Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 10, 2010

Kitendawili cha Hatima ya Nguza na Wanawe kufumbuliwa kesho!!!!!

KESHO huenda ikawa ni siku ya kicheko ama huzuni kwa familia ya mwanamuziki Nguza Viking kwa kuwa Mahakama ya rufani inatarajia kutoa uamuzi wa rufani dhidi ya hukumu ya adhabu ya kifungo cha maisha waliyoitumikia kwa muda mrefu. Hayo yamekuja baada Mahakama ya Rufani Tanzania, kutoa uamuzi wa rufani dhidi ya hukumu ya adhabu ya kifungo cha maisha kilichotolewa kwa mwanamuziki Nguza Vicking almaarufu kama ‘Babu Seya’ na watoto wake watatu.Uamuzi huo utasomwa kesho mbele ya jopo la majaji watatu ambao ni Jaji, Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati ambao waliosikiliza rufaa hiyo.Rufaa hiyo ilipelekwa Desemba mwaka jana katika Mahakama hiyo na kusema kuwa haki ya kisheria haikutendeka kwa mujibu wa sheria.Mahakama hiyo ya Rufaa iliambiwa kuwa, Hakimu Addy Lyamuya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam aliongeza maoni yake katika kutoa adhabu ya kifungo cha maisha dhidi yao badala ya kufuata utaratibu wa kisheria.Pia Mahakama hiyo iliombwa kuwaachia huru wafungwa hao kwa kuwa ushahidi uliotumika kuwafunga ulikuwa na mapungufu ya kisheria.Wakili wa wafungwa hao, Mabere Marando, alidai kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha kwamba Babu Seya na watoto wake walitenda kosa la kuwalawiti watoto 10 wenye umri wa chini ya miaka minane.Aidha, Marando aliiambia Mahakama hiyo kuwa, watoto tisa kati ya 10 waliotoa ushahidi hawakuapishwa na Mahakama, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.Awali katika hukumu hiyo, Juni mwaka 2004, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Babu Seya na wanawe walihukumiwa na Hakimu Lyamuya kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha, baada ya kukutwa na hatia ya makosa 10 ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo.Hata hivyo wafungwa hao Januari 27, 2005, waliwasilisha rufaa kupinga adhabu hiyo katika Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Thomas Mihayo ambaye hata hivyo alitupilia mbali rufaa yao ya awali iliyofunguliwa na wakili wao Herbert Nyange.Awali kesi hiyo ilifikishwa mahakamani kwa mwanamuiki huyo n wanawe kwa kukabiliwa na mashitaka yapatayo 11.Ilidaiwa kuwa, washitakiwa hao wote kwa pamoja walidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Aprili na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam.Katika kesi hiyo, mwalimu wa Shule ya Msingi ya Mashujaa, Sigirinda Ligomboka, alishtakiwa kwa makosa mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa ya kubaka na kulawiti kwa kuwaruhusu baadhi ya watoto hao kutoka madarasani, lakini Hakimu Lyamuya alimuachia huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.Hivyo kesho katika mahakama hiyo ya rufaa kunaweza kukatokea mambo mawili makubwa ambayo watanzania wanasubiria kwa hamu aidha wafungwa hao kuachiwa huru ama kuendelea na kifungo hicho gerezani

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote