Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 3, 2010

Ugonjwa wa ajabu wamfanya aonekane kama mtu mzima, umri wake halisi ni miaka 13 tu

Je unaweza kukisia umri wa mtu huyu pichani? ukweli ni kwamba Zara Hartshorn wa Rotherham nchini Uingereza ambaye umri wake halisi ni miaka 13 anakabiliwa na ugonjwa unaoitwa lipodystrophy aliourithi toka kwa mama yake mzazi ambao humfanya aonekane mzee sana kuliko umri wake huku akiwa na tabia za kitoto kama watoto wenzake.Mama yake Zara bi Tracey Pollard ilibidi achukue uamuzi wa kumsimamisha masomo Zara kwakuwa alikuwa akitaniwa sana na wenzake akiitwa "Bibi" na kubandikwa majina kadhaa ya fedheha.Ugonjwa unaomkabili Zara umewahi kuwatokea watu 2,000 tu duniani ambapo tabaka la chini la mafuta la ngozi hutoweka na kuifanya ngozi izeeke kwa spidi ya ajabu sana.Ugonjwa wa lipodystrophy hauna tiba hivyo Zara ataendelea kuzeeka mapema jinsi anavyozidi kuendelea kukua.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote