Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, February 11, 2010

Hatima Ya Nguza Familly - At least Haki imetendeka ingawa sio 100% Papii na baba yake kurudi gerezani Kutumikia Kifungo, Mbangu na Fransic huru tena!!

Mahakama ya Rufaa nchini imeamuru mwanamuziki Nguza Vikingi na mwanae Johnson Nguza "Papii" warudishwe gerezani kwenda kutumikia kifungo cha maisha baada ya kuonekana kuwa na hatia ya kutenda makosa hayo. Mbali na wawili hao kurudishwa gerezani mahakama hiyo imewaachia huru watoto wa mwanamuziki huyo ambao wote walikuwa wanatumikia kifungo hicho baada ya mahakama hiyo kuona washitakiwa hao walibambikiziwa kesi.Walioachiwa huru ni mshitakiwa wa tatu Mbangu Nguza na mshitakiwa wa nne, Fransic Nguza ambao ni watoto wa mwanamuziki huyo wameonekana kutokuwa na hatia na hawakuhusika katika ubakaji huo.Nguza na Johnson “Papii” wamerudishwa gerezani kwa kupatikana na mashitaka matano ambayo yaliwarudisha rumande kati ya mashitaka 23 yaliyokuwa yanawakabili awali.Hivyo hukumu hiyo ilioyotolewa mahakamani hapo leo asubuhi ndio mahakama ambayo ina mamlaka ya mwisho dhidi ya rufaa iliyowasilishwa na washitakiwa hao na hawataweza kuachiwa huru tena labda msamaha wa rais uweze kuwakomboa wanamuziki hao.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote