Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 18, 2010

Mamia wahudhuria mazishi Musoma

MKUU wa Mkoa wa Mara, Kanali Enos Mfuru jana aliongoza maelfu ya wakazi wa Musoma mjini katika mazishi ya watu 17 wa ukoo mmoja waliouawa kikatili na watu wasiojulikana kwa kile kilichodaiwa ni kulipiza kisasi juzi. Akizungumza muda mfupi kabla ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu hao katika Kata ya Butare wilayani humo, Mfuru aliwahakikishia waombolezaji na wananchi wote wa mkoa wa Mara kwamba serikali itawalinda waliobaki na kwamba watadhibiti vitendo hivyo. Alisema msaada huo utajumuisha udhamini katika masomo ya kijana mmoja aliyesalimika katika tukio hilo na madawa kwa ajili ya majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara. Mfuru aliwataka wananchi wa mkoa kushirikiana kwa pamoja na maofisa wa polisi kuhakikisha kwamba, wauaji hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka. "Nawahakikishia wananchi wote wa Mara kwamba, uongozi wenu wa mkoa utafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa mnapata ulinzi wa kutosha ili kuepukana na mauaji kama hayo pamoja na kukomesha kabisa matukio ya namna hii," alisema Mfuru. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Dk Benedicto Mwijarubi, alisema hali ya majeruhi mmoja kati ya watatu waliofikishwa hapo Maria Kawawa (18), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Buhare ni mbaya. "Anakabiliwa na maumivu makali kichwani, jicho lake la kushoto, shingoni na mkono wake wa kushoto umeondolewa moja kwa moja na wauaji hao," alisema Dk Mwijarubi. Alisema mwanafunzi huyo amepoteza zaidi ya lita mbili za damu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa tukio hilo na kwamba, waganga wa hospitali hiyo wanafanya juhudi kuokoa maisha yake. Alifahamisha kuwa hali ya majeruhi wengine wawili Moris Mgaya (40) na Maximillian Roba (20) inaendelea vizuri hospitalini hapo ambapo wamelazwa wakipatiwa matibabu. Miongoni mwa ndugu hao wa ukoo mmoja waliopoteza maisha juzi kwa kukatwakatwa kwa mapanga ni Nyasinde Moris, Mgaya Moris, Mage Moris, Maheri Moris, Alice Moris na Kado Moris. Wengine ni pamoja na Kawawa Kinguye, Angelina Kawawa, Kinguye Kawawa, Mengi Kawawa, Nyarukende Kawawa, Juliana Kawawa, Nyambona Kawawa, Nyanyama Kawawa, Dorika Mgaya, Umbera Mgaya na Sospeter Sopereti. Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Mara Robert Boaz, alisema maofisa wa polisi kwa kushirikiana na wananchi hadi jana jioni inawahoji watu watano ambao wanahusishwa na tukio hilo la kinyama.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote