Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, February 15, 2010

Nyota wa Muziki wa Pop wa kundi la "No Angels" wa Ujerumani hatiani kwa kuwambukiza Ukimwi Wanaume Watatu

Waendesha mashtaka wa Ujerumani jana ijumaa walimuona msanii maarufu wa kundi la "No Angles" Nadja Benaissa mwenye umri wa miaka 27 ana hatia ya kuwaambukiza ukimwi wanaume watatu aliofanya nao mapenzi bila kinga. Nadja anadaiwa kufanya mapenzi na wanaume hao kati ya mwaka 2000 na 2004 bila kuwataarifu kuwa yeye ni muathirika.Nadja alikuwa akijitambua fika kuwa yeye ni muathirika tangia mwaka 1999, nyaraka za mahakama zilisema."Alikuwa akijua wazi kuwa kwa kufanya mapenzi bila kinga atawaambukiza maradhi yake wanaume hao", alisema mwendesha mashtaka katika mji wa Darmstadt ulio jirani na Frankfurt.Mmoja wa wanaume hao watatu ameishathibitishwa kuwa ameambukizwa virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi.Kundi la No Angeles liliibuliwa na mashindano ya vipaji kwenye luninga mwaka 2000 na baada ya kujipatia umaarufu mkubwa walifanya ziara nyingi sana barani ulaya kabla ya kundi hilo kuvunjika mwaka 2003.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote