Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 11, 2010

Hijabu yazua Kasheshe Uarabuni

Balozi mmoja katika nchi za kiarabu jina kapuni alizivunja sherehe za harusi baada ya kuiona sura ya mkewe kwa mara ya kwanza muda mfupi baada ya kufunga naye ndoa na kugundua ana makengeza na vinyweleo kwenye kidevu chake (ndevu za wanawake).Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News balozi huyo alikuwa akikutana na mwanamke huyo mara chache sana kabla ya siku ya harusi na wakati wote mwanamke huyo alikuwa akiufunika uso wake kwa Niqab (Vazi linalofunika uso na kuacha macho pekee wazi).Baada ya ndoa kufungishwa balozi huyo alitaka kumbusu mkewe na ndipo alipofanikiwa kuiona sura yake kwa mara ya kwanza na kugundua ana vinyweleo kwenye kidevu na ana macho yenye makengeza.Balozi huyo alikata shauri la kuivunja ndoa hiyo kwenye mahakama ya sharia za kiislamu katika falme za kiarabu akisema kuwa aliingizwa mkenge wa ndoa na mama wa mwanamke huyo baada ya kuonyeshwa picha za dada yake badala ya zake.Balozi huyo alitaka ndoa hiyo ivunjwe na pia alimtaka mwanamke huyo amlipe fidia ya dirham 500,000 kwa mikufu, nguo na zawadi zingine alizomnunulia.Mahakama ilikubali kuivunja ndoa hiyo lakini ilitupilia mbali madai ya fidia ya balozi huyo.Taarifa iliyotolewa haikutaja jina la balozi huyo na wala haikutoa maelezo zaidi kuhusiana na sakata hilo.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote