
Kampuni ya teknolojia ya Google inatarajia kutoa simu zinazotafsiri lugha zaidi ya 6000 zinazozungumzwa duniani ili kuwawezesha watu wanaozungumza lugha tofauti kuelewana.Google ambao awali walijiingiza kwenye biashara za simu kwa kutoa simu zao zinazoitwa Nexus One, tayari wanatamba na programu yao waliyoitoa ambayo inatafsiri maandishi katika lugha tofauti tofauti.Wiki iliyopita lugha ya Haiti "Creole" iliongezwa katika programu hiyo na hivyo kuzifanya lugha ambazo zinawezwa kutafsiriwa maandishi yake na programu ya Google kufikia 52.Hadi sasa Google imeishawawezesha watumiaji wa simu kutumia mfumo wa kutambua sauti kusachi vitu kwenye google kwa kuvitamka badala ya kuviandika.Google itaziunganisha teknolojia zake hizo mbili ili kuweza kutoa simu zitakazokuwa zinafanya kazi kama mkalimani.Kama ilivyo kwa watu wanaofanya kazi ya ukalimani, Simu hizo pia zitakuwa zikisiliza sentensi nzima mtu anayoongea ili kuelewa kinachosemwa kabla ya kuanza kuitafsiri.Mkuu wa huduma ya ukalimani ya Google, Franz Och, amesema kuwa wanachohangaikia kwa sasa ni kuuongeza usahihi wa kutambua sauti na kuweza kutafsiri kwa usahihi.Simu hizo mpya za Google zinatarajiwa kuingia madukani ndani ya miaka michache ijayo.
No comments:
Post a Comment