Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 10, 2010

Wanafunzi wa Sheria Mbaroni kwa Vyeti FEKI

Wanafunzi tisa wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wanashikiliwa na Polisi wilayani Lushoto mkoani Tanga, baada ya kubainika waliwasilisha vyeti vya kughushi wakati walipojiunga na chuo hicho Septemba, mwaka jana. Hatua ya kukamatwa kwa wanachuo hao inatokana na utaratibu ulioanzishwa na Uongozi wa chuo wa kuvifikisha vyeti vya wanafunzi kwenye Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kwa ajili ya uhakiki kufuatia kuwepo kwa tatizo sugu la kughushi vyeti kwenye maeneo mbalimbali nchini. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Ntemi Kilekamajenga, amesema jumla ya wanachuo 413 walijiunga na chuo hicho Septemba mwaka jana ambapo 248 walikuwa wa kozi ya Stashahada ya Sheria na 165 walikuwa wa ngazi ya Cheti na kueleza kuwa kati ya hao tisa ndio waliothibitishwa na Necta kuwa walighushi vyeti. Kilekamajenga aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faida Mulunga, Esther Said, Sofia Mjembe, Gideon Mgombela, Mohamed Said, Bastian Risso, Joyce Joseph, Ally Mganga na Victoria Shomari. Alisema miongoni mwa wanachuo hao wanaotuhumiwa kughushi vyeti wengine walidanganya matokeo ya ufaulu, wengine walitaja vituo vya mitihani ambaavyo kwa wakati huo havikuwepo sambamba na kubadili majina kwa kutumia majina yasiyo ya kwao kwenye vyeti hivyo. Kabla ya kukamatwa kwa wanachuo hao, Afisa Upelelezi wa Wilaya ya Lushoto, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Madafu Abdallah, aliwafeleza watuhumiwa hao sababu za kukamatwa kwao.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote