Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, February 15, 2010

Rais Kikwete atangaza Malaria Janga la Taifa

RAIS Jakaya Kikwete ameutangaza ugonjwa wa malaria kuwa ni Janga la Taifa na kuwaambia Watanzania kuwa Serikali yake imeanza safari ya kuutokomeza ugonjwa huo nchini. Malaria ndiyo ugonjwa unaoua Watanzania wengi zaidi kuliko mwingine wowote. Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa marais wanaopambana na malaria barani Afrika alisema kwamba, ugonjwa wa malaria ni vita ambavyo ni lazima Watanzania wavishinde kwa vile nia ipo, sababu ipo na uwezo upo. Aliongeza kusema kuwa, lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa malaria inakuwa ugonjwa wa historia kwa Tanzania kwa kuwa hata nchi nyingine zimefanikiwa kuutokomeza. Alisema kuwa kila siku ya Mungu, kiasi cha watu kufikia 291 hufariki kwa ugonjwa wa malaria, wengi wao wakiwa watoto wadogo, vifo ambavyo alivielezea kuwa vinaweza kuzuilika na kutibika. "Kila siku ya Mungu, hapa nchini, wanakufa watu hadi 291 kwa ugonjwa wa malaria. Kwa maneno mengine, kila saa inayopita, wanakufa watu zaidi ya 10 kwa ugonjwa wa malaria." Rais Kikwete aliliambia taifa usiku wa kuamkia jana. "Hawa ni watu wengi mno. Hivyo, malaria ni Janga la Taifa letu. Lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba malaria ni ugonjwa unaoweza kuzuilika na kutibika. Ndiyo maana tumeamua kuwa wakati tunaendelea kushughulikia kutibu wagonjwa wa malaria, tuelekeze nguvu zetu katika kuzuia kwa kuanza juhudi za kutokomeza malaria nchini." Rais Kikwete alikuwa akizungumza moja kwa moja na taifa wakati anazindua Kampeni dhidi ya Malaria katika burudani maalumu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club mjini Dar es Salaam juzi usiku.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote