Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 4, 2010

TFF yatangaza kibarua kwa wazawa?

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza nafasi za ukocha kwa wazawa katika mchakato wa kupata mrithi wa Marcio Maximo anayemaliza mkataba wake mwezi Julai. TFF imeeleza kuwa wazawa wanaweza kuomba nafasi hiyo ya kuifundisha Taifa Stars na kuwa wao watapewa kupaumbele kama ilivyo kwa wenzao wa kigeni. Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa tayari wamepata maombi mengi yakiwamo ya makocha kutoka nchi za Afrika na Ulaya na kuongeza kuwa bado wanawapa nafasi wazawa nao ili waombe nafasi hiyo. Alisema hadi sasa wamepata maombi kutoka nchi za Venezuela, Zambia, Uingereza na Ureno. "Tuna walimu (makocha) wengi wazuri na wenye uwezo wa kufundisha Taifa Stars, hivyo ni wakati wao wa kujitokeza na kuomba nafasi hiyo kwani tutawapa kipaumbele kwa asilimia kubwa, ingawa pia tumepata maombi mengi toka kwa makocha wengine kutoka Ulaya na Afrika. Kwa jumla idadi ni kubwa na wote wana vigezo ambavyo tunahitaji,"alisemaMwakalebela.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote