Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, February 5, 2010

Phiri atoa sababu ya kutoa sare

BAADA ya kutoka sare ya bao 11, Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema kikosi chake kilishindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar kwa sababu wachezaji wake walibweteka baada ya kupata ushindi mfululizo na uchovu wa safari. Katika mpambano kati ya timu hizo uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Simba ilishindwa kufurukuta mbele ya wenyeji Kagera Sugar na kuambulia sare ya bao 1-1."Tatizo ni kwamba tulipata bao tukaona tumemaliza kila kitu badala ya kuimarisha ulinzi tukajisahau," Phiri aliliambia gazeti moja la kila siku.Alisema baada ya Simba kushinda mechi 14 wachezaji wake walijisahahu na hali ya ushindi huku wakisahau kuwa wanatakiwa kucheza kufa na kupona hadi mwisho.Phiri ambaye kabla ya kuja kanda ya ziwa alitamba kunyakuwa pointi sita zote ikiwa ni katika mchezo dhidi ya Toto African pamoja na Kagera Sugar amejikuta akiambulia pointi nne."Hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi kwa sababu ya hii sare lengo letu liko pale pale kutwaa ubingwa na hakuna shaka kwamba tutaifunga Manyema katika mchezo unaofuata na kukamata pointi zote tatu,"alisema Phiri.Mara baada sare hiyo, baadhi ya mashabiki wa Simba walisikika wakisema hawatasafiri tena na timu hiyo mikoani kwa sababu walitarajia wangeshinda lakini mambo yamekuwa kinyume.Simba inayoongoza ligi kwa pointi 43, baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar watani wao wa jadi Yanga yenyewe wamefikisha pointi 33 kufutia ushindi wao mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru na sasa kutofautiana kwa ponti 10.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote