Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 10, 2010

Kipawa wapokea fidia kwa shingo upande

KAZI ya kulipa fidia kwa wakazi zaidi ya 200 wa Kipawa jijini Dar es Salaam waliogoma kupokea fidia zao kwa sheria ya zamani ilianza jana huku kasoro mbalimbali zikiibuka kwenye mchakato huo. Kasoro hizo ni pamoja na baadhi ya watu kukosa vitambulisho na wengine majina yao ya kwenye vitambulisho yakitofautiana na yaliyopo kwenye hundi za malipo. Mwenyekiti wa kamati ya malipo ya wakazi hao Edgar Japhet aliyaambia baadhi ya magazeti kuwa kasoro hizo zimekwamisha utaratibu waliokuwa wameupanga wa kulipa fidia kwa siku moja na kwamba kazi hiyo sasa itafanywa kwa zaidi ya siku moja ili kuhakikisha kasoro hizo zinarekebishwa na wakazi wote wanalipwa fidia zao. Alisema kamati yake haiwezi kulipa fidia kwa watu ambao hawana vitambulisho pamoja na wale ambao majina yalipo kwenye vitambulisho yanatofautiana na majina yaliyopo kwenye hundi za malipo. Kwa upande wa wakazi hao walipokea fidia hizo wa shingo upande huku wakilalamika kuwa wameamua kupokea kutokana na hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuwavunjia makazi yao. Mwenyekiti wa kamati ya wenye nyumba Kipawa Magnus Mulisa alisema fedha walizolipwa ni ndogo na si hiyari yao bali ni kutokana na kubomolewa nyumba zao na wao kukosa mahali pa kuishi. "Hakuna mkazi hata mmoja anayepokea fedha hizo kwa hiyari yake kwani wote walipinga kuchukua kwa sheria ya zamani, bali ni kutokana na kitendo cha kubomolewa nyumba zetu hivyo na sisi kukosa mahali pa kuishi,"alisema Mulisa. Mulisa alisema mara baada ya kuchukua fidia hizo wakazi hao wanatarajia kutinga mahakamani kuishitaki Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (Taa) na Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart ya jijini Dar es Salaam kwa kitendo chake cha kubomoa nyumba zao bila ya kufuata sheria. Aliituhumu kampuni hiyo kuwa imefanya kazi yake kinyume na taratibu za udalali kwa kitendo chake cha kubomoa nyumba hizo bila ya kutoa taarifa za siku 14 kama sheria inavyowataka kufanya. Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama alitetea uamuzi wa serikali kubomoa nyumba za wakazi wa Kipawa kwa kusema bomoa bomoa hiyo ni halali na ilifanywa kwa mujibu wa sheri za nchi.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote