Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, February 16, 2010

SMZ yamwaga Ajira 500 kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), inatarajia kuajiri walimu 500 ili kupunguza upungufu wa watalaam hao katika shule za msingi na sekondari visiwani. Hayo yalielezwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amal, Haroun Ali Suleiman, baada ya kujitokeza upungufu wa walimu kwa baadhi ya shule. Alisema walimu hao wapya wanataaluma ya cheti na Stashahada na kazi hiyo itafanyika katika wilaya tatu ambazo zimeonekana kuwa na upungufu wa walimu Zanzibar. Waziri Haroun, alisema serikali imo katika mikakati ya kuimarisha sekta ya elimu kwa vile ina umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Serikali wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini kwa wananchi wake. Wilaya zitakazonufaika na mpango huo ni Micheweni na Mkoani Kisiwani Pemba na Wilaya ya Kaskazini A Kisiwani Unguja. Aidha alisema serikali inaendelea na mpango wake wa kujenga nyumba za walimu ili waishi karibu na vituo vya kazi.Hata hivyo, alisema mpango wa kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar pia utazingatia maslahi ya walimu kama vile mishahara na posho ili kuwawekea mazingira mazuri ya kazi. Tayari serikali imeamua kurejesha posho la asilimia 25 la kufundishia kwa walimu ili kuwapunguzia ukali wa maisha, kama ilivyokuwa imeamuliwa na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani mwaka 2007. Hata hivyo, shule nyingi hivi sasa Zanzibar zinakabiliwa na uhaba wa walimu wa sayansi na hisabati na kuathiri maendeleo ya wanafunzi wengi visiwani katika masomo

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote