami nimewashuhudia,"alisema Hakimu Liwa. Alisema awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha, lakini walifuatiwa mashtaka na kuachiwa huru mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mapya. Kwa hiyo jana walifikishwa mahakamani hapo mapema tu kwa ajili ya kusomewa tena mashtaka hayo upya. Walifikishwa mapema tu lakini walipoitwa kuingia mahakamani kusomewa mashtaka walikataa wakidai kuwa wanataka kuonana na mimi, alisema Hakimu Liwa na kuongeza; "Ndipo nilipoamua kwenda kuwaona ili kuwasikiliza lakini nikawakuta wako uchi wa mnyama kama walivyozaliwa, na baada ya kuwakuta katika hali hiyo nikawambia siwezi kuzungumza nao wakiwa katika hali kama hiyo, hivyo wakawambeleza wakavaa nguo ndipo nikazungumza nao." Hakimu Liwa aliongeza kuwa washtakiwa hao walimlalamikia kuwa wamechoka na mashtaka wanayofunguliwa kwani wanakamatwa na kubambikiwa kesi na wanapelekwa mahakamani lakini hakuna ushahidi. "Lakini niliwaeleza wazi kuwa walichokifanya ni makosa kwani kwani walitakiwa watii kwanza kuingia mahakamani na kama wana malalamiko mengine ndio yangefuata na si kuvua nguo, alisema Hakimu Liwa, na kuongeza; "Hivyo kwa kuwa mimi nilikuwa ninaondoka kwenda Mahakama Kuu, nilimwagiza Hakimu Rose Kaliwa ambaye ndiye alikuwa awasomee mashtaka mapya ya leo, awasomee mashtaka ya kuvua nguo mbele ya hadhara"

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote